@Jambotv_ Mama umeongea sana hasa kwenye viti maalumu! Hivyo viti maalumu ni kwaajili ya nani? Au ndo waheshimiwa wanaweka mademu zao kuwa maalumu kwao?
VIDEO:
"Nyinyi kama watu wa Iringa, na Watanzania wote popote walipo wahakikishe mwaka ujao wa uchaguzi wa madiwani, wabunge na Rais, wanawaambia vyama vyote vya siasa kwamba chama chochote ambacho hakitaweka suala la katiba mpya kipaumbele, chama hicho kisipigiwe kura kwasababu hakina nia njema na wananchi"- Dkt. Nkya.
Mwenyekiti wa Bodi ya Jukwaa la Katiba Tanzania (JUKATA) Dkt. Ananilea Nkya amezungumza hayo katika kongamano la Katiba lililoendeshwa na JUKATA mwishoni mwa wiki jana mkoani Iringa.
SALA YA ASUBUHI
+Kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Amina.
Tuusifu Utatu Mtakatifu wa Mungu mmoja, sasa na siku zote na milele amina. Ee utatu Mtakatifu wa Mwenyezi Mungu; +Baba, +Mwana na +Roho Mtakatifu. Ninasadiki kuwa upo hapa na mahali pote.
Ee Mungu wangu, umeniumba, umenikomboa, umenifanya mkristu, umenizidishia neema zako, umenitayarishia makao yangu mbinguni.
Ee Mungu wangu, nakuabudu, nakushukuru, nakuomba toba, nakupenda. Ee Mungu wangu, ninakutolea roho yangu, na mawazo, na maneno, na kazi na furaha, na mateso yangu, uyapokee unipe neema yako nisitende leo dhambi, Amina.
BABA YETU.
Baba yetu uliye mbinguni, jina lako litukuzwe. Ufalme wako ufike. Utakalo lifanyike duniani kama mbinguni.
Utupe leo mkate wetu wa kila siku. Utusamehe makosa yetu, kama tunavyowasamehe na sisi waliotukosea. Usitutie katika kishawishi, lakini utuopoe maovuni. Amina.
SALAMU MARIA.
Salamu, Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe, umebarikiwa kuliko wanawake wote, na Yesu, mzao wa tumbo lako, amebarikiwa.
Maria mtakatifu, Mama wa Mungu, utuombee sisi wakosefu, sasa na saa ya kufa kwetu. Amina.
KANUNI YA IMANI.
Nasadiki kwa Mungu, Baba Mwenyezi, Muumba wa mbingu na dunia; na kwa Yesu Kristo Mwanae pekee, Bwana wetu, aliyetungwa mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, akazaliwa na Bikira Maria, akateswa kwa mamlaka ya Ponsyo Pilato, akasulubiwa, akafa, akazikwa, akashukia kuzimu; siku ya tatu akafufuka kutoka wafu, akapaa mbinguni; ameketi kuume kwa Mungu Baba Mwenyezi; kutoka huko atakuja kuwahukumu walio hai na wafu.
Nasadiki kwa Roho Mtakatifu, Kanisa takatifu Katoliki, ushirika wa Watakatifu, maondoleo ya dhambi, ufufuko wa miili, na uzima wa milele. Amina.
AMRI ZA MUNGU.
1. Ndimi Bwana Mungu wako, usiabudu miungu wengine.
2. Usilitaje bure jina la Bwana Mungu wako.
3. Shika kitakatifu siku ya Mungu.
4. Waheshimu baba na mama; upate miaka mingi na heri duniani.
5. Usiue.
6. Usizini.
7. Usiibe.
8. Usiseme uongo.
9. Usitamani mwanamke asiye mke wako.
10. Usitamani mali ya mtu mwingine.
AMRI ZA KANISA.
1. Hudhuria Misa takatifu Dominika na Sikukuu zilizoamriwa.
2. Funga siku ya Jumatano ya Majivu; usile nyama siku ya Ijumaa Kuu.
3. Ungama dhambi zako walau mara moja kila mwaka.
4. Pokea Ekaristi Takatifu hasa wakati wa Pasaka.
5. Saidia Kanisa katoliki kwa zaka.
6. Shika sheria katoliki za ndoa.
Ee Maria Bikira Mtakatifu, Mama wa Mungu na Mama yangu, nawe Mtakatifu Yosefu, Nawe Malaika Mlinzi wangi, Nanyi watakatifu somo wangu, nanyi Watakatifu wote, Niombeeni nipate kuacha dhambi, nilindeni siku ya leo na siku zote, na saa ya kufa kwangu, Amina.
MALAIKA WA BWANA
•Malaika wa Bwana alimpasha habari Maria, Naye akapata mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu.
~Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe. Umebarikiwa kuliko wanawake wote, na Yesu mzao wa tumbo lako amebarikiwa. Maria mtakatifu Mama wa Mungu, utuombee sisi wakosefu. Sasa na saa ya kufa kwetu. Amina.
•Ndimi mtumishi wa Bwana, Nitendewe ulivyonena.
~Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe. Umebarikiwa kuliko wanawake wote, na Yesu mzao wa tumbo lako amebarikiwa. Maria mtakatifu Mama wa Mungu, utuombee sisi wakosefu. Sasa na saa ya kufa kwetu. Amina.
•Neno wa Mungu akatwaa mwili, akakaa kwetu.
~Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe. Umebarikiwa kuliko wanawake wote, na Yesu mzao wa tumbo lako amebarikiwa. Maria mtakatifu Mama wa Mungu, utuombee sisi wakosefu. Sasa na saa ya kufa kwetu. Amina.
Utuombee Mzazi mtakatifu wa Mungu, tujaliwe ahadi za Kristo.
Tuombe:
Tunakuomba, ee Bwana, utie neema yako mioyoni mwetu, ili sisi tuliojua kwa maelezo ya Malaika kwamba Mwanao amejifanya mtu, kwa mateso na msalaba wake utufikishe kwenye utukufu wa ufufuko. Tunaomba hayo kwa njia ya Kristo Bwana wetu Amina.
SALA KWA MALAIKA MLINZI
Malaika mlinzi wangu, unilinde katika hatari zote za roho na za mwili. Amina.
Moyo Mtakatifu wa Yesu, Utuombee
Roho za waamini marehemu wapate rehema kwa Mungu wapumzike kwa amani.
+Kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Amina.