Bwana Chalamila, Mimi nimehudumu kwenye kamati ya Nishati na madini ya bunge kwa miaka mitano.
Najua utaratibu wa uagizaji wa mafuta kama ninavyojua kiganja cha mkono wangu.
BPS imeundwa nikiwa mbunge nimeshiriki .
Mnatakiwa kujibu maswali rahisi nyie watetezi mafisadi na Cartels.
1. Mafuta yanatumia siku ngapi kuanzia kununua mpaka yanafika Dar?
2. Mgogoro umeanza tarehe 28/2/2026, mafuta hutumia siku 50 mpaka 60 kufika bandari yetu ya Dar, hivyo mafuta yaliyonunuliwa baada ya mgogoro kuanza na bei kuanza bado hayajaingia nchini.
Kwanini mafuta yaliyonunuliwa na kuingia Nchini kwa bei ya chini yauzwe kwa bei ya juu?
3. BPS wananunua mafuta kwa wingi na mara zote yanatumika miezi mitatu au minne kama alivyosema katibu mkuu wa wizaraโฆ imekuaje mafuta ya kwenye reserve yapande bei?
4. Kuna tozo na kodi kwenye lita moja ya mafuta zaidi ya 18 au 31% yaani kila sh 100 anayotoa Mtanzania kununua mafuta anakatwa sh 31, achilia mbali 4% ya logistics ikiwemo Demurrage ambayo ni uzembe unasababisha Watanzania kubeba mzigo huu.
5. Muhimu sana tenda ilitangazwa lini na wapi? Nani na nani walishindana? Nani alishinda na kwa bei ipi? Wewe umesema mama ndio aliwambia TPDC waagize!!! Hii ni sawa na Richmond nyingine.. sheria inasemaje?
Sisi tunasema:
1. Mafuta yaliyopo hayastahili kupanda bei kwasababu yaliagizwa na kuingia kwa bei ya chini.
2. Mzigo wa kodi na tozo uondoke kwasababu ni nyingi na kubwa mno kuliko Nchi zote Afrika mashariki, ndio maana hata Nchi zisizo na bandari zinauza mafuta chini kuliko sisi.
3. Kuendelea kukandamiza Watanzania na dhuluma hii ya wazi kutaleta balaa kubwa kwenye maisha hasa ya mtu wa chini.
Maana mafuta yakipanda kila kitu kinapanda..
Bwana Chalamila na yule kijana jifunzeni kwanza mambo haya.
Wakati tunasubiri Tume ya Uchunguzi kutupa taarifa na majibu ya kina kuhusu mauaji ya 29 Oktoba, uwajibikaji stahiki na mbinu za kuliponya taifa tusimpe shetani nafasi kutugawa zaidi kwa kisingizio cha propaganda uchwara za udini kwa kuwatumia vijana wasiojitambua kuwashambulia viongozi wa dini zetu mbalimbali. Ni fedheha. Kama ilivyo kwa sisi wazee, ni wajibu wa viongozi wa dini wawe wa TEC au BAKWATA au KKKT na CCT kutulea katika maadili mema ya haki na upendo na kutukumbusha amri za Mwenyezi Mungu. Usiue. Usiibe. Usiseme uongo, nkd, ili kudumisha amani. Tusiwakasirikie na kuwadhihaki wanapofanya kazi zao vizuri. Ni faida kubwa kuwasikiliza. Ndiyo HESHIMA na HEKIMA.