Kuna jaribu limetupitia, tumeona mahali Kanisa limefika, watumishi wa Mungu walivyo waoga. Nilikuwa najaribu kuwaza kwa sauti, mfano Mpinga Kristo akaja sasa akasema hakuna kununua wala kuuza bila chapa ya 666, tuna Kanisa la kukubali kufa kwa ajili ya Kristo kweli???
AMEANDIKA MSANII ROSE NDAUKA
Rafiki yangu,kaka yangu JOHN HECHE upo wapi jamaniii hii inauma sana kwakweli,Mwenyezi Mungu ingilia kati familia zinalia kwakukosa kujua watoto wao wako wapi,watoto wanateseka Kwa kushindwa kuwaona Baba zao,wake wanalia Kukosa kuwaona waume zao na kufurahi nao kwa pamoja...
Mungu tuongeleshe tunaenda wapi..?Moyo unavuja damu ndugu zetu wanapotezwa bila Sisi kujua walipo...Naomba Mungu tujue upo kituo gani cha Police ..
wazazi wetu sasa hawana Amani wanajua muda wowote lolote linaweza kumkuta mtoto wake Mwenyezi Mungu tuokoe .
HII HAIKUBALIKI ๐ญ๐ญ๐ญ
Lakini sasa, BWANA aliyekuhuluku, Ee Yakobo, yeye aliyekuumba, Ee Israeli, asema hivi, Usiogope, maana nimekukomboa; nimekuita kwa jina lako, wewe u wangu.
Upitapo katika maji mengi nitakuwa pamoja nawe; na katika mito, haitakugharikisha; uendapo katika moto, hutateketea; wala mwali wa moto hautakuunguza.
#Isaya43:1-2 #FreeJohnHeche
Jana Jeshi la polisi Kanda MAALUMU (MURILO & MAFWELE) walisema Makamu mwenyekiti John Heche kasafilishwa kwenda TARIME.
Jeshi la Polisi TARIME asubuhi ya leo wanasema JOHN HECHE hajafikishwa mikononi mwao.
Mnakumbuka niliwaambia kuna NJAMA za kumuua MAKAMU kwa njia ya AJALI? Bila shaka njama zingine za kufanikisha hilo takwa lao la Kumuua zinaendelea.
Tuungane kulitaka jeshi la polisi Kutoa Taarifa kuwa Yupo wapi JOHN HECHE @tanpol
Watag hapa waambie #FreeJohnHeche
#TUTAKUWEPO๐ซต๐พ๐