Hebu fikiria hili.
Asubuhi moja ya Novemba 1925, wafanyakazi 32 walipanda meli kubwa ya mizigo, wakiwa na matumaini, mazungumzo ya furaha, na matarajio ya safari fupi kuelekea Cuba.
Hawakujua kwamba walikuwa wanapanda safari ya mwisho, safari ambayo ingetoweka katika hadithi za fumbo la dunia kwa karibu karne.
Ni simulizi ya kweli kuhusu meli ya SS Cotopaxi — na leo nakupeleka hatua kwa hatua ndani ya safari hii iliyogeuka kuwa fumbo kubwa la bahari.
Thread 🧵
Kama ulisoma Uzi niliyo kuwekea Jana kuhusu "Barafu ya Thwaites" au "Barafu ya siku ya mwisho",
Ukiunganisha na huu uzi Uta gundua Mengi na ya kushangaza Kama kweli hii barafu ikiendelea kuyeyuka kama wana sayansi wanavyo sema...😳🤔👇
Katika historia ya binadamu, maji yamekuwa chanzo cha uhai na maendeleo, lakini pia yamekuwa na nguvu ya kuharibu na kufuta kabisa miji mizima...
Wakati mwingine, mafuriko, mitetemeko ya ardhi, au hata kuongezeka kwa kina cha bahari kumesababisha baadhi ya miji kutoweka kabisa chini ya maji, ikisalia kuwa sehemu ya hadithi na mabaki ya kihistoria...
🧵Leo, tutazama katika simulizi za miji mitano iliyomezwa na maji, baadhi ikiwa ni matokeo ya mabadiliko ya tabianchi, mengine kutokana na matetemeko ya ardhi, na mengine kwa sababu za kibinadamu...
Hadithi hizi ni ushahidi wa jinsi historia inaweza kusahaulika, lakini pia jinsi sayansi inavyotusaidia kuifufua...👇👇👇👇👇👇👇👇👇