Mahakama ya Rufani ya Tanzania imetupilia mbali shauri la marejeo lililofunguliwa na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) dhidi ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tundu Lissu ambalo lilitaka kupitiwa mwenendo na uamuzi wa Februari 24, 2026 katika kesi ya uhaini iliyopo Mahakama Kuu Masjala Ndogo Dar es Salaam.
Uamuzi huo umrtolewa leo Julai 30, 2026 na Majaji wa Rufani Mwarija, Muruke na Khamis baada ya kukubaliana na pingamizi la awali la Tundu Lissu kwamba notisi ya upande wa mashtaka haikuwa sahihi kisheria ikibainisha kuwa Kifungu cha 308 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA) hakitumiki kuleta ushahidi mpya wa shahidi ambaye ushahidi wake ulisomwa tangu awali katika hatua ya ukabidhi (committal proceedings).
Ikumbukwe Februari 22, 2026 upande wa Jamhuri uliwasilisha mahakamani notisi ya ushahidi wa ziada wa ACP Mahamba juu ya ripoti ya matukio yaliyotokea wakati na baada ya uchaguzi ambapo Lissu alipinga vikali kupokelewa kwa notisi hiyo akieleza ni kinyume na sheria hoja ambayo Mahakama iliikubali.
Hata hivyo, mahakama imekataa ombi la Tundu Lissu la kutaka alipwe fidia na DPP kwa madai ya kucheleweshwa kwa shauri hilo, ikieleza haina mamlaka hayo kwa sasa huku kesi ya msingi ikiwa bado inaendelea.
#KitengeUpdates
Kwa kuwa, maamuzi ya maombi ya marejeo (Revision) yaliyofunguliwa na DPP dhidi ya Tundu A.M Lissu, katika mahakama ya rufaa Tanzania yamesoma na Tundu A.M Lissu AMESHINDA.
Upande wa Jamhuri una machaguo mawili; turudi mahakama kuu kuendelea na tulipoishia katika kesi ya uhaini wa mchongo, au waifute hiyo kesi (nolle prosequi) na kumuachia huru Tundu A.M Lissu.
Huko Mahakama Kuu ndiyo kuna wale mashahidi wao wa siri kwenye kichumba cha joto, na wamewamaliza na walitaka kuingiza mashahidi wengine wapya. Ushahidi wao wa msingi ulikataliwa mapema.
Kama upande Jamhuri wakiamua kuendelea na kesi hiyo, tunakwenda kwenye hatua ya ‘No Case To Answer’ na Tundu A.M Lissu akikutwa na kesi ya kujibu anatakiwa kuanza kujitetea mara moja.
Mashahidi wa TAL unawakumbuka? TUONDOKEEE….
Hiyo Kesi ni Uthibitisho kwamba; “KUNA TOFAUTI KATI YA ELIMU NA AKILI”. Lakini pia, TUNDU LISSU amethibitisha kwamba; “AKILI HAZIFUNGWI PINGU”. Kajipigia KAVU KAVU.😂😂
I'm really proud of this dude. He's a rare gem in our ongoing liberation struggle. He's gone above and beyond, and he keeps pushing forward with incredible perseverance. Mungu linda huyu mwana mwema. Sisi tunakuamini Wewe na ahadi zako. Na hakika zitatimia!
SC Tundu AM Lissu ameshinda hii kesi akitokea jela.
Alijiandaa akiwa jela, amejitetea peke yake akitokea jela, na ameshinda kwa sauti kubwa akiwa jela.
Ajabu ni Majaji kuchukua miezi mitano kusikiliza na kuamua kesi hii. Jitafakarini.