#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 116
Anaendele Shahidi Samuel Elibariki Kaaya
Tunafanya huu uhakiki kwasababu programu endeshi ndiyo inayoendesha hardware computer, kwa maana nyingine kama programu linzi isipokuwa compatible / isipoendana na hardware kwa maana ya compute hiyo, it cannot execute any task.
Sambamba na hilo programu chunguzi lazima iwe compatible na programu endeshi ili iweze kufanya majukum yake mahususi.
Waheshimiwa majaji hali ya programu kwa siku hiyo ya tarehe 08/04 ilikuwa timilifu kwa maana programu zilikuwa updated/zilikuwa salama kwaajili ya kufanya majukumu yake mahususi.
Waheshimiwa majaji baada ya kufanya uhakiki wa vifaa nilifanya uchunguzi wangu wa awali kwa maana ya preliminary examination.
Nilifungua computer yangu maalum kwa maana ya kuiwasha, nilichukua flash disk aina ya XIOXIA kwaajili ya kuifanyia uchunguzi.
Baada ya kufungua computer yangu niliiweka kwenye universal serial bus (USB).
Baada ya kuiweka kwenye USB niliifungua ili kutazama kilichopo ndani ya flash.
Baada ya kuifungua nilikuta ina nywila yaani passwords hivyo niliwasiliana na mamlaka iliyoleta vielelezo kwa ajili ya kupata nywila.
Baada ya kupata nywila niliendelea na uchunguzi wangu wa awali na nilikutana na video mjongeo moja ilikuwa na heading Tundu Lissu uso kwa uso na watia nia majimboni, no reforms no election njia panda.
Na hiyo Video ilikuwa na urefu wa masaa matatu na dakika 38 na ilikuwa katika mfumo wa MP4 file format.
MP4 inatokana na neno MPEG part 14 (kirefu cha MPEG ni Movable Picture Expert Group).
Huyu Bwana Samweli Elibariki Kaaya nae miongoni mwa kitu anatufurahisha hapa Mahakamani ni kujifanya anapenda vingereza fulani kutaja misamiati yake ya kitaalamu.
Sasa anakosea sana kutamka hayo maneno Mh. Lissu kuna muda anauliza mara mbili mbili kuwa umetamka nini?
Akirudia anawaambia tamkeni vizuri jamani kingereza cha wapi hicho, Nafikiri kama Taifa hili swala la kizungu ni ugonjwa mkubwa, inafaa utafutiwe dawa halafu huu ugonjwa kwa mapolisi unaweza kuwa ni mkubwa sana kuliko makundi mengine yote. πππ
Thawabu Issa: Kingine nini uliona:
Shahidi: Waheshimiwa majaji pia niliona maudhui yafuatayo:
Wanasema hivi msimamo huu unaashiria uasi ni kweli maana tutazuia uchaguzi hivyo tutahamasisha uasi na hiyo ndio namna pekee ya kuapata mabadiliko, tunakwenda kukinukisha sana sana tunaenda kuuvuruga uchaguzi huu, tunaenda kukinukisha vibaya sana.
Waheshimiwa majaji maudhui haya yanapatikana kwenye lisaa la pili na dakika 58.
Pia nilibaini mwendelezo wa matukio kwa maana ya continuity, pia nilibaini jup shoot kwa maana ya kuwa hakukuwa na kukatika kwa picha.
Nilibaini pia necessary or unnecessary movements, kulikuwa na movement za watu mbalimbali au mtu mmoja mmoja kutoka sehemu moja Kwenda sehemu nyingine.
Nilibaini pia uwepo wa rangi halisi na mwanga halisi wa picha mjongeo.
Naomba nifafanue kuhusu rangi na mwanga halisi.
Waheshimiwa majaji unaporekodi picha au picha mjongeo kuna kitu kinaitwa white balance.
White balance kazi yake ni kuseti mwanga na rangi asili ya vitu vinavyorekodiwa.
Hii white balance ina component chache kwa ajili ya kufanya hayo.
Mfano kama unarekodi wakati wa mvua utaiseti camera yako kwenye cloud setting, kama ni kwenye kivuli utaseti camera yako kwenye shadow, kama ni majira ya kawaida ya jua utaseti kamera yako kwenye day.
White balance ilituonyesha kwamba video hii ina mwanga halisi.
Waheshimiwa majaji pia nilitazama mstari mshazari na ninaomba nizungumzie hapa ili pakae sawa.
Katika mizania ya informatics object near the length of the camera is much greator than the object far from the length of the camera.
Mfano mzuri ni mtu anapojipiga selfie, sehemu ya Kichwa itakuwa ni kubwa kuliko sehemu ya miguu ambayo iko mbali na camera.
Kwa maana hiyo waheshimiwa majaji focal length is the basic attribute in this fact.
Part 117 itaendelea kwenye post inayofuata
Naomba Repost yako kwenye tweet hii.
Kama umesoma either degree/diploma na huna kazi avoid wasee disrespectful na wenye hamsaidiani. Otherwise utakula disrespect mpaka depression ikushike uanze kujichukia.