Mwishoni mwa mwaka 2024 nilitengeneza hii package inayolist ya Mikoa yote, Wilaya, Kata na Postcode zake. Mpaka leo inatumiwa na developers 165.
Unaweza install hapa kwa kutumia composer https://t.co/XRGWLk9Ey2
MAN TO MAN
Maisha yanapokunyookea, usianze kuwaona wanaume wengine kama wasio na maana au wasiojituma katika maisha. Kumbuka muda wowote hali hubadilika jifunze kuwa mnyenyekevu
Mwanaume usichekelee kamwe anguko la mwanaume mwenzako. Wanaume hatupaswi kuchekana wala kudharauliana. Badala yake, tupeane moyo na kushikana mikono katika mapambano yetu, Maana sote tunaishi kwa akili na kula kwa jasho
BRO TO BRO
“Nitafanya kesho" hii kauli ni ugonjwa unaoua ndoto zako polepole.
Hakuna ndoto inayokufa ghafla nyingi zinakufa kwa kuahirisha.
Kila kesho unayosema leo, ni hatua moja nyuma.
Wanaume wengi hawakushindwa sio kwa sababu hawana uwezo, bali walishindwa na uzembe.
Kaa kitaalamu anza sasa hata kama hujajiandaa. Bora ushindwe kwa kujaribu kuliko ujutie baadae kwa kushindwa kujaribu
Ukisubiri mood, pesa, au muda sahihi utazeeka ukiwa na mawazo tu.
Kumbuka Watu wengi wanaofanikiwa hawangoji kesho. Wanafanya leo.
Unajua kwanini Afrika haiwezi kuendelea, hatujafundishwa kuzalisha. Kila mtu kafundishwa kuchukua tu. Kufanya kazi kupata mshahara peke yake. Hakuna ujasiriamali wala utoaji wa huduma ambao unalenga kuboresha maisha ya wanadamu. Kila mtu anawaza taking only. Akili za masikini.
Ukubwa wa Mungu haupungui kwa sababu ya changamoto zako. Badala yake, changamoto zako hupungua unapomtazama Mungu alivyo mkubwa, mwaminifu, na mwenye uwezo wote. 🙏🏼