KUJUA NA KUJITOA ENDAPO CM YAKO IKIWA IMEDUKULIWA
》 piga *#61# kama imeandikwa neno FORWARDED uje kuna mtu anasikiliza mazungumzo/sms zako. Na ikionyesha neno NOT FORWARDED basi uko salama.
》piga ##21# ili kuondoa *monitoring device* kwenye namba yako.
#wapwatuinuane
Leo IMF na Benki ya Dunia wametoa ripoti mbili muhimu sana. Nilichokiona ni kwamba, taasisi hizi mbili zimefika kwenye hitimisho moja. Dunia imebadilika, lakini Afrika bado haijabadilika kwa kasi inayotakiwa.
IMF inasema:
- Afrika sasa haishindani na Ulaya. Inashindana na Asia.
- Mapinduzi ya AI, semiconductors na data centres yanafanyika nje ya Afrika.
- Bara linakosa productivity revolution. Uchumi unakua, lakini uzalishaji wa kila mfanyakazi bado ni mdogo.
- Bei za chakula na mafuta zinaendelea kuliumiza bara kuliko maeneo mengi duniani.
- Misaada inapungua wakati mahitaji yanaongezeka.
Benki ya Dunia inasema:
- Hakuna nchi ya Afrika iliyopanda daraja la kipato mwaka huu.
- Afrika inazalisha utajiri, lakini Waafrika wengi hawaongezi kipato kwa kasi hiyo.
- Maliasili peke yake hazitoshi. Manufacturing, exports na taasisi imara ndizo zinazopandisha uchumi.
- Nchi nyingi zimekwama kwenye Lower Middle Income Trap.
- Changamoto kubwa ya Afrika siyo umasikini. Ni uzalishaji mdogo.
Kwa kifupi, taasisi hizi mbili zinasema jambo lilelile kwa lugha tofauti.
Karne iliyopita waliokuwa na maliasili walipata tija. Karne hii inawalipa wanaozalisha zaidi kwa kila mfanyakazi, wanaongeza thamani ya bidhaa zao, na wanaojenga taasisi imara.
Hapo ndipo mjadala wa kweli wa maendeleo ya Afrika unapaswa kuanzia.