"Kimbizana na ndoto yako usikimbizane na watu kwa sababu:
1. Si kila anayekimbia na wewe mko nae mbio moja;
2. Si kila anayekujia mbio anakukimbiza, wengine wanakukimbilia; na
3. Wengine hapo unapopakimbia ndio kilele cha safari yao." ~Togolani Mavura.
MUNGU akukutanishe na akuunganishe na watu sahihi watakao kuwa sehemu ya kukusogeza kwenye Mafanikio yako. Watu watakao kunoa na kukufanya uwe bora zaidi, watu watakao kujenga na sio kukubomoa, watu watakao kueleza ukweli na kukuinua wala sio kukushusha chini. Tuseme Amen
Leo nataka kuzungumza na boys; wadogo zangu wapiganaji kabisa:
1.) Maisha siyo rahisi sana. Mafanikio siyo rahisi kabisa. Yatakujaribu. Yatakukatisha tamaa. Usikubali. Komaa, pambana! Kukata tamaa ni dhambi. Kurudi nyuma ni mkakati kabisa vitani. Wewe siyo mwepesi kiasi hiiicho!
2.) Wewe ulikuwa mgumu sana ndiyo maana Mungu aliamua uwe wa kiume mwanangu. Komaa kiume dogo.
3.) Kumbuka kuwa una dhamana kwa familia yako, dhamana hii ni kubwa zaidi kama hautoki kwenye familia tajiri, maana familia tajiri inatakiwa kutokana na wewe.
4.) Mtu aliyefanikiwa leo, ujue alianguka mara nyingi sana jana na juzi.
5.) Kufanya biashara ni kitu kigumu sana lakini pia kuwa kuajiriwa mpaka umri wa miaka 60 kila siku kuamka kuwahi kazini ni kazi ngumu pia. Chagua chako kimoja.
6.) Kama mkeo hakutii hasira, basi huyo siyo mkeo. Pole sana kaka.
7.) Kuwa na vyanzo vya pesa ni kitu kizuri zaidi kuliko kuwa na chanzo kimoja. Mkeo akiwa na kazi ama biashara ni nafuu kwako ila usimuulize anatumiaje pesa zake, timu za wajibu wako wa kumhudumia, usipigie hesabu pesa yake.
8.) Pesa haitafutwi kwa kulalamika, inatafutwa kwa ubunifu na juhudi. Ukiwa unalalamika sana badala ya kutafuta suluhisho, utaishia kuangalia wenzako wakifanikiwa. Simama, tafuta njia, usikubali kushindwa.
9.) Heshimu muda wako na muda wa wengine. Usipoteze muda kwa starehe zisizo na tija, badala yake utumie muda wako kujifunza, kufanya kazi, na kujenga mustakabali wako.
10.) Marafiki zako ni taswira ya maisha yako ya baadaye. Ukiwa na marafiki wavivu, wasio na maono, na wanaopenda majungu, basi ujue upo kwenye njia mbaya. Tafuta marafiki wanaokutia moyo, wanaokufundisha, na wanaokuinua.
11.) Jifunze kusema โhapanaโ. Usikubali kila jambo, kila ombi, na kila fursa kama haina maslahi kwako. Usihadaike na โmuda wote uko availableโ. Jua thamani yako.
12.) Afya ni utajiri. Unaweza kuwa na pesa nyingi lakini bila afya njema, utajiri wako hauna maana. Fanya mazoezi, kula vizuri, na epuka anasa zinazoathiri afya yako.
13.) Siku zote jifunze kitu kipya. Usiwahi kufikiri unajua kila kitu. Dunia inabadilika, biashara zinabadilika, fursa zinabadilika. Mwanaume anayejifunza kila siku ndiye anayeendelea kushinda.
14.) Usiishi kwa kushindana na watu, ishi kwa kushindana na jana yako. Kama leo unafanya vizuri zaidi ya jana, basi unashinda. Weka malengo yako binafsi, usipoteze muda kujilinganisha na wengine.
15.) Jifunze kuvumilia na kustahimili maumivu ya mafanikio. Hakuna aliyefanikiwa bila kupitia mateso, misukosuko, na changamoto. Ukikataa tabu za kujenga, utapitia tabu za maisha kwa kukosa. Chagua tabu zako!
#HK #Fighter #NjeYaBox
Kijana mwenzangu MUNGU akikupa nafasi nyingine ya kuanza Upya hakikisha haurudii makosa ya Zamani. Ota ndoto kubwa, fanya kazi kwa bidii na ishi kwa Unyenyekevu daima.