Nimesoma kwa Dr Mashamba kwamba Rwanda wamebadili saa za masomo na kazi. Shule zitaanza saa 2.30 asubuhi na kumaliza saa 11 jioni. Saa za kazi ni saa 3 -saa 11. Hii ni kuwaongezea watoto muda wa kulala na kuwawezesha wazazi kunywa chai na wao kabla ya kwenda kazini. WOW!
Ukifungua biashara bongo, kodi ya frame, umeme, maji, mfanyakazi, OSHA, Leseni, Kodi TRA, mara Service levy, kama unaagiza mzigo kuna custom levy, vyote hivi on your shoulders.
Serikali yenyewe inakupa benefit au unafuu gani kwenye maisha?
Kuna siku unaamka na mzuka utaki biashara za magumashi wala wasiwasi
roho inakutuma kwenda kulipa kodi TRA
Basi hao maafisa wenyewe wa TRA sasa,kila Mmoja anakusukumia kwa mwezie (Nenda Meza ile)
Wakikuona unakiherehere sana wanakwambia MTANDAO UPO CHINI kaa pale usubiri..Daah
Kuhamisha shughuli nyingine za bandari Dodoma ni dalili ya tatizo kubwa zaidi. Ufanisi wa shughuli nyingi umeathirika sana na ofisi kuhamia Dom bila mpango thabiti (km kimtandao) wa kuhakikisha shughuli hazicheleweshwi. Km mara nyingi inabidi kusafiri hadi Dom kupata kibali tu
Only in Africa boss wako mwenye mshahara mara 10 yako ndiye anapata allowances zote, wewe mwenye uhitaji zaidi mshahara wako huo huo mdogo ndio utalipia rent,mafuta,chakula,umeme,communication na ada za watoto wako.
Mimi ningepewa Mamlaka ya kuwa mshauri au Mwamuzi wa masuala ya nchi yetu jambo la kwanza kabisa Ningefuta makampuni yote yanayoendesha michezo ya kubashiri (Betting) na kamari za aina zozote zile.
Najua nitaikosesha Serikali mapato ila nitaokoa kizazi ambacho kinaangamia vibaya.