Thamani ya uhai wa binaadamu inazidi kupotea mikononi mwa vyombo vyetu vya ulinzi na usalama. Visa vya mauaji yanayofanywa na askari wa hifadhi TFS na TANAPA ni rekodi mbaya sana ya ulinzi wa haki za binaadamu dhidi ya haki za wanyama na misitu. Wajibu wa askari ni kulinda usalama wa raia, raia akifanya kosa afikishwe mahakamani. Nchi inaelekea kuwa na kiwango cha chini kabisa cha utawala wa sheria. Taifa linalojiongoza kutokuwa na utii wa sheria ni Taifa linalokwenda jiangamiza lenyewe. @tanpol acheni haya mambo
Uko sahihi dada @MariaSTsehai . Sisi @ACTwazalendo tuna maslahi na uhai wa raia wa pande zote mbili za muungano. Hatuungi mkono mauaji ya raia wa Zanzibar yalofanywa na Rais mkapa mwaka 2001 na Rais magufuli mwaka 2020 kama vile tunavyoendelea kulaani mauaji ya Raia yaliyofanywa na Rais Samia mwaka 2025 kwa Tanganyika. Tumeweka rekodi hii kwa maamuzi ya vikao vya chama na kwa matamko ya wazi kwa ummah. As long as nina appreciate kazi kubwa ya utetezi wa haki za binaadamu unayoifanya, mimi kama kiongozi siungi mkono kabisa jitihada za kuwagombanisha raia wa nchi hii kwa misingi ya u Tanganyika na u Zanzibar. Tatizo la muungano wetu ni msingi uliojengwa na viongozi wa kisiasa kwa maslahi yao na si raia. Wa Tanganyika na wa Zanzibar hawakushirikishwa kabisa na hivyo wote ni wa hanga. Wa Zanzibar na wa Tanganyika waliweka wazi msimamo wao mbele ya tume ya jaji warioba kwamba wao wanataka muungano wa serikali tatu yaani tuwe na serikali ya Tanganyika, Serikali ya Zanzibar na Serikali ya Muungano. Msimamo huu wa wananchi ndiyo msimamo wa @ACTwazalendo wazalendo. Sisi tunaona tatizo la msingi la nchi hii ni uongozi wa @ccm_tanzania bila kujali ni wa upande gani wa muungano. Wote ni waovu na wameloa damu za Wa Tanzania. Sisi hatutofanya kosa la kumtetea CCM wa Zanzibar kwa kuwa Rais wa CCM anayeua Zanzibar ni m Tanganyika kama ambavyo hatumtetei CCM yeyote wa Tanganyika kwa hoja dhaifu kama Rais ni m Zanzibar. Wakati Mkapa anaua 2001 makamu wake alikuwa M Zanzibar so alihusika no excuse,Magufuli alipoua wa Zanzibar 2020 makamu wake alikuwa M zanzibar na ni muhusika kamili. Mauaji ya 2025 ya Samia haya waondoi CCM Wa bara wakiwemo makamu wake Mpango na sasa Nchimbi. Wote ni wahusika na wanapaswa kuwajibika. Kama hawaungi mkono wajiuzuru na watoke hadharani kulaani . U Tanganyika siyo excuse.
Inna lillah wa inna illaih Rraajioun. Hakika Huu ni Msiba mzito kwa Familia ya ACT Wazalendo. Mwenyezi Mungu akupe Maghfirah ndugu yangu Ponda Mjumbe wa kamati kuu ya chama chetu
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Othman Masoud Othman amesema kuwa Nchi nyingi zilizopiga hatua, hususan za visiwani, zilifanikiwa kutokana na misingi mbalimbali ikiwemo uwajibikaji na utulivu wa kisiasa.
Akizungumza leo Julai 9, 2026 Othman amesema Zanzibar ni Nchi inayotegemea huduma za kibiashara, hivyo hatua zinazochukuliwa katika kipindi hiki hazilengi manufaa ya kisiasa pekee, bali ni juhudi za kujenga na kuipeleka mbele Zanzibar kwa manufaa ya Wananchi wote.
Aidha, Othman amesema mchakato unaoendelea umeibua Makundi matatu ya mitazamo miongoni mwa Wananchi na Viongozi.
“Naomba tukiri kwamba pamoja na yote, tumefika mahali hapa tukiwa katika makundi matatu, wapo Viongozi na Wananchi waliofurahia hatua hii, wameiombea dua na wanatamani ifanikiwe, lakini bahati mbaya hawana sauti, mamlaka au ushawishi.”
Ameeleza kuwa kundi la pili linaundwa na watu waliokata tamaa kuhusu mchakato huo.
“Kundi la pili ni wale waliokata tamaa na kusema ni yale yale, hakuna jipya na wengine wanaapa na hata kuweka rehani vitu vyao.”
Kwa upande wa kundi la tatu, amesema linaundwa na Watu wanaopinga mchakato huo na wako tayari kuupinga ili usifanikiwe.
“Kundi la tatu ni wale wasioukubali mchakato huu na wako tayari kuupambana ili lolote lisifanikiwe. Hawa hawapingi mchakato huu pekee, bali wanapinga hata uwepo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa.”
#MillardAyoUPDATES
Tamko hili la Pamoja linabainisha azma ya pande mbili kuendelea kufanya kazi kwa pamoja ili kupata ufumbuzi wa kudumu na endelevu wa changamoto zinazoikabili Zanzibar kisiasa, kijamii na uendeshaji wa shughuli za umma.
#ZanzibarMpya#ZanzibarMoja#MamlakaKamili@ACTwazalendo
Mikutano ya hadhara ya vyama vya Siasa ni haki ya Msingi inayolindwa na katiba na sheria za nchi. Waziri wa Mambo ya Ndani hana mamlaka yeyote ya kuvunja Katiba. Agizo lake ni HOTAIR na Bwana IGP akitii agizo hili atakuwa ni mtu wa hovyo.
Mamlaka ya kutoa ulinzi wa Mikutano ni ya OCD, IGP hatajwi popote kwenye sheria ya vyama na hata huyo OCD hana mamlaka ya kutoa au kutotoa kibali. Vyama haviombi vibali vya mikutano, vinatoa Taarifa.
Bwana Katambi sijui kitambi amejiongelesha tu na OCD yeyote atakayefuata maelekezo haramu na ya kisiasa ATASHTAKIWA KAMA MTU BINAFSI
Leo nimepata fursa ya kufanya mazungumzo ya kina na viongozi wa @NgomeyaVijana ya @ACTwazalendo taifa katika ukumbi wa Juma Duni Haji, uliopo ndani ya jengo la maalim Seif ,makao makuu ya chama.
Vijana ndiyo nguvu ya mabadiliko,walinzi wa matumaini ya wananchi na injini ya mapambano ya kidemokrasia,haki na maendeleo. Chama chochote chenye vijana imara,wenye uelewa na ari ya kujitolea, kina hazina kubwa ya ushindi wa sasa na wa baadaye
VIDEO:
Makamu Mwenyekiti wa chama cha ACT Wazalendo Zanzibar, Ismail Jussa Ladhu amesema kuwa chama hicho kimeandaa mkusanyiko mkubwa ili kuzungumzia matokeo ya tume ya Rais iliyopewa jukumu la kuchunguza matukio ya Oktoba 29, 2026.
Jussa amesema hayo akihutubia Kongamano la Kitaifa la Wadau wa Demokrasia nchini leo Jumamosi, Mei 16, 2026, jijini Dar es Salaam. Amesisitiza kuwa kwa sababu ripoti kamili ya serikali ilibaki kuwa siri (binafsi), uongozi wa chama hicho ulifanya uchambuzi wa kina kulingana na muhtasari uliotolewa na Jaji Chande, na baadaye kupelekea azimio rasmi la ndani la kuongoza mjadala wa umma.
Amesisitiza kuwa tukio hili limekusudiwa kuwa mjadala mpana wa kitaifa badala ya kuwa mkutano wa kivyama, likilenga kuunganisha wadau mbalimbali ili kutafakari juu ya mustakabali na utulivu wa Tanzania.
Zama za Ofisi ya Msajili wa Vyama kuwa mchezaji namba 12 wa CCM FC zimekwisha.
Dola isome alama za nyakati. The writing is on the walls!
Msajili STOP THIS NONSENSE ya kutaka kufuta CHADEMA. Utafutwa wewe, No doubt about this!
Tume ya Chande iliyoundwa na Rais imetoa Taarifa inayosema wananchi wanailalamikia Ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa kutokutenda haki kwenye kusimamia shughuli za vyama vya Siasa. Badala ya Msajili kuchutama, kuwajibika na kubadilika anarudia makosa yaleyale yaliyopelekea mauaji yaliyoanza Oktoba 29.
Msajili anajua, Watanzania wanajua na Dunia inajua kuwa Kuna ushahidi wa kutosha wa CCM kufanya makosa makubwa kuliko hata ambayo msajili ameituhumu Chadema, hatukuwahi kuona hatua zozote zimechukuliwa na Ofisi hii ya Msajili.
Ofisi ya Msajili ijue WATANZANIA SIO MABWEGE. Tunachukulia tishio lolote dhidi ya CHADEMA ni tishio dhidi ya Demokrasia. An attack to one, is an attack to all.
Iacheni CCM ifanye Siasa za Ushindani dhidi yetu. Nasi tufanye siasa za ushindani dhidi yao.
Acheni kuwa mbeleko ya CCM. Mtaanguka nayo. Ujumbe huu sio wa Msajili tu bali pia ni kwa VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA pia. Kaeni pembeni acheni vyama vya Siasa vifanye Siasa.
Mnataka watu wangapi wafe ili mpate somo?