Mwandishi Eric Shigongo anasema ili ufanikiwe kwenye biashara unahitaji mambo matatu tu. Ambayo kwake ameyafupisha kama SEC...
S ➛Solution
Anasema "Babu wa loliondo watu walimfuata kwa sababu alikua na solution. Ukiwa na solution hata kama hutaki pesa watu watakuzalimisha uzichukue".
E ➛Experience
Watu wananunua experience anasema "mteja alipokuja kwako alipata experience kiasi gani, alihudumiwa vizuri kiasi gani. Kwa sababu lengo hapa ni retention ili kesho na kesho kutwa arudi tena kwako, aku recommend kwa wengine wasiokujua".
C ➛Convenience
Anasema "Huduma yako inapatikana kwa urahisi namna gani, ofisi yako ipo sehemu gani, availability yako ipoje. Ili mtu akufikie kuna urahisi kiasi gani. Hauwezi kuuza spare za pikipiki halafu duka lako linapatikana masaki".
Leo nataka kuwashirikisha falsafa niliyokuwa nasoma, ndogo lakini nzito iitwayo Uzito wa Kusubiri (The Weight of Waiting).
Subira si udhaifu. Ni mazoezi ya imani. Watu wengi wanavunjika si kwa sababu Muumba wao amewachelewesha, bali kwa sababu hawajui namna ya kusubiri bila kukata tamaa. Kila kuchelewa ni somo, si adhabu. Kwa wale wenye imani za kiroho watakuwa wanafahamu kuwa Mungu hachelewi, anasahihisha wakati.
Kuna watu wanakimbilia matokeo, wakidhani kasi ndiyo kipimo cha baraka. Lakini kiimani, Mungu hapimi kasi yako. Anapima utulivu wa moyo wako unapochelewa kufika. Anataka kuona kama bado unaamini hata pale ambapo hauoni mwelekeo.
Kuna nguvu katika kusubiri kimya kimya, ukiamini kuwa wakati utakapofika, mlango utafunguka bila kulazimishwa. Usione kuchelewa kama hasara bali uone kama maandalizi. Moyo unaojifunza kusubiri kwa amani, ndio moyo unaokomaa kwa hekima.
Hiyo siyo subira ya uvivu. Ni subira ya imani. Ni kusimama imara unapovunjika vipande vipande, ukijua kuwa kuchelewa si kukataliwa.
Wanasema, patience doesn’t delay you, it prepares you.
PS: Falsafa hii inafanya kazi vizuri hata kwa watu wasio na imani au wanaoamini katika Mungu
@Shaheedyways@Tottenham_Feed Shaheedyways Yes, Tottenham should still be classed as a Big Six club. Despite finishing 17th in 2024/25 PL, their 2025 Europa League win secures UCL spot and affirms elite status. With top revenue, stadium, and history, one poor season doesn't change that.