Taifa na bara la Africa ili liweze endelea lazima watu wake wabadili mtazamo wa maana ya mafanikio.
Raia zinaamini mafanikio ni kua na pesa nyingi hata kama ni kwa kukandamiza haki, kuminya na kuiba au kudhulumu stahiki za wengne.
Hawa wanawake wa siku hizi walioiva kupitiliza na mpaka kuungua jikoni wengine ni shida.
Bora upate ambayo haijaiva unaweza irudisha jikoni ukaiivisha vizuri.
#ndoachangamoto
Wao sio tu wanajeuri ya kufanya na kuonyesha ubaya wao ila ni sababu wana nyumbu wanaowakingia kifua kwa nderemo wakajiona ni makatili.
Ila mtu anajifanya mbaya ukimbananisha vizuri mbona atatoa milio kama yote.
Kwenye maisha ni kutegemea ulichonacho upate ambacho huna.
Maisha jinsi yalivyo na ukweli wake.
Unaweza kua bora na mbobezi wa mambo na bad siku moja ukafa na mishe zikaendelea kama kawaida tu na ukasahaulika.
Ardhi imekula wengi sana waliojiona miamba, hawagusiki, hawatakufa, na hakuna kama wao.
Ishi vyema na tenda mema.
Tumekubaliana kua waamuzi wetu wenye nembo za fifa hawana uwezo kuchezesha mpira wa miguu wetu.
Taifa lenye watu millioni 60 na ushee. Ni aibu sana.
Ndio maana hata kusimamia maswala mengine ya maendelelo, haki ba usawa tumeshindwa.
Hili swala la kuwapeleka watoto shule mpaka Jumamosi, Je?
Ni kwamba tunaamini mafanikio na njia zake katika maisha ya watoto/vijana wetu waalimu wanazijua?
Na wakati huo hakuna mwalimu tajiri. Na angekuwepo asingekua kaajiriwa.
Elimu inaweza kuharibu fikra.
Kunyamaza haimaanishi kuwa wewe ni dhaifu. Inamaanisha una ujasiri na umakini. Watu wanyenyekevu hupata heshima zaidi kuliko wale wanaojaribu kujithibitisha.
Kwa hivyo, kadri thamani yako inavyoongezeka, kaa rahisi, kaa kimya, na kaa mnyenyekevu.
#kimyakimya#mafanikio
Sarafu hutoa kelele nyingi, lakini pesa za karatasi hubaki kimya. Vivyo hivyo, watu wasio na thamani kubwa mara nyingi huzungumza sana ili kujionyesha, huku watu wenye thamani ya kweli wakibaki watulivu na wanyenyekevu.
Unapokua, kufikia mafanikio, au kupata maarifa, hakuna haja ya kujionyesha au kuzungumza kwa sauti kubwa kuhusu hilo. Kazi yako na matokeo yako yatazungumza kwa niaba yako.
Hua nikiingia X online nafata habari za maana zenye tija. Nikiona zile posts za connection hua najua mtego.
Kwanza naasess situation kisha nachukua maamuzi ya "not interested in this posts" tu.
Agenda muhimu acha niendelee fatilia sio kutoka kwenye reli kizembe.
No porn video
Hawa wanawake wa mjini na wa siku hizi kwa kupenda sherehe na bata, sasa ndio nini kuja na mtoto mchanga kwenye sherehe ya harusi na kunyonyesha.
Na mwanaume yupo naye anang'aa macho tu.
Tatizo hili.
Askofu Musomba Akemea Uchawa, Asisitiza Ukweli—Azungumzia Watu Kushangilia Vifo: 'Tumepotea Sehemu'
Akizungumza katika katika Ibada ya Ijumaa Kuu iliyofanyika leo Aprili 03, 2026, katika Parokia ya Bikira Maria wa Mlima Karmeli Bunju, Askofu Stephano Musomba wa Jimbo Katoliki la Bagamoyo, ametahadharisha juu ya uelekeo wa jamii ya Tanzania akigusia mambo kama uchawa, utengano na dhuluma katika jamii.
"Mila zetu za kiafrika si kawaida mtu anakufa leo unashangilia, si kawaida," Musomba ameeleza akizungumzia matukio ya hivi karibuni
"Tukae chini tujadili pamoja tumekosea wapi,tuelimishane tueleweshane. Pengine anashangilia kwa sababu hakuna anayeniangalia, pengine haki yangu haijatendeka, ndio maana anashangilia. Kwahiyo tuangalie nini chanzo kinachotufanya tuwe tulivyo kwa nini tumefika katika hali hiyo," amesesisitiza Musomba.
Askofu Musomba pia amekemea utengano wa kisiasa, ambapo ameonesha kushangazwa na watu wanaotenga binadamu wenzao kwa sababu ya tofauti ya vyama vya siasa.
"Tulitendee haki taifa letu, tulikotoka na tunakoelekea siyo kuzuri.Tulikotoka kuzuri sana lakini tumepotea sehemu," alionya Askofu Musomba.
Katika mahubiri hayo ambayo amesisitiza suala la ukweli, Askofu Musomba amechambua pia nadharia ya viongozi wa dini kuambiwa wanaingilia siasa, ambapo ameeleza siasa haifuti uumini wa mtu katika dini, na viongozi wa dini wana nafasi ya kuonya. Musomba ametumia muda katika mahubiri yake kukemea kasumba ya uchawa katika jamii
“Sasa ukimweka mwanadamu ni Mungu kosa kubwa sana,na ndio maana tunao wajibu kama viongozi wa dini kufufua dhamiri za waumini wetu,” anaeleza zaidi katika mahubiri yake.
“Zamani tulikuwa tunaogopa sana chawa, tena ukionekana we una chawa unakimbiwa usije ukaniambukiza. Lakini saa hizi ukiwa na chawa wewe ndiyo wewe.Mijamaa inakunyonya mpaka unakiona cha moto, wanasema we ni mzuri katika dunia hii kumbe huna lolote.”
“Kumbe huna lolote,kwa sababu hii michawa inanyonya tu uchafu wako. Hakuna uzuri wowote hapo ndiyo maana tunasema ukweli, unaleta maendeleo….na ndio maana tunahitaji watu kusikiliza watu wanapokuambia we umekosea. Usiwashambulie, lakini mwanadamu wa leo ni mgumu sana anapenda kusikia yale anayotaka kusikia."
PWANI: Askofu Stephano Lameck Musomba, OSA, amesema hayo Aprili 3, 2026 katika Ibada ya Ijumaa Kuu iliyofanyika Parokia ya Bunju, Jimbo Katoliki la Bagamoyo.
Zaidi bofya https://t.co/IG9QJ4itJz
#JamiiForums#Siasa