Acheni kutumia DOLA kuzimisha sauti za mageuzi. Nyakati zimebadilika sana. Mtawaumiza watu wengi sana lakini hamtofanikiwa kuwanyamazisha watu waliochoka na utawala dhalimu wa CCM. You can jail revolutionaries, but you can't jail the revolution. Muacheni huru @TanzaniaOneJezi
Rais Putin amefika UAE, pia ataenda Saudi Arabia. Putin ana hati ya Kukamatwa na kufikishwa kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Uhalifu, lakini ameweza kusafiri na kwenda nchi hizi kwa sababu nchi hizi sio wanachama wa Mahakama hiyo na hivyo hawawezi kumkamata Putin.
Uandishi wa kimkakati!
September 2023 EWURA walitangaza bei kikomo ya mafuta ya petroli ambayo ilipanda kwa zaidi ya shilingi 500 (17%) kwa kila lita moja.
Millard Ayo, ukisema mafuta yameshuka bei Disemba hii, unatakiwa utueleze, Je lita 1 tunaipata chini ya Tsh. 1,887 aliyoikuta Samia Machi 2021?
Mafuta ya Petroli yalipanda bei kwa Tsh. 500 (17%) kwa kila lita moja baada ya miezi 3 wanapunguza Tsh. 116 na vyombo vya habari mnasherehesha?
Kuanzia Desemba 6, 2023 Dar es Salaam Petroli ni Tsh. 3,158. Dizeli Dar es Salaam itauzwa Tsh. 3,226. Hii ni bei mara mbili ya bei aliyoikuta SAMIA.
Ingelipendeza endapo mngeliwaeleza watanzania kwamba “mafuta yashuka bei kwa shilingi MIA MOJA Disemba hii” na mngelitutendea haki.
MMM, Mtikila.
IGA SIO YA WATANZANIA, NI YA WALE WALIOISAINI IKULU: WAKILI MWABUKUSI
"Tumeona wao wakiandamana hasa CCM, kwahiyo hatuoni sababu ya kutuzuia sisi kuandamana kwahiyo uamuzi unakuja tarehe 14 Disemba 2023, niwaombe Watanzania haki hizi tunazozidai sio za mtu hivyo tuungane tushikamane kwasababu kuna watu wanasema IGA imeshapita haijapita wananchi wote wameukataa ule mkataba, IGA haijaridhiwa na Watanzania, haijawahi sainiwa na Watanzania kesi yake iko mahakama ya rufani na watanzania wote tumekataa kwahiyo IGA ni ya wale waliosaini kule Ikulu na kuweka sahihi zao pale sio za Watanganyika, sisi tumekataa na sheria imekataa iko upande wetu (wananchi)", Wakili Boniface A.K. Mwabukusi.
Mchana wa leo Dicember 05,2023 Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Nyasa Mhe.@MsigwaPeter alipokuwa kwenye ziara yake Mkoani Songwe Jimbo la Momba kata ya Chitete amelazimika kutumia Mtumbwi kuvuka mto Nkana baada ya kushindwa kuvuka kwa kutumia usafiri wake wa Gari....
UTEKAJI UMERUDI TENA
Silvester Nyangi mfanyabiashara Tarime vijijini mpakani mwa kenya na Tanzania katika mpaka wa Gwitembe kata ya Nyanungu.
Alitekwa na watu walio jitambulisha kuwa ni askari wakiwa silaha za moto na kumchukua kwa nguvu, nakuondoka nae wakiwa na gari lenye namba za usajili DFPA 401, Familia imejaribu kufatilia police bila mafanikio yoyote
wakiambiwa polisi haijahusika.
Silvester alichukuliwa tangu tarehe 23/11/2023
Tunamtaka RCP wa Tarime Rorya atuambie alipo huyu bwana, kama ana makosa sheria ichukue ifuatwe katika kushughulikia makosa yake sio utekaji.
UTEKAJI UMERUDI TENA.
Charles Chacha Waitinyi Kutoka Serengeti: aliyetekwa na task force Serengeti.
Alitekwa tarehe 12 October 2023 muda wa saa 8 mchana na inasadikiwa alipelekwa Mwanza.
Pikipiki yake ilikuwa imefichwa nyuma ya kituo cha Polisi Mugumu lakini baadae ikaondolewa.
RPC Mara tunataka kujua alipo Charles, kama ana makosa utaratibu wa kisheria ufuatwe. Familia imefuangua RB NO…
MUG/RB/4313/2023
TAARIFA
@ombeni_t Front gani ambayo unasema tuje? Front hiyo utatokea? Hapa Twitter penyewe umeficha sura yako na jina lako, ukiitwa hiyo front utatokea? Jana tulikuwa Vingunguti, ulitokea?
@IAMartin_ Martin Umekua Mashuhuri sana Kutueleza madhaifu Mengi ya Serikali na namna ambavyo wamefeli Kabisaaa.
Sasa Shida ni kwamba Nyie mnalalamika tu, Kuwaondoa hawa Umoja unahitajika na Umoja huo lazima utengenezwe, Njoon front basi Mtuongoze kwa Hoja tuwaondoe hawa, Peacefully!
Reli ya Tanganyika/Reli ya kati ilikuwa na urefu wa kilomita 1,245 ikitumia geji (upana wa njia) mita 1, ilijengwa kwa miaka 9 kati ya mwaka 1905 - 1914.
Reli ya TAZARA ina urefu wa kilomita 1,860. Ujenzi ulianza mwaka 1970 hadi 1976. ilijengwa kwa miaka 6. Reli ya TAZARA ilianza kutumika mwaka 1976.
SGR - Dar es Salaam kwenda Morogoro. 300 kilometres (186 mi). Ujenzi wa mradi umeanza April 2017. Hadi kufikia leo, December 2023 ni miaka 6.
Kipande cha DSM—Morogoro (300km) hakijaanza kufanya kazi. 2,000km za mtandao wote wa SGR, serikali ya CCM inaweza kutumia miaka 60 kujenga.
Hadi Standard Gauge Railway (SGR) ikamilike chini ya utawala katili wa CCM, wengi wetu tutakuwa WAFU. Kila siku wanajaribu vichwa vya Escape from Sobibor
Mkoloni aliwezaje kutengeneza reli 1,245km kwa mikono ndani ya miaka 9 wakati CCM na wataalam wao kilometa 300 mwaka wa sita hawajamaliza?
MMM, Mtikila.
Poleni sana watu wa Hanang, poleni wananchi wa Manyara na watanzania wote waliofikwa na matatizo haya.
Tunaitaka serikali hii kutoa vifaa vyote vya uokozi, chopa zinazorushwa kusafirisha watu binafsi ndio wakati wake huu kutumika kuokoa watu wetu..
Watu wamepoteza ndugu zao, wengine wamepoteza mali zote.
Ni muhimu serikali ikatoa msaada wa dharura na haraka.
Ni muhimu pia kuwapa fidia wote waliopoteza mali zao ili waanzie maisha.
Dr. Philip Mpango kufanyiwa upasuaji wa koo, Seoul, South Korea, tafsiri yake, huduma za afya Tanzania ni mgogoro na ukithubutu kutibiwa ni kama una’beti na kifo. Kwanini watawala wanatibiwa nje ya nchi? Huduma nzuri. Hospitali za ndani ni kwa ajili ya nani? Ugua pole daktari. 🙏🏽