Wanaotuhumiwa makosa mbalimbali kufuatia matukio ya Oktoba 29, wafikishwa Mahakamani. Jennifer Bilikwija Jovin maarufu kama Niffer ni mmoja waliofikishwa leo Mahakamani.
@Ndolezi_Petro@helman_joshua Mbona @zittokabwe
Hajaongea lolote kuhusu watu wake kupewa kesi ya wizi wa kutumia silaha?
Au ni danganya toto ili ionekane wote wanakamatwa halafu baadae wa kwenu wanachiwa.
Leo Tar. 08/10/2025.
Ni siku nyingine tutakwenda kumsikiliza Shahidi wa Jamhuri (PW1) ambae ni ACP George Wilbad Bagyemu akiendelea kuulizwa maswali ya Dodoso na Mshitakiwa Mhe.Lissu.
Labda niwapatie Dondoo Chache zilizojiri jana.
1. George anasema alipeleleza kesi ya uhaini kwa siku nne kuanzia tar. 04 hadi 06 ya Mwezi wa 4, 2025. Ilipofika Tar. 08/04 akaletewa DCP Amin Mahamba kutoka Makao Makuu ya Polisi Dodoma.
2. Na yeye ndie aliyeamua kwamba kesi ile ni ya uhaini bila kushurutishwa na mtu yeyote na bila kupokea ushauri wa mtu yeyote ikiwemo ofisi ya DPP. Wakati kiutaratibu DPP ndio huamua aina ya mashitaka ya kufungua. Amesema pia hakuwasiliana kabisa na Ofisi ya DPP.
3. Anasema aliunda timu ya Upelelezi ambayo wakat anatoa ushahidi wake hakuitaja kwa majina lakini timu hiyo pia licha ya kuwa ilipeleleza haipo kwenye orodha ya mashahidi watakaoletwa mahakamani.
Sijui why hawajaletwa na pia kwanin aliwaficha wakat anaanza kutoa ushahidi wake
4. Amesema katika ushahidi wake kuwa ilimchukua miaka mitatu tu ndani ya jeshi la Polisi kupanda vyeo hadi kufikia cheo na ngazi ya Inspector wa Polisi. Aliingia Jeshi 2003 na mwaka 2006 akawa Inspector. Polisi wanafahamu namna vyeo vya kipolisi husotewa. Huyu Mwamba amepanda vyeo kama upepo.
5. Kesi ambazo amewahi kupeleleza kubwa zinazowahusu wanasiasa zote hazijawahi kufika kokote. Mfano wa kesi ya Dr. Slaa ambayo iliondolewa, kesi ya Pili ya John Heche alimwambia Rais ana akili ya tope ambayo nayo iliondolewa (Nolle Proseque) Kesi nyingine ya James Lembeli akiwa mgombea Ubunge wa Jimbo la Kahama hiyo hajui hata iliishaje na ya mwisho ni hii ya Tundu Lissu.
In short kajibu kuwa hajawahi kupeleleza kesi ya Political Figure yeyote ikafika hata mwisho na mahakama kutoa hukumu. Zote zilifutwa njiani hii maana yake amekuwa akipeleleza kesi za kusingizia watu.
6. Kwamba alijiandika maelezo yake mwenyewe kama shahidi ambae ni Mpelelezi
Utaratibu wa kisheria lazima shahidi yeyote aandikwe maelezo na afisa wa polisi hata kama na yeye ni afisa wa polisi lengo ni ili akuonye na akutahadharishe useme ukweli asa George alijionya mwenyewe, akajiandikia mwenyewe na kuyasaini mwenyewe, alimaliza kila kitu mwenyewe kibabe kabisa kwamba mtanifanya nin kwa mfano? π
7. Amekiri kuwa kosa la Lissu ni kutoa na kusambaza maneno yanayosadikika kubeba uhaini lakini maneno hayo anakiri kwenye mashitaka kuwa yalisambazwa kupitia Jambo TV.
Sasa akaulizwa Je Lissu ni mfanyakazi wake Jambo TV? Je ni lini aliipata password ya kuingia kwenye mitandao na channel ya Jambo ya Jambo TV kusambaza hizo video. Kumbuka kosa kwa maelezo yao ni kwamba Lissu alisambaza ila ushahidi wa Jamhuri ikiwemo yule shahidi "P" anasema ni wao Jambo TV ndio walisambaza.
8. Licha ya yeye kuwa Mpelelezi Mkuu kwa zile siku nne lakin hakuwahi kusoma maelezo ya mashahidi wengine ambayo yalikuwa yakiwasilishwa kwake lakin bado ndani ya siku zote aliamua kujiridhisha na kusema linapaswa kufunguliwa shitaka la uhaini.
Kumbuka ili uamue shitaka la aina gani lifunguliwe lazima ujiridhishe na ushahidi ulioukusanya na zoezi hilo linafanywa na ofisi ya DPP sio yey ila George msaidizi wa Mafwele alimaliza kila kitu Mwenyewe.
9. Pia alikuwa anataka kujaribu kuwasemea mashahidi wengine Mh. Lissu akamwambia apunguze kiherehere kwasababu kila shahidi atakuja ikiwemo yule wa KAZI NA UTU.π anamaanisha SAMIA.
10. Wakati anamuuliza maswali alikuwa anamuita George NSHOMILE π Msomi wa Jeshi la Polisi ambae kuita waandishi wa habari ni kosa la uhaini, wamezoea kusingizia watu kesi, ataendelea nae leo na kuendelea inategemea na atakavyotoa ushirikiano.
Pia alisema anaitaka Mahakama iseme kuhusu Mgeni wake Dr. Stephanie ambae anashikiliwa na idara ya Uhamiaji. Alikamatwa pale Mahakamani akiwa anaingia kufuatilia kesi ya Mh. Lissu, leo mahakama imesema italitolea ufafanuzi Jambo hilo.
Acha tuone nini kitakachojiri kwenye maswali ya Dodoso (Cross Examination) muda mfupi ujao.
Mhabarishaji wenu Hilda Newton Chadema
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Leo Oktoba 8, 2025
Jana tuliishia Part 64 so leo tunaendelea na
Part 65
Mhe. Lissu ameshaletwa hapa.
Amepiga Kombati ya Kaki ya CHADEMA.
Shahidi nae amaingia amevaa shati la kanisani kabisa lina maua maua.
Utafikiri amekuja kuongea ukweli vile.π
Sauti ya Courtttttt imesikika.
Majaji wanaingia na Mh. Lissu anatoa vitu vyake kwenye mifuko yake.
Makabrasha mengi sana na mavitabu.
Majaji wanaandika kidogo hapa.
Anaitwa Karani anasoma jinai na 19605/2025 Jamhuri dhidi ya Tundu Lissu.
Jaji anawaita Mawakili wa Serikali wajitambulishe anaongoza Kazi hiyo Renatus Mkude, Wakili Mkuu wa Serikali akiwa pamoja na wenznake akina Ajuaye Zengeli, Nassoro Katuga, Ignas Mwinuka, Thawabu Issa, Harrison Lukosi, Cathbert Mbiringe na Winiwa Kasawa. Mshitakiwa yupo na anajitetea mwenyewe. Tuko tayari upande wa Jamhuri.
Jaji anamuuliza Mshitakiwa na Lissu anajibu na mimi niko tayari Waheshimiwa Majaji.
Jaji anamuonya Shahidi kuwa yuko chini ya kiapo. Akumbuke hilo.
Sasa kabla hatujaendelea kulikuwa na lile jambo kuhusu mmoja ya watu uliowaorodhesha alikuwa Na. 12 kwenye orodha.
Tulimwambia Msajili kuwa alifuatilie na uhalisia ni kwamba uhamiaji walisema wanahitaji nyaraka kwa mtu huyo na tumeambiwa Bwana mmoja anaitwa Heche alikuwa analifuatilia.
Kwahiyo nasisi mahakama tutaendelea kulifuatilia pia.
Tuendeleee.
Maswali yanaanza.
Mhe. Lissu : Habari ya asubuhi shahidi
George: Nzuri.
Mhe. Lissu: Mhe Jaji hiyo usiirekodi.
Mhe. Lissu: shahidi kuna mambo nataka tumalize haraka haraka katika maelezo yako ya juzi ulisema ulishika madaraka pia ndani ya hii miaka yako 22 ya upolisi ulikuwa Deputy RCO wa Rufiji 2008.
George: Ni kweli kabisa.
Mhe.Lissu: Ulikuwa Rufiji lini?
George : Nilikuwa kuanzia tar. 01/07/2018 hadi Tar. 17/07/2019.
Mhe. Lissu: waeleze majaji kama Rufiji ni mkoa wa kipolisi au wilaya ya kipolisi?
George: Rufiji ni Mkoa wa kipolisi wenye wilaya nne.
Mhe. Lissu: Ni nani alikuwa RPC wako?
George: SACP Onesmo Lyanga.
Mhe. Lissu : NANI ALIKUWA RCO?
George: Alikuwa anaitwa ACP Faustine Mafwele na mwingine SSP Richard Mchomvu.
Mhe. Lissu : Mafwele huyu huyu?
George: Kimya
Mhe. Lissu : Nilikwambia jana uwe unajibu maswali yangu usiwe na kiherehere.
Mhe. Lissu : Je kipindi kile ukiwa Deputy RCO mkuranga, kibiti, kulikuwa na mauaji mengi?
George : Ni kipindi hicho hicho kweli nilikuwa Deputy RCO.
Mhe. Lissu : JE unakumbuka idadi ya waliouawa?
George: Sikumbuki idadi yao.
Mhe. Lissu : Je unaweza kueleza sababu ya mauaji hayo mengi?
George : Kulikuwa na makosa mengi ya kigaidi ndo maana yalikuwepo.
Mhe. Lissu : Na wewe ulikuwa Deputy RCO na hujui idadi ya watu wengi waliokufa?
George : Ungenipa muda ningekuja na idadi hiyo halisi.
Mhe. Lissu : Wakati unaonyeshwa ile video ulikuwa na police notebook?
George: Yes nilikuwa nayo na hiyo notebook niliitumia kurekodi yale muhimu.
Mhe. Lissu: Naomba ueleze kama uliwasilisha hiyo Police notebook?
George: Sikuiwasilisha.
Mhe. Lissu : Ulizungumza kwa kiasi kidogo juu ya mashahidi waliopatiwa ulinzi wa mahakama?
George : Ndio ni sahihi.
Mhe. Lissu: Waeleze Majaji kama ulihusika kuwahoji hao mashahidi wa siri?
George: Sikuhusika kabisa kuwahoji.
Mhe. Lissu : Ieleze Mahakama kama unawafahamu hao mashahidi wa siri?
George: Siwafahamu kwa majina.
Mhe. Lissu : Waeleze majaji kama uliona maombi yaliyopelekwa mahakama kuu kuwaombea ulinzi?
George : Sikuyaona kabisa.
Mhe. Lissu : uliona hati ya viapo ya AMIN MAHAMBA NA MOSSIE KAHIMA?
George: Sikuona kabisa.
Mhe. Lissu : Je unajua chochote kuhusu kilichofanya katika jambo hilo la mashahidi wa siri?
George : Mimi ninachojua waliopatiwa ulinzi huo ni raia tu.
Part 66 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba repost yako kwenye tweet hii.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 66
Mhe. Lissu : Matukio ya tarehe 07/04 ulisema Andrew Churu alitoka Makao Makuu ya polisi Dodoma na kuja Dar es Salaam kukuletea vifaa kadhaa na maelezo ya shahidi P?
George: NI KWELI VYOTE ALIKUJA NAVYO. NILIPOKEA.
Mhe. Lissu: Ulimuelekeza akabidhi vitu hivyo kwa Peter Malugala.
George: Ni sahihi kabisa.
Mhe. Lissu: Ulimwambia pia aandike maelezo yake yeye Mwenyewe?
George: Nilisema aandike maelezo.
Mhe. Lissu: Ulisema maelekezo yaandikwe na nani?
George: Sikujali nilisema tu aandike maelezo.
Mhe. Lissu : Kwahiyo hukujali kama anaaandika mwenyewe?
George: Yes sikujali.
Mhe. Lissu : Andrew Churu alijiandikia Mwenyewe?
George: Sikusoma maelezo yake.
Mhe. Lissu : Alijiandikia na kujionya mwenyewe?
George: Mimi sikusoma kiukweli.
Mhe. Lissu: Kesi ya ugaidi husomi mashahidi?
George: Mahamba ndio alisoma hilo sio mimi.
Mhe. Lissu : Baada ya kuwa umeletewa memory card na maelezo ya P ulisema umefahamu kuwa ile video ilikuwa picha halisi?
George: Yes ni kweli nilisema hivyo.
Mhe. Lissu : Je wakati unafikia hiyo conclusion je ulikuwa umeshapata taarifa ya kitaalamu ya Kaaya ambae ni mtaalamu wa forensic?
George: Nilikuwa sijapata hiyo taarifa kabisa.
Mhe. Lissu : Waeleze majaji kulikuwa na sababu gani ya wewe ulishajua hiyo video ya kweli kwanini ulimpa Kaaya aende akachunguze hiyo video wakati ulishajua ni halisia?
Grorge: Sababu ya meta data lakini kuona kwa macho huwezi kugundua kama video ni halisi. π
Mhe. Lissu : Umeiwasilisha hiyo video hapa mahakamani?
George: Sijaiwasilisha mimi kiukweli, niliiona ile siku.
Mhe. Lissu : Kwahiyo kama uliona wewe na majaji wameshaona?
George: Watakuja kuiona huko mbele.
Mhe. Lissu : Je wewe sasa umeleta?
George: Sijaleta.
Mhe. Lissu : Je umesoma report ya hiyo video kutoka kwa mtaalamu?
Grorge: Mimi sikuisoma.
Mhe. Lissu : Je maelezo ya Kaaya ulisoma?
George: Nilisoma ndio.
Mhe. Lissu : Je Inspector Kaaya alisema kwamba walioingiza mtandaoni ni P?
George: Si kweli hakusema hivyo.
Mhe. Lissu anasema ngoja twende kwenye statement yako hapa.
Naomba nimsomee yafuatayo kutoka kwenye maelezo yako wewe mwenyewe. "Mnamo tarehe 06 nilimtafuta kiongozi wa Jambo nikimtaka anipatie picha halisi aliniambia muhusika na kifaa viko Dodoma" haya ni yako?
George: Yes niliandika mimi hapo.
Mhe. Lissu : Haya twendeleee kama unayatambua.
Mhe. Lissu : βbaada ya kuletwa memory card na maelezo ya shahidi kwamba nj yeye aliyerekodi na kuchapisha mtandaoni nilijiridhisha ni video halisi" haya maneno ni ya kwako au sio ya kwako?
George: Ni ya kwangu kabisa.
Mhe. Lissu : Haya ni maneno uliyoandika tar. 08/04/2025 ?
George: Ni kweli kabisa.
Mhe. Lissu : Sasa tuzungumze kuhusiana na Uhaini.
Ulisema kwamba nilielekeza uchunguzi wa uhaini kwasababu Lissu alisema atahamasisha uasi?
George: Ni kweli kabisa.
Mhe. Lissu : Mheshimiwa nimekosea we sio mheshimiwa sasa kuna mahali kokote umetafsiri neno uasi?
George : Kuzuia uchaguzi, vitisho kwa serikali basi sikusema neno moja moja. kwahiyo sikutoa tafsiri ya neno uasi.
Mhe. Lissu : Je katika hati ya mashitaka ninayoshtakiwa nayo kuna ufafanuzi wa neno tutahamasisha uasi?
George: Huo ufafanuzi upo.
Mhe. Lissu : Sasa tuambie upo wapi? Hapo kwenye hati ya mashitaka? Nakusomea hati ya mashitaka ilivyosema? Neno uasi limetajwa mara mbili. Je kuna mahali kokote imeandikwa?
George: Uasi ilitafsiriwa.
Mhe. Lissu : Una akili timamu wewe afisa wa polisi?
George: Nina akili timamu ndio maana ni afisa wa Polisi.
Mhe. Lissu : unaweza kuwa afisa wa polisi nchi hii na ukawa huna akili timamu.
Part 67 itaendelea kwenye post inayofuata
Naomba repost yako kwenye tweet hii.
Leo ni Tarehe 07/10/2025 Mahakamu Kuu, Dar es salaam kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema taifa inaendelea.
Tayari Mawakili wa Serikali wamefika,
Viongozi wa Chama na wanachama wapo.
Zoezi tunalolisubiri leo kufanyika ni maswali ya Dodoso kwa PW1 (Shahidi Na. 1 wa Jamhuri ambae ni ACP George Wilbard Bagyemu) Kwahiyo utaratibu nitakaoutumia kuandika swali na jibu.
Ni jukumu lenu kujua maswali yataulizwa na Mh. Tundu Lissu na atakaejibu ni huyo Msaidizi wa Mafwele niliyemtaja hapo juu.
Hakikisha umekunywa chai, hakika simu iko full charged bila kusahau bundle la kutosha
Jana tulishuhudi kituko cha Wakili wa Serikali Thawabu Issa akirusha ngumi.
Jambo lile lingefanywa na Mawakili wa Lissu lingekuwa ni story kubwa sana na pengine wangefutiwa uwakili kabisa.
Mahakama inakaribia kuanza muda huu.
Naona tayari Mhe. Lissu ameshaletwa.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Leo Oktoba 7, 2025
Jana tuliishia part 53 so leo tunaendelea na
Part 54
Imepigwa High Courrrrrttttttttttt ni sauti ya Askari inatoka kizembe kabisa.
Watu wote wanasimama kwa utii mkubwa sana.
Majaji wanaingia na kutoa heshima ya kuinama mahakama yote inafanya bowing.
Mh. Lissu ameingia anawaambia watu changanyachanganya ile style ya kukunja ngumi na kuizungusha.
Muda huu anatoa makabrasha yake ni mengi sana.
Anayafungua fungua kwa vibe.
Shahidi hajaingia bado Mahakamani.
Namuona anaingia amevaa kaunda na kanyoa kipara.
Huyu Afande George ni mfupi wa kimo.
Leo amepanda kizimbani anacheka cheka.
Majaji wanaandika hapa.
Kesi haijaanza.
Kimya kidogo kimetanda hakuna kinachoendelea kama dakika 5 hivi.
Anasimama karani Criminal session No. 19605/2025.
Anasimama Renatus Mkude, Wakili Mkuu wa serikali, Johari, Katuga, Mrema, Cathbert Mbiringe na Winniwa Kasawa.
Amemaliza kuwatambulisha mawakili wake.
Mhe. Lissu anaulizwa kama yuko tayari.
Nasikitika kusema Dr. Stephen amezuiliwa kuja mahakamani na amezuiliwa na afisa wa uhamiaji.
Idara ya Uhamiaji wanazuiaje mtu kuingia mtu mahakamani.?
Lakini pia mgeni aliyeingia ndani ya nchi na ana Visa hawezi kukatazwa kuingia mahakamani.
Sasa hawa Uhamiaji wanahusika nini na hawa watu wanaozuia watu kuja mahakamani.?
Mimi jukumu langu ni kusema tu hata ikija kutokea mkaamua kunipeleka kokote mtakapoamua baada ya uamuzi wetu nitaenda huko nikiwa na amani (happily) lakini siwezi kunyamaza.
Niko tayari kuendelea.
Majaji wanaandika hapa.
Majaji wameteta kidogo hapa. Kuhusu swala alilolizungumza Mh. Lissu.
Jaji anawasha kipaza sauti muda huu, tumekusikia mshitakiwa tutafuatilia na tutawasiliana na Msajili.
Mhe. Lissu anadakia kuwa huyo yupo na hataondoka nimemwambia asiondoke kabisa.
Jaji anasema ni sawa.
Jaji anamkumbusha shahidi kuwa yuko chini ya kiapo. Lissu anaanza.
Mhe. Lissu . Jina lako ni George
George : ni jina langu.
Sasa nakuuliza maswali nataka ndio au hapana.
Nikisema toa maelezo toa.
Sitaki rongorongo.
George : sawa.
Mhe Lissu. Wambie majaji kama uliandika maelezo huko nyuma.
George . Ndio niliandika.
Mhe Lissu : ni kweli au si kweli uliandika maelezo mara mbili. Tar. 08 na 10 April 2025.
George : Niliandika mara moja aaaaaa ni kweli niliandika mara mbili.π
Mhe. Lissu : waeleze kama ukionyeshwe hayo maelezo yako utayatambua?
George :Nikionyeshwa nitayatambua.
Mhe. Lissu : Na mimi ninayo. Sasa niliyo nayo ni copy. Waheshimiwa majaji naomba shahidi aonyeshwe maelezo ya maandishi ya mkono wake nisitumie haya copy ya kwangu.
Mawakili wa Serikali: wanatafuta hayo maelezo, wanafungua makabrasha yao hapa.
Part 55 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba repost yako kwenye tweet hii
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 55
Anaendelea Mhe. Lissu
Mhe Lissu : umeyapata eee?
George : nimeyapata.
Mhe Lissu. Sasa waeleze majaji hivyo ni vitu gani? anza na ya kwanza tafadhali.
George : Ya kwanza ni karatasi ya maelezo yak wangu SSP George.
Mhe. Lissu . Hati ya maelezo yako? Sahihi ni yangu.
George : ya pili pia ni maelezo yangu ya Nyongeza ya tarehe 10.
Mhe.Lissu : je hayo maelezo yana sahihi na wamabie ni za kwako?
George : ni za kwangu sahihi zote.
Mhe. Lissu : Wambie majaji kama ni za kwako kama uko tayari ziingie kama ushahidi wa vielelezo vya utetezi?
George : Hii ya kwanza niliandika
Mhe.Lissu : umeelewa swali langu kweli?
George : niko tayari ziingie mahakamani kama sehemu ya ushahidi.
Mhe. Lissu : Waheshimiwa Majaji naomba hizo nyaraka ziingie kama kielelezo E01.
Anasimama Wakili wa Serikali: Renatus Mkude sijui anataka kusema nini.
Anasema Wah. Majaji naomba Igans semboka aseme. Anasimama Ignas hapa. Waheshimiwa Majaji sisi upande wa Jamhuri mshitakiwa hajazingatia taratibu kwasababu misingi ya kisheria ya maelezo ya shahidi ni kwa ajili ya impeachment purpose na waheshimiwa majaji utaratibu wa kuzingatiwa wa namna ya kuwasilisha maelezo umefafanuliwa na maamuzi lukuki wa mahakama ya rufani ni kifungu cha 154 ambacho kwa sasa ni kifungu cha 163 kwenye R.E 2023. Kinasomwa kwa pamoja na 164 na 173 vya EVIDENCE ACT.
Kimsingi katika vifungu hivi anaweza kuempeach kwa kumuonesha maelezo yake na akitaka kumuonesha lazima afuate utaratibu.
Naomba niwarejeshe katika mashauri matatu.
Shadrack Sospter Mkaruka Mangangari vs Jamhuri Rufaa No. 233/2022 Tanzlii 14/03/2025.
Lilian Jesus vs Jamhuri shauri la rufaa no. 151/2018 Mahakama ya Rufaa.
Shauri la Mahakama ya rufaa ambalo la Ruchere Mwita vs Jamhuri shauri la rufaa no. 348/2013.
Waheshimiwa Majaji mashauri haya yote yalieleza utaratibu wa kuzingatia na naomba ninukuu.
Mhe. Lissu: wanaaongea hizo kesi hawanipatii, wanasema ziko tanzlii mfungwa anafikaje huko.
Jaji: mpatieni tafadhali.
Kumbe hawana. Wameambiwa wakatafute.
Sasa anaendelea.
Mh. Jaji kwenye kesi zote tatu Mahakama ya rufaa ilisema
Jaji huwezi kusema kesi zote tatu, tuambie unasoma kesi gani muda huu.
Wakili: samahani Jaji ni ukurasa wa 26 kesi ya Jesus hii Mahakama ilisema kuhusu hatua za ku impeach shahidi.
Shauri la Jamhuri vs Mnawara hamis Nyanda na wenzake 9 la mwaka 2022. Tanzlii. Jaji Manyanda alisema zipo taratibu 8 za kuzingatia maamuzi ya maelekezo ya mahakama ya rufani.
Hivyo Mh. Jaji tunaona mshitakiwa hajazingatia vigezo.
Anasimama Ajuaye Wakili wa Serikali, Waheshimiwa Majaji lengo la kutumia maelezo ni msimamo wa sheria kwamba yanatumika kwa impeachment peke yake.
Test credibility ya shahidi na yale aliyoyaandika kabla ya kuja mahakamani na ndio maana S.
163 Cap.6 R.E 2023 anakisoma na kukifafanua anavyojua yeye.
Kwahiyo tunaona procedure hazijafuatwa na ombi lake lisikubaliwe.
Anasimama Katuga anasema Waheshimiwa Majaji naunga mkono kilichosemwa na mawakili wenzangu ni msimamo wa sheria kwamba kielelezo kabla hakijapokelewa ni msimamo wa sheria lazima kifuate utaratibu wa kisheria.
Kesi ya Mwanjilisi and 3 others Criminal Appeal no. 154/1994 imesema pia kuhusu utaratibu.
Kifungu cha 163 Cap. 6 kinatoa njia mbili. Kwa kumuonyesha au kutokumuonyesha.
Mashauri waliyosema wenzangu ndio sasa yanaelezea taratibu za kufuatwa.
Naomba maelezo hayo yasipokelewe.
Part 56 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba repost yako kwenye tweet hii
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 56
Wamemaliza amesimama Lissu kujibu hilo pingamizi.
Kwa vile ni sheria.
Shahidi amesema yeye hana shida maelezo ni yake na yapokelewe.
Mawakili wake hawataki kabisa yapokelewe wanasema kama lengo ni kufanya impeachment sasa kama hana lengo hilo wamejuaje mapema hivi kwamba yasipokelewe kabisa.π Ngoja tuone lakini.
Mhe. Lissu anasema Waheshimiwa Majaji nimewasikiliza mawakili wa serikali na jibu langu ni fupi, nakubaliana nao, nakubali kuwa nilikosea kuanzia hatua ya tatu ili nisipoteze muda niko tayari nianze upya kwa utaratibu ambao mahakama ya rufani imemuelekeza.
Anasema siwezi kufanya ilivyo sahihi kwasababu ya Estoppel. Kwasababu I'm estooped.
Kifungu cha 131 cha Evidence Act kinasema ukifanya jambo na upande mwingine ukachukua hatua, Mawakili wa serikali wamepinga wakati nyaraka bado haijapokelewa na mimi nimewakubalia.
Estopel haihusiki hapa hili jambo wao linawaathiri nini kama shahidi ni wakwao na maelezo ni ya kwao.
Hakuna wanachoathirika.
Majaji wanaandika hapa
Anaitwa Katuga kwa ajili ya rejoinder anasema kifungu cha 131 cha Evidence Act kinatuzuia kurudi nyuma anapokuwa amekosea.
Intentionally kinatuzuia, tunamalizia kuwa pingamizi letu liko kishseria na limeletwa kwa ajili ya kulinda integrity.
Lissu anasema hii ya integrity nayo kaitoa wapi? Katuga anasimama anasema basi naomba niitoe.
Watu wanacheka ππππ
Wanaandika majaji kwa muda sasa kama dakika 15 hivi
Wamemaliza na kuanza kujadili kidogo.
Majaji wanasema ni endapo una concede PO mahakama inapaswa kufanya nini?
Mahakama ya rufani imeshatoa maelekezo kwahiyo PO kama itakuwa sustained basi itakuwa sustained na kuidismiss kwasababu upande wa Pili na inareject hiyo nyaraka. Nyaraka haijapokelewa.
Maswali yanaendelea sasa.
Mhe : Elimu yako ulisema jana. Ulisoma kozi ya kwanza Moshi mieizi 6?
George : Ni kweli.
Mhe.Lissu : na baada ya hiyo course ukafuzu na kupata cheti? Jibu: Ni sahihi kabisa.
George : ukaajiliwa kama Polisi Constable?
George : ni sahihi kabisa.
Mhe.Lissu : Baada ya hapo ulienda kusomea Course ya Mkaguzi Msaidizi wa Polisi hapa Dar es Salaam.
George : Ni kweli.
Mhe.Lissu : hayo mafunzo ya mkaguzi msaidizi wa polisi yalichukua miezi mingapi?
George : Miezi 9.
Mhe. Lissu : na baada ya hiyo miezi 9 ulipata cheti?
George: Kweli nilipata cheti.
Mhe. Lissu : Ukapandishwa cheo pia?
George : Kweli nilipandishwa cheo kuwa Assistant Insp. of Police.
Mhe. Lissu : Sasa shahidi baada ya mafunzo hayo ulienda kusoma course ya tatu, Gazette officers course
George : ni sahihi kabisa, nilienda chuo cha Polisi Dar ni kweli.
Mhe. Lissu : na ulisoma kwa miezi 9.
George : kweli kabisa,
Anasema kweli kwa nguvu sana huyu shahidi.π
Mhe. Lissu : Baada ya hapo hujawahi kusoma tena na kupata cheti hadi leo? Kwa mujibu wa ushahidi wako?
George : nimesoma course nyingine ndogondogo.
Mhe. Lissu : Sijakuuliza ndogo ndogo.
George: Nimesoma refresher course kwa mwezi mmoja.
Mhe. Lissu Chuo gani?
George: Mwezi mmoja pale Kidatu. Nikapata cheti.
Mhe. Lissu : na Chuo gani kingine?
George: Mubarak Police Academy kule Egypt miezi miwil kipo Cairo.
Mhe. Lissu : Ukapata shahada gani?
George: Nikapata vyeti viwili pale.
Mhe Lissu: Sasa naomba uwaeleze majaji kama kuna mafunzo mengine uliyohudhuria yaliyokupa kitu kingine zaidi ya Cheti? Nataka kujua mafunzo mengine uliyowahi kupata.
George : nina advance diploma ya uhasibu nilimaliza 2001, Post Graduate Diploma in finance Chuo cha Sauti.
Part 57 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba repost yako kwenye tweet hii
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 57
George: Pia nimesoma masters of Bussiness administration nilimalizia Kisii University nchini Kenya.
Nikasoma Masters of Human Resource Management Chuo Kikuu huria cha Tanzania. Nikapata pia cheti. Na sasa nimeanza PHD.
Mhe. Lissu : ni sahihi nikisema kwamba kwa mujibu wa PGO za 2021 wewe ni Professionally qualified member of the Police Officer?
George: NI SAHIHI KABISA ANAJIBU.
Mhe. Lissu : Unatambulika kama ni professionally officer?
George; Ni sahihi kabisa.
Mhe. Lissu : Sasa naomba waeleze kama maelezo haya ya hiki kisomo umeyaweka kwenye hati yako ya maelezo ya mashahidi?
George: Nimeweka elimu yangu ya Kipolisi tu.
Mhe. Lissu: Naomba nikusomee maelezo yako ya Tar. 08/04 umesema hivi kuhusiana na elimu yako. Mimi mtajwa nimeajiriwa na kufanya kazi mikoa mbalimbali...... Anaendelea hapa.
Anamsomea maelezo yake.
Sasa katika niliyosoma kama kuna chochote kinahusiana na vyuo vya Polisi ulivyotaja jana?
George : hakuna kabisa hayo mambo niliyosema jana kuhusu vyuo vya Kipolisi na vyeti nilivyopata.
Mhe. Lissu : ieleze mahakama kama mafunzo yako mengine nje ya upolisi hayo madiploma ya uhasibu na mengine ya sauti kama yapo kwenye hati yako ya maelezo wambie kama yapo?
George : kwenye hiyo hati haipo ila jana nikiwa naulizwa nilisema.
Mhe. Lissu ; Ulitaja au hukutaja jana?
George: Sikutaja haikuwa na umuhimu na jana sikuulizwa ndio maana sikutaja.
Mhe.Lissu : na hizo masters hukutaja pia?
George: Ndio sikutaja kwasababu sikuulizwa ila leo umeniuliza ndio maana nimetaja.
Mhe. Lissu : twende kwenye ushahidi wako wa siku ya tar. 04/04/2025 uliiambia mahakama kwamba uliletewa taarifa za video clip yenye uhaini na ASP John Kaaya.
George : Ni kweli.
Mhe. Lissu : Ulisema pia ASP John kaaya alikwambia aliona video clip kwenye mtandao wa YouTube wa Jambo TV yenye kichwa cha habari uso kwa uso na watanzani ni sahihi?
George : ni kweli heading ilikuwa inasomeka hivyo.
Mhe. Lissu : Sasa wambie majaji kama maneno yako hayo yapo kwenye maelezo yako ya mashahidi?
Mhe. Lissu : Hayo maneno hayapo kwenye maelezo yangu.
Mhe. Lissu : ulisema kwamba baada ya kuambiwa hivyo ulimwambia ASP John Kaaya. Akuonyeshe hiyo video clip?
George: Ni kweli ilikuwa hivyo.
Mhe. Lissu : pia jana ulisema kwamba ASP kaaya alikuonyesha sehemu sehemu?
George: Ni kweli alifanya hivyo kwa siku ya tar. 04.
Mhe. Lissu : Waeleze kama haya maneno ya alikuonyesha sehemu sehemu hakukuonyesha yote kama yapo kwenye hati yako ya maelezo.
Yapo au hayapo?
George : Sidhani kama ipo nadhani haitakuwepo. Haipo sawa.
Mhe. Lissu anamsomea na kumuuliza ni kweli au sio kweli.
George : uwa ni kweli.
Mhe. Lissu : Mtu anayetoa maudhui ya uchochezi ni kosa la uhaini. Kweli au si kweli?
George : naomba nitoe maelezo.
Mhe.Lissu : Sitaki maelezo we jibu maudhui ni kosa la uhaini au sio kosa la uhaini.
George : ni kweli ni kosa la uhaini.
Mhe. Lissu : sasa jana ulitaja kifungu cha uhaini ni 39?
George: Ni kweli we anza kusoma kwenye execution..
Mhe. Liissu : unasema??????
George: Samahani ni EXECUTIVE.
Mhe. Lissu ningeshangaa na kisomo chako chote usijue kingereza?
George: Nimekosea hapo.
Anamsomea hicho kifungu cha 39(d).
Mhe. Lissu : Je video uliyoisoma hayo maudhui ya uchochezi yanaingia kwenye 39(2)d?
George: Ndio yanaingia.
George: Naona kama vingine unaruka kwenye hicho kifungu.
Mhe. Lissu : twende taratibu tutamaliza vyote.
Mhe. Lissu : naomba nikusomee maneno nikiyoshitakiwa nayo. Maneno ya uhaini yanasema hivi WANASEMA KITU KIMOJA HAPA WANASEMA HIVI MSIMAMO HUU UNAASHIRIA UASI NI KWELI NI KWELI KWASABBAU TUNASEMA TUNAENDA KUZUIA UCHAGUZI NA TUTAUVURUGA NA TUTAENDA KUKINUKISHA.
Swali langu Je haya niliyosoma yapo kwenye hati ya mashitaka?
George: Hayo uliyosoma hayapo.
Part 58 itaendele kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako kwenye tweet hii.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 58
Mhe. Lissu : ukaelezea sababu za kumwambia kufungua jalada kwamba ulitaka kujua kama ni halisi au laa?
George: Ni kweli kabisa ilikuwa hivyo.
Mhe. Lissu : hayo maelekezo kwa Michael Gyumi ulitoa tarehe ngapi?
George: Ilikuwa Tar. 04/04/2025.
Mhe. Lissu : waeleze majaji kama hayo maneno kwamba ulimuelekeza Michael Gyumi afungue hilo jalada tar. 04/04.
George : yapo hayo maelezo.
Mhe. Lissu amempa maelezo asome ili kuonesha hayo maelezo. Anayasoma hapa.
Mhe. Lissu: Tafuta sehemu ambayo tar. 04 ulimuelekeza Michael Gyumi afungue hilo jalada. Naona unasoma tu hueleweki hata unasoma nini?
Shahidi anatafuta hapa.
Kimya kidogo.
George: Niliamuru jalada kufunguliwa ila Jina la Insp. Gyumi halipo kiukweli.
Mhe. Lissu : Je nilitaka kujua kama hiyo video halisi au laa?
George: Hayo maneno hayapo kwenye maelezo yangu
Mhe. Lissu : wakati unaangalia sehemu sehemu za video clip ulisema ulikuwa na police notebook na kuandika aliyokuwa anakwambia Kaaya.
George: Ni sahihi kabisa.
Mhe. Lissu : Je hayo maneno kwamba ulikuwa na Police notebook yapo kwenye maelezo yako au hayapo?
George : maneno hayo hayapo kabisa, ningeandika kurasa 200.
Mhe. Lissu: Kweli au si kweli kwamba ASP Gyumi linajitokeza Tar. 08/04 kwa mara ya kwanza?
Anamsomea alichoandika tarehe 08.
George : si kweli alishaonekana nilitaja timu mimi.
Mhe. Lissu : wambie majaji kama umewahi kutaja majina ya hiyo team yako?
George: Hiyo timu sikuwahi kutaja kabisa.
Mhe Lissu : Je ASP Kaaya alikuwa ni mmoja wa hiyo timu?
George : Yeye hakuwepo kwenye hiyo timu alikuwa anapeleleza kivyake.
Mhe. Lissu : Je Andrew Churu alikuwepo au hakuwepo?
George: Huyo nae hakuwepo.
Mhe. Lissu : Je ASP malugala nae alikuwepo kwenye timu uliyounda wewe?
George: Hakuwepo pia.
Mhe. Lissu : Je Elibariki Kaaya?
George: Hakuwepo.
Mhe. Lissu : Katika hati yako ya ushahidi kuna jina la Polisi yeyote ambae uliyeunda wewe lipo kwenye orodha ya hiyo timu yako.?
George : kuna timu mbili hapo,
Alikuwepo ASP Michael Gyumi, ASP Ibrahim, Senior Superitendent Reuben Mwakabonga, ASP Nunu, Detective Koplo Ibrahim, Mimi Mwenyewe, Detective Copro Ramadhani.
Mhe. Lissu : wote uliowataja na hao wengine saba kuna mahali umewataja kama timu ya upelelezi?
George : Kwenye maelezo yangu sijawataja.
Nafikiri hawa ndio wasiojulikana leo tumetajiwa pia.ππππ
Mhe. Lissu : Tar. 07/04/2025 ulisema majira ya mchana nilimuelekeza kupakua na kuitunza kwenye flash disk?
George: Ni kweli kabisa nilimwambia hivyo.
Mhe.Lissu : Naomba uwasomee Majaji maneno yanayoanzia siku ya tar. 07/04/2025 mpaka yanapoanza tarehe 08/04/2025.
Kwenye hayo maelezo hakuna mahali kokote kuwa ulimuagiza apakue hiyo clip, ni kweli au si kweli.
George : hayo yapo.
Mhe. Lissu: haya soma tuone.
George anasoma hapa ila Sauti imekauka anatetemeka.πKumbe na wao kuna mahali huwa wanakuwa wadogo.
Mhe. Lissu : Sasa yote uliyosoma kuna mahali nilimuelekeza Kaaya kuipakua.
George : Kwa haya niliyosoma sasa hivi hayupo huyo mtu anayeitwa Kaaya.
Mhe. Lissu : umemtaja hapa DCP Ramadhani Ng'anzi?
George: Ni kweli nilimtaja
Mhe. Lissu : Na kwenye ushahidi wako jana ulisema kwamba baada ya kufungua jalada ulimpigia DCI Ramadhani Kingai?
George: Ni kweli anaitwa Kingai.
Mhe. Lissu : na ulisema ulimpa taarifa kuhusu jalada hilo la uchunguzi?
George: Ni kweli nilifanya hivyo.
Mhe. Lissu : na alikwambia mawasiliano nae uwe unapitia kwa Ramadhani Ng'anzi ndo alivyokwambia Kingai?
George : ni kweli aliniambia hivyo kwenye jalada hili.
Mhe. Lissu : hata mimi nakuuliza kuhusu jalada hili.
Mhe. Lissu : je unafahamu kuhusu Chain of command?
George: Nafahamu vizuri.
Mhe. Lissu : ni kweli au sio kweli Boss wako ni ZCO wewe kama Deputy wake?
George : Ni kweli.
Mhe. Lissu : ZCO Boss wake ni ZPC?
George: Yes ni kweli Boss wake ni ZPC.
Mhe. Lissu : Nataka unisomee 6(16) PGO.
Part 59 inaendelea post inayofuata,
Naomba Repost yako kwenye tweet hii.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 44
Jaji Nduguru anamuuliza
Mshitakiwa unasemaje?
Mhe. Lissu anasema Waheshimiwa Majaji baada ya kusikia orodha ya mashahidi na vielelezo naomba kusema yafuatayo.
Nina mambo mawili yakusema.
Ninalo lakwanza na la pili ni maelekezo ya Mahakama.
1. Lengo la PH ni kuokoa muda ili tusibishane kwa mambo yasiyo ya maana.
Kifungu cha 198 kinazungumzia mambo ya nyaraka hapa.
Hizo nyaraka zao zote mimi sina ugomvi nazo nazikubali wasije kutuletea hapa wakaja kutupotezea muda.
Mimi navikubali vyote. Hizo nyaraka.
Sihitaji watu wa kuja kunipotezea muda hapa.
Lingine la pili ni kuhusu mashahidi wangu naomba na mimi niwaseme mashahidi wangu.
Wafuatao.
1. Samia Suluhu Hassani anuani yake ni Ikulu ya magogoni na nyingine ikulu ya ugogoni yaani Chamwino.
Kama hatapatikana hapa Dar nendeni Ikulu ya Chamwino.
2. Philip Isdory Mpango huyu anapatikana Ofisi ya MAkamu wa Rais mji wa Serikali mtumba Dodoma.
3. Kassim Majaliwa Majaliwa huyu anapatikana Ofisi ya Waziri Mkuu Dodoma.
4. IGP, Camilius Wambora Makao Makuu ya Polisi Dodoma.
5. Kamishina wa Polisi Ramadhani kingai huyu anapatikana ofisi ya Makao Makuu ya Polisi Dodoma.
6. Mkurugenzi Mkuu wa Usalama wa Taifa na Ujasusi simfahamu jina nataka aje atoe ushahidi.
Anapatikana Makao Makuu ya usalama wa Taifa.
7. Ramadhani Ng'anzi
8. Agatha Atuhaire yupo Kampala Uganda. Huyu ndio yule aliyetekwa nyara na kutupwa.
9. Boniface Mwangi yuko Nairobi Kenya nayeye alitekwa Nyara na kuteswa kwenda kutupwa mpakani horohoro.
10. John Marwa Mkurugenzi wa Jambo TV.
11. Amani Sam Gorugwa, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema.
Huyu ndio anajua mkutano uliitishwaje?
12. John Wegesa Heche, Makamu Mwenyekiti wa Chama huyu anajua nilikuwa wapi toka tarehe 03 hadi tarehe
09 nakamatwa.
13. John John Mnyika ni Katibu Mkuu ndio namuita kama shahidi wangu wa mwisho.
14. Dr. Willy Munyoki Mutunga anapatikana Nairobi Kenya.
15. Martha Wangari Karua anapatikana Nairobi Kenya.
Pia Waheshimiwa Majaji naomba ku reserve right yangu ya kuita mashahidi wa ziada kama itahitajika.
Anasimama Katuga sasa.
Waheshimiwa Majaji tuko aware na kif. Cha 198 cha CPA kuwa PH ikikamilika kusikilizwa kuanze haraka
Hatukuwa na summons za kuita mashahid na hatuna mashahidi kwa sasa so kwa kusema hayo kifungu hicho kinaipa mamlaka mahakama kuahirisha shauri hili.
Kwasababu hizo tunaomba shauri liahirishwe kupangiwa kuanza kusikilizwa.
Majaji wananong'ona.
Anamuita Lissu.
Lissu anasema Wakili wa Serikali amesema vizuri kuwa kesi inapaswa kuanza kuitwa mara moja kwa kifungu cha 198 cha CPA.
Na kwa vile hawajasema watakuwa tayari lini? Sasa naomba niseme mashahidi 11 kati ya 30 wako Dar es salaam wengine ndo wako mikoani.
Sasa mimi nafikiri hawa ambao wako Dar es salaam na wanafikika muda mfupi waitwe na hao watatu wapo humu ndani. Akina George, Kaaya na wenzake.
Anasimama Katuga anasema ametuita wenzake wakati yeye alikataaa.
Jaji anasema lakini aliyekataa ni yeye na sio wewe sasa why unakataa muda huu?
Watu wanachekaπ
Anaendelea Mh. Lissu
Anasema naomba sasa shauri liendelee. Mimi niko tayari na kama sio leo basi kesho, mimi sikai Shelaton Hotel niko Magereza nakaaa na watu wa kunyongwa kule, waitwe hawa mashahidi
Jaji anawaita Jamhuri kama wana cha kurejoin?
Katuga anasema tunaomba kurudia tuliitwa kwaajili ya PH hatukujiandaa
na mashahidi. Jaji anasema wewe ulisema unaomba muda gani sasa? Anajibu muda ambao msajili ataona inafaaa.
Watu wamesonya sana.
Anamalizia kuwa muda ambao mahakama itaona unafaaa.
Jaji: anaandika na kujadili na mwenzake.
Mahakama imesikiliza kuhusu hoja zote na shauri litaanza kusikilizwa tarehe 06/10/2025.
Watu wamembishia Jaji kuwa aaa! Jaji anajitetea kuwa shauri hili litaanza tarehe 06 na litasikilizwa mfululizo. Saa tatu asubuhi. Minong'ono ni mikubwa sana.
Jaji anaomba watu wasipige kelele, anasema sisi tumemaliza.
High courtttttt
Watu wote wamesimama.
Tunatoka
Naomba repost yako
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 43
Anasimama mdada mmoja pembeni ya karani ana mwili kidogo na mweusi wa rangi anapanda kule juu kwa jaji na kuzungumza nae.
Huyu naambiwa ni Msaidizi wa Jaji kwa mujibu wa utaratibu hawa wasaidizi wa Majaji ni MAHAKIMU WAKAZI.
Anayemsaidia Jaji kazi zake ni Hakimu Mkazi anaweza kufanya kazi pale Kisutu au mahakama nyingine yoyote ya Wilaya.
Kazi yake akiwa msaidizi wa Jaji naambiwa ni kumsaidia Jaji kufanya tafiti za kisheria kama vile kupata authorities yaani kesi za kisheria.
Wamemaliza kuongea ni kama ametoka na Flash pale juu.
Nadhani ameenda sasa kutoa ile nakala ambayo itahitajika kusainiwa na Mhe. LISSU kuhusu mambo aliyoyakataa.
Wale Majaji wawili bado wanaendelea kuzungumza kama kawaida yao.
Huyu mwingine yeye ni mikausho mikali, hana habari.π
Mh. Lissu nae anatumia muda huu kupiga story za kimya kimya na watu waliopo mahakamani.
Siunajua kama zile story ambazo wanafunzi huwa wanapiga Darasani muda ambao mwalimu yupo Darasani na pengine anaandika ubaoni au anasahihisha madaftari akiwa darasani.
Huwa kuna story zinapigwa kimya kimya sana na kwa utulivu basi ndo kinachoendelea hapa.
Askari Magereza waliojificha sura leo wako wawili tu wengine tunaonana nao uso kwa macho.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Chama yupo Mama yetu Ruth Mollel,
Namuona Brenda Rupia, Mkurugenzi wa Habari na mawasiliano wa Chama.
Sasa yule Madam msaidizi wa Jaji amerudi na makaratasi mkononi na Jaji anayapitia na kuzungumza zae muda huu ni zoezi ambalo limegharimu kama nusu saa hapa kusubiria hizo MEMORUNDUM OF AGREE FACTS kuwa printed na kuletwa Mahakamani kusainiwa.
Naambiwa hapa hizo facts zinasainiwa ili wakati wa kutoa ushahidi zisiwe na haja ya kuthibitishwa na kitakachothibitishwa ni kile ambacho amekikataa.
Yule Msaidizi wa Jaji ambae nimewaambia kuwa ni Hakimu Mkazi kwa cheo anazungumza na majaji kwa sasa takribani dakika ya 6 wanajadili pale mbele.
Kwa mbali kule mbele namuona Boniface Jacob anateta jambo na Makamu Mwenyekiti.
Ni kama kuna story anampigia hivi maana Boni Yai kwa story hajambo hata humu huwa anatupigia story zake muda mwingine huwa haziishi.π
Mahakama imesimama kusubiri hiyo michakato ya ku print hiyo nyaraka ya kusainiwa.
Ni mchakato ambao umechukua muda mrefu sana.
Bado zoezi limekuwa gumu kukamilika. Amerudi huyu Msaidizi wa Jaji na makaratasi tena. Wanayaangalia ila mara hii amerudi kwenye kiti chake amewaachia Majaji hayo makaratasi.
Jaji anamuita sasa Karani wake anateta nae jambo muda huu.
Anampatia nyaraka kadhaa naona Wanazungumza pale mbele.
Jaji anasema naomba sasa tuendelee.
Karani anashuka kutoka kule juu anampelekea Mh. Lissu hayo makaratasi kwa ajili ya kusign.
Mhe. Lissu anayachukua na kusoma kwa umakini mkubwa hapa.
Anatafuta kalamu yake na wanaelekezana asaini wapi? Anafungua ile karatasi na amemaliza kuisaini.
Karani anazunguka upande pia wa Mawakili wa Serikali na anawapatia pia na wao makaratasi hayo wasaini.
Zoezi hilo limekamilika na makaratasi yanarudishwa kule mbele kwa Jaji.
Jaji Ndunguru anapokea na kuyaangalia kama yako sawa.
Anawaita Upande wa Mashitaka.
Waheshimiwa Majaji tutakuwa na mashahidi wafuatao.
1. George Kagemu
2. PF 22863 ASP John
3. PF 20.. Andrew Churu.
4. ASP Samwel Kaaya
5. P
6. P1
7. P2 anazosoma hizo pia hadi 16
Anawasoma akina Masaranga, Michael, Maugala, Lugano Gwasa, Geoffrey Lutufye, ASP Amin Mahamba, Michael Gyumi, Peter Mwitwa, Boni Mgogo na Asia Abdalah Mohamed.
Hao ni mashahidi 30.
Anasoma vielelezo sasa. Forensic Report, PF145, PF 145 nyingine anasoma hapa hivyo vielelezo yakiwemo maelezo ya onyo ya Tundu Lissu, Video Clip iliyopo kwenye flash disk anasoma vielelezo vyote hapa.
Anayefanya kazi hii ni Thawabu Issa, Wakili wa Serikali.
Amemaliza kusema Wakili wa Serikali amekaa chini.
Part 44 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako