Miaka ya nyuma kidogo nakumbuka nilimtongoza binti wa jirani yangu japo yeye alikuwa ni mkubwa kidogo kwangu akagoma na akatangaza kwa baadhi ya mashoga zake
Ikapita miezi kadhaa ndani ya huo huo mwaka akaolewa Arusha akaenda huko Arusha kwa mme wake! Imepita miaka kama 2 hivi tukapata msiba wa bibi yangu akaja kuhani
Sasa katika ile โjamani poleniโ mimi nikamjibu tu kawaida โAhsanteโ akaniuliza โmbona haunifurahii na nimetoka mbali kabisa kuja huku au hujasahau tu lile ombi lako?โ
Mimi kimkazo nikamjibu โombi lipi?โ Nikajifanya kama nimesahau ili kurahisisha mambo akanijibu โjaribu kukumbuka,ukikumbuka nijibu kabla sijaondoka tuyamalize tuache kununiana maana nimeshakuwa saivi natambua tupo kwa ajili yenu wanaumeโ
Basi bhana story yetu imeishia hapo japo mimi na yeye tushamaliza ugomvi wetu saivi tunapigiana sana simu na huwa akitoka kwa mmewe akirudi huku nyumbani kwao tunaonana tunasalimiana
Siku ya leo nmepigiwa simu asubuhi kuwa Mama yangu kafariki,
Nilikuwa siamini mpaka pale ambapo nimeambiwa nipande gari kwaajili ya kurudi nyumbani kumzika Mama yangu..
Eeh Mwenyezi Mungu naomba unipe uvumilivu,kila nikijikaza nashindwa kujizuia..๐ญ๐ญ๐ญ๐ญ