@PolycarpMDM Wew ndo hujaelewa lengo lilikuwa ni kujenga mwendokasi usafiri wa umma. Na si usafiri wa watu binafsi. Hata wangepanua barabara 4 zingekuwa hazina maana kama zinaenda kuishia mwenge mataa alafu foleni linaendelea kama kawaida.kupanua barabara ni ghali itakubidi ulipe fidia watu
Oohh hakuna Gari la MILIONI
Haya hii hapa, inahitaji rangi tu.
TOYOTA DUET #BMN 🔥🔥
▪️CC. 1300
▪️ENGINE SAFI
▪️GEARBOX SAFI
▪️FULL DOCUMENTS✅️
#TZS 1,800,000/=
IPO DAR
SAFARI POPOTE
CALL/WHATSAPP-0719542184
Nikihitimisha ziara yangu ya Kitaifa katika Shirikisho la Urusi, leo pamoja na mambo mengine nimepata fursa ya kuhutubia Jukwaa la Biashara kati ya Tanzania na Urusi pamoja na Jukwaa la 29 la Kimataifa la Uchumi la St. Petersburg (SPIEF), ambayo yamekutanisha viongozi, wataalamu wafanyabiashara na wawekezaji kutoka mataifa mbalimbali.
Nimewahakikishia wawekezaji kuwa Tanzania ni sehemu salama na bora kwa mitaji yao, tukijivunia mazingira wezeshi ya kisheria, amani na utulivu, miundombinu bora, ukuaji imara wa uchumi, uwepo wa nguvu kazi na fursa ya kufikia soko la zaidi ya watu milioni 500 ukanda wa Mashariki na Kusini mwa Afrika. Pia, nimebainisha sekta za kimkakati ambazo ni kipaumbele katika uwekezaji zikijumuisha madini, kilimo, nishati safi, mafuta na gesi, afya pamoja na usafiri na usafirishaji.
Habari njema zaidi ni kuwa, kuanzia Julai 2026, Kampuni ya Ndege ya Tanzania (ATCL) itaanza safari za moja kwa moja kati ya Dar es Salaam, Zanzibar na Moscow. Hatua hii muhimu itaimarisha zaidi utalii, biashara na uwekezaji, na kufungua ukurasa mpya katika historia ya uhusiano na ushirikiano kati ya Tanzania na Urusi.
@SuluhuSamia Asante kwa uchapakazi wako uliotukuka Mheshimiwa Raisi wetu, Nguvu uliyoitia katika kuliunganisha izidi mara dufu mpaka mikoa yote iungane kwa barabaracza lami Tuamie kwenye Wilaya.
Siku ya kwanza ya ziara yangu ya kitaifa katika Shirikisho la Urusi ambapo pamoja na mambo mengine, nimepata heshima ya kukutana na kufanya mazungumzo na Mheshimiwa Rais Vladimir Putin jijini Moscow.
Kwa pamoja tumepongeza ukuaji wa biashara kati ya nchi zetu uliofikia asilimia 72 katika kipindi cha mwaka 2020 hadi 2025. Hata hivyo, kwa kuzingatia historia kubwa ya ushirikiano na uhusiano wa kirafiki kati ya mataifa yetu, tumekubaliana kuongeza juhudi za kukuza biashara na uwekezaji ili kuleta manufaa makubwa zaidi ya kiuchumi na ustawi wa wananchi wa nchi zetu.
Aidha, kwa lengo la kufungua fursa zaidi kwa wananchi na kuharakisha maendeleo ya kijamii na kiuchumi, tumejadili namna ya kuimarisha ushirikiano katika sekta mbalimbali za kimkakati, zikiwemo sayansi na teknolojia, elimu, nishati, madini, kilimo, miundombinu na utalii.