Maendeleo ni kutathimini ulipotoka ulipo na unapoelekea kwa kutazamaa hayo tunaiona Tanzaia ilipo kwa sasa tangu ilipotokea kule 1961 ilipokuwa Tanganyika hakika tunajivunia viongozi imara walioivusha Tanzania.
Sasa Dr SAMIA SULUHU HASAN anaiendeleza vyema
# matoke chanya
#IkuluWIkiHii Tazama muhtasari wa matukio yote muhimu aliyoyafanya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika wiki hii
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Jerry Silaa amesema kuwa baadhi ya akaunti za mitandao ya kijamii, ikiwemo zile za taasisi za Serikali zilizovamiwa jana, tayari zimerejeshwa na ziko salama.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiteta jambo la Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kabla ya uzinduzi wa Sera ya Mambo ya Nje ya mwaka 2001 Toleo la Mwaka 2024, katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam tarehe 19 Mei, 2025.
Rais wa Jamhuri ya Namibia, Mhe. Dkt. Netumbo Nandi-Ndaitwah akisalimiana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na Mhe. Mama Gertrude Mongella kwenye hafla ya chakula cha jioni alichoandaliwa na mweji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 20 Mei, 2025.
Kuwaona wanawake wenye uwezo mkubwa na hekima kiasi cha kuongoza nchi inatupa matumaini juu ya mabadiliko ya mitazamo hasi hongera sana Rais wetu pamoja na Raisi wa Namibia kuwa vioo bora kwa binti yangu.
#Mslac#sisinitanzania
##Nchiyangukwanza#matokeochanya
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akimkaribisha mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Namibia Mhe. Netumbo Nandi-Ndaitwah mara baada ya kuwasili Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 20 Mei, 2025.
Karibu Tanzania.
Karibu Nyumbani.
Ikulu jijini Dar es Salaam leo nimempokea Rais wa Jamhuri ya Namibia, Mheshimiwa Dkt. Netumbo Nandi-Ndaitwah. Kama ilivyokuwa enzi za waasisi wa mataifa yetu, Hayati Mwalimu Julius Nyerere na Hayati Sam Nujoma, tunaendelea kuimarisha udugu na ushirikiano ambao ulianza tangu kipindi cha kupigania uhuru, ambapo baada ya kupata uhuru wa kisiasa, sasa tunajikita katika kuimarisha uchumi na ustawi wa nchi zetu.
Katika mazungumzo yetu tumeazimia kukuza uhusiano uliopo, na kufungua fursa mpya za ushirikiano kupitia sekta mbalimbali zikiwemo biashara na uwekezaji, mifugo na uvuvi, uchumi wa buluu, utalii na lugha ya Kiswahili, kwa manufaa ya wananchi wetu.
Mheshimiwa Dkt. Netumbo ni dada kwangu. Nimefarijika kumkaribisha tena nchini Tanzania, mahali alipoishi kuanzia mwaka 1980 hadi 1986 akiwa nguzo muhimu katika mapambano dhidi ya ukoloni na ubaguzi wa rangi nchini Namibia.
Tanzania Yapiga Hatua Kubwa Katika Sekta ya Utalii (2021-2024)
Tanzania imefanikiwa kupiga hatua kubwa katika sekta ya utalii kati ya mwaka 2021 na 2024, ikiweka rekodi za kipekee katika ukuaji wa utalii wa ndani na kimataifa. Kwa mujibu wa takwimu za Wizara ya Maliasili na Utalii, utalii wa ndani umeongezeka kwa asilimia 307.9%, huku utalii wa kimataifa ukiongezeka kwa asilimia 132.1% ndani ya kipindi hicho.
Ukuaji huu wa kasi umetokana na juhudi za makusudi za serikali chini ya uongozi wa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan. Kupitia kampeni kama Royal Tour, Tanzania imefanikiwa kuvutia watalii wa kimataifa huku ikiimarisha ari ya Watanzania kutembelea vivutio vya ndani.
Serikali pia imewekeza katika miundombinu muhimu ya utalii, kuboresha barabara, viwanja vya ndege, na huduma za malazi. Kampeni za kuhamasisha utalii zimeimarishwa kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii, hatua iliyochangia kuongeza mwamko wa wananchi na wageni kuhusu vivutio vya kipekee vya Tanzania.
Matokeo ya ukuaji huu si tu kuimarisha mapato ya taifa kupitia sekta ya utalii, bali pia yamechangia kuongeza ajira na maendeleo katika maeneo mbalimbali ya nchi. Tanzania sasa inajitokeza kama mfano wa mafanikio barani Afrika katika kukuza sekta ya utalii kwa njia endelevu.
Mafanikio haya ni ushahidi wa dhamira thabiti ya serikali ya awamu ya sita katika kutumia sekta ya utalii kama chombo cha maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
#Sisinitanzania #nchiyangukwanza #matokeochanya #kaziiendelee #kazinaututunasongambele #katibanasheria #mslac #SSH