@said_kulin90311@MO29TV That is not about chadema brother its about justice. Misingi ikiharibika hakuna anayebaki salama kaka. Nchi zote tunazoona zina mifumo mizuri zimepitia njia hizi hizi za boycott kwenye international gathering
@nulphin Binafsi sioni anayeweza kua bora kuliko mwenzie. Hata Juma aweso bado wizara yake inachangamoto nyingi sana. Imagine mji wa kibiashara kama Dar lakini maji ni changamoto kubwa. Ukitembelea maeneo ya nje ya mji kama Chanika kila mtu amechimba kisima. Hakuna hata dalili ya Dawasa
KANUNI YA MSAMAHA YA WAYAHUDI.
(Tafsiri yangu Isiyo Rasmi)
1. Sisi Wayahudi huwa hatusamehi kabisa na ndiyo maana mnatuona tuna uhuru wa kutenda kile tunachokiamini.
2. Ninyi mmefundishwa Kusamehe na kusahau
3. Sisi tumefunzwa kutunza kumbukumbu za makosa yako na kuchukua hatua za tahadhari ili kujilinda.
4. Ninyi mnafundishwa kusamehe watu ambao hawajakiri makosa yao na kuomba radhi na mnaliita jambo hilo Uponyaji wa Taifa.
5. Kumsamehe mtu asiyetambua na kuwa tayari kuwa jibika kwa makosa yake na kuomba radhi kwetu ni Kama kumpa mtu huyo kisu ili akushambulie na kukuumiza tena
6. Baba yangu alinifundisha kuwa kumsamehe mtu ambaye hayuko tayari kutubu na kujutia makosa yake na kuwajibika ni sawa na kumpa mtu huyo nafasi ya kuumiza tena.
7. Siyo sahihi kusamehe watu ambao wamefanya makosa na hawaoni haja ya kutubu na kuwajibika
8. Acha kujidanganya kwamba unalinda amani ambayo tayari kwa uhalifu wao walikwisha iharibu.
BAK MWABUKUSI.
@MK47TA @godbless_lema Kaka mbona kama wewe ni wakiume au naona vibaya!!! Wivu hadi kwa mwanaume mwenzio au ndo unatamani hiyo bahati ya kwenda kupokelewa heapoti upewe wewe?
Somo kutoka kwa wayahudi!
Tunalea Wajenzi, Sio Watumiaji
Unawafundisha watoto wako kutafuta ajira…
Sisi tunawafundisha kuunda ajira.
Unawaambia, “Someni kwa bidii mpate alama nzuri.”
Sisi tunawaambia, “Someni kwa bidiina ulizeni maswali bora zaidi.”
Unawalea ili waendane na wengine…
Sisi tunawalea wasimame wawe tofauti.
Unathamini utii
Sisi tunathamini udadisi.
Akiwa na miaka 5, mtoto wako anatumia masaa kuangalia katuni…
Wetu wanakaa mezani, wakisikiliza mazungumzo ya watu wazima kuhusu biashara, maisha, na fedha.
Sio kwa sababu tunawalazimisha
Ni kwa sababu tunawahusisha.
Unawaficha watoto wako matatizo yako…
Sisi tunawafundisha kwamba matatizo ndiyo darasa lao.
Unawalinda wasipate kushindwa…
Sisi tunawafundisha kwamba kushindwa ni ada ya mafanikio.
Baba yangu aliniambia:
“Kama hujawahi kushindwa, hujawahi kujaribu kitu chenye thamani.”
Unawapa watoto pesa bila wajibu…
Sisi tunawapa wajibu kabla ya pesa.
Unawanunulia wanachotaka…
Sisi tunawafundisha namna ya kukipata kwa juhudi zao.
Mwisho wa siku—
Unalea watumiaji…
Sisi tunalea wajenzi
Mzigo Mzito Zaidi Mara Nyingi Huwepo Akilini Tu”
Kauli hii haimaanishi kuwa matatizo ya kweli hayapo…
Bali inaonesha ukweli mmoja mkubwa:
Akili yako inaweza kuumba mzigo ambao maisha hayajakupa.
1. Mzigo wa “Vipi Kama…”
Unajitesa kwa mambo ambayo bado hayajatokea.
•Vipi kama nitashindwa?
•Vipi kama watanicheka?
•Vipi kama mimi siwezi?
Hakuna hata moja lililotokea…
Lakini moyo unahisi kama tayari limetokea.
Unabeba hofu ya mawazo, sio hali halisi.
2. Mzigo wa Maoni ya Watu
Unahisi watu wanakuangalia, wanakuchambua, wanakuhukumu…
Lakini ukweli ni huu:
Kila mtu yuko bize na maisha yake mwenyewe.
Hata hivyo, wewe:
•Unajizuia kujaribu
•Unaogopa kusema ukweli wako
•Unaishi maisha ya kujificha
Unabeba macho yasiyokuwepo.
3. Mzigo wa Zamani
Kitu kilishapita… lakini bado unakibeba.
•Makosa ya zamani
•Aibu
•Kushindwa
Unakirudia tena na tena kichwani.
Tukio limeisha—
lakini mawazo yako yanaliweka hai.
4. Mzigo wa Kutaka Kudhibiti Kila Kitu
Unataka kila kitu kiende kama unavyotaka:
•Watu
•Matokeo
•Muda
Isipokuwa hivyo, unapata msongo wa mawazo.
Unabeba vitu ambavyo havikuwa chini ya uwezo wako.
Kwa Nini Mzigo Huu Unahisi Mzito Sana?
Akili yako haitofautishi vizuri kati ya:
•Hatari ya kweli
na
•Hatari ya kufikirika
Ndiyo maana hata bila tatizo halisi… bado unahisi umelemewa.
Ukweli wa Maisha
Watu wengi wamechoka si kwa sababu maisha ni magumu sana…
Bali kwa sababu wanabeba:
•Mawazo yasiyo na uhakika
•Hofu zisizo na msingi
•Hukumu za watu ambazo hazipo
•Taswira za mambo ambayo hayajatokea
Wanapigana na vita ambavyo havipo.
Jinsi ya Kuachia Mzigo
Jiulize:
•“Hii inatokea kweli sasa hivi?”
•“Nina ushahidi au ni mawazo tu?”
•“Hili litakuwa na maana baada ya mwaka mmoja?”
Kama jibu ni hapana…
Achia hapo hapo.
Mabadiliko ya Nguvu
Badala ya kusema:
“Vipi kama mambo yataharibika?”
Anza kusema:
“Vipi kama mambo yataenda sawa?”
Ukweli wa Mwisho
Uchovu wako hauji kwa sababu maisha ni magumu…
Unatokana na hadithi unayoijenga kichwani mwako.
Hivyo kuwa makini na unachobeba.
Kwa sababu mara nyingi…
umechoka kubeba kitu ambacho hakipo.
Yeremia 20:11 Lakini Bwana yu pamoja nami, mfano wa shujaa mwenye kutisha; kwa hiyo hao wanaonionea watajikwaa, wala hawatashinda; watatahayarika sana. Kwa sababu hawakutenda kwa akili, wataona aibu ya milele, ambayo haitasahauliwa kamwe. @Dr_DGwajima
@ayubu_madenge Na hio ndo suluhu ya foleni katika miji yote yenye idadi kubwa ya watu. Wekeza kwenye usafiri wa uma. Watu wataacha magari yao nyumbani na kupanda usafiri wa uma hence case solved. Sisi tunajua kushawishi watu wawe chama tawala tu!!!!
Happy birthday, mkubwa wa Taifa. Mama mwenye kiu na ndoto ya kuiona Tanzania bora yenye maadili na uchumi bora. Mungu akutunze siku moja uje uwe shuhuda wa kazi njema ya mikono yako. @Dr_DGwajima
@Dr_DGwajima@alvinsswai Mama hongera nimekupenda bure, si kwa sababu umejibu comment yangu bali jinsi unavyomjibu kila mtu kwa maoni yake. Nakuombea baraka zaidi katika majukumu yako. Unafanya kazi takatifu. Ila mama naomba tena, nifollow back tafadhari. 0744 914 924 nahitaji ushauri mama sio zaidi
@Dr_DGwajima@MwijakuBurton Asante waziri wangu, nmefarijika kwamba umenijibu kwa Hoja na nasio kwa...!!!!
Sasa naomba unifollow back mama yangu kipenzi. Natanguliza shukurani