Tanzania ni moja kati ya nchi ambayo karibu kila mkoa wake yanapatikana madini yenye thamani kubwa duniani!
Madini ni utajiri! Kipande kidogo kinaweza badili maisha yako. Karibu tujifunze pamoja.
#MadiniYetu#MadiniTanzania
UTAFITI WA UANZISHWAJI MGODI MKUBWA WA DHAHABU WAANZA WILAYANI HANANG
▪️Waziri Mavunde aipongeza Kampuni kwa kukidhi masharti ya Leseni ya Utafiti
▪️Asimamia kwa vitendo lengo la kuongeza eneo la utafiti kutoka 16% hadi 50% ifikapo 2030*
▪️Ni utekelezaji wa maelekezo ya Mhe. Rais Samia
▪️Wananchi kunufaika kiuchumi na kijamii mradi ukianza kutekelezwa
📍 Manyara
Waziri wa Madini, *Mhe. Anthony Mavunde (Mb)*, ametembelea na kushuhudia utekelezaji wa utafiti wa kina wa madini kwa kutumia teknolojia ya ndege nyuki (drone) katika Kata ya Basotu, Wilaya Hanang, mkoani Manyara. Utafiti huo wa jiofizikia unalenga kubainisha maeneo yenye hifadhi ya madini utakaopelekea kuanzishwa kwa mgodi mkubwa wa dhahabu wilayani humo.
Ziara hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, *Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan* aliyoyatoa wakati akihutubia Bunge Oktoba 13, 2025 ambapo alitaja utafiti wa madini kama kipaumbele kwa mwaka 2025 - 2030 utakaopelekea kufikia angalau asilimia 50 ya utafiti wa kina wa madini nchini ifikapo mwaka 2030.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Waziri Mavunde amesema utafiti huo ni hatua muhimu kwa maendeleo ya wananchi wa Hanang na Mkoa wa Manyara kwa ujumla, kwani matokeo yake yanatarajiwa kuongeza ajira, kuvutia uwekezaji na kuchochea utekelezaji wa miradi ya kijamii kupitia leseni za uchimbaji madini.
“Tunatarajia utafiti huu utaleta matokeo chanya yatakayobadilisha maisha ya wananchi. Serikali itaendelea kusimamia sekta hii ili iwe chachu ya maendeleo kwa wote,” amesema Mavunde.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Hanang, *Mhe. Almish Hazal*, amemshukuru Waziri Mavunde kwa kutembelea eneo la mradi huo na kuendelea kusisitiza umuhimu wa tafiti za madini katika wilaya yake pia, ameiomba Wizara ya Madini kuendeleza kasi hiyo katika maeneo mengine ya Hanang yenye uwezekano wa kuwa na madini.
Naye, Mkurugenzi Mtendaji wa Cobra Resources Ltd, *Bw. Amos Nzungu*, amempongeza Waziri Mavunde kwa ushirikiano na uzalendo anaouonesha kwa kufuatilia utekelezaji wa miradi ya utafiti wa madini na kuahidi kukabidhi matokeo ya utafiti mara tu yatakapokamilika.
Kwa upande wa Meneja wa Kampuni ya SkyPM Solution inayofanya utafiti huo, *Bw. Paul Madata* amesema matumizi ya teknolojia ya ndege nyuki yamerahisisha na kuongeza ufanisi wa utafiti wa awali, kwani inaweza kupima hadi zaidi ya kilomita tatu chini ya uso wa ardhi kwa muda mfupi.
Awali, Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Manyara, *Mhandisi Godfrey Nyanda* ametoa taarifa ya maendeleo ya sekta ya madini mkoani hapo, akibainisha kuwa hadi kufikia robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2025/26 (Julai–Oktoba), wamekusanya asilimia 35.21 ya lengo la makusanyo ya Shilingi Bilioni 2.2 lililopangwa kwa mwaka mzima.
“Tutaendelea kusimamia kikamilifu maagizo ya Mhe. Rais na ya Waziri wetu Mhe. Mavunde ili kuhakikisha sekta ya madini inaendelea kukua na kuimarika hapa Manyara,” amesema Mha. Nyanda.
Ilikua ni siku nzuri kukutana na balozi wa Tanzania nchini DRC 🇨🇩 @TanzaniaInDRC Mh. S. J. Mshana na kuzungumza masuala mbali mbali ya kijiolojia na uchakataji wa madini katika nchi hizi mbili.
merci beaucoup!
🇹🇿🇨🇩
@MadiniTanzania@Madini_Yetu
Mazungumzo hayo ambayo yalihusu fursa ya Biashara, Masoko na Uwekezaji, yaliwahusisha Wafanyabiashara kutoka Tanzania ambao ni Faisal Shahbbhai, mmiliki wa Tanzanite Forever Lapidary Ltd na Zanzibar Marine Hatchery akiwemo na Godwin Msigwa kutoka Kampuni ya Canopus.
*YAJUE MADINI YAPATIKANAYO MKOANI KWAKO. JIPATIE NAKALA YAKO YA KITABU KINACHOONESHA MADINI YAPATIKANAYO KATIKA MKOA, WILAYA, KATA MPAKA KIJIJI KWA BEI NAFUU FIKA KATIKA OFISI ZA GST AU WASILIANA NASI KWA NAMBA 0262323020. KARIBU TUKUHUDUMIE*
@GeologicalT@JamiiForums
Mhe Said J Mshana, Balozi wa Tanzania Nchini DRC amefanya mazungumzo na Mhe Jean P Massala, Balozi wa DRC Nchini Tanzania kuhusu maandalizi ya ziara ujumbe wa Kituo cha Uwekezaji DRC (ANAPI), itakayofanyika nchini Tanzania 13-21 Machi 2023 kwa lengo kutangaza fursa zilizopo DRC
Nawatakia Kwaresma njema Wakristo wote. Katika hija hii ya kiroho mnayoianza leo kwa Jumatano ya Majivu, endeleeni kuiombea nchi yetu na Dunia nzima amani na upendo. Majivu katika paji la uso yawakumbushe ubinadamu wenu na kumrudia Mwenyezi Mungu, mkiomba ulinzi wake kwetu sote.
Kituo cha China Diamond & Gem Exchange cha China kitashirikiana na Ubalozi wa Tanzania kuyatangaza Madini ya Tanzanite katika soko la China sambamba na kuwezesha wafanyabiashara wa Madini wa Tanzania kulifikia soko la China kuuza madini yao kupitia kituo hicho jijini Macau.