#TANZANIA:MAHAKAMA YAFUTA KESI YA KUPINGA UBUNGE WA BABA LEVO KIGOMA
Mahakama Kuu, Masjala Ndogo ya Kigoma, imeifuta kesi ya kupinga matokeo katika uchaguzi wa Jimbo la Kigoma Mjini yaliyompa ushindi kada wa CCM, Levocatus Chipando maarufu Baba Levo.
Akitoa uamuzi huo leo Julai 16, Jaji Victoria Nongwa, anayesikiliza kesi hiyo, ametoa uamuzio huo akisema ushahidi uliowasilishwa hauwalazimishi walalamikiwa kujitetea.
Kesi hiyo ya uchaguzi namba 28949 ya mwaka 2025, inayotokana na Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, ilifunguliwa na wananchi wanne wanaojitambulisha kama wapiga kura wa jimbo hilo, Johary Kabourou, Luma Akilimali, Pendo Kombolela na Lumu Mwitu.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi amesema Serikali inaendelea na uchunguzi kuhusu madai ya kutoweka kwa Mwanasiasa Humphrey Polepole.
Kauli ya Katambi inakuja ikiwa ni siku 274 tangu kutoweka kwa Polepole alfajiri ya Jumatatu, Oktoba 16, 2025 katika Makazi yake ya Ununio, Wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es salaam hadi kufikia leo Julai 16, 2026.
Kupitia mahojiano maalum na AyoTV, Waziri Katambi amesema, “Katika hayo ya utekaji kulikuwa na sura nyingi, sura ya kwanza mambo ya utekaji yalikuwa yanafanyika na Watu wenyewe unakuta ni raia kwa raia labda ni ugomvi, uhasama, chuki ama ubabe na kwasababu wanatofautiana misimamo fulani fulani mwisho inaonekana imefanyika na Watu kutoka Mamlaka za Serikali, utakumbuka juzi mauaji ya James Temba (aliyekatwa kichwa) walisema Serikali imefanya, Super Sami alitekwa wakasema Serikali ila uhalisia ukagundulika sivyo, na mifano mingine mingi kama yule Bonge wa Kimara (Tarimo) haikuwa Serikali”
“Sisemi kwamba natetea tu Serikali, upande pia wa Serikali naweza nikafanya mimi Mwajiriwa wa Serikali kwakuwa nina visa na Mtu lakini sio kwamba nimetumwa na Serikali na wapo Askari ambao wamebainika kufanya makosa na wamechukuliwa hatua, Serikali haiteki inakamata na kumpeleka Mtu kwenye vyombo vya sheria”
Katambi ameongeza kuwa uchunguzi wa masuala ya aina hiyo unahitaji muda wa kutosha ili kuhakikisha haki inapatikana kwa pande zote zinazohusika.
“Ukiharakisha shauri haraka unaweza kuzika haki za Watu na ukichelewesha haki umeinyima pia haki hiyo, kuhusu Polepole taarifa ya mwisho Vyombo vya Ulinzi na Usalama vilisema vinaendelea na uchunguzi na upelelezi juu ya jambo hilo na hata aliyekuwa anatoa taarifa hiyo niliiona kupitia Ayo TV, alisema inasadikika hakuwepo Nchini lakini kuna taarifa zinasema alikuwa Nchini kwahiyo kama ni kweli au sio kweli upelelezi unaendelea,”.
#MillardAyoUPDATES
Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa CHADEMA Kanda ya Kati, Aquilin Claud, amemtaka Katibu Mkuu wa chama hicho wa kuunda tume kuchunguza tuhuma zinazohusu matumizı ya fedha za wadau, akısısıtiza kuwa kiongozi yeyote anayetuhumiwa anapaswa kujiweka pembeni kupisha uchunguzi.
Hakuna aliye juu ya sheria! Hata tukiwa na sera thabiti ya maridhiano inayounganisha watu, sheria itaendelea kuchukua mkondo wake kwa kila mtu bila kujali cheo chake.
Aliyekuwa Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoa wa Morogoro Barnabas Okolla amesema amesikitishwa na kauli za Katibu Mkuu wa Chama hicho John Mnyika kwamba wamepewa hongo ya Shilingili Milioni mbili kumchafua Makamu Mwenye kiti wa Chama hicho John Heche tuhuma ambazo hazija thibitisha.
Amesema kama kiongozi na mwanachama wa Chadema anayo haki ya kutoa maoni kuhusu mwenendo wa Chama hicho na kwamba bado msimamo wake ni kumtaka Mnyika kuunda chombo cha Kuchunguza tuhuma za ufisadi dhidi ya Heche.
" Nilitoka maoni kama maoni, lakini pia nikazungumzia yale yanayoendelea mitandanoni kuhusu ufisadi wa Makamu wetu mwenyekiti taifa, lakini Cha kusikitisha Katibu Mkuu ametoka hadharani na kunishambulia" amesema Okolla
Amesema kitendo cha Katibu Mkuu KUTOKA hadharani na kusema wamepewa rushwa ya Sh2Milioni ni kashafa ambayo haijathibitishwa hivyo anatakiwa kuthibtisha kwani yeye hadhi yake sio ya kiwango hicho cha pesa
VIDEO:
Kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Joseph Selasini amekiasa chama hicho kutumia vyombo vyake vya ndani kufanya uchunguzi wa tuhuma za kifedha ili kuwasafisha viongozi na kuimarisha imani ya wanachama wake.
Akizungumza hivi karibuni kutokana na tuhuma za ubadhirifu dhidi ya Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA bara, John Heche ambazo zimekuwa zikitolewa na baadhi ya wanachama na viongozi mbalimbali wa chama hicho ambao wengine wamesimamishwa na uongozi wa CHADEMA kwa kuhoji suala hilo, Selasini amesisitiza kuwa vyama vya upinzani vinapaswa kuwa tofauti na CCM kwa kile alichokiita kuficha mambo. Amedai kuwa upinzani unaikosoa CCM kwa kuficha mambo, hivyo ni lazima wao waoneshe mfano kwa kuwa wawazi zaidi katika taratibu zao.
“Ninachosema tu ni kwamba tumemsikia Katibu Mkuu na kwasababu chama chetu ni chama cha kidemokrasia ni matumaini yangu kwamba hilo jambo litawekwa wazi zaidi kwa maana kwamba chama kina vyombo. Sasa kama kina vyombo ili kuwa-contain wanachama, kuwaleta wanachama pamoja, kuleta ule uaminifu wa pamoja ni vizuri vile vyombo vikafanya kazi yake na kazi ikiwa nzuri maana yake viongozi wanasafishika”, ameeleza Selasini”, ameeleza Selasini.
Hata hivyo, akizungumza na wanahabari Julai 10, 2026, Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika alisema kama kuna mwanachama yeyote wa chama hicho ambaye ana taarifa zozote za malalamiko anapaswa kufuata taratibu za kikatiba za chama hicho na Zaidi akaeleza kuwa walikuwa na taarifa kuwa wale ambao wamekuwa wakitoa tuhuma dhidi ya viongozi wamekuwa wakilipwa fedha mpaka milioni mbili kwa lengo la kuchafua viongozi.
Very complicated. Watuhumiwa wanatakiwa kufikishwa mahakamani saa 48 baada ya kukamatwa. Wiki 2 wanashikiliwa vituoni polisi. Nani hasa anayevunja sheria??
Hili CHAGA jinga sijawahi ona
Linaongea upumbavu mwingi, Mdude , Soka na Polepole kuna evidence kabisa
Mimi mwenyewe @daviddjumbe na @MariaSTsehai watekaji wametufanyia utekaji mbele za watu na baadhi wamekamatwa
Halafu huyu mpumbavu anasema hakuna utekaji? Ngoja tu nyakati za kuwajibika zikifika, hizo pesa mnapewa tunzeni.
Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa CHADEMA Kanda ya Kati, Aquilin Claud ameshauri Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika aunde tume ya kumchunguza Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, John Heche kufuatia tuhuma zinazomkabili.
Mwenyekiti wa Kituo cha Wanahabari Watetezi wa Rasilimali za Taifa(MECIRA) Habibu Mchange ameeleza kuwa anatamani kuona Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kutoa nafasi ya kuwasikiliza viongozi wao kabla ya kuwavua uongozi.
Mchange amesema hayo leo Julai 12 2026 na kueleza kuwa hata wakati anafukuzwa CHADEMA alipewa nafasi ya kusikilizwa.
Mtafukuza wanachama na vipngozi wengi sana hadi itafika atabaki Heche tu chamani na bado sio jibu sahihi kufunika tuhuma hizi za Heche. Jibu sahihi ni kujibu tuhuma za heche kula mabilioni ya michango ya wadau kama alivyotuhumiwa na wajumbe wa cc Lema, Sugu, Boniyai na Leonard
Ukitaka kujua huu ni mradi wa Serikali ya CCM ni hivi press ya aliyekuwa Kiongozi wa kilindi Tanga na Katibu wa Morogoro zote zimefanyika nyumbani kwa aliyekuwa katibu wa Chadema Morogoro!. kiongozi wa Kilindi kasafirishwa hadi Morogoro kufanya press. Ujinga tuu
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wilaya ya Kilindi Mathias Cosmas Kamiliwe amesema hana wasiwasi juu ya kufukuzwa mara baada ya kukosoa chama chake kutokana na kuwa wamesema ukweli.
Amesema hayo akizungumza na waandishi wa habari tarehe 9, 2026 na kueleza kuwa yupo tayari.
Nae Mwenyekiti wa chama hicho Wilaya ya Mkinga Amour Shindo ameeleza kuwa ikitokea watafukuzwa haki itendeke ndani ya chama chao.
Updates:Kuhusu Neema Chozaile
Napenda kuwafahamisha wanachama,wapenzi wa demokrasia na umma wa Watanzania kuhusu hatua zilizofikiwa leo katika kufuatilia suala la Mwenyekiti wa CHADEMA Jimbo la Geita, Bi. Neema Chozaire, ambaye amekuwa akishikiliwa na Jeshi la Polisi.
Leo, tarehe 9 Julai 2026, viongozi wa chama pamoja na timu ya mawakili walifika Ofisi ya Kamanda wa Polisi wa Mkoa (RPC) Geita kwa lengo la kufuatilia mwenendo wa suala hilo na kuhakikisha wanapata fursa ya kumuona Bi. Neema pamoja na kujiridhisha kuhusu hali yake ya kiafya.
Baada ya mazungumzo ya muda mrefu na viongozi wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita, pande zote zilikubaliana kwamba Bi. Neema aletwe pale Ofisi ya RPC. Hatimaye aliletwa kutoka eneo alikokuwa ameshikiliwa, na viongozi wa chama pamoja na mawakili wakapata nafasi ya kuzungumza naye kwa takribani saa moja.
Katika mazungumzo, Bi. Neema ameeleza kuwa amefanyiwa vitendo vya ukatili akiwa mikononi mwa vyombo vya dola. Alidai kuwaamepigwa sana kiasi kwamba hadi sasa anapata shida kutembea, hali ambayo ilionekana wakati wa mazungumzo . Aidha, alieleza kuwa maelezo yaliyorekodiwa na mamlaka za uchunguzi hayakuwa ya hiari yake, lakini yalitolewa baada ya kupigwa na kulazimishwa. Kwa mujibu wa maelezo yake, kwa kipindi cha takribani siku kumi amekuwa akipigwa mchana na usiku ili akiri tuhuma ambazo anasisitiza si za kweli.
Baada ya mazungumzo hayo, Bi. Neema amehamishiwa katika Kituo Kikuu cha Polisi Geita, ambapo sasa ameruhusiwa kuonana na watu mbalimbali, ikiwemo timu yake ya mawakili.
CHADEMA tayari imemkabidhi mahitaji muhimu, huku timu ya mawakili ikiwa imekamilisha maandalizi yote muhimu ya kuhakikisha anapata msaada wa kisheria na haki zake zote za msingi zinalindwa katika hatua zote za mchakato wa sheria.
Bi. Neema anatarajiwa kufikishwa mahakamani siku ya Jumatatu.
CHADEMA itaendelea kufuatilia kwa karibu suala hili na kuhakikisha haki inatendeka. Tunatoa wito kwa mamlaka husika kuheshimu Katiba, sheria za nchi na haki za msingi za kila raia, ikiwemo haki ya kutofanyiwa mateso, ukatili au kulazimishwa kutoa maelezo dhidi ya utashi wake.
Gaidi ni nani?, Askofu Gwajima kapinga utekaji na mauaji, kanisa lake likafungwa. Simbachawene kataka Polisi wafuate Sheria na Katiba katika utekelezaji wa majukumu yao, akaondolewa. NANI GAIDI?
Wadau wajadili onyo kwa wanaharakati: 'Taifa limejengwa na wanaharakati'
Wadau wanaoshiriki katika Jukwaa la Demokrasia Tanzania linaloendelea Zanzibar leo Julai 09, 2026, wamechangia maoni yao juu ya onyo lililotolewa kwa wanaharakati, ambapo wengi wameshauri, uhanaharakati usiharamishwe kwani taifa limejengwa na wanaharakati.