Leo March 30/2020 Spika Job Ndugai amesema muda wa vikao vya Bunge umepunguzwa kutoka saa 9 hadi nne kwa kila kikao, na idadi ya wabunge katika ukumbi wa Bunge itakuwa 150 kwa kila kikao
Ujerumani imetoa ndege ICU (ICU plane), Airbus A310 MedEvac, kwa ajili ya kuwachukua wagonjwa wa corona kutoka Italia kuwapeleka kwenye Hospitali mbalimbali Ujerumani. Ndege hiyo ina vitanda 44 ambapo 16 ni kwa ajili ya wagonjwa mahututi, pamoja na Maafisa Afya 25.
SUMAYE RASMI CCM
Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye leo Machi 29, 2020 amerudi rasmi ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kupokelewa na Katibu Mkuu wa Chama hicho, Dk Bashiru Ally katika ofisi za CCM mkoa wa Dodoma ambapo pia amekabidhiwa kadi ya chama hicho.