DAR: Wakili wa Kujitegemea, Peter Madeleka aliyasema hayo Agosti 19, 2026 wakati akizungumza na Waandishi wa Habari.
Zaidi tembelea https://t.co/OLSzxbDkQL
#JamiiForums#Uwajibikaji#HakiZaBinadamu
Mashahidi wa Mh @TunduALissu mwenyekiti wa chama cha @ChademaTZ2 tunao na tunatamba nao.
Hii sio kesi ya kuku tunataka Mashahidi wote wa mtuhumiwa Mh @TunduALissu wapelekewe wito wa kufika mahakamani waje watoe ushahidi wao.
State si mmeyataka wenyewe haya twende mpaka mwisho.
VIDEO:
Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dkt. Rugemeleza Nshala amesema chama hicho kitaendelea kutumia Sheria na Katiba kudai HAKI zake, inazopambania mara zote
Dkt. Nshala amesema chama hicho hakiwezi kuwa chanzo cha vurugu au uvunjifu wa amani, na kwamba mara zote kitasimama kidete kuhakikisha misingi ya kuanzishwa kwa vyama vingi vya siasa inalindwa na kuhemishimiwa
Hayo amezungumza katika mahojiano maalum aliyoyafanya na Royal TV Plus
Katibu Mkuu Mhe. @jjmnyika, Naibu Katibu Mkuu Bara, Mhe. @amanigolugwa, pamoja na Wajumbe wa Kamati Kuu, Wenyeviti wa Kanda na viongozi mbalimbali, tayari wamewasili Mahakamani kufuatilia mwenendo wa kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Taifa, Mhe. @TunduALissu.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Godbless Lema, amesema Mahakama haina sababu ya kuhitaji ujasiri wa ajabu kutoa uamuzi kwamba Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, hana kesi ya kujibu.
Lema amesema kwa kuzingatia ushahidi uliowasilishwa Mahakamani, hakuna msingi wa kimantiki na kisheria unaoonyesha kuwa umejengwa msingi wa Lissu kuwa na kesi ya kujibu.
Amesema baadhi ya mambo yaliyoshuhudiwa wakati wa mwenendo wa kesi hiyo yalionekana zaidi kama vituko kuliko ushahidi wenye mashiko unaoweza kumfanya mtu awe na kesi ya kujibu.
Kwa mujibu wa Lema, uamuzi wa Mahakama kusema Lissu hana kesi ya kujibu haupaswi kuonekana kama ujasiri, bali unapaswa kuwa matokeo ya kawaida ya kutenda haki kwa kuzingatia sheria, ushahidi na dhamira njema.
Aidha, amesema Mahakama inapaswa kushinda jaribu hilo si kwa ajili ya CHADEMA, Serikali au Lissu, bali kwa ajili ya Tanzania na mustakabali wake.
Lema amesema haki inapowekwa mbele ya maslahi ya kisiasa, Taifa hushinda.
#KitengeUpdates
Nilikuwepo bungeni wakati mwenyekiti anayasema haya..
Polepole alikuwepo na alikua Mwenezi wa ccm kama huyu kijana Kihongosi wa sasa.. alikua chini ya Magufuli na aliamini haya yatawakuta Chadema tu.
Nyie mnaotumika kudhuru kuumiza na kutesa watu.
Your time will come. Acheni upuuzi huo mara moja.
Rais sio Mungu lazima atasemwa na atakosolewa.
JANA TAREHE 19.8.2026 WALIMU 3O WAMEUA MWANAFUNZI KWA KIPIGO BUNDA.
"Sisi wanafunzi wa shule Sekondari Makongoro, Wilaya ya Bunda, Mkoa wa Mara, tunaomba msaada kwa serikali kwa hali iliyompata mwenzetu Peter Kisumo Mahira, ambaye ameuawa kwa kupigwa fimbo na walimu wasiozidi 30"
Naomba tuisaidie kushare hii post wanafunzi wapate haki
Kama kuna mtu “ANANISHITAKI” kwa JINAI, ahakikishe ANAJUA SHERIA, vinginevyo, sitaki LAWAMA huko mbeleni. Maana HAWAKAWII kuanza kusema; “oooh….Madeleleka, AMEDHARAU MAHAKAMA”. 😂😂
Mwanasheria wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Rugemeleza Nshala, ameibua hoja za kisheria na kikatiba kuhusu sheria na taratibu zinazotoa marupurupu au mshahara kwa wenza wa viongozi wakuu kutokana na uhusiano wao na viongozi hao.
Dkt. Nshala amerejea Ibara ya 29(3) na 29(4) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akisema vifungu hivyo vinakataza raia kupewa haki, hadhi au cheo maalumu kwa misingi ya nasaba, jadi au urithi.
Akizungumzia maslahi yanayotolewa kwa mke au mume wa viongozi wakuu, Dkt. Nshala amehoji uhalali wa utaratibu huo iwapo mtu anapata maslahi hayo kwa sababu ya kuolewa au kumuoa kiongozi, badala ya utumishi wake binafsi.
Aidha, amerejea Ibara ya 13 ya Katiba inayoweka msingi wa usawa wa watu mbele ya sheria, akilinganisha hali hiyo na walimu, manesi, wakunga na wahandisi ambao wenza wao hawapati marupurupu au mishahara ya ziada kwa sababu ya taaluma za wenza wao.
Dkt. Nshala amesisitiza kuwa utoaji wa maslahi maalumu kwa misingi ya uhusiano wa kifamilia unapaswa kuchunguzwa kwa kuzingatia misingi ya Katiba na usawa wa wananchi.
Amewahimiza wananchi na wadau wa sheria kupinga mahakamani sheria au taratibu wanazoona zinakinzana na Katiba, akisema hatua hiyo ni muhimu katika kulinda usawa na haki za wananchi wote.
Leo ni siku muhimu kwa Tanzania na wapenda haki Duniani.
Asanteni Wananchi na wanachama wa CHADEMA kanda ya Pwani kwa kujitokeza ktk kushuhudia siku hii ya kihistoria.
Mwenyezi Mungu amtangulie Tundu Antipas Lissu.
‼️VIDEO YA CCTV CAMERA IKIONYESHA UTEKAJI KARIAKOO‼️
Huyu kwenye video Anaitwa Peter Richard Mushi ni fundi simu Kariakoo
alipigiwa simu tarehe13/8/2026 na mtu aliyejitambulisha kuwa ni mteja anahitaji kutengenezewa simu
Alimwelekeza alipo lakini mteja akataka ndugu peter amfuate maeneo ya china plaza alipofika china plaza
Alikutana na huyo mteja aliyekuwa anampigia simu kumbe hawakuwa wateja bali ni watekaji 💔 walikuja na gari toyota crown rangi nyeupe aina plate namba ndugu wamezunguka vituo vyote vya police hospitali zote mochwari zote bila kupata majibu
Ukumbi namba 01 wa mahakama kuu Kanda ya DSM umejaa tayari kusubiria uamuzi wa mahakama kuu kama Kuna kesi ya kujibu au haipo katika muendelezo wa kesi ya Mheshimiwa @TunduALissu
VIDEO:
Royal TV Plus imefanya mazungumzo na Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CHADEMA Freddy Mbwambo kuelekea maadhimisho ya siku ya Vijana Duniani itakayofanyika hapo kesho, Jumanne Agosti 12.2026
Freddy anasema inapokaribia siku za aina hii, kumbukumbu zake mbaya ni kutokuwa karibu na rafiki yake wa muda mrefu Deus Soka ambaye hadi sasa haijulikani halipo.
NB: YouTube ya Royal TV Online ina undani wa mahojiano haya.
Kada wa ACT-Wazalendo, Luhaga Mpina, ni miongoni mwa watu waliojitokeza kusikiliza kesi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu, ambayo leo imeanza tena baada ya kusimama kwa zaidi ya miezi mitano.
Mbali na Mpina, wapo pia viongozi wa juu wa Chadema, akiwemo Makamu Mwenyekiti, John Heche, Katibu Mkuu, John Mnyika pamoja na wajumbe wengine wa Kamati Kuu ya Chadema.
Kesi hiyo inayosikilizwa katika Mahakama Kuu, Masjala Ndogo Dar es Salaam, inatarajiwa kuendelea mfululizo kuanzia leo baada ya kusimama tangu Februari 24, 2026.