Jana usiku, David Djumbe (@daviddjumbe), ambaye ni msaidizi binafsi wa Mwenyekiti wa CHADEMA, @TunduALissu, alitekwa na watu wenye silaha nje ya lango la nyumba yake iliyopo Bunju, Dar es Salaam. Hata hivyo, kutokana na ujasiri wa madereva wa bodaboda waliolifuatilia gari la watekaji hao, wahalifu hao walilazimika kusimama na kufyatua risasi hewani ili kuwatawanya. Licha ya kufanyiwa ukatili na kuumizwa vibaya, David Djumbe alifanikiwa kutoroka mikononi mwao akiwa bado amefungwa pingu.
MaCCM mnataka nini hasa? Hamtaki kabisa tufanye siasa? Hamtaki uwepo wa vyama vya upinzani?
‼️🚨 Onyo kwa Raia na Asasi Dekio!‼️
Kwa takribani mwezi mmoja sasa kumekuwa na harakati nyingi sana za
kusafisha tuhuma za dhahiri za mauaji ya Watanganyika Wazalendo wasio na hatia ya Oktoba 29, 2025. Hadi sasa wameibuka, watu, makundi na taasisi ambazo zimekuwa wasemaji wa tume haramu inayoongozwa na Jaji Mohamed Chande Othman iliyoundwa na Samia
Suluhu Hassan
Tunasisitiza kwamba HAKUKUWA NA UCHAGUZI uliofanyika nchini tarehe 29 Oktoba, 2025. Siku inayodaiwa kuwa wa
uchaguzi, wapiga kura na raia wengi walipigwa risasi za moto, wakatekwa nyara, wakalawitiwa, wakafirwa, wakabakwa, wakapotezwa kwa lazima na maelfu wakauliwa na magenge ya polisi na vikosi vingine vya usalama.
Tunawaonya wale wote hasa taasisi za kimataifa zinazoshirikishwa katika mpango huu kufahamu kwamba tunafuatilia kwa ukaribu hila zao zote za kushiriki kama dekio la kusafisha damu za raia wa Tanganyika waliouliwa bila hatia.
Tunawaonya viongozi wa dini, wanahabari, asasi za kiraia na watu
mashuhuri kwamba KUNA MAISHA BAADA YA SAMIA. Wasikubali kuzika
uadilifu na werevu wao kwa vipande vya fedha. Samia atapita au kuzama na wafuasi wake watabaki na aibu.
Tumeshinda!
#SamiaMustGo
ANAANDIKA MWANASHERIA MKUU WA CHADEMA
DR. @rugemeleza
Kwa vyovyote itakavyotolewa na kusema Tume ya Jaji Chande Othmani Juu ya Vurugu na Mauaji ya October 29, 2025 ni batili na haramu tokea ilipoundwa. Kwa sababu zifuatazo:
1. Imeundwa na Samia Suluhu Hassani ambaye ndiye mtuhumiwa namba Moja kwani ndiye alitoa amri ya kuwapiga risasi waandamanaji na watu ambao hawakuwa waandamanaji.
2. Samia alisema wakati wa Kampeni haramu za Udanganyifu Mkuu kuwa wanaosema hakutakuwa na uchaguzi wakumbuke kuwa yeye ndiye Amiri Jeshi Mkuu na kuwa hakutakuwa na nywinywi wala nywinywinywi.
3. Waandamanaji hawakuwa na silaha za moto ajabu yake walipigwa risasi kinyume kabisa na taratibu za kimataifa na nchi yetu za kukabiliana na waandamanaji ambazo ni matumizi ya mabomu ya machozi, maji ya kuwashawasha, hewa ya pilipili na ikilazimika risasi za plastiki.
4. Kuwekwa kwa zuio la kutoka nje na kutembea lililotangazwa na IGP Camillius Wambura ilikuwa kinyume Cha Sheria kwani hana mamlaka hayo.
5. Kuzimwa Kwa mtandao wa intaneti kwa siku sita ilikuwa kinyume Cha Sheria. Kwa kuzimwa kwake mauaji mengi yalitokea na yalisababisha watu kutokupata taarifa za kiwakati juu ya maovu makubwa yaliyofanywa na vyombo hivyo vya dola.
6. Kuzimwa kwa mtandao na zuio la kutoka nje sehemu nyingi za nchi yetu ilimaanisha hata wafanyakazi na mawakala wa Tume ya Udanganyifu Mkuu ya Jacobs Mwambegele haikuwa na uwezo wa kupata matokeo ya uchaguzi huo haramu. Ajabu yake Mdanganyifu huyo Mkuu asiyeheshimu kazi na maadili ya ujaji akatangaza matokeo kama kwamba uchaguzi ulifanyika na kura kuhesabiwa na matokeo kutangazwa katika Kila kituo na hatimaye kutumwa kwa Tume hiyo haramu!
7. Stargomena Tax ambaye alikuwa Waziri wa Ulinzi katika serikali ya Samia wakati wa udanganyifu huo ni mjumbe katika Tume hiyo ya Chande! Ni kanuni ya kisheria na haki kuwa huyu ana mgogoro wa kimaslahi na ni sehemu ya waliopaswa kuchunguza imekuwaje akageuka kuwa mchunguzi.
8. Jaji Othmani Chande na Jaji Ibrahimu Juma wanajua, kama wajuavyo wanasheria na wasomi wote, kuwa huwezi ukawa hakimu au muamuzi katika kesi yako mwenyewe(Nemo judex in causa sua) sasa imekuwaje wawe katika Tume ambayo ina kasoro hii kubwa? Je, si inafahamika kuwa pale Tume inapokuwa na kasoro hiyo yote iliyoyafanya hata kama ni mazuri, kisheria Huwa batili?
9. Wakati Tume inaanza kazi Samia ametoa matamshi ya kuingilia kati au kutoa majibu kwa Time ikiwa ni pamoja na kusema "nguvu iliyotumika ilikuwa sahihi" na kuwa "kwa nini wazazi hamkuwazuia watoto wenu kutoka nje?". Sasa hapo nini kinachunguzwa?
10. Tume ilizuia uwazi wa watu waliotoa maelezo yao kwa kuvikataza vyombo vya habari kuendelea kutoa maelezo ya waathirika wa mauaji hayo ya kinyama yaliyofanywa na vyombo vya dola. Kukosekana kwa uwazi ulikuwa mkakati wa kuleta giza na kuzuia ukweli wa mauaji hayo kufahamika na hivyo kile kitakachosemwa na Tume kuwa eti ndicho kilichosemwa na waathirika kichukuliwe kuwa ni cha ukweli.
11. Tume yenyewe imeanza kampeni ya kuuandaa umma kupokea ripoti yake na imekuwa na wasemaji wake. Hiyo inaashiria nia mbaya ya Tume hiyo.
Ni kwa msingi na sababu hizo nasema kuwa Tume hiyo ni batili na chote kitakochotolewa nayo ni batili.
Samia kama amkupanga kufanya mambo haya mpaka mkahusisha madaktari kwa nini mlibadilisha sababu za vifo ?!
Mlitafuta silaha wewe na mwanao
Mkapanga madaktari na hospital kubadilisha sababu za kifo au kuiba miili
Mkachoma maili ya watu
https://t.co/p2ZWt4ebmk
Nani anaweza kusema huu ni uongo…
Bunge la hovyo lisiloweza kusimamia serikali..
Tulia na bunge lake waliogopa kujadili hata suala la utekaji, kama hauwezi kujadili jambo hilo la wananchi upo kwaajili ya nani?
Kuna sababu gani ya kuwa na muhimili unaitwa bunge kama hausaidii wananchi?
Bado Tulia na kujipendekeza kote!!!!
Mzee Joseph Sinde Warioba,
Makamu wa Rais wa Tanzania
Waziri Mkuu wa Tanzania
Mwanasheria Mkuu wa Tanzania
Wakili Mahakama Kuu Tanzania
I wasn't familiar with your game, grandpa. Take a bow. Watu wa mkoa wa Mara, TUNAJIVUNIA. 👏
Incase kama hukuandamana tar 29, hukwenda kwenye msiba waliouwawa kwa risasi, hukwenda hospital kuangalia rafiki alopogwa risasi ama hukwenda jela kusalimia mtu aliepewa uhaini, jua tu kwamba watu wana maumivu sana, please usiwabeze
Asante Rachel Dangwa huu ni uwendawazimu na familia ndugu na jamaa wa hawa vijana waambiwe hii itawaletea kesi ya madai kama Musiba waachane nayo! ❌ Tuko serious wasizingue na mambo ya kuungaunga!
Bora wasubiri wiki moja #D9 tutaikomboa Taifa maana hata mtoto mdogo leo amesikia dharau na chuki ya Jezebel. Tumekubaliana #SamiaMustGo si kwa masimango haya!
Sasa Hivi Watu Kibao Wanaamua kuachana na mfumo sasa unajua watafanywa nini? ....soma hapo Chini👇
1.👉 Red Exit Betrayal or Strategic Defection
System huona wanaoihama kama threats, si tu kwa sababu wameondoka bali kwa sababu wana access ya ndani, yaan operations, weaknesses
Amini wakali nawajuza baada ya kilicho tokea system itaanza kitu inaitwa soft infiltration kwa hela ahadi, na lifestyle kama njia ya kupasua mioyo ya vijana kabla hawajakomaa kimkakati Inaitwa 👇
OP: Golden Trap
01👉Baada ya kila mapambano makali, system huvaa sura ya tabasam
Kuna wakati natamani kuamka nikute ninayosikia na kuyaona nilikuwa nimeota. Bado ingekuwa ni ndoto kwamba Balozi Pole Pole hajapatikana na watu wako kimya, Tundu Lissu yuko gerezani TZ, Wanasiasa wanadakwa kama kuku na wananchi wote wanatakiwa kunyamaza. Bado ningefunga na kuomb
VIDEO:
Askofu wa Jimbo Kuu Katoliki la Mwanza, Mhashamu Renatus Nkwande, amesema baada ya taarifa za kutoweka kwa Padre Camilius Nikata na baadaye kupatikana, walitarajia kupokea maneno ya kutia moyo, badala yake wamepewa maneno aliyoyaeleza kuwa ni ya kuudhi.
Askofu Nkwande ameeleza hayo Oktoba 18, 2025, katika adhimisho la Misa takatifu jimboni humo, ambapo pia amekosoa taarifa zilizodai kuwa Padre huyo alipanga kuachana na upadre na hakusikilizwa.
"Badala ya kupata maneno ya kutia moyo tusikate tamaa, tunapewa maneno ya maudhi tunaudhiwa", amesema Askofu Nkwande.
Amesema, kwa asili Padre Nikata anatoka Jimbo la Songea, lakini kwa wakati huu alikuwa akihudumu kama Padre katika jimbo la Mwanza, huku akisema suala la Padre yeyote kutaka kuacha Upadre linaenda sambamba na utoaji taarifa, jambo ambalo hakuna aliyekuwa na taarifa hizo.
"Padre aliyepotea ndugu zangu ni Padri wa Songea, kwa asili ni Padre wa Songea, lakini anafanya kazi katika jimbo hili, kwa muda huu ni Padre wa Mwanza, kama alishawahi kupanga kuacha Upadre mimi napaswa kujua, si mwingine tena, mimi sijui, Askofu wa Songea hajui. Watu wamesema kwamba eti alishaomba hakusikilizwa”, ameeleza Askofu Nkwande.
Amewataka waumini jimboni humo kuomba amani kwa taifa, huku akiwasihi viongozi kutafuta fursa ya kutia moyo na kulifariji taifa kutokana na mgawanyiko na mahangaiko yaliyopo.
"Leo tunatembea huku hatujiamini, Watanzania tulikuwa tunaheshimika katika ulimwengu, wapo wanaoniuliza sasa nyie mkiwa hivi itakuwaje sasa, tutakimbilia wapi, hapa tunaanza kufanyiana hivyo kwa sababu ya nini? tatizo ni nini? Tunahitaji kweli amani, lakini tutambue kwamba kama tunataka amani lazima iwepo haki", ameongeza Askofu Nkwande.
Aidha katika jitihada za kutafuta alipokuwa Padri Nikata, Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma chini ya kamanda wake Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Marco Chilya, limesema Padre Nikata hakutekwa kama ilivyodhaniwa, bali alijipoteza kutokana na sababu za msongo wa mawazo ikiwemo kutosikilizwa na uongozi wake.
Katika taarifa ya Polisi, imeelezwa kwamba Padre Nikata amepatikana katika mashamba ya Kijiji cha Mawa, kilichopo kata ya Hanga, Wilaya ya Namtumbo ambako ndiko nyumbani kwao Padre Nikata.