@PMadeleka Wewe ulikamatwa mwenzio alishambuliwa tena eneo la mahakama ambapo ni eneo lake la kazi, wewe ulikamtwa huko vichochoroni iweje ufananishe kosa lako na unyanyasaji aliofanyiwa Mahinyila?
😀😀 Naona @azamtvtz mmefuta na kupost upya huku mkiwa mmefunga comments 🙌🏽
Huku @X mmetuacha kidogo ngoja tuongeze comments!
Msifunge comments bana sasa mtapokeaje maswali au mmeamua kumsafisha?
Nasema #TutaelewanaTu
‼️UPDATE: wamefuta kabisa post 😀‼️
Vipi bilionea haji tena?
NI ZAMU YA VYOMBO VYA HABARI..?
Waandishi wa habari nguli na maarufu wa radio na TV maarufu hapa Jijini Dar es Salaam wamefungiwa na Bodi ya ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) kutangaza au kufanya kazi ya uandishi wa Habari kwa kile kinachoitwa "kushindwa kujisajili katika bodi ya ithibati"
Mpaka naandika habari hii Wahusika na mwaajiri wao wamefanya siri kwa mujibu wa maelekezo waliyopewa na serikali kuwa "wasifanye kazi ya uandishi wa habari na wasiseme lolote kuhusu kuzuiwa kwao"
Kwa mujibu wa kifungu cha 19 cha sheria ya huduma za habari sura ya 229 kina weka masharti kuwa
"waandishi watakaoshindwa kujisajili hawataruhusiwa kufanya kazi za kihabari"
Waandishi hawa wamewekewa kikwazo hiki baada ya kuwa mwiba katika vipindi vyao na mahojiano yao kwa wakati huu nchi inapoelekea katika uchaguzi Mkuu
Uchunguzi unaonyesha Masoud Kipanya ameingia katika kifungo hiko baada ya kuchora mchoro wa katuni uliowakasirisha watawala uliolenga kutaka media zisitumike kama Toilet Paper
Mwenyekiti wa Jukwa la Wahariri Tanzania Balile aliongea na kuonyesha hadharani kukasirishwa na mchoro huo huku akiahidi Masoud Kipanya achunguzwe na mamlaka za nchi.
Masoud Kipanya na Ciza Wameshindwa kujisajili kwa sababu ya kukosa sifa ya kusomea taaluma ya uandishi wa Habari kinyume na sheria kama inavyoelekezwa katika kifungu cha 24 cha sheria ya huduma za habari sura ya 229.
Rungu la namna hii pia linaonekana kumkumba mwanahabari na Mkurugenzi wa Jambo TV, John Marwa ambaye amekuwa mwiba katika mahojiano mbalimbali na kuendesha vipindi vilivyo wakwaza watawala.
Duniani kote watu wenye uzoefu na kazi ya uandishi wa habari kwa zaidi ya miaka 10 kama Masoud Kipanya, SIZA, na John Marwa walipaswa automatically kuwa na sifa za kusajiliwa na bodi ya ithibati ya Waandishi wa Habari kwa kigezo cha uzoefu na muda waliofayia kazi tasnia ya habari.
Hawa ni baadhi ya Waandishi wa Habari wakubwa Duniani ambao hawakusomea taaluma ya uandishi wa Habari Anderson Cooper (CNN na ABC News) Stephen A. Smith (ESPN) na Trevor McDonald (ITN na ITV)
N.B
Kwa upande wa mmoja mtangazaji maaurufu wa radio na Tv kutoka ofisi hiyo hiyo, kwake maarufu kama imekuwa tofauti kidogo. Pamoja na kukidhia sifa zote za Sheria ya Huduma ya Habari na Kujisajili katika Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari
Wenye Mamlaka wamepiga simu kwa mwajiri wake na kumtaka aondolewe katika majukumu yake kwa kile walichokiita "mkosoaji sana"
Boniface Jacob
The voice of the Silenced Majority.
NI CHUKI ZA KUPANDIKIZWA NA UROHO WA MADARAKA..!
1.ASKARI WAZURI
Ukifikishwa kituo cha Polisi au Mahabusu ya Jela kama ni mwanasiasa wa upinzani haswa kutoka CHADEMA utaona Polisi wanagawanyika makundi mawili.
Wapo wanaojua tunachokipigania na hali tunayopitia ila sheria za Kazi na mazingira hayawaruhusu kuzungumza au kusaidia lolote kwa wakati huo.
Utawaona na kuwagundua vile wanaguswa Kupitia matendo yao ya huruma na lugha za ukarimu muda wote utakapokuwa katika Kituo chake cha kazi.
Muda mwingine watakushauri namna ya Kuishi vizuri katika kituo hicho cha kazi ili usiumizwe au kufanyiwa Jambo la Kikatili au Kunyanyaswa na wenzake kama .
Au kama anakacheo Kidogo anaweza akatoa maagizo kwa askari wa chini wasikunyanyase utakapokuwa kituoni kwake
Macho yao huwa hayakubaliana na udhalimu ila wanafungwa na sheria za kazi pamoja maagizo kutoka Juu
Wanajua kuna leo na Kesho ,unaye mnyanyasa leo uwezi Kujua kesho atakuja kuwa nani mbele yako.
Mungu ndiyo anajua hatima ya Kila mtu Duniani
2.ASKARI WABAYA
Utafiiti wangu unaonyesha kwamba watu wa namna hii wanakuwa wamepandikizwa chuki mbaya mioyoni mwao na Viongozi wao tangu wanalipokuwa wanaingia kazini (Depo)
Wao wanaamini mtu anaitwa mpinzani ni adui wa Taifa hapaswi kuishi Duniani.
Huaminishwa kwamba matendao ya kikatili dhidi ya Viongozi wa Upinzani ni ngazi ya wao Kupata vyeo na madaraka kutoka kwa Viongozi wa Chama tawala ambao wanawatumia kuwaumiza Viongozi wa Upinzani
Huaminishwa kwamba ugumu wake wa kazi na hali ngumu ya mazingira yake ya kazi yana sababishwa na uwepo wa Vyama vya upinzani ktk nchi yake
Badala ya Kuwa na hasira na waajili wake (chama tawala) yeye hupeleka hasira zake kwa Viongozi wa Upinzani
Mtendo yake mbele ya camera ya kumnyanyasa Mheshimiwa Tundu Antipas Lissu siyo ya bahati mbaya.
anajua kuwa kuna Waandishi wa habari wengi na Kuna vyombo vya habari vingi.
anajaribu Kutaka kuonekana kwa watawala kwamba kazi waliyompatia ya Kunyanyasa Lissu anajua kuifanya vizuri na anawaonyesha kwa vitendo hadharani
ili wamkumbuke katika ufalme wao ilitokea kuna kupandishwa vyeo yeye CV na sifa yake isiwe Kwenda chuo cha maafisa na kufaulu bali iwe "alimtesa sana Lissu"
Askari wa namna hii husababishia hata askari wenzao matatizo kazini.
huripoti vitu vya uongo na habari za uzushi kwa wakubwa Juu ili wao waoenakane wanajua kazi kuliko wengine eneo la kazi kwa dhumuni la Kutafuta madaraka kwa kuharibia wenzie.
Kwa bahati nzuri watu wa namna hii mwisho wa maisha yao huwa mabaya na majuto sana.
‼️USIPITE BILA KUSOMA NA KUSIKILIZA‼️👇🏾
Msikilize Nabii Denis @SuluhuSamia
Lissu anapambana na HATMA 🔥
We ni sehemu ya Hatma yake ili yale makubwa yaliyoandikwa kuhusu hatma yake yatimie! Kama ambavyo mfalme Herode au Pilato au Yuda walikuwa sehemu ya hatma ya Bwana wetu Yesu Kristo ili YATIMIE! Kama ambavyo ndugu zake Yusufu waliomwuza walikuwa sehemu ya HATMA ya Yusufu kutimiza aliyopangiwa!
We siyo starring bali supporting cast in this movie called #Tanzania 😁
Na utaelewa very soon
#TutaelewanaTu
Hatimaye CCM waanza rasmi kumlilia Tundu Antipas Lissu na CHADEMA!
Leo nimepokea simu zaidi ya 20 zote za watia nia ubunge kwa tiketi ya CCM ambao majina yao yamekatwa bila sababu ya msingi katika vikao vya CCM ngazi ya wilaya.
Ujumbe wao kwa pamoja ni....
1.Viongozi wa CCM wanaokaa vikao vya mchujo wamejawa na kiburi na dharau kwa sababu wanajua CHADEMA haishiriki Uchaguzi Mkuu
2.Viongozi wa CCM ngazi za wilaya na Mkoa hawaangalii ubora wa wagombea bali mifuko ya wagombea kwa neno kwamba ukipita katika vikao vyao tayari wewe ni mbunge ni kama wanauza ubunge.
3.Kukosekana kwa CHADEMA katika uchaguzi Mkuu wa 2025 kumefanya Viongozi wa CCM wanaochuja wagombea kutojali ubora wa wagombea wanasema hata jiwe linashinda mwaka huu.
4.Wagombea wanasema nchi inaenda kubaya kama CHADEMA itaendelea kukosekana katika uchaguzi basi wananchi wasitarajie viongozi bora katika mazingira haya.
5.Wanakataa kuvitambua kama vikao vya CCM ngazi ya Wilaya na mkoa siyo vikao vya mchujo bali ni "MNADA WA UBUNGE"
6.Viongozi wa Juu wanatumia vikao vya mchujo vya CCM ngazi ya wilaya na mkoa kama njia ya kulipa visasi kwa wapinzani wao wa kisiasa waliotofautiana nao zamani.
7.Duniani hakuna utaratibu ambao wagombea wanakatwa baada ya kujaza fomu kabla ya kusikilizwa sera zao na mipango yao.
8.Fedha, vimemo na kujuana ndiyo kigezo kikubwa cha jupitisha majina matatu ya wagombea ngazi ya Wilaya na Mkoa.
9.Maelezo ya Mwenyekiti wa CCM Taifa na Katibu Mkuu kwamba ni lazima Wabunge waliomaliza muda wao wawe katika tatu bora hayazingatiwi na inaonekana uongozi wa CCM Taifa ulitumia kauli hiyo kama njia ya kulainisha wabunge wapitishe bajeti kiulaini.
10.Hatimaye mwisho wote wanakubaliana na CHADEMA kwamba hapa tulipofika kama nchi ili tupate chaguzi za haki na Viongozi bora ndani na nje ya vyama basi "NO Reforms No Election" haiepukiki.
Boniface Jacob
Tanrod mkoa wa morogoro mpaka ajali itokee iue watanzania ndio mrekebishe hii barabara, au mnataka ajali itokee ili mseme dereva mzembe? Injinia hii ndio kazi yako tafadhali okoa maisha ya watanzania kabla ya hatari, MSIMBA to IYOVI ...MIKUMI.
Huyu sasa mtu unaweza kusema ni mwanafunzi wa chuo kikuu, huyu unaweza kumuita Msomi wa chuo.
Hapa unapata fikra na uelewa sio uchawa na kujipendekeza hongera vijana.
‼️🚨TAHADHARI HECHE! HUYU RCO ANA NJAMA OVU DHIDI YAKO🚨‼️
Aliye karibu na @HecheJohn amfikishie huu ujumbe
Huyu Mohamed Mirabo aliyefanikisha utekaji wa @DEUSDEDITHSOKA na wenzake alipokuwa OC CID Temeke amepandishwa cheo kwa kazi “nzuri” ya utekaji na Bi Kizimkazi na sasa ni RCO Kinondoni na anamsaka Heche amkamate kwa mazingira tatanishi ya kutumia nguvu kupita kiasi amwumize vibaya na akae ndani hadi Jumatatu au zaidi!
Lengo ni kumzuia asionekane wala kusikika katika media na mitandao! Na kusambaza HOFU! 🚮
Ila @SuluhuSamia una habari kuwa kwa sasa utashindwa kwenda hata Comoros kwa mtindo huu wa kuumiza wapinzani na wakosoaji? Maagizo gani haya umetoa?
Ndani ya jeshi la polisi wamekuchoka pia isipokuwa hawa watekaji! 🚮
Eniwei Heche awe makini kwa sasa @tanpol kama mna shida naye pelekeni wito kwa mwanasheria wa chama aende kwa mahojiano si huu upumbavu wa kukamatana kihuni
#NoReformsNoElection #TutaelewanaTu
"Hatuwezi kumaliza hii taharuki kwa kuzomeana ama kubezana, lazima tuzungumze kwanini tumefika hapa, ni kitu gani kilichotufikisha hapa. Padri amezungumza aliona Mchungaji ana bodyguard 20, karibia 30, pengine amenusa shida. Mimi sijafika hapo kwasababu ni Mungu mwenyewe atanilinda usiku na mchana, akiamua kuniachia basi, nitamshukuru.
Majuzi nilikuwa naenda mahali fulani, nimekimbizwa na gari hizi za wakubwa zetu hizi, ni usiku tunakimbizana, tuliposimama, kwamba tuipishe iende yenyewe ikakaa pembeni yetu tena nikajiuliza hawa ni watu wa aina gani hawa. Inawezekana alikuwa mhuni tu lakini kama haya yanatokea wakati haya mengi tunayasikia, lazima uwe na wasiwasi." Askofu Renatus Leonard Nkwande, Jimbo kuu la Mwanza, wakati wa mazishi ya Mzee Silvin Mongella Juni 08, 2025.
Mwenye kufiwa na kipenzi chake kisha akasema:Inna lillahi wa inna ilayhi raji’un Allahumma ajirni fi musibati wa akhlif li khayran minha (Hakika sisi ni wa Allah na Kwake https://t.co/OxVORIifej Allah nijalie ujira katika msiba wangu huu na nibariki kwa kilicho bora zaidi)basi Allah atamjalia kilicho bora zaidi.(Muslim)
Thank you @LawSocietyofKe@ICJ_org@ICJKenya@LawyersofAfrica@SadcLawyers@ug_lawsociety@TanganyikaLaw and law society of Zambia 🔥
“Injustice to One is injustice to all” ✊🏽
Walisahau madhulmat kuwa @TunduALissu ni wakili pia 🙄 sasa wapambane na mawakili na wanasheria duniani kote!
Chekini orodha hii:
East African Law Society
International Commission of Jurists Kenya
International Commission of Jurists
Law Association of Zambia
Law Society of Kenya
Pan African Lawyers Union
SADC Lawyers Association
Tanganyika Law Society
Uganda Law Society
Next up tunaenda nje ya Bara la Afrika kupata solidarity kama hii!
Mwambieni @SuluhuSamia ajipange! Hii kesi ya Lissu itamshinda mapema sana 😁
#FreeTunduLissuNow
#FreeTunduLissu
Jipe muda – sikiliza kwa makini, tafakari kwa kina, na jiulize mara nyingi: Je, mfumo tulionao unatosha kuleta haki na uwazi katika uchaguzi?
Kwa mifano hii michache—na mingine mingi mnayoishuhudia kila siku katika maeneo yenu—ndiyo maana sisi CHADEMA tunasimamia msimamo wetu thabiti:
BILA MABADILIKO, HAKUNA UCHAGUZI. [No Reforms, No Election]
Hatutashiriki katika mchakato usio wa haki, usio na uwazi, na usio na mabadiliko ya kweli kwa mustakabali wa taifa letu.
“Hii tume ya uchaguzi wamebadili jina kuiita Tume Huru ya uchaguzi ni sawa na kumchukua nguruwe na kumpaka lipstick kisha umfanye Ms. Kinondoni” Jeneral Ulimwengu,
April 14, 2025- @SautiWatanzania Club House.
Kampeni ya #NoReformNoElection in Tanzania sasa hiyoo imefika nje ya Tanzania. Imefikaje kwa haraka hivyo?.Bila shaka kesi ya uhaini dhidi ya Tundu Lissu imechangia kutangaza kampeni hii kujulikana kimataifa. Msikilize huyu hapa. https://t.co/ONRVnqVoN2