#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Leo Agosti 24, 2026
Last time tuliishia part 261 so leo tunaendelea na -;
Part 262
Inapigwa Courtttttttt
Mwenyekiti Mhe. Lissu anaingia.
Majaji nao wanaingia muda huo huo.
Mwenyekiti Mhe. Lissu amevaa Tshirt nyeupe ya Stronger Together, No Reforms, No Election na Jeans ya Dark Blue kama kawa halafu Dread zake zinamea kwa kasi sana.
Majaji wanateta kidogo na kujiandaa na kesi kuanza.
Karani anawasha MIC na kusoma namba ya kesi, Jamhuri vs Tundu Lissu.
Anasimama Wakili wa Serikali Ajuaye Zengeli, Nasoro Katuga, Job Mrema, Ignas Mwinuka, Thawabu Issa, Winiwa Kasawa kikundi chote kinaiwakilisha Jamhuri. Na wanadai wako tayari.
Jaji Ndunguru: Sasa shahidi endelee au nikukumbushe ulipoishia?
Mhe. Lissu: Naomba nikumbushe.
Jaji Ndunguru anasema uliishia pale uliposema kuanzia 2020 umefanya utafiti wa masuala ya uchaguzi toka ukoloni.
Mhe. Lissu asante, sasa naomba niendeleeee.
Waheshimiwa Majaji siku ya kwanza nilisema hii ni kesi ya kisiasa na kusema Taasisi mbalimbali zimelaani ikiwemo Jumuiya ya Ulaya, Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa, Jumuiya ya Madola.
Hizo zote ni taasisi za kimataifa na bado zipo zingine taasisi za kikanda zipo na taasisi za Waafrika wenzetu sio wazungu peke yake.
Kesi ilipofunguliwa mwaka jana Taasisi za Kisheria za nchi yetu wenyewe na nchi jirani na sisi zilitoa matamko hadharani za kulaani mashtaka haya na kuyaita mashitaka ya uonevu. Na matumizi mabaya ya mfumo wa uendeshaji wa Mahakama.
Taasisi hizo ni pamoja na-;
1. Chama cha Mawakili wa Afrika ya Mashariki
2. Chama cha Wanasheria wa nchi wanachama wa SADC
3. Muungano wa Wanasheria Afrika (Pan African Lawyers Union)
4. Chama cha Mawakili wa Zambia
5. Chama cha Mawakili wa Kenya
6. Chama cha Mawakili wa Tanganyika. ambacho nilikuwa Rais wake mwaka 2017 kwa muda mfupi.
Taasisi zingine zilizotoa matamko kuhusu mimi kuonewa na kuwekwa ndani visivyo
1. Tume ya wanasheria Duniani, International Commission of Juris Kenyan Chapter
2. Armnest International Regional Office for Estern and Southern Africa
3. Ugandan Law Society
Waheshimiwa Majaji pia kauli za kulaani mashitaka haya zimetolewa na
1. Democratic Union of Africa, inayojumuisha vyama barani Afrika vyenye mrengo wa kisiasa Afrika sawa na CHADEMA.
2. Platform of African Democracy (PAD) ambalo ni jukwaa la vyama vya kidemokrasia kutoka nchi 17 hapa Afrika.
Waheshimiwa majaji kwa kipekeee kabisa.
Tarehe 30/07/2025 Tume ya Haki za Binadamu na Haki za Wananchi ya Afrika, ambayo ni chombo cha Umoja wa Afrika cha kusimamia haki za binadamu yenye Makao yake Arusha, Tanzania. (ACHPR)
Ambacho ni chombo mahsusi kilifanya kikao cha dharula kujadili mashitaka haya na katika kikao chake ikapitisha azimio linaloitwa AZIMIO KUHUSU HALI YA HAKI ZA BINADAMU KATIKA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.
Azimio HACHPR/RES.640 (LXXXIV) Kikao cha 84 cha Tume/2025. Azimio hilo linazungumzia kwa masikitiko makubwa kwa kufunguliwa kwa kesi hii na kukamatwa kwangu.
Tume ya Umoja wa Afrika ilisema Serikali ya Tanzania ina wajibu wa kufuata matakwa ya haki za binadamu kama ilivyoridhia mwaka 1984. (Bill of right). Sasa nilitaka kuongezea haya kuhusu mimi ni nani? Na kwanini kesi hii imeletwa.
Sasa kwa leo naomba nianze kwa kuzungumza juu ya mchango wangu kama Mwanaharakati wa Haki za binadamu na Demokrasia kwa nchi hii.
Na ushahidi huo utathibitisha kuwa kesi hii ni kwasababu hizo za msimamo wangu wa miaka mingi ni kazi niliyoifanya kwa miaka mingi sana.
Kwahiyo ni Political Persecution kwasababu ya msimamo wangu katika masuala ya haki na utawala bora. Sio kwasababu mimi ni MHAINI ni kwasababu ya kazi niliyoifanya na nitakayoendelea kuifanya.
Point to Note: Anachokifanya Mwenyekiti ni kwamba si mliyataka basi tulieni. Ataongea siku tatu huyu.๐๐๐
Part 263 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
Different years, same tight bonds.....{THEN vs NOW} ๐ฅ
Britney Spears alongside her two young sons, Sean Preston and Jayden James.
๐ท 2013.
๐ท 2026.