Wakati mwingine mtu huzoea mwanga kiasi kwamba husahau kulinda taa. Taa inapopungua si kwa sababu ilichoka kuwaka, bali kwa sababu ilichoka kuwaka peke yake.
✍
Usikate tamaa hata kama mambo yamekuwa magumu. Kila unachopitia kina sababu na kina mwisho wake.
Leo inaweza kuwa ngumu, lakini kesho inaweza kuwa mwanzo mpya.
Endelea kupambana kimya kimya, Mungu anaona juhudi zako. Subira yako leo ndiyo furaha yako ya kesho💪!
Kubali kuwa maisha yana vipindi
Maisha hayakai sawa muda wote. Kuna wakati wa furaha na wakati wa majaribu.
Uvumilivu unaanza pale unapokubali kuwa changamoto ni sehemu ya safari, si mwisho wa maisha.!
Kabla hujaunda picha ya mtu moyoni mwako, mpe nafasi ajieleze kupitia matendo yake, si kupitia hadithi za watu.
Maana kuamini kila unachosikia ni kosa linaloweza kukufanya umpoteze mtu mwema kwa sababu ya maneno yasiyo na mizizi ya ukweli.
Usimuone mtu mbaya kwa sababu tu umeambiwa ni mbaya.
Watu wengi wanahukumiwa kwa maneno ya wengine, si kwa matendo yao wenyewe.
Maisha yamenifundisha kuwa si kila anayekusimulia ubaya wa mtu ana ukweli mkononi; wengine huongeza chumvi kwa chuki, wivu au maslahi yao binafsi.
Maisha yana njia ya kutufundisha kupitia machungu, Na wakati mwingine, yanaweza kutupiga hadi ukajikuta unakosea kila unachofanya.
ALL IN ALL TUMSHKURU MUNGU NA KUSEMA ALHAMNDULILLAH 🙏
Tunakosa Usingizi ili wanaotutegemea wapate kulala Vizuri!
Furaha ya kweli katika maisha ni pale mtu anapokuwa na Amani ya Moyo bila kujali hali ya maisha aliyonayo.