#SaragossaFitnessCenter ni kituo cha mazoezi kilichopo Mbweni, DSM. Wakazi wa Ununio, Boko, Bunju, Mabwepande na Mbweni wanakaribishwa kutembelea kituo kwa ajili ya kupata taarifa zaidi.
Dansi ya #zumba inasaidia kupunguza lehemu (mafuta yasiyotakiwa mwilini), kuupa mwili wepesi, kuondoa msongo wa mawazo, kuchangamsha na kuimarisha afya ya moyo! #zumba na #yoga ipo kila wiki siku ya Jumanne jioni kati ya saa 12.30 jioni na saa 02.00 usiku. Karibuni sana 😎👊🏼💪🏼
Matumizi ya #steppermachine husaidia kuimarisha misuli sehemu ya chini ya mwili (kuanzia kiunoni, mapaja, miguu). Zoezi hili likifanyika vizuri husaidia pia kuimarisha misuli sehemu za tumbo na kuimairisha mfumo mzima wa upumuaji (cardio system). #karibu#saragossafitness 😎💪🏼👊🏼
UKWAJU: Unajua juisi ya ukwaju ni kinywaji kizuri kwa kinga ya mwili. Pia husaidia kupunguza uzito na hatari ya magonjwa ya kisukari, moyo, kansa na kukosa choo.
Pia huimarisha mfumo wa neva, huzalisha seli za ubongo na kupunguza michirizi kwenye ngozi.
#tubongelishe
#Elimika✍🏽 #Boxing 🥊 inahusisha misuli tofauti mwilini mwako sehemu ya juu na chini. Ni zoezi zuri linalosaidia mapigo ya moyo kuongezeka na kupelekea kuimarisha moyo, kukata mafuta, uzito, kupunguza madhara ya shinikizo la damu na magonjwa mengine ya moyo pamoja na kisukari.
#lateralshuffle linasaidia zaidi kujenga na kuimarisha misuli kuanzia sehemu ya kiuno mpaka chini kwenye mapaja,miguu. Zoezi linakujengea wepesi kwenye viungo vyako ili uweze kufanya mazoezi vizuri zaidi. Wacheza Tennis 🎾,mpira wa miguu ⚽ au kikapu 🏀 hupendelea hili zoezi pia.
#Elimika ✍ #SpinnningBike inasaidia kuimarisha afya kwa ujumla.Aina hii ya baiskeli inasaidia kuimarisha misuli kwenye mapaja, miguu, tumbo, hips, na mabega. Mazoezi kwenye kifaa hiki yanasaidia kuchoma mafuta kwa haraka na kupelekea kupungua uzito.#SaragossaFitness#Tunakujali
Unywaji wa pombe huufanya mwili upoteze kiasi kikubwa cha folate ambayo hushirikiana na Vitamin C pamoja na Vitamin B12 katika kutengeneza protini mpya,kuzitumia pamoja na kuzivunja vunja. Spinach ni mboga nzuri kwa wanywaji wa pombe, huwa na folate nyingi kufidia upotevu huo!
#Elimika ✍ #Planks -- Zoezi hili lina faida nyingi kwenye mwili wako. Zoezi hili linasaidia kuimarisha misuli kwenye sehemu tofauti za mwili, haswa kwenye maeneo ya mikono, tumbo na miguu. #Karibu#SaragosssaFitness#MbweniDSMTZ
#Elimika ✍ #BackExtensionExercise ni zoezi linalohusisha misuli ya mgongo, linasaidia kunyoosha na kuimarisha uti wa mgongo. Zoezi hili pia ni zuri sana kwa wale wanaokaa muda mrefu maofisini na wanaotumia zaidi magari kwenye mizunguko. #Karibu#SaragossaFitness
#Elimika ✍ #ElipticalMachine au #CrossTrainer ni salama kwa magoti yako. Aliye na maumivu ya miguu akitumia mashine hii atakuwa amefanya zoezi sawa na aliyefanya zoezi la kukimbia kawaida. Imarisha misuli kwenye miguu na mikono kwa kutumia mashine hii. #Karibu#SaragossaFitness