@fbuyobe She is the one of the best actors when it comes to relationships,and life in general,she's always up to something when money signal comes but mostly her hole is open for everyone in need.
@godbless_lema Tumwache huyu,yumo kwenye mfumo ule ule unaotesa na kuharibu maisha ya watu,hafai kuja kwenu zaidi akae huko huko alipo,kama anataka kutubu basi atubu akiwa huko na abadilishe mambo akiwa huko.
Kitendo cha kuja kwenu ni kuwaletea matatizo zaidi huku yeye akipata shida zaidi.
@StateDRL@nulphin Why don't you guys abduct him instead of designating him? It's okay for him not to visit the US. He will continue his brutal actions as long as he's getting help from the top government officials.
You have to do more than that.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mussa Azzan Zungu akiwa na Mchezaji wa zamani wa Timu ya Taifa ya Uingereza na Klabu ya Manchester United, Rio Ferdinand mara baada ya mchezaji huyo kutembelea Bunge hilo kuona linavyofanya kazi leo Mei 20, 2026 Jijini Dodoma.
Natoa pole nyingi sana kwa Msaidizi wa Mheshimiwa Tundu Lissu, Ndugu Jumbe, kufuatia tukio baya na la kinyama lililomtokea. Huu si utamaduni wa Watanzania, wala si maadili yanayopaswa kupewa nafasi katika jamii yetu.
Tofauti za kisiasa zisigeuke sababu ya chuki, vitisho, au mashambulizi dhidi ya watu. Taifa lenye afya ya kisiasa hujengwa juu ya ushindani wa hoja, heshima ya utu wa binadamu, na kulinda haki ya kila mtu kuwa salama bila kujali itikadi yake.
Wananchi, wakati umefika wa sisi sote kupaza sauti na kukemea matukio ya aina hii bila kujali tofauti zetu za kisiasa. Ukimya mbele ya uovu unaweza kuupa nguvu uovu wenyewe.
Namtakia Ndugu Jumbe uponaji wa haraka na nguvu katika kipindi hiki kigumu. Pia naomba vyombo husika vifanye uchunguzi wa haraka, wa haki, na wa uwazi ili wote waliohusika wakamatwe na kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.
@YoungAfricansSC Yafaa mkaze,sio kituletea masihala kwenye machi zilizobaki,mchezaji anakosa goli anakenua meno kwa furaha kama vile ni kawaida tu kucheka cheka huku tunataka matokeo
Ukiachana na huo utani wa “Millennials” na “Gen Z”, kuna eneo moja nakubaliana na Gen Z 100%. Ni ukweli kwamba Millennials tumelifikisha Taifa letu matopeni. Hatuwezi kuiwajibisha Serikali hata inapokosea.
Millennials ndiyo uti wa mgongo wa utumishi wa umma kwa sasa; sisi ndiyo injini ya nchi. Lakini injini hii ikikubali kufanya kazi kwenye matope bila kuhoji kwanini barabara haitengenezwi, nchi inabaki palepale.
Kizazi chetu kwa sehemu kubwa ndiyo watumishi wa umma, hata tusipoongezwa mshahara na marupurupu kwa miaka 10, tunaona ni sawa tu. Tunaona ni kawaida na ndiyo kitu ambacho kama watumishi, tunastahili.
Kizazi cha wasomi wengi kimegeuka kuwa kizazi cha “ndiyo mzee.” Millennials wamekuwa watulizaji (stabilizers) wa mfumo hata kama ni mbovu. Gen Z ni wavurugaji (disruptors) wa mfumo ili ukae sawa.
Hofu ya kupoteza mshahara inayoweza kusababisha watoto wakose ada/familia ikose chakula imewafanya Millennials kuwa waoga (risk-averse). Hii imetengeneza kizazi kinachopendelea diplomasia ya unyenyekevu.
Kwa sababu ya familia, tumekuwa kizazi cha viumbe wabinafsi sana. Hatujui kudai haki zetu, na tumezalisha machawa na wapambe wengi. Kizazi chetu kimeasisi mfumo wa kusifu na kuabudu (sycophancy).
Tazama, hata machawa wakubwa na wazito (pro-max) wanaosifu na kuabudu Serikali hii ni kizazi cha Millennials. Wasanii wakubwa wa muziki wa kizazi kipya ambao ni wafuasi wa watawala ni Millennials.
Gen Z wengi bado hawajazama kwenye majukumu mazito ya kifamilia, hivyo wana ujasiri wa kupaza sauti bila kuwaza “kesho nitalishaje watoto.” Hawalazimiki kuwa machawa ili waweze kuendesha maisha yao.
Gen Z wanakuja na utamaduni tofauti: wako ‘connected’ na wanatumia teknolojia ipasavyo. Wanaona wenzao duniani wanavyowajibisha serikali zao, hawaamini katika uvumilivu wa miaka 10 bila ongezeko la maslahi.
Hawahitaji mikutano ya siri; wanatumia simu kuanzisha mijadala, kuumbua ubadhirifu, na kuungana kwa kasi ya ajabu. Hii imepunguza nguvu ya machawa ambao walizoea kutawala simulizi za mtandaoni. Safi sana.
Wakati Millennials walifundishwa kuwa na shukrani hata kwa kidogo (ile dhana ya bora mkono uende kinywani), Gen Z wanauliza: “Kwanini iwe kidogo wakati rasilimali zipo?” Hapa ndipo sasa nawakubali madogo hawa.
Hawa Gen Z wana uwezo wa kuungana kama kizazi bila kujali itikadi za vyama, kitu ambacho Millennials wengi wameshindwa kwa sababu ya kuweka mbele maslahi ya ajira zao. Wamekataa mambo ya “Status Quo.”
Gen Z wamevunja mwiko. Millennials wamefungwa na nidhamu ya uoga au hofu ya kupoteza walichonacho, sasa wanatazamana na kizazi kinachoongozwa na kanuni moja kuu: “Haki haiombwi, haki inadaiwa.”
Labda shinikizo hili la Gen Z litatumika kama kioo cha kuwafanya Millennials wajione walivyojipoteza. Binafsi, wananikosha sana. Gen Z wanaupiga mwingi. Mimi nawatia moyo, wasiogope. Kaka zao tupo pamoja nao.
Gen Z, take a bow, fellas.
Tanzania haihitaji hofu zaidi.
Inahitaji uponyaji.
Kwa sababu taifa lililojeruhiwa, mwishowe huanza kujijeruhi lenyewe.
Leo tunapaswa kusema ukweli
si kwa chuki,si kwa kisasi,bali kwa hofu ya kweli kuhusu mustakabali wa nchi yetu.
Kama Michael Jackson alivyowahi kusema:
“Tunapaswa kuponya dunia yetu iliyojeruhiwa. Machafuko, kukata tamaa, na uharibifu usio na maana tunaouona leo ni matokeo ya watu kujisikia wametengwa kutoka kwa wenzao na mazingira yao.”
Kauli hii kwa sasa
Inakuwa onyo hata kwetu sisi Watanzania, kama sehemu ya dunia
Wananchi wanapoanza kujisikia:
hawasikilizwi, wametengwa, wananyamazishwa, wanadhalilishwa,
au wanachukuliwa kama maadui kwa sababu tu wana mawazo tofauti.
umbali wa hatari huanza kujengwa kati ya wananchi na dola.
Na historia inatufundisha jambo moja la kuogopesha:
Mataifa mengi hayaanguki kwanza kwa sababu ya adui wa nje.
Huanzia kudhoofika ndani
wakati imani ya wananchi inapokufa.
Nchi haiwezi kujenga amani ya kudumu:
kama hofu inakuwa kubwa kuliko uhuru, kama utii unakuwa muhimu kuliko ukweli, kama taasisi zinaonekana kuwa za upande mmoja, au kama ukosoaji unatafsiriwa kama usaliti.
Kwa sababu jamii iliyojeruhiwa huzalisha wananchi walioumia.
Na wananchi walioumia mwishowe huzalisha:
hasira, mgawanyiko, msimamo mkali, kukata tamaa,au chuki ya kimya kimya.
Viongozi wanapaswa kuelewa:
si kila ukimya ni amani.
Wakati mwingine watu wananyamaza kwa sababu:
wamechoka,wanaogopa,au wamekata tamaa.
Na kukata tamaa ni hatari kwa taifa lolote.
Tanzania ilijengwa juu ya msingi imara ya : utu,umoja,mazungumzo,
uvumilivu,na hisia ya kuwa taifa ni la wote.
Julius Nyerere alielewa jambo kubwa sana,taifa haliishi kwa nguvu pekee (power)
linaishi pia kwa uhalali wa kimaadili.
Wananchi wakianza kuhisi kwamba:
haki inategemea upande wa kisiasa, ambao mtu yupo, taasisi si huru tena,
au demokrasia ipo kwenye maneno lakini si kwenye vitendo,
ule mkataba wa kihisia kati ya taifa na wananchi huanza kupasuka.
Kwa hiyo haya si mashambulizi.
Hili ni onyo.
Onyo kwamba:
siasa zinapokuwa za uhasama kupita kiasi,
mamlaka zinapoanza kuogopa ukosoaji,
wapinzani wanapoonekana maadui,
na wananchi wanapopoteza imani kwa mifumo ya taifa
taifa lenyewe huanza kujeruhiwa kihisia.
Na taifa lililojeruhiwa huwa taifa lisilo tulivu.
Hatuhitaji kulewa kisiasa zaidi.
Tunahitaji hekima.
Hatuhitaji viongozi wanaotaka kusifiwa tu.
Tunahitaji viongozi wenye uwezo wa kusikiliza ukweli usiofurahisha.
Kwa sababu uzalendo si ukimya.
Wakati mwingine uzalendo ni ujasiri wa kusema:
“Kuna jambo linaenda vibaya kabla hatujachelewa.”
Kama Tanzania inataka kubaki imara,
basi uponyaji lazima uwe sera ya taifa.
Uponyaji:
kati ya viongozi na wananchi,kati ya dola na upinzani,kati ya mamlaka na uwajibikaji,kati ya sheria na haki.
Kwa sababu hakuna taifa linaloweza kuishi milele kwa:
hofu, propaganda,au mgawanyiko wa kihisia.
Mwisho wa yote,
taifa huwa imara zaidi pale wananchi wake wanapoamini kwamba:
wao ni sehemu ya taifa,wanalindwa,
wanasikilizwa,na utu wao una thamani.
Mungu ailinde Tanzania isije kuwa nchi ambayo wananchi wanaogopana kuliko kuaminiana.
Na viongozi wetu wakumbuke:
historia haitawahukumu viongozi kwa barabara, madarasa , vituo vya afya walivyojenga pekee,
bali pia watahukumiwa kwa hali ya kihisia walizoliachia taifa.
Usisahau:
“Jamii iliyojeruhiwa huzaa watu waliojeruhiwa…
na watu waliojeruhiwa huongeza machafuko zaidi.”
Rev Petet simon Msigwa!
Iringa
Familia ya James Temba wamerudi upya msibani. Wiki jana walimzika Temba bila kichwa. Ndugu mwingine kafariki palepale msibani. Leo kichwa cha Temba kimepatikana. Watafukua kaburi wamuunganishe, au watazika kaburi tofauti? Haya mambo yanavumilikaje? Mungu awafariji. RIP Temba!
@ayubu_madenge Kuna faida wenzetu wanapata kupitia makampuni haya yanapopewa nafasi za uwekezaji huku wakipata uhakika wa uwekezaji wao kwenye nchi husika.