My Bro , Husein Mwinyi.
Ninakuandikia kwa masikitiko makubwa kufuatia kauli zinazoendelea kutolewa na baadhi ya viongozi kutoka Zanzibar ambazo, kwa mtazamo wangu, zinaonesha ubaguzi wa wazi dhidi ya Watanganyika. Kwa muda mrefu nimekuwa na imani kwamba fikra za namna hiyo haziwezi kupata nafasi katika uongozi wako. Ikiwa nimekosea katika tathmini hiyo, basi nitakuwa nimekosea kwa kiasi kikubwa sana.
Kauli hizi si hatari kwa mshikamano wa Muungano pekee, bali pia ni mbegu ya mgawanyiko wa kijamii na kisiasa ambayo inaweza kuzaa matokeo mabaya kwa Taifa letu. Kinachonisikitisha zaidi ni ukimya wako. Katika mazingira ya sasa, ukimya huo unaweza kutafsiriwa kama ridhaa au baraka kutoka mamlaka za juu, jambo ambalo linaweza kueleza kwa nini kauli hizi zinaendelea kutolewa kwa mfululizo, zikiwa na simulizi moja na bila hofu yoyote.
Kwa kweli, naogopa hata kuingia katika mjadala wa nafasi na fursa ambazo Wazanzibari wamewahi kushika au wanazoendelea kushika katika Muungano huu. Kufanya hivyo kungekuwa ni kuushusha mjadala kwenye kiwango ambacho siamini kinafaa kwa Taifa letu. Historia inaonesha wazi kuwa Wazanzibari wamepewa na wameendelea kupata nafasi kubwa za uongozi katika Jamhuri ya Muungano, ikiwemo nafasi ya Rais wa Tanzania. Hivyo, hoja za kuwatenga au kuwadharau Watanganyika hazina msingi wa haki wala busara.
Ninaamini kwamba maneno yana nguvu. Yanajenga, lakini pia yanaweza kubomoa. Kauli za ubaguzi zikipewa nafasi ya kukua bila kukemewa, zitajenga chuki, zitaongeza mgawanyiko, na hatimaye kila upande utajikuta umepoteza. Taifa lolote linaloruhusu ukweli kunyimwa nafasi huku upendeleo na ubaguzi vikipewa sauti, hujenga mazingira ya migogoro ambayo baadaye huwa vigumu kuyarekebisha.
Sioni mustakabali mwema ikiwa mwenendo huu utaendelea. Wakati wa kukemea na kusimama upande wa haki ni sasa. Kesho inaweza kuwa imechelewa.
Kuna mjeda mmoja anayo hela chafu sana ila low key hadi anapitiliza.
Kuna siku tumeenda nae kwenyw viwanja vya washua mimi mgonga ulimbo nimewaka vibaya mno kama naenda kuposa.
Yeye kapoa kiyakuza tu kala zake kandambili, kipensi mchaniko, na tshirt ya pale karume zile za 2k anapush BMW.
Ile tumeingia maeneo wale wahudumu wakanichangamkia mimi kichizi mfukoni pumbu tu jamaa wakamuona kama fala ila yupo bize na kiswaswadu chake.
Tukaketi mwana akamuita muhudumu akaagiza Don julio😁dizaini mhudumu kashtuka akamwambia we kaka nilipe kwanza kama upo siriazi..
Kamanda kwa upole akawa ameanza kuzama atoe kadi apanguse, Muda huo huo akatokeo owner wa lile chimbo mwenyewe moja kwa moja akaja hadi meza yetu akamsalimia kwa heshima kamanda kumbe ni business partiner na akatoa order kwa muhudumu kuwa hebu wapeleke VIP upesi.
Yule dada alitetemeka nahisi alitamani kujikojolea, dakika moja mbele ile meza yetu ikawa na wahudumu hawakauki na don julio ikaletwa na myoto mingi sana na kibango juu😁
Yule dingi alivo kiroho safi yule mhudumu aliyeleta miyeyusho akamtip kama elfu tisini hivi📌
Nahisi alijifunza kuwaheshimu watu kwa lugha ya uchungu sana.