Hata kama mwanaume ni mvutaji hatotaka kuoa mwanamke mvutaji
Hata kama mwanaume ni mlevi hatotaka kuoa mwanamke mlevi
Sasa dada endelea kudanganywa wanawake wote wa kaskazini lazima wavute na kunywa
Kuna yule dogo wa Kigoma aliyesema anataka kusoma lugha Kiingereza, Kifaransa na Kiarabu, kuna mahali alisema shuleni kwao hakuna waalimu wa kutosha ila ukiangalia upande mwingine wa Comedy au Simba na Yanga kila goli ni hela kwahiyo hata kwa Serikali mwenye nacho ndo anaongezewa
Zamani tulikua tunaenda kwa jirani kuangalia TV.
Tena tulipanga mawe tupande ili tuweze kufikia dirishani tutazame japo kidogo tu.
Tunaangalia kidogo punde si punde mtoto wa mwenye nyumba anafunga dirisha
Ila Mungu ni nani
Leo na sisi tuna TV magetoni na hatuna muda wa kuangalia
Hautukuti kwenye meza za watu
wanawaongelea vibaya watu
wengine kwa sababu tunajua watu
hao hao wakikaa na watu wengine
tofauti na sisi watatusema vile vile
Jamii inayomwonesha mwanaume kuwa hastahili upendo hata kiduchu kwa sababu hana pesa,
Ndiyo hiyo hiyo jamii inayotaka mwanaume awe mwaminifu akiwa tajiri
Lakini kwani mwanaume asiye na pesa hastahili upendo? Au tusemeje sasa, kwamba mwanaume tajiri hapaswi kuwa mwaminifu??