Watanzania tusimwangushe huyu baba………..
Angalau akitoka ndani akute tumepiga hatua kubwa kwenye maendeleo.
KUCHANGIA TUMA PESA:
M-Pesa
Namba: 0744446969
Jina: CHADEMA HQ
NMB Bank
Namba ya Akaunti: 22606600140
Jina la Akaunti: Chama cha Demokrasia na Maendeleo
#UPDATES_KESI_YA_MAWAKILI_WA_MHE_LISSU_DHIDI_YA_MKUU_WA_MAGEREZA
Part 9
Mahakama imereje saa nane na dakika arobaini mchana.
Anasimama Wakili Kalokola, anasema kwenye jopo lao anamuondoa Wakili Francis Wisdom.
Sasa Wakili wa Serikali Kalokola anaanza kumuhoji maswali Shaidi ambae ni Wakili wa Mhe. Lissu Paul Kisabo.
Jaji anasema tunakukumbusha bado uko chini ya kiapo.
Kalokola endelea.
Wakili wa Serikali Kalokola: Nitaanzia eneo la mwisho. Uliambiwa kanuni ya fair trial iliyopo kwenye katiba haiwezi kupuuzwa kwa kuangalia kanuni za Magereza.
Wakili Kisabo: Ndio haziwezi.
Wakili wa Serikali Kalokola: kwenye madai yenu sio hoja kwamba kanuni za magereza ziko kinyume na katiba?
Wakili Kisabo: Hauko sahihi. Kesi hii sio ya kulalamikia kifungu chochote.
Wakili wa Serikali Kalokola: Unafahamu taratibu zote?
Wakili Kisabo: Nyingi nazifahamu.
Wakili wa Serikali Kalokola : mahabusu anapaswa kupewa huduma za matibabu na serikali?
Wakili Kisabo: Sifahamu.
Wakili wa Serikali Kalokola: Mfungwa anaweza kupewa pesa na zinaweza kuhifadhiwa na askari magereza?
Wakili Kisabo: Sijui
Wakili wa Serikali Kalokola: Umetaja jina la ambae huwa unampa pesa za Lissu ukimpelekea.
Wakili Kisabo: huwa nawapa askari magereza. Na wewe kalokola sio askari magereza.
Wakili wa Serikali Kalokola: Uliwahi kulalamika kuwa Lissu hapewi Chakula?
Wakili Kisabo: Sijawahi
Wakili wa Serikali Kalokola: Una elimu inayohusiana na mawasiliano?
Wakili Kisabo: nina elimu ya sheria. Mawasiliano pia yana sheria.
Wakili wa Serikali Kalokola: Kuna sheria inasema mawasiliano yaweje?
Wakili Kisabo: Confidentiality tu ndio kanuni.
Wakili wa Serikali Kalokola: mazungumzo ya oral yalikuwa preserved?
Wakili Kisabo: Tulizungumza, walitusikiliza. Kwahiyo hakukuwa na siri.
Wakili wa Serikali Kalokola: Mliyozungumza ni yapi?
Wakili Kisabo: Hayo mazungumzo ni siri kati yangu na mteja wangu.
Wakili wa Serikali Kalokola : Ni kweli mmekutana mara kadhaa na Mh. Lissu huko Ukonga?
WakiliKisabo: Nimesema hadi kwenye kiapo. Kuwa tulikuwa tunakutana wapi yaani ofisini kwa 3rd respondent.
Wakili wa Serikali Kalokola: Je kanuni ya 33 ndio mnayoilalamikia hii kanuni ya usimamizi wa magereza?
Wakili Kisabo: hapana.
Wakili wa Serikali Kalokola: Mtu yeyote akiingia magereza anakuwa classified?
Wakili Kisabo: Ndio uniambie sasa?
Wakili wa Serikali Kalokola: Mkuu wa Gereza anawajibika na usalama wa wafungwa?
Wakili Kisabo: sio kanuni ya 33(1)(a) itumike kwa Liss maana Lissu hajahukumiwa kunyongwa.
Kwa Kifupi Wakili Kisabo anapiga miguu yote, yuko taratibu lakini anapiga sana kwenye mshono.
Wakili wa Serikali Kalokola: ulioneshwa maoni mbalimbali ya Mkuu wa Gereza?
Wakili Kisabo: Niliona.
Wakili wa Serikali Kalokola: Kila anayeona anasikia.
Wakili Kisabo: Yes inategemea na mazingira.
Wakili wa Serikali Kalokola: umewahi kuwapima masikio maaskari magereza wa Ukonga ukajua wamesikia au hawajasikia?
Wakili Kisabo: watu nikifika naongea nao wananijibu. Ukisema hawasikii tena labda uwe na tatizo lako wewe.
Wakili wa Serikali Kalokola : Sasa mawasiliano ya simu kwenye chumba chenye vioo na ukasema kuna uwezekano wa kusikilizwa.
Wakili Kisabo: Yanasikilizwa.
Wakili wa Serikali Kalokola: Ulitaja kifaa kinachorekodi.
Wakili Kisabo: Sikijui, lakini simu yenyewe inarekodi. Sasa unataka kifaa gani kingine.
Wakili wa Serikali Kalokola: Unafahamu kwenye gereza la ukonga na magereza mengine kuna mtu anaitwa Principal Officer ambae yuko juu ya wakuu wa magereza?
Wakili Kisabo: Hawanihusu kama wakili mimi.
Wakili wa Serikali Kalokola: Ulienda au hukuenda kupeleka malalamiko kwa askari magereza wa juu?
Wakili Kisabo: Nimeshajibu hilo swali.
Wakili wa Serikali Kalokola: Mahakama hii ina uwezo wa kutekeleza maamuzi ya working group ya UN? Na uamuzi wa Jaji Mkwizu. Inaweza kutekeleza?
Kisabo: Kwanini isiweze. Kama jambo ni la kisheria. Lazima litekelezwe.
Part 10 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_MAWAKILI_WA_MHE_LISSU_DHIDI_YA_MKUU_WA_MAGEREZA
Part 8
Anaendelea Mhe. Lissu.
Wakili Kisabo: Ni sahihi nilikuletea lakini admission officer aliichukua akaisoma na kuwapa wengine na baada ya hapo wakasema hatuwezi kuruhusu umpatie Tundu Lissu hii nyaraka.
Jaji: Unasema mwenyekiti wa kikao unamaanisha nini?
Wakili Kisabo: Ni mtu aliyekuwa anasimamia yale mazungumzo yetu.
Mhe. Lissu: Sasa katika ofisi hiyo ya naibu Mkuu wa gereza kuna uwezekano wa kuzungumza bila kusikilizwa upo kweli?
Wakili Kisabo: Huo uwezekano haupo kabisa.
Mhe. Lissu: Kesi yangu ya uhaini imeendeshwa kwenye chumba hiki hiki cha mahakama?
Wakili Kisabo: Ni kweli
Mhe. Lissu: Na kila ninapoletwa na kwamba hata mara moja mmewahi kuruhusiwa kuja kuniona huko lockup?
Wakili Kisabo: huwa tunazuiwa kabisa.
Mhe. Lissu: Je hapa mahakamani mmewahi kuruhusiwa kunipa nyaraka yoyote?
Wakili Kisabo: Huwa wanazichukua hawa maaskari magereza hata kama ni mbele ya Jaji.
Mhe. Lissu: Ilikuwaje ulipotaka kunipa uamuzi wa Jaji Mkwizu kuhusu malalamiko yangu ya kutopewa haki zangu?
Wakili Kisabo: Walipokonya hawakukupatia.
Mhe. Lissu: Vipi unasemaje kuhusu utendaji kazi wa Mkuu Wa Gereza?
Wakili Kisabo: Hafuati sheria kabisa. Anajiamulia tu.
Mhe. Lissu: Jaji Mkwizu alitoa amri kuwa utaratibu wa sheria ufuatwe lakini amri hiyo imepuuzwa?
Wakili Kisabo: Ni kweli kabisa.
Mhe. Lissu: Na nyie mawakili mlilalamika sana toka Kisutu pia?
Wakili Kisabo: Ni sahihi kabisa.
Mhe. Lissu: Ni kweli kikosi kazi cha umoja wa mataifa kimesema mawasiliano kati yangu na mawakili wangu iheshimiwe?
Wakili Kisabo: imesema hivyo lakini halijawahi kuzingatiwa na hawa mapolisi.
Mhe. Lissu: Je mmekosea kuja kulalamikia mambo haya.
Wakili Kisabo: Mahakama hii ya Kikatiba ndio eneo sahihi kabisa.
Wakili Lissu: Ni kweli Mahakama hii ina ushahidi mwingi kuhusu jambo hili ukiachana na ushahidi wangu na ushahidi wenu?
Wakili Kisabo: Ni sahihi kabisa. Maana mambo mengine yametokea mbele ya mahakama hii Kuu na pia nyaraka za mwenendo wa mashauri yaliyopo hapa.
Mhe. Lissu: Ni kweli wajibu maombi haya akiwemo mkuu wa gereza katika majibu yake na kiapo chake ametusaidia kutuwekea nyaraka nyingi sana zinazotusaidia kwenye kesi yetu.
Wakili Kisabo: Kwakweli ametusaidia sana kutuletea mavitabu ya kuonesha walivyokuwa wanatuandika majina na kusema sababu za tusimamiwe na kusikilizwa.
Mhe. Lissu: Nimemaliza.
Anasimama Wakili wa Serikali Kalokola anasema tunaomba break ya lisaa.
Kesi imeahirishwa baada ya lisaa limoja.
#UPDATES_KESI_YA_MAWAKILI_WA_MHE_LISSU_DHIDI_YA_MKUU_WA_MAGEREZA
Leo July 21, 2026
Jana tuliishia part 6 so leo tunaendelea na-;
Part 7
Leo Mhe. Lissu aanaendelea kuhoji Mawakili wake ambapo anamuhoji Wakili Paul Kisabo.
Mhe. Lissu : Nitakuuliza maswali kuanzia Tar. 16/06 hadi November 15.
Tar. 16/06 pale Kisutu Nililalamika kuhusu mawasiliano yangu na mawakili wangu?
Wakili Kisabo: Ni kweli na ukasema umetuondoa kazini.
Mhe. Lissu: Baada ya hapo utaratibu wa mawasiliano ulibadilika?
Wakili Kisabo: Ni kweli
Mhe. Lissu: Utaratibu ulibadilika na tukawa tunazungumza kwenye admission office.
Wakili Kisabo: Ndio na walikuwa wanatusikiliza
Mhe. Lissu: Kwenye kiti cha wakili anachokaa pale admission kuna askari anapiga type anaandika. Na wengine wengi wanaandika humo ndani na Insp. Mwingine wa sheria na mwingine wa usalama.
Wakili Kisabo: ni kweli kabisa.
Mhe. Lissu: Na kule kwenye kile chumba cha awali tunachoongea na simu ni kweli wanakusimamia na kukusikia unachoongea kwenye hiyo simu?
Wakili Kisabo: Ni kweli.
Mhe.Lissu: Kuna CCTV camera hapo kwenye kale ka Chumba?
Wakili Kisabo: Ni kweli.
Mhe. Lissu: Na turudi kwenye admission office napo CCTV zipo?
Wakili Kisabo: Ni kweli zipo.
Mhe. Lissu: Je unapozungumza na mteja wako kuna usiri wowote?
Wakili Kisabo: hakuna usiri maana wanakusikiliza na kutusimamia kwa kila kitu.
Mhe. Lissu: Soma kanuni ya 33(1)(a) ya Kanuni za Magereza. Je kwa kanuni hiyo utaratibu unaotumika kunisimamia mimi kama huo utaratibu ni wafungwa wa kifo au wafungwa wengine kawaida?
Wakili Kisabo: Huo ni utaratibu wa wafungwa waliohukumiwa kifo sio mtu kama wewe.
Mhe. Lissu: Soma sheria ya magereza na kanuni zake. Je mahabusu kama mimi anaruhusiwa kusimamiwa hivyo kama ninavyosimamiwa mimi?
Wakili Kisabo: Hakuna mahali kokote inaruhusiwa kwenye sheria.
Mhe. Lissu: Baada ya 15/11/2025 utaratibu ukabadilika kutoka admission office kwenye kwa naibu mkuu wa gereza ofisi ambayo yupo pia mtu wa usalama wa gereza?
Wakili Kisabo: Haswaaa ilikuwa hivyo.
Mhe. Lissu: Ofisi ya mkuu wa jela tumekutana mara ngapi ukazungumza na mimi?
Wakili Kisabo: Zaidi ya mara tatu.
Mhe. Lissu: Tulipofanya kwa mkuu wa gereza tulikuwa peke yetu?
Wakili Kisabo: Alikuwepo Mkuu wa Gereza, Walinzi wako na maaskari wengine wanajaaa mle.
Mhe: Lissu: Ni kweli hujawahi kupima ukubwa wa ofisi ya Mkuu wa Gereza?
Wakili Kisabo: sijawahi kupima.
Mhe. Lissu: Je sasa kuna uwezekano wa kusikia au kutosikia tunachoongea?
Wakili Kisabo: Lazima watusikie. Wametusikia mara zote.
Mhe. Lissu: Kwanini unasema wanatusikia.
Wakili Kisabo: Kwanza wako karibu na sisi chumba ni kidogo. Kuna muda tukicheka wanacheka na kuna muda tukisikitika na wao wanasikitika. Maana yake wanatufuatilia.
Kicheko kwa mbali kinatokea. 😂😂😂
Mhe. Lissu: Sasa kule kwa naibu mkuu wa gereza kukoje?
Wakili Kisabo: Na kwenyewe walikuwa wanajazana na kusikiliza kila kitu. Kulikuwa hakuna faragha kabisa.
Mhe.Lissu: Tuzungumze mabadilishano ya nyaraka, Ni kweli mmeniletea nyaraka mbalimbali kuhusu kesi inayonikabili Mahakama kuu.
Wakili Kisabo: Ni kweli lakini kabla hatujakupa wanazichukua na kuzisoma.
Mhe. Lissu: Na hadi unapoondoka huwa bado wako nazo wao?
Wakili Kisabo: Ni sahihi
Mhe. Lissu: Ni kweli mara nyingi nimewalalamikia kuwa sipati hizo nyaraka mara nyingine?
Wakili Kisabo: Mara nyingi sana umelalamika hata ile hotuba ya Jaji Chande kuhusu ripoti ya uchunguzi wa matukio ya oktoba 29 hujapata hadi leo.
Mhe. Lissu: Unafahamu kama mawakili wa serikali walisema Mahakamani wanataka kuongeza ushahidi kuniunganisha na matukio ya oktoba 29
Wakili Kisabo: Ni kweli na nyaraka ile nilikuletea ujiandae na utetezi.
Mhe. Lissu: Ni kweli mwezi uliopita uliniletea nyaraka kutoka umoja wa mataifa ikisema niachiwe kwa kesi hii.
Part 8 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_MAWAKILI_WA_MHE_LISSU_DHIDI_YA_MKUU_WA_MAGEREZA
Part 6
Anaendelea Mhe. Lissu
Mhe. Lissu: Duuh sasa mawakili binafsi neno utaratibu halijasemwa kokote lakini hawa wa Serikali neno Utaratibu ndio limewekwa. Haya soma pia kokote walipokuja mawakili wa serikali pameandikwaje?
Wakili Maduhu: Wasikilizwe na wapewe nafasi.
Mhe. Lissu: Kwahiyo kuna ubaguzi kati ya mawakili wa serikali na mawakili binafsi?
Wakili Maduhu: Ni kweli kabisa.
Mhe. Lissu: Ubaguzi wa aina hii unaruhusiwa kwa sheria za Tanzania?
Wakili Maduhu: Hauruhusiwi kabisa kabisa.
Mhe. Lissu: Mawakili waliotendewa hivi ni zaidi ya mawakili 36 ukiachana na wakwangu ni mawakili wa watu wengine pia.
Wakili Maduhu: Kwa kiasi kikubwa mawakili wote tunatendewa huo unyama.
Mhe. Lissu: Annexure A3 ni hukumu ya Jaji Mkwizu ya Tar. 11/07/2025 haya malalamiko ya kuingiliwa mawasiliano kati ya mawakili wangu sikuyafikisha mahakamani ya yakatolewa maamuzi na mahakamu kuu.
Wakili Maduhu: Sahihi kabisa.
Mhe. Lissu: Na malalamiko haya yanahusiana na ukiukwaji wa kanuni ya 13 ya uendeshaji wa Magereza?
Wakili Maduhu: sahihi kabisa.
Mhe. Lissu: Licha ya maelekezo hayo ya Jaji Mkwizu kwamba watekeleze sheria je ulitekelezwa na magereza?
Wakili Maduhu: Haukutekelezwa kabisa.
Mhe. Lissu: Je mambo haya niliyaeleza pia kule Kisutu kuhusu mawasiliano yangu?
Wakili Maduhu: Sahihi. Hata hapa Mahakama Kuu ukisema hayo Mahakama kuu kwenye kesi yako ya uhaini.
Mhe z Lissu: Kwahiyo malalamiko yangu nimeyawasilisha kwa watu wanaotambulika kisheria.
Wakili Maduhu: Sahihi.
Mhe. Lissu: Twende annexure A4 kwamba kikosi kazi kinachoshughulikia watu wanaofungwa hovyo hovyo cha umoja wa mataifa mimi nimetajwa na kesi yangu kwasababu kikosi kazi cha umoja wa mataifa kimepelekewa malalamiko yangu na wamesema haya mambo yakomeshwe? Kweli au si kweli.
Wakili Maduhu: Ni kweli kabisa.
Mhe. Lissu: Sasa hawa ambao hawataki kutii sheria akiwemo Bwana Jela wakati kuna mwongozo wa umoja wa mataifa?
Wakili Maduhu: Sijui wanataka waambiwe na nani hawa.
Mhe. Lissu: au wanataka twende kwa Mungu tufe ndio tutapata hiyo haki yetu?
Wakili Maduhu: Nafikiri hatujakosea kuja hapa mahakamani.
Mhe. Lissu: Nimemaliza mimi.
Anasimama Wakili wa Serikali Kalokola na yeye anataka kumuuliza swali Wakili Maduhu william.
Anasimama Lissu anasema hilo jambo hawakuomba.
Jaji anasema Stanley Kalokola na wewe uulize hayo maswali yako.
Wakili wa Serikali Kalokola: Wewe ni Wakili.
Wakili Maduhu: Sahihi.
Wakili wa Serikali Kalokola: Una uzoefu wa miaka mingapi?
Wakili Maduhu: Miaka 6.
Wakili wa Serikali Kalokola: Respondent wa nne nae mmemshitaki hapa? Ambae ni Lissu.
Wakili Maduhu: Sahihi.
Wakili wa Serikali Kalokola: kuna mahali kokote ulililalamikia suala hili kwa Jaji Mkwizu?
Wakili Maduhu: Halipo.
Wakili wa Serikali Kalokola: Ulibaguliwa kwasababu ya rangi yako kuna muhali umesema kwenye kiapo chako?
Wakili Maduhu: Siwezi kuwa na uhakika.
Wakili wa Serikali Kalokola: Onesha uliposema asikilizwe?
Wakili Maduhu: ameonesha maeneo matatu.
Wakili wa Serikali Kalokola: ulitembelea magereza mara nyingi na je jina lako lipo kuonesha uliandikwa jina?
Wakili Maduhu: niliandikwa mara tatu tu baada ya hapo sikuwahi kuandikwa tena licha ya kwenda.
Wakili wa Serikali Kalokola: Je waliokuwa wanakusikiliza ni akina nani?
Wakili Maduhu: Mkuu wa gereza na wenzake walikuwa wananisikiliza. Surveilance ya kufa mtu.
Wakili wa Serikali Kalokola; Ni hayo tu Waheshimiwa majaji.
Wakili Maduhu William amemaliza kuhojiwa sasa muda unaangaliwa kama unatosha. Tayari saa 10 na nusu kwahiyo Wakili wa Serikali ameomba waahirishe tuanze kesho asubuhi.
Majaji wanasema tukutane kesho asubuhi saa tatu.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_MAWAKILI_WA_MHE_LISSU_DHIDI_YA_MKUU_WA_MAGEREZA
Part 2.
Anaendelea Mhe. Lissu
Mhe. Lissu: Nenda ukurasa wa 27 angalia defence counsels angalia jina la Kulwa Maduhu na Paul Kisabo kama hayapo?
Wakili Maduhu: Yapo majina ya hao mawakili.
Mhe. Lissu: Ukurasa wa 40 kwenye huo mwenendo wa Kisutu angalia upande wa corum useme kama Paul Kisabo na Kulwa Maduhu.
Wakili Maduhu: Wapo wote wawili.
Mhe. Lissu: Sasa waeleze majaji kama kuna utaratibu wowote wa kisheria wa unaopaswa kuufuata kumuona mteja?
Wakili Maduhu: Hakuna utaratibu wowote wa kisheria zaidi ya kuonesha kitambulisho tu cha uwakili.
Mhe. Lissu: Haya Maneno ya Bwana jela kuwa sijakutambulisha ni maneno ya bure tu?
Wakili Maduhu: Kabisa maneno ya bure kabisa.
Mhe. Lissu: Unazifahamu kanuni za maadili za mawakili?
Wakili Maduhu: Nazijua ndio.
Mhe. Lissu: Je kwa kanuni hizi wakili anaruhusiwa kumuonesha makubaliano yake na mteja mtu anayeitwa Bwana Jela?
Wakili Maduhu: Duty to confidentiality hairuhusu. Kwahiyo siruhusiwi kabisa kutoa siri za mteja wangu.
Mhe. Lissu: Sasa unasemaje kuhusu hizi habari za Bwana Jela kuwa sijakutambulisha kwake?
Wakili Maduhu: Hizo ni kauli za bure kabisa. Mimi silazimiki kufanya hivyo. Nina miaka 6 ya uwakili kwa sasa huo utaratibu haupo kabisa.
Mhe. Lissu: Nenda Ukurasa wa 41 hadi 43 wa proceedings za Kisutu. Soma Tar. 16/06 sema kama mahakama ya Kisutu haikuandika malalamiko yangu kuhusu mawakili wangu kunyimwa kuniona.
Wakili Maduhu: Ni kweli malalamiko yapo.
Mhe. Lissu: Ni kwamba nilikuwa nazuiwa kuonana na mawakili wangu?
Wakili Maduhu: Kweli yapo hapa
Mhe.Lissu: Kwamba ni kinyume na kanuni za uendeshaji wa magereza?
Wakili Maduhu: Ni sahihi kabisa yapo yote kwenye hizi kurasa za mambo ya Kisutu.
Mhe. Lissu: Pia kuna malalamiko specific kuwa kitendo hicho cha mimi kuninyima nisionane na mawakili wangu ni kinyume na sheria na kanuni za kimataifa?
Wakili Maduhu: Ni sahihi kabisa.
Mhe. Lissu: Nikalalamika kuwa naishi na wafungwa waliohukumiwa kifo? Na natendewa sawa na watu hao?
Wakili Maduhu: Kweli kabisa ulisema.
Mhe. Lissu: Baada ya hayo nilisema nitajiwakilisha mwenyewe kwasababu sitaki mawakili wangu waje kulaumiwa bure?
Wakili Maduhu: Ni kweli ulisema hivyo na ikawa hivyo.
Mhe. Lissu: Ulipoamua kujiwakilisha mwenyewe nilisema waendelee kunisahuri na kunipa nyaraka wakati kesi inaendelea. Nilisema hivyo?
Wakili Maduhu: Ni kweli kabisa.
Mhe. Lissu: Sasa waeleze toka siku hiyo tar. 16/05/2026 hadi leo mmeendelea kunipa ushauri wa kisheria na kunipa nyaraka Gerezani?
Wakili Maduhu: Ni kweli tumeendelea kufanya kazi hiyo.
Mhe. Lissu: Je una kumbukumbu za kilichotokea Mahakama Kuu kuhusu shauri hilo lilipofika Mahakama kuu niliwaeleza waheshimiwa majaji kuwa nina mawakili wanaonisaidia kwa research na ushauri.
Wakili Maduhu: Ni sahihi ulisema.
Mhe. Lissu: Naomba nimuonyeshe proceedings za Mahakama Kuu. Tuambie from page 4 to 6 wambie majaji kama huo mwenendo unaonesha niliwaambia Majaji wa Mahakama kuu nina mawakili ambao wananisaidia na nikaomba waingizwe kwenye corum.
Wakili Maduhu: Nimeona ndio.
Mhe. Lissu: Na Katuga alipinga ombi langu hilo.
Wakili Maduhu: Ni sahihi naona hapa.
Mhe. Lissu: Mahakama ikasema hatutawaingiza kwenye corum lakini mawakili wako waendelee kukusaidia?
Wakili Maduhu: Naona iko hapa.
Mhe. Lissu: Kwahiyo ni kweli sio tu Kisutu hata Mahakama kuu hii inakutambua wewe na wenzako kama mawakili wangu?
Wakili Maduhu: Ni kweli kabisa.
Part 3 itaendelea kwenye post inayofuata
Naomba nisaidie kushare ujumbe uende mbali.
#UPDATES_KESI_YA_MAWAKILI_WA_MHE_LISSU_DHIDI_YA_MKUU_WA_MAGEREZA
Part 4
Anaendelea Mhe. Lissu
Mhe. Lissu: Twende Annexure SUPP 6 angalia Tarehe 12/12/2025 mtu wa pili ameandikwa Paul Emanuel Kilasa Kisabo na yeye alikuja kuniona na akaruhusiwa?
Wakili Maduhu: Sahihi kabisa.
Mhe. Lissu: Kwa Mawakili wangu aliyekatazwa kuja kuniona ni wewe peke yako?
Wakili Maduhu: Ni sahihi.
Mhe. Lissu: Sasa tuje kwenye sababu za kukukatalia wewe kuja kuniona. Soma Annexure SUPP 3 entry ya Tar. 28/10/2025 je siku hiyo ulikwenda Gereza la Ukonga na Wakili mwenzako Gaston Garubindi?
Wakili Maduhu: Ni kweli
Mhe. Lissu: Nenda kwenye SUPP 1 ile orodha na wambie majaji kama Gaston Garubindi yupo kwenye hiyo orodha?
Wakili Maduhu: Jina lake ni namba 3.
Mhe. Lissu: sasa angalia hiyo nyaraka sawasawa imeandika mambo mengi kule mwisho kuna maoni ya OC ni officer in charge yaani BWANA JELA.
Ameandika maoni yake kuwa aruhusiwe kumuona ambae yupo kwenye orodha ya mawakili. Na huyo mwingine asiruhusiwe kwasababu hayupo kwenye hiyo orodha.
Wakili Maduhu: Niliambiwa toka hapa haupo kwenye orodha.
Mhe. Lissu: Je kuna Wakili mwingine ameandikiwa maoni ya namna hiyo kwenye orodha ya mawakili wangu kuwa asinione hayupo kwenye majina niliyompa Bwana Jela?
Wakili Maduhu: Hakuna wakili mwingine.
Mhe. Lissu: Je kuna utaratibu wa kisheria kuhusu mambo haya?
Wakili Maduhu: nimekutana nao ukonga. Haujawahi kuwepo.
Mhe. Lissu: Kwani wewe una makosa gani ya Bwana Jela wa Ukonga?
Wakili Maduhu: Sifahamiani nae sijui nilichomkosea.
Mhe. Lissu: Wakati umeruhusiwa kuja kuniona Juma Mwaibako ndio alikuwa anakaimu ukuu wa gereza?
Wakili Maduhu: Ndio
Mhe. Lissu: Huyu aliyekuzuia ni Andrew Shabani ndio aliyekuzuia?
Wakili Maduhu: Sahihi kabisa.
Mhe. Lissu: Wewe una tatizo la ngozi? Albinism?
Wakili Maduhu: Sahihi.
Mhe. Lissu: Kwenye hili Taifa kuna ubaguzi wa watu wenye albinism?
Wakili Maduhu: Sahihi kabisa.
Mhe. Lissu: Sasa Wakili aliyezuiwa ni wewe mwenye albinism?
Wakili Maduhu: Ni mimi peke yangu ndio nimekataliwa by implication.
Mhe. Lissu: ulipenda uwe albino?
Wakili Maduhu: Sikupenda. Ila ndio nimebaguliwa hivyo.
Mhe. Lissu: Nilisema naomba samahani.
Shahidi ametoa machozi na kuumia sana juu ya vitendo hivi. Watu wameumia sana hapa Mahakamani wanaofuatilia kesi hii. Matendo haya ni ya kinyama sana.🥹
Mhe. Lissu: Niliandika orodha ya pili na kuwaongeza wewe na Kisabo kwenye hiyo orodha ya pili. Niliwaongeza wewe na Kisabo na hatimaye Kisabo akaanza kuruhusiwa na wewe ukaendelea kuzuiwa kuingia.
Wakili Maduhu: Ni kweli.
Mhe. Lissu: Nikaandika orodha nyingine na kuwaongeza Wakili Deogratias Mahinyila, Dickson Matata na mawakili wengine kwenye hiyo orodha ya pili.
Wakili Maduhu: Ni sahihi kabisa.
Mhe. Lissu: Anayetunza hizo nyaraka ni Mjibu maombi wa tatu ambae ni Bwana Jela?
Wakili Maduhu: Sahihi kabisa.
Mhe. Lissu: Waeleze Majaji kama mawakili ambao hawapo kwenye hiyo orodha na wameruhusiwa kuja kuniona.
Neema Saruni
Denis Luwis
Nyaronyo Kichere
Unafahamu kama wameruhusiwa kuja kuniona na hawapo kwenye orodha ya mawakili waliokuja kunitembelea.
Wakili Maduhu: Nafahamu ndio.
Mhe. Lissu: Waeleze Majaji kama ni kweli au si kweli kwamba mara ya kwanza mlipokuja kuniona hatukuonana ana kwa ana bali mlipelekwa kwenye chumba chenye ukuta wa kioo?
Wakili Maduhu: Ni sahihi.
Mhe. Lissu: Kwahiyo msingeweza kunipa mkono mkasema Mwenyekiti Pole?
Wakili Maduhu: Sahihi kabisa.
Mhe. Lissu: Na namna pekee ya mawasiliano kwa siku hiyo ilikuwa ni simu upande wenu na upande wangu?
Wakili Maduhu: Sahihi kabisa.
Part 5 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_MAWAKILI_WA_MHE_LISSU_DHIDI_YA_MKUU_WA_MAGEREZA
Part 1
Maombi haya yanasikilizwa na jopo la majaji watatu ambao ni Mh. A. Mruma, Dr. A. Rumisha na Dr. E. Longopa.
Kiongozi wa Jopo hili ni Mheshimiwa A. Mruma.
Nawaona waleta maombi wote wapo. Lakini pia Mawakili wao wapo ambapo jopo la mawakili wao linaongozwa na Wakili John Seka, akisaidiwa na Edson Kilatu na Selemani Matauka.
Lakini pia Chama cha Mawakili Tanganyika kinawakilishwa na Wakili Emmanuel Ukashu.
Namuona Mkuu wa Gereza la Ukonga tayari ameshaingia hapa Mahakamani amekaa nyuma ya mawakili pale. Ni Dingi mmoja mrefu, mweusi amevaa Kaunda Suti na kitambi kile cha maaskari wa magereza.
Maandalizi ya majaji kuingia yamechukua muda mrefu sana.
Wanaingia sasa imepigwa High Courtttttttttt.
Mhe. Lissu hajaingia bado.
Majaji ni kama wanashangaa, mbona Lissu hayupo maana hawamuoni kizimbani.
Anatoka karani kwenda kuwatafuta magereza kwasababu hawapo kabisa hapa Mahakamani.
Wameanza kuingia maaskari magereza wa kutosha. Wanajipanga, muda sio mrefu ataingia Mwenyekiti. Tunamsubiri.
Ameshaingia akiwa na na Kombati yake ya Kaki na mifuko yake iliyobeba nyaraka zake, anazitoa taratibu pale anaweka mezani na majaji wanateta.
Anasimama Wakili wa Serikali baada ya jalada kusomwa hapa.
Naitwa Stanley Kalokola, Wakili wa Serikali nitasaidiwa na Francis Wisdom. Mjibu maombi wa nne yupo mbele ya Mahakama yenu na interested party TLS wapo.
Tuko tayari kuendelea na zoezi la DODOSO kwa siku ya leo.
Wamehojiwa waleta maombi na pande zingine wote wako tayari.
Mhe. Jaji Mruma anasema sasa 4th Respondent usikae kwenye kizimba ukae huku kawaida maana hii ni kesi ya Kikatiba.
Mhe. Lissu amesema naomba nikae hapa hapa maana nina meza na nitakaa vizuri nikiwa hapa.
Jaji Mruma akasema hakuna shida kaaa hapo hapo.
Basi ameitwa mleta maombi wakwanza Maduhu William aanze kuulizwa maswali ya Dodoso na Mhe. Lissu.
Jaji anasema ni vema ukaapa kwanza. Wewe ni afisa wa Mahakama unajua kuapa haya apa sasa.
Wakili Maduhu: Nina miaka 36 ya kuzaliwa. Mkristu, na anaaapa hapa tena.
Jaji: Bwana Tundu Lissu karibu.
Mhe. Lissu: shaidi naomba nikuulize maswali kuhusu kiapo ulicholeta mahakamani na kesi uliyoileta Mahakamani dhidi ya sisi walalamikiwa wanne.
Waeleze majaji kama hapo ulipo una nakala ya hati ya madai na kiapo chako.
Wakili Maduhu: Vyote ninavyo hapa.
Mhe. Lissu: Je una nakala ya hati ya viapo kinzani yaani counter affidavit za walalamikiwa wakwanza hadi wanne pamoja na interested party.
Wakili Maduhu: Ninazo hizo nyaraka zote.
Mhe. Lissu: Tuanze na hati yenu ya madai na kiapo chako katika aya ya kwanza ya originating summons na aya ya pili ya kiapo chako.
Angalia Je kwenye hizo aya umesema wewe ni mmojawapo wa mawakili wangu katika kesi ya jinai iliyopo katika mahakama hii. Umesema wewe na wenzako ni mawakili pia wa kesi yangu iliyopo kisutu.
Wakili Maduhu: Ni kweli
Mhe. Lissu: Naomba uangalie aya ya nne ya hati ya kiapo kinzani ya wajibu maombi wa kwanza hadi watatu na hicho kiapo kilitolewa na Andrew Shaban kilitolewa Tarehe 09/04.
Huyu Andrew anasema wewe hujawahi kutambulishwa kwake kuwa ni mmoja wa Mawakili wangu.
Wakili Maduhu: Ni kweli huyu Andrew amesema mimi sio Wakili wako.
Mhe. Lissu: Ni kweli au si kweli hii kesi iliyopo Mahakama Kuu ilianzia Mahakama ya kisutu ambako ilikuwa ni (P.I)
Wakili Maduhu: Ni kweli.
Mhe.Lissu: Na hiyo kesi ilikuwa mbele ya Kiswaga pale Kisutu?
Wakili Maduhu: sahihi.
Mhe. Lissu: Angalia majibu yangu kwenye hili shauri lenu, kwenye majibu yangu kuna viambatanisho kadhaa. Angalia annexure A2N24R umekiona?
Wakili Maduhu: Nimekiona.
Mhe. Lissu: Nenda Ukurasa wa 19 wa hizo proceedings angalia waliokuwepo Mahakamani tar. 06/05 angalia corum kuhusu mtuhumiwa. Je jina la Maduhu lipo?
Wakili Maduhu: Ni kweli lipo.
Part 2 itaendelea kwenye post inayofuata.
#UPDATES_KESI_YA_MAWAKILI_WA_MHE_LISSU_DHIDI_YA_MKUU_WA_MAGEREZA
Part 1
Maombi haya yanasikilizwa na jopo la majaji watatu ambao ni Mh. A. Mruma, Dr. A. Rumisha na Dr. E. Longopa.
Kiongozi wa Jopo hili ni Mheshimiwa A. Mruma.
Nawaona waleta maombi wote wapo. Lakini pia Mawakili wao wapo ambapo jopo la mawakili wao linaongozwa na Wakili John Seka, akisaidiwa na Edson Kilatu na Selemani Matauka.
Lakini pia Chama cha Mawakili Tanganyika kinawakilishwa na Wakili Emmanuel Ukashu.
Namuona Mkuu wa Gereza la Ukonga tayari ameshaingia hapa Mahakamani amekaa nyuma ya mawakili pale. Ni Dingi mmoja mrefu, mweusi amevaa Kaunda Suti na kitambi kile cha maaskari wa magereza.
Maandalizi ya majaji kuingia yamechukua muda mrefu sana.
Wanaingia sasa imepigwa High Courtttttttttt.
Mhe. Lissu hajaingia bado.
Majaji ni kama wanashangaa, mbona Lissu hayupo maana hawamuoni kizimbani.
Anatoka karani kwenda kuwatafuta magereza kwasababu hawapo kabisa hapa Mahakamani.
Wameanza kuingia maaskari magereza wa kutosha. Wanajipanga, muda sio mrefu ataingia Mwenyekiti. Tunamsubiri.
Ameshaingia akiwa na na Kombati yake ya Kaki na mifuko yake iliyobeba nyaraka zake, anazitoa taratibu pale anaweka mezani na majaji wanateta.
Anasimama Wakili wa Serikali baada ya jalada kusomwa hapa.
Naitwa Stanley Kalokola, Wakili wa Serikali nitasaidiwa na Francis Wisdom. Mjibu maombi wa nne yupo mbele ya Mahakama yenu na interested party TLS wapo.
Tuko tayari kuendelea na zoezi la DODOSO kwa siku ya leo.
Wamehojiwa waleta maombi na pande zingine wote wako tayari.
Mhe. Jaji Mruma anasema sasa 4th Respondent usikae kwenye kizimba ukae huku kawaida maana hii ni kesi ya Kikatiba.
Mhe. Lissu amesema naomba nikae hapa hapa maana nina meza na nitakaa vizuri nikiwa hapa.
Jaji Mruma akasema hakuna shida kaaa hapo hapo.
Basi ameitwa mleta maombi wakwanza Maduhu William aanze kuulizwa maswali ya Dodoso na Mhe. Lissu.
Jaji anasema ni vema ukaapa kwanza. Wewe ni afisa wa Mahakama unajua kuapa haya apa sasa.
Wakili Maduhu: Nina miaka 36 ya kuzaliwa. Mkristu, na anaaapa hapa tena.
Jaji: Bwana Tundu Lissu karibu.
Mhe. Lissu: shaidi naomba nikuulize maswali kuhusu kiapo ulicholeta mahakamani na kesi uliyoileta Mahakamani dhidi ya sisi walalamikiwa wanne.
Waeleze majaji kama hapo ulipo una nakala ya hati ya madai na kiapo chako.
Wakili Maduhu: Vyote ninavyo hapa.
Mhe. Lissu: Je una nakala ya hati ya viapo kinzani yaani counter affidavit za walalamikiwa wakwanza hadi wanne pamoja na interested party.
Wakili Maduhu: Ninazo hizo nyaraka zote.
Mhe. Lissu: Tuanze na hati yenu ya madai na kiapo chako katika aya ya kwanza ya originating summons na aya ya pili ya kiapo chako.
Angalia Je kwenye hizo aya umesema wewe ni mmojawapo wa mawakili wangu katika kesi ya jinai iliyopo katika mahakama hii. Umesema wewe na wenzako ni mawakili pia wa kesi yangu iliyopo kisutu.
Wakili Maduhu: Ni kweli
Mhe. Lissu: Naomba uangalie aya ya nne ya hati ya kiapo kinzani ya wajibu maombi wa kwanza hadi watatu na hicho kiapo kilitolewa na Andrew Shaban kilitolewa Tarehe 09/04.
Huyu Andrew anasema wewe hujawahi kutambulishwa kwake kuwa ni mmoja wa Mawakili wangu.
Wakili Maduhu: Ni kweli huyu Andrew amesema mimi sio Wakili wako.
Mhe. Lissu: Ni kweli au si kweli hii kesi iliyopo Mahakama Kuu ilianzia Mahakama ya kisutu ambako ilikuwa ni (P.I)
Wakili Maduhu: Ni kweli.
Mhe.Lissu: Na hiyo kesi ilikuwa mbele ya Kiswaga pale Kisutu?
Wakili Maduhu: sahihi.
Mhe. Lissu: Angalia majibu yangu kwenye hili shauri lenu, kwenye majibu yangu kuna viambatanisho kadhaa. Angalia annexure A2N24R umekiona?
Wakili Maduhu: Nimekiona.
Mhe. Lissu: Nenda Ukurasa wa 19 wa hizo proceedings angalia waliokuwepo Mahakamani tar. 06/05 angalia corum kuhusu mtuhumiwa. Je jina la Maduhu lipo?
Wakili Maduhu: Ni kweli lipo.
Part 2 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba nisaidie kushare ujumbe uende mbali.
Miaka 2 iliyopita nilitoka jela. Mwaka jana nikanusurika jaribio la kuuawa na kuporwa pesa kadhaa.
Kitu pekee naweza kuwaambia ndugu zangu maisha yamenifundisha kuwa unaweza kupoteza kila kitu, lakini ukibaki na pumzi bado una nafasi ya kuanza upya.
Happy Birthday to me 🎊
1+
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 227
Anasimama Wakili wa Serikali Mrema
Anasema naomba kuongeza kidogo kwenye mawasilisho yaliyofanywa na Wakili mkuu wa Serikali Katuga, naomba kuongeza yafuatayo.
Waheshimiwa Majaji hii obligation inayowasilishwa mbele ya mahakama ya rufani lazima iwe na uwezo wa kuondoa shauri hilo lililoko mbele ya Mahakama hii, nikirejea shauri alilolilejea, shauri la DPP dhidi ya Mohammed Ussi naomba kuialika Mahakama hii kwenye kifungu cha 5 kifungu kidogo cha 2.
Mleta maombi amefanya reference kwa kifungu ambacho kimepitwa na wakati it's not applicable.
Kifungu hiki kukihusianisha na kesi ya Mohammed Ussi na kukileta kwenye Sheria ya sasa it's not applicable.
Kifungu cha 8 kinazungumzia mashauri ya madai, swali la kujiuliza ni je shauri hili ni la madai.
Jaji anawasha kipaza anauliza. Katuga ulisema Mrema anaongezea sasa mbona anarudia yaleyale.
Watu wanacheka😂😂😂😂😂
Jaji anamwambia Mrema aendelee ila asirudie mambo ambayo tayari Katuga ameongea.
Mrema anasimama anasema waheshimiwa Majaji ni hayo tu.
Watu wanacheka maana ni kama alichosema Jaji kimemto kabisa Mrema kwenye mood.😂😂😂😂
Anasimama Mhe. Lissu
Waheshimiwa Majaji naomba mniruhusu nijibu hoja za waleta moambi.
Wanacholalamikia siyo order wanalalakikia findings.
Waheshimiwa Majaji wanacholalamikia wamekileta wenyewe kwenye hati yao ya maombi hicho kiko kati ya ukurasa wa 428-431 wanalalamikia rulling, uamuzi.
Uamuzi wanaoulalamikia unajadili ushaidi wanaotaka kuuingiza, na Mahakama ikajadili ushaidi huo kwamba ni kinyume na Sheria hautaingizwa.
Kama wasingekuwa wanalalamikia hii ruling wasingeileta mbele ya Mahakama yako. Finding is not similar to a decision.
Waheshimiwa tuasume Mawakili hawa wako sahihi finding is similar to decision, tuangalie Mahakama inasema nini juu ya aina hii ya ushaidi, Mahakama ikasema ni kinyume na Sheria hauruhusiwi kuingia.
Mawakili waleta maombi wameleta kesi muhimu sana kesi ya Peter Michael Madeleka, kuna mahali katika kesi hiyo ambako Mawakili wa Serikali wamepakimbia kama ukoma, ukurasa wa 9 Mahakama ilisema hivi kuhusiana na hicho kifungu hayampi mamlaka ya kuimove Mahakama.
Mhe. Lissu anawambia Mawakili wa Serikali ahsanteni sana kwa kuleta kesi ya Madeleka.
Watu wanacheka 😂😂😂😂 maana akina Katuga wameleta kesi ambayo badala ya kuwasaidia kumkandamiza Mhe. Lissu yenyewe ndo imekuwa msaada kwa Mhe. Lissu.
Anaendelea Mhe. Lissu
Mamlaka ya Mahakama ya rufani kuitisha Suo moto ni mamlaka yake yenyewe haiwezi kuwa moved na waleta maombi.
Kama Mahakama haijaiona yenyewe haiwezi kuletewa maombi.
Wanasema nisiwafundishe lakini mkiangalia record waliandika barua, walileta maombi kisha wakaandika barua wanataka kuimove Mahakama.
Katuga amesema maombi yao wameyaleta under 6.3, Waheshimiwa Majaji nawaomba muangalie maombi hayo kama kuna sehemu wametaja kifungu hicho. In their notice of motion hakuna sehemu wametaja ni 6 ipi kati ya vifungu 6 vya Sheria hiyo hawawezi kuja hapa kuzungumza kitu tofauti na maombi yanavyozungumza.
Nirudi kwenye hoja ya Job Mrema, mmealikwa Majaji kukubaliana na hoja kwamba Sheria imeshabadilika ni vifungu tofauti, Waheshimiwa Majaji mimi nina revised Act of 2023 inasema section 5 haina marekebisho ya kabla ya 2023 kwa hiyo hii hoja ya kwamba kuna Sheria imebadilika ni vitu tofauti ni hoja ambayo nachelea kusema haina mashiko.
Waheshimiwa Majaji wakili ametaja rule 48.1,
Waheshimiwa Majaji inazungumzia PO must have a capacity to dispose of application na kwa maana hiyo anasema pingamizi langu halina uwezo wa kumaliza madai,
Je kwenye hoja ya kwangu hii kwamba maombi haya hauruhusiwi kwasababu hayana uwezo wa kuyafuta maombi kama inasema imeletwa chini ya kifungu cha 8.2.d? hakuna hoja hapo.
Part 228 itaendelea kwenye post inayofuata
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Leo July 3, 2026
Last time kwenye ya Uhaini dhidi ya Mhe. Lissu tuliishia part 224 so leo tunaendelea na -;
Part 225
Mheshimiwa Tundu Lissu anaingia ndani ya chumba cha mahakama, ukumbi namba 01 wa Mahakama Kuu.
Anaonekana mwenye tabasamu na furaha usoni kwake kama ilivyo siku zote.
Upande wa Jamhuri wapo kama kawaida yao
Inapigwa Court…..
Jopo la Majaji watatu wanaingia,
Kesi inatajwa
Anasimama Wakili wa Serikali anajitambulisha jina lake Ajuaye kisha anatambulisha Mawakili wenzake.
Jaji anaamuliza Mhe. Lissu kama yupo tayari
Mhe. Lissu anasema yuko tayari kuendelea.
Kama kawaida yao anasimama Wakili wa Serikali Katuga kuweka pingamizi.
Mhe. Lissu anapendekeza maombi yake ya sikilizwe kwanza ndo pingamizi lao lijibiwe.
Majaji wanasema tuanze kwanza kusikiliza PO, kisha taratibu nyingine zitafuata.
Anaanza Mhe. Lissu Waheshimiwa Majaji kesi hii inatokana na maombi namba 19065 ya mwaka 2025, Juu ya maombi ya kuongeza ushahidi katika muendelezo wa kesi, uamuzi wa tarehe 24 February 2026 wa Mahakama Kuu wa kukataa kuingizwa kwa ushahidi mpya.
Waheshimiwa Majaji uamuzi wa February 24, 2026 ni uamuzi mdogo, uamuzi ambao haujamaliza shauri na kwa mantiki hiyo kisheria kabisa haupaswi kukatiwa rufaa au pingamizi.
Waheshimiwa Majaji wa rufaa, Mahakama hii katika kesi ya Mkurugenzi wa Mashitaka dhidi ya Mohammed Mussa Ussi criminal appeal namba 521 ya mwaka 2023 Mahakama ikiwa imeketi Zanzibar ilisema msingi wa kukataza rufaa ama mrejesho (revision) ya jinai msingi wa hiyo hoja ni kifungu cha 8.2.d kutokana na marejeo ya mwaka 2023 mahakama hii ilisema uamuzi huo hauwezi kukatiwa rufaa kwani ni uamuzi usiomaliza shauri.
Anaendelea Mhe.Lissu
Kesi ambazo nimeziwasilisha mbele yenu waheshimiwa Majaji zinazungumzia uamuzi mdogo ni wa aina gani na uamuzi unaoweza kutolewa kama uamuzi wa mwisho unaoweza kuombewa revision ni wa aina gani.
Uamuzi unaomaliza kesi na kunyima haki za wadaawa ndiyo unaopaswa kukatiwa rufaa, uamuzi unaokuwa treated as the final order ndiyo unaomaliza haki za msingi za wadaawa lakini kama uamuzi haufanyi hivyo hauwezi kukatiwa rufaa.
Sasa waheshimiwa Majaji baada ya kuwapitisha kwenye kesi hizo nirudi kwenye hoja yangu ya msingi je uamuzi wa February 24 mwaka huu ulimaliza kesi hii?
Kama ni hivo ulimaliza kesi hii na kwamba Sasa hivi sina kesi ya uhaini basi hoja yangu haina msingi na maombi haya hayawezi kusikilizwa.
Hoja yangu waheshimiwa Majaji ni kwamba uamuzi wa Mahakama Kuu wa February 24, 2026 haukumaliza kesi namba 19065/2025 na kwasababu haukumaliza maombi haya ya revision yanakatazwa kuletwa Mahakama ya Rufaa.
Anaendelea Mhe.Lissu
Waheshimiwa Majaji uamuzi huo unasema nini, ili tujue kama ulimaliza kesi lazima tuusome huo uamuzi unasema nini.?
Rulling yenyewe iko ukurasa wa 405-432, kwenye ukurasa wa 431 paragraph ya mwisho waheshimiwa Majaji mtaona Mahakama ilichokiamua.
Kilichokataliwa kupokelewa na Mahakama ni notice of additional substance of evidence, Mahakama Kuu haikusema kesi haitaendelea. Mahakama kuu ilitoa Mwongozo haikutoa uamuzi wa mwisho wa kesi, uamuzi wao ulikataa subodinate issue.
Waheshimiwa Majaji ushaidi mwingine huko kwenye maombi yenyewe yaliyoletwa. Mahakama inasema ilijadili na kukataa notice yao ya kuongeza ushahidi haisemi kesi ilifia hapo kutokana na uamuzi huo.
Mahakama imekata notice of additional substance of evidence, kwahiyo wanalalamikia uamuzi wa notice kukataliwa.
Jambo la pili ni Je mleta maombi anayo mamlaka ya kuiambia Mahakama itumie mamlaka yake ya kupitia kumbukumbu ili kuridhisha matakwa yake mwenyewe?
Jibu ni hapana hiyo siyo haki yao kisheria kwani wajibu wa kuangalia record ni wa mamlaka yenyewe.
Part 226 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 226
Anaendelea Mhe. Lissu.
Waheshimiwa Majaji uamuzi uliotolewa na Mahakama ya rufani katika kesi ya Katibu Mkuu wa CHADEMA na bodi ya wadhamini wa CHADEMA vs Saidi Issa Mohammed na wenzake inasema kwamba kama mdaawa (Mleta maombi) analeta maombi mwenyewe ni yale yaliyoko kifungu cha 6 kifungu kidogo cha e, maombi mengine ni Mahakama yenyewe ndiyo inaamua bila kusukumwa na yeyote au kuletewa maombi yenye hati ya kiapo.
Waheshimiwa Majaji kwa vyovyote vile maombi hayo hayako halali mbele ya mahakama hii kwani hayakuletwa katika utaratibu wa kisheria kwani Mahakama hii haijaamua maombi haya yaje yenyewe Suo moto kwa hiyo Mahakama isikubali kusikiliza maombi hayo kwasababu ambazo nimezisema.
Anaendelea Mhe. Lissu
Sasa waheshimiwa Majaji sijui kama mnaniruhusi niendelee au wajibu kwanza.
Jaji anasema Jamhuri wajibu kwanza PO kisha tutaendelea.
Anasimama Wakili Katuga anasema Waheshimiwa Majaji tukirejea mapingamizi yake ya awali yameletwa chini ya kifunga cha 8.2.d hiki ni kifungu mahususi kwa mashauri ya madai.
kifungu hiki kilikopwa kikatumika kwenye madai kwenye mashauri ya rufaa, hata kama Mahakama yenu tukufu kwa rejea hizo za Mahakama hii ikakikopa kitumike kwenye maombi yetu haya bado tunasema kwamba maombi yetu yako sahihi mbele ya mahakama hii tukufu tofauti na kile ambacho mjibu maombi amekileta kama pingamizi la awali.
Maombi yetu yameletwa chini ya kifungu cha 6 specifically kifungu kidogo cha 3 cha Sheria ya mamlaka ya Mahakama. Kanuni ya 65 na kanuni ya 45 ya kanuni za Mahakama ya Rufani inasuport maombi yetu.
Anaendelea Wakili wa Serikali Katuga
Waheshimiwa Majaji ukiyasoma maombi yetu kwenye notice of motion hakuna sehemu yeyote tunayoiomba Mahakama hii tukufu ipitie order ya Mahakama au uamuzi wa Mahakama, pale mwisho tunasema Mahakama idiscuss kukataa ushahidi hatujazungumzia kukataa notice, sisi tunazungumzia kuuchambua na kuukataa ushahidi.
Hakuna sehemu kwenye maombi haya tunalalamikia order, Mahakama yenu itaona kwamba pingamizi la mjibu maombi limekuwa mislead hakuconsue sawasawa maombi yetu.
Pale ambapo neno or litatumika kwenye Sheria yeyote maana yake maneno haya hayako similar yanatumika tofauti, Waheshimiwa Majaji nimewarejesha humu muweze kukitafsiri kifungu cha sita. Haya maneno yanatakiwa yatafisiriwe tofauti hayaendi pamoja ama hayategemeani, inaweza kuwa kimoja wapo kati ya haya.
Kama mahakama yenu imekikopa kifungu cha 8.2.d kinazungumzia katazo la decision or order ndo hauwezi kuziombea appeal or revision.
Sasa tunapata wapi nguvu za kuleta pingamizi kwa tafsiri hiyo tunaiomba Mahakama hii ikaangalie maana ya maneno haya.
Waheshimiwa nawarejesha kwenye kamusi kwa sababu nayo ni kati ya vitu vinavyopaswa kutumika kutafsiri Sheria. Katika ukurasa wa 129 kamusi inadefine order ni nini?
Kwenye application yetu hakuna sehemu tumeombea decision or order, kwenye kifungu cha 8 hata kama kimekopwa hakiwezi kucocer maombi yetu.
Mahakama yenu ilishawahi kuiamulia hili kwenye kifungu 394 cha CPA, katika kesi ya Peter Michael Madeleka dhidi ya jamhuri.
Kutaja kitu fulani means exclusion ya kitu kingine, kitendo cha kifungu cha 8 kutaja findings and order means haijatuzuia kwa maana hiyo findings hapa haijazuiwa kwa maana hiyo tunachotaka kuiambia Mahakama yako ni kwamba ule ushahidi ulikataliwa kabla ya wakati wake.
Anaendelea Wakili wa Serikali Katuga
Waheshimiwa naomba niishie hapo kwenye hilo ili tusiende mbali kwa kuyasema hayo mtaona kwamba kesi ambazo mshitakiwa amewapitisha ni distinguishable kwenye mazingira yetu.
Hii kauli ya kwamba hatuna mamlaka ya kuomba Mahakama iitishe ‘Suo moto’ sisi tunasema mamlaka tunayo.
Katiba anasema naomba Mrema anisaidie anayo nyongeza.
Anasimama Wakili wa Serikali huyu anaitwa Job Mrema anakipara kama Mrema wa ubwabwani, sijui na yeye huwa anakunywa visungura kama mwenzake, anyway
Part 227 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
🚨‼️HUYU NDO MKE WA AWADHI JUMA HAJI, ALIYETOA ORDER YA ‘SHOOT TO KILL’ OCTOBER 29‼️
Jina lake anaitwa Eliza Joseph, huko mitaa ya Facebook anajiita Ellyzer Joseph
Eliza amesoma shule ya Tarakea High School.
Hapo awali Eliza alikuwa Askari wa usalama barabarani ila baada ya kuolewa na Awadhi alimuhamisha huko kwenye uTraffic na kumfanya kuwa Polisi wa kawaida ambapo kituo chake cha kazi ni Oysterbay Polisi.
Eliza na Awadhi wanamtoto wa kike anaitwa Tiffa, wanaishi maeneo ya UNUNIO, Jiji Dar es Salam
Namba yake ya simu ya Eliza ni +25565230655x
Mkimuona huko njiani basi mjue ni mme wake ndo alitumika kutoa order ya kuuwa Watanganyika wenzetu Oktoba 29.
SPAIN Away Jersey 🔥🙌
Naomba RT Yako🙏
Available, Player Version
PRICE: 30000
CONTACT: ☎️ 0682123872
LOCATION: Kkoo Mchikichi Na Manyema
DELIVERY: Ndani Ya Nchi Na Nje Ya Nchi
SIZE: M,L,XL,2XL
Bonyeza Link👇 Uje Direct WhatsApp
https://t.co/oJuwLwxb57
Mama Anna Makinda Spika Mstaafu wa awamu zilizopita amenukuliwa akisema
Katika Bunge aliloongoza alipata kuwa na wabunge wenye akili kupita kiasi,
Akatolea Mfano wa baadhi ya Kanuni walizokuwa wanapitisha Lakin kuna Sehemu wanakwama, na waliowengi wa CCM walikuwa wanataka zipite Hivo Hivo Ila yeye akawa anasema tumsikilize @TunduALissu anasemaje, na alikuwa akitatua mkwamo Mara nyingi akasema “niliwaambia Hakikisha mnapomsikiliza lissu si kuhojiana na anachosema bali kubalianeni naye Kwakuwa kila mkitaka kumuhoji zaidi ndipo tunajichanganya”
Ameeleza na pia akisisitiza siasa si uadui