@SuluhuSamia umefanya propaganda wiki nzima kuwahadaa Watanzania kuwa Marekani inakusapoti mtu ambae umeua wananchi ili ubaki madarakani ila leo Trump kaiingiza rasmi Tanzania kwenye nchi zenye partial travel ban to the US. Na wewe na wenzio wooote mlioshiriki kuua wananchi waliokuwa wanadai haki zao mnapigwa full ban ya kuingia Marekani na soon Europe pia wanawapiga ban.
Mnahangaika kutafuta uhalali baada ya kuua watu?? Wewe ni Rais batili ulieua wananchi zaidi ya elfu 10 ili ubaki ikulu.
@SuluhuSamia kama jinsi mlivyofosi vyombo vya habari vyote Tz kuposti uwongo wenu kuwa mnasapotiwa na Marekani na UN wapeni ruhusa waposti na hii.
Alafu mnachekesha mnooo, nyie si mliwaambia hawa ‘who are you? , mbona sasa mnahaha kukubalika na kina ‘who are you?’ . Nyambaf roho zinawaenda mbio kukosa mikopo ya kununua ma Bugatti na kufanya anasa. NA BADO!!!!!
Grateful for another year and looking forward to life’s journey! As the Chinese curse says “may you have an interesting life”
It has been very interesting so far 😅 but I am very thankful!
Mungu bariki - safari yangu inaendelea - nashukuru kwa uhai 🙏🏽
Iko hivi👇
Juzi niliripoti tukio la jaribio la watu kuniteka.
Watu wale wakitumia gari tatu aina ya Land Cruiser na Subaru Forester nyeusi walitaka kuniteka nikiwa naendesh gari langu.
(Sijui walitumia muda gani kujua gari ninalotumia, Sijui walijua vipi makazi yangu)
Bahati nzuri sikuwa naendesha gari hilo. Walimfukuza dereva aliyekuwa na gari na akafanikiwa kuwapoteza kwenye vichochoro vya Kigamboni.
Baada ya kukosa gari. Watekaji wakajikosha kumtafuta mjumbe wa mtaa wangu. (Sijui walimjuaje kwani ilikuwa ni ndani ya muda mfupi sana tangu dereva kunipigia na mjumbe kunijuza kuwa kuna askari wanataka awalete nyumbani kwangu)
Askari walipofika kwangu hawakutaka kushuka. Wakiwa kwenye gari lililo tinted wakamwambia mjumbe ashuke aniulizie.
Binti yangu bila kujua kuwa baba yake yupo kwenye jaribio la kutekwa akamjuza mjumbe kuwa mimi nimeondoka tangu asubuhi which was true.
Taarifa hii ilinifanya kufika kituo kikuu cha polisi kuulizia kama ninatafutwa kwa shida yoyote ambapo nilijibiwa hakuna kesi yoyote dhidi yangu.
Nilitumia pia my insiders kujithibitishia hilo.
Sikuridhika.
Kwa uchunguzi wangu nikapata namba ya mmoja wa waliopaswa kuwa watekaji wangu.
Namba hapa chini, haimilikiwi na mtu binafsi.
Namba hii inamilikiwa na RCO Temeke
+255 774 175 485
Nilipiga namba hii na kuuliza kwa nini wananitafuta kihuni bila wito maalumu.
Wamenivizia kwenye gari. Wamefika kwangu kuniulizia na kuondoka bila kuacha wito kwangu au kwa mjumbe.
Hawakuwa na jibu na badala yake wakaniambia nina kesi Chang’ombe wanataka nifike.
Nikawajuza waniambie ni kesi gani? Inahusiana na nini? Nani mlalamikaji wangu? RB namba yangu ni ipi? Wakashindwa kunijibu.
Nikawajuza kuwa bila hizo taarifa sitaweza kufika.
Jana jioni, watu hao wamefika tena katika makazi yangu.
Bila kutoa search warrant wakaingia kupekua hadi ndani ya chumba changu wakiwa na mitutu ya bunduki wakanikosa.
My family is so so distressed.
Wanahisi Je, baba yao ni Jambazi?
Ninaomba nitoe wito kwa yeyote anayenitafuta afate taratibu za kisheria ATANIPATA
Namba hii nimeipeleka sehemu. Naamini nitapata HUDUMA
MSIJE KUSEMA HATUKUSEMA.
Tanzania ni kati ya nchi 30 zenye maambukizi makubwa ya ugonjwa wa kifua kikuu zinazochangia 87% ya wagonjwa duniani, ikiwa na makadirio ya kiwango cha maambukizi ya 195 kwa kila watu 100,000
Ripoti mpya ya shirika la Afya Duniani (World Health Organization – WHO) mwaka 2025 inasema Duniani kulikuwa na wagonjwa wapya wa kifua kikuu milioni 10.7 na kati ya hao wagonjwa milioni 1.2 walifariki.
2021 Tanzania ilikua na wagonjwa wapya wa kifua kikuu 133,000 sawa na wagonjwa 222 kwa kila watu 100,000 na kiwango kikubwa cha maambukizi ya VVU cha 16.4% miongoni mwa watu wenye kifua kikuu.
Watu 70 hufariki kila siku kwa Kifua Kikuu na watu 25,800 hufariki kila mwaka Tanzania kwa kifua kikuu. Watu 10.5 milioni wanaambukizwa Kifua Kikuu kila mwaka Duniani na kati ya hao 1.6 milioni hufariki.
Watu wenye vimelea vya TB wako kwenye hatari ya kuugua TB kwa 10% katika maisha yao. Watu wenye upungufu wa kinga mwilini, utapiamlo, kisukari, wanaovuta sigara wako katika hatari ya kuugua.
Maambukizi ya (VVU) Virusi vya UKIMWI yamesababisha ongezeko kubwa la wagonjwa wa Kifua Kikuu (tuberculosis - TB) Duniani hususani katika ukanda wa kusini mwa jangwa la Sahara ikiwemo Tanzania.
50% ya wagonjwa wa Kifua Kikuu (tuberculosis) wana maambukizi ya Virusi vya UKIMWI (VVU) Duniani. Takwimu za WHO za mwaka 2018 zinaonyesha wagonjwa 40,000 wa TB walikuwa na maambukizi ya VVU.
Chanjo ya Bacillus Calmette–Guérin (BCG) ni chanjo inayotumika dhidi ya maambukizi ya kifua kikuu. BCG ilitumika mara ya kwanza mwaka 1921. Chanjo ipo katika Orodha ya Dawa Muhimu ya Shirika La Afya Duniani,
Isoniazid ni kati ya dawa inayosaidia matibabu ya Tuberculosis ikiwa pamoja na dawa nyingine kama Rifampin, pyrazinamide na ethambutol. Hutumika kwenye daraja la kwanza la matibabu ya kifua kikuu.
Hizi dawa na chanjo zinatoka kwa mabeberu. Mabeberu hawa ambao naona inatembea hashtag ya “WHO ARE YOU?”. Dawa na chanjo hizi hazitengenezwi na PERAMIHO. Chanjo na dawa hizi zote ni msaada.
Kifua Kikuu (tuberculosis) ni ugonjwa hatari unaosababishwa na ‘mycobacterium tuberculosis’. TB huathiri mapafu, pia inaweza kudhuru sehemu nyingine za mwili kama vile mifupa, figo, au ubongo.
2018 kiasi cha $63.941 Milioni zilihitajika ili kukabiliana na Kifua Kikuu Tanzania. 41.6% ya fedha zinazohitajika zilipatika. 3% fedha za ndani na 39% fedha za nje kutoka kwa wahisani. WHO Global TB Report 2019.
Mwaka 2019 Tanzania ilipokea mgao wa Sh1.33 trilioni kutoka Global Fund, Sh828.19 bilioni zilielekezwa kushughulikia UKIMWI, Sh407.15 bilioni MALARIA na Sh97.67 bilioni KIFUA KIKUU mwaka 2020/2022.
January 31, 2024 Tanzania na Global Fund zilisaini hati za mikataba ya msaada yenye thamani ya $606.9 Milioni (sawa na zaidi ya TZS 1.4 trilioni) kwa ajili ya kupambana na maradhi ya UKIMWI, Kifua Kikuu, Malaria)
Kufikia Januari 2024 Tanzania imepokea misaada ya Global Fund kwa vipindi vinne ambavyo ni Julai 2012 – Desemba 2014, Julai 2015 – Desemba 2017, Januari 2018 – Desemba 2022 na Januari 2021 -Desemba 2023.
Msaada wa Global Fund kuanzia Januari 2024 - Desemba 2026 itatekeleza miradi ya Sekta ya Umma na Binafsi, Wizara ya Fedha ni Mpokeaji Mkuu wa Sekta ya Umma , (MDH) ni Mpokeaji Mkuu kwa Sekta Binafsi
Msaada wa Global Fund 2024 hadi 2026. Unalenga kuboresha mifumo ya maabara, mitungi ya Oksijeni, mazingira ya watumishi wa afya, kuimarisha mnyororo wa thamani na kuboresha mifumo ya Afya.
Wakati tunapiga kifua, tunatakia kurejea ubaoni na kujiuliza maswali hayo ya msingi. Je, tunazo dawa za kufubaza makali ya virusi vya UKIMWI? Je, tunazo dawa na kupambana na maambukizi ya Kifua Kikuu?
Kama tupo vizuri, tusonge mbele. Vinginevyo, wagonjwa WATAKUFA. Maradhi ya kifua kikuu (tuberculosis) na UKIMWI kwa pamoja siyo vita ya mchezo. Nawatakia mapambano mema katika eneo hilo. Au revoir.
Anaandika Mwanasheria mkuu wa CHADEMA DR. Rugemeleza Nshala.👇🏾
Samia na wenzake wote waliotwaa madaraka ya nchi kinyume cha demokrasia kushiriki katika mchakato wa kuliokoa na kulileta Taifa pamoja. Wote hawa wanatakiwa kujiuzulu mara Moja.
1. Samia atueleze Watanzania na Dunia Nzima ni nani aliyetoa amri ya kuuawa kwa Watanzania waliokuwa wakidai uchaguzi huru na haki?
2. Je ni Sheria ipi katika Jamhuri ya Muungano ya Tanzania inayompa Raisi madaraka ya kuzuia raia kuandamana na kusema "hakutakuwa na nywinywi Wala nywinywinywi"?
3. Je, kauli yake hiyo si ndiyo ilikuwa amri kwa Jeshi la Polisi la kuwafyatulia raia risasi za kuua kuzuia wasiandamane?
4. Je, anaifahamu na kuielewa ibara ya 14 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania inayosema kuwa Kila mtu anayo haki ya kuishi na kupata hifadhi ya maisha yake kutoka kwa jamii kwa mujibu wa sheria?
5. Kama anaifahamu je anakumbuka kuwa ni miongoni mwa ibara alizotuapia na kutueleza kuwa atazilinda na kuzitetea mnamo tarehe 19 Machi 2021? Na Kwa Nini hakufanya hivyo mnamo na baada ya tarehe 29 Oktoba 2025?
6. Kama Raisi, wakati uchaguzi unafanyika, nani alitoa amri ya kuzimwa intaneti kwa siku tano?
7. Ni nani aliyempa mamlaka IGP Wambura kuweka zuio "curfew" kwa wakazi wa Dar es Salaam na amri hiyo kutekelezwa katika sehemu mbali mbali nchini wakati hakuna Sheria inayomruhusu kufanya hivyo?
8. Kama si yeye, alichukua hatua gani za kinidhamu na kisheria dhidi ya IGP Wambura na wote hao waliojivika madaraka wasiyo kuwa nayo kisheria?
9. Ni nani aliyetoa amri ya miili ya waliouawa kuchukuliwa na kupotezwa bila kukabidhiwa kwa ndugu zao?
10. Ni nani aliyeamuru wapendwa wetu hao kutupwa na kurundikwa kwenye na nje ya mochuari kama mizoga?
11.. Ni nani aliyezuia Taifa kuwaomboleza waliouawa kinyama na Jeshi la Polisi na vikosi vingine vya Usalama?
12. Je Samia anafahamu msemo usemao za "buck stops at the president" ikimaanisha uwajibikaji katika serikali humwangukia raisi?
13. Sasa kama anafahamu msemo huo anasubiri nini yeye na genge lake kuondoka madarakani?
MWISHO
REPOST 200
TUTAKUWEPO🫵🏾😎