🔙🔛🔝
#FilmIsOurLife#GripGangstars#trial-After-Adjustment
@Dir_Trader
Keep your best wishes, close to your heart and watch what happens
#😎 @ Zanzibar, Tanzania https://t.co/hFablTks8m
@Shaykh_Issa 100% ndoa inakupa stara ya kimwili na akili(matamanio) ukiwa mtulivu juu ya hivyo basi rahisi kufanya ibada zoote kwa utulivu,
Ila uwe umefata misingi ya ndoa na si matamanio ya kimwili ama kufata mkumbo.
Allah atuongoze
Usiku mwingine wa Ijumaa umetanda juu ya majumba yetu. Tuwe wenye kutumia usiku huu kumswalia Mtume wa Mwenyezi Mungu, swala na salamu zimwalie, kwa pamoja kama familia. Kufanya hivyo kutasaidia kuimarisha mapenzi juu ya Mtume kwetu na kwa watu wetu wa ndani, hasa watoto.
Pupa yake Habib Umar, kwenye unadhifu ilikuwa kubwa tangu kwenye chakula mpaka vinywaji, nguo, malazi na mahali anapoishi. Na unadhifu ni sehemu ya imani, alikuwa havai nguo isipokuwa nadhifu na yenye kunukia vizuri. Na yeye mwenyewe husikii isipokuwa harufu nzuri kutoka kwake.
Na usiache wingi wa mashughuli na mishughuliko ya kutafuta maisha ikakuzuia kutafuta ilmu, na wala kukosekana kwa yule ambaye kwa dhahir atakuandaa kwa hayo kwa pale ulipo au atakupa sifa za kupata ilmu, ukimtafuta kwa dhati kama atafutae maji baridi mwenye kiu, hakika utampata.
Mimi ni mjalisi wa mwenye kunidhukuru. Na anapo-Nidhukuru mja baina ya mkusanyiko wa watu, na Mimi humdhukuru kwenye mkusanyiko ulio bora zaidi, na anapo-Nidhukuru ndani ya nafsi yake, Nami humdhukuru ndani ya nafsi Yangu. - Hadithi Qudsi.
Wadhania kuwa wewe ndio maradhi hali ya kuwa wewe ndio tiba, wakati mwengine hufikiria kuwa wewe ni kufuli hali ya kuwa wewe ndiye funguo, vipi unataka kuwa kama mwengine kwa kuwa unashindwa kutambua thamani yako! Hakika hakuna aliye bora zaidi yako, pindi ukitambua thamani yako.