Eew Allah..!
Naamini kesho yaja, na naamini kesho yangu ni bora zaidi kwa baraka zako Allah..
Nakuomba Allah ifanye kesho yangu iliyo bora iwe karibu Allah..
Na usinifanye kuwa "mjivuni" katika kipindi hicho cha "kesho bora"..
Allahumma aamin 🤲🤲
Kuna kipindi utapitia maumivu zaidi, kuna kipindi utapitia changamoto zaidi ili uwe imara zaidi..
Katika nyakati zote hizo, shikamana katika Subra na Swala..✍️
Kipimo cha uaminifu ni kutekeleza ahadi; Kipimo cha wema ni uaminifu..
ili upate ridhaa ya mola wako, huna budi kuwa mwema..
Timiza ahadi, fanya matendo yako kwa haki na uaminifu.. maisha ya duniani ni daraja tu, huko tuendako unahitajika wema na uaminifu.
Unaweza kuhisi huna bahati, unaweza kukata tamaa ya kutafuta kwa sababu tu umekosa kile ulichotaraji;
Amini kuwa, Mungu ana makusudi yake katika utoaji..
✓Unaweza kupenda kitu kumbe ni Shari kwako;
✓Unaweza kuchukia kitu kumbe ni kheir tupu kwako...✍️✍️
Tuifanye fursa ya kuona mwaka mpya kama nafasi ya kujitathmini na si muda wa kufurahia sana na kusherehekea.
Mwaka mpya unapoingia ndivyo hivyo nafasi yetu ya kuishi katika ulimwengu huu uliojaa starehe na mateso, inazidi kupungua😢😢.
Isituhadae dunia, na pumzi ✍️✍️
Shikilia, kamatia kwa nguvu zote hicho kidogo ulichonacho, kwani hicho ndicho cha thamani zaidi kwako bila kujali uchache wake..
Watakudharau na kukuona kama MWENDAWAZIMU kutokana na "udhalili" wa hicho ushikacho, usithubutu kukiachia, huenda ndiyo daraja la mafanikio yako...
Ukitaka iwe nzuri kesho yako, anza leo kuiandaa...
Hakuna wakati mwingine baada ya leo, kwani kesho ni siku ya kuvuna matunda ya leo, na MAJUTO kamwe hayatabadili ukweli wa kiwango cha jitihada zako..
Usiumie sana, usisikitike sana ukamkosea Muumba wako kwa kukosa leo, huenda Mungu amekupangia siku muafaka kwako..
Kwani, hakuna ajuaye ya kesho yake, kwani maisha ya dunia ni mfano wa "chungwa", tunategemea ladha ndani yake, lakini hatujui kama kuna "tamu" ama "chachu"..
Tunajongea katka safar ya maisha huku tukifahamu ni wapi tulipotoka, lakin tuendako kumebaki "kiza" na kitendawili kischopata mteguaji😢
Basi tuondoe vikwazo katka njia tupitazo ili kurahisisha safar kwa wasafir wa baadaye, huenda kwa wema huo tukapata wepesi katka safar yetu hii
Huwa nawaza ule msemo kwamba "subira yavuta heri"; kwa sababu, wakati tunaposubiri "bwana heri" afike, huwa muda hautungoji..🤔🤔
Basi ukiwa unamsubiri "bwana heri", macho yako yaelekeze katika saa yako ya "Ukutani"..
Na pia zingatia, muda si rafiki wa kudumu.. ✍️✍️
Hapana shaka kwamba binadamu amekosa uwezo wa kujua hatma yake; lakini mawazo, fikra na akili aliyobarikiwa ni "zana" muhimu sana katika kuchagua ni hatma gani aiandae.
Pia jamii ina nafasi ktk kutengeneza hatma hiyo.
Muhimu ni kutokudharau nafasi ya mtu yeyote katika maisha yako
Mategemeo makubwa tunayowekeza kwa watu ni sababu kuu inayopeleke anguko lisilotarajiwa..
Jitihada zako ziwe kipaumbele kabla ya matumaini na mategemeo kwa wengine, kwani, msingi wa mafanikio yako huanzishwa na wewe mwenyewe, bali wengine ni wasaidizi tu...