#TajiriLaKihaya
Hoja yako ina sehemu muhimu, Haki inaweza kucheleweshwa na momentum ya kisiasa inaweza kubadilika. Lkn hapa ndipo nadhani hoja yako inahitaji kujengwa upya.
Siku zote kucheleweshwa kwa haki si ushahidi kwamba mapambano yameshindwa.
Nakujibu kwa mifano 👇
1/7
2015 Sirjeff aliitwa SA 🇿🇦 akatoa presentation mbele ya Billgate Billgate nae alikuwa SA 🇿🇦 mind you Billgate alikuwa tajiri no 1 duniani
Siku hiyo Jeff akapewa tuzo ya mjasiriamali bora wa mwaka
Bongo tulipata bahati ya kupata Genius mwenye IQ kubwa baada tumtumie tumemfunga
HUU NI UONGO FLAVA
It’s sad to see, Wasanii wanatumika kisiasa hadi kuruhusu Muziki wao kushushwa thamani ili Serikali Haramu ijihalalishe.
NINI KINASHEREKEWA? LINI KIMETIMIZA MIAKA 30?
Neno Bongoflava lina miaka takriban 32, which means na Muziki wenyewe ni older than 30. Sasa hiyo 30 imetoka wapi? Na lini tulikubaliana kuwa kila muziki wa Tanzania ni Bongoflava? Maana show ilijaa Rappers? nachojua ni kwa ujumla tunaitaga “Muziki wa Kizazi Kipya” na Bongoflava huwa ina refer Muziki wa Waimbajii. Ni kama Watu wame-force narrative!
UNAADHIMISHAJE MIAKA 30 YA KITU BILA KUHUSISHA WAASISI?
Yaani Show yao ilijaa watu ambao ni wa miaka 15-25 iliyopita na sio 30; kama kweli unataka kuenzi Muziki wetu, unapaswa uanze 34 - 30 years ago. Saleh Jabir, Mr II Sugu, Hard Blasters, Kwanza Unit, Mawingu Band, Unique Sistaz, GWM, Deplowmatz, etc Inabidi ushirikishe Taji Liundi, Mike Mhagama, Radio One, TVZ, ITV… Kiufupi mmepuyanga na kuudogosha muziki!
Ilikuwa golden opportunity ya kuwa na proper documentary, full representation ya Waasisi na ikiwezekana kuwaenzi Jukwaani, ila nyie mmejiwaza wenyewe tu na kutaka kuIhalalisha Serikali Haramu.
“BRIDGING THE GAP” & WHERE ARE THE FLAG BEARERS?
Ukiongelea kitu cha miaka 30, haimaanishi uwe na watu waliofanya Zamani tu. Show imekuwa ndogo sababu current flag-bearers wanao uwakilisha muziki hawakuwepo. Pengine wasingeimba nyimbo zao, bali kuimba za Wakongwe. Imagine Diamond na Ali Kiba wanaimba “Anakudanganya” wa B Love M, Zaiid anaimba “Kukuru Kakara Zako” wa Sos B, Young Lunya na OMG wanaimba “Kula Kona” ya Manzeshe Crew, au “Cheza Mbali na Kasheshe” wa GWM, Temayai waimbe “Run Tings” wa Kwanza Unit, Abby Chams na P Mawenge wanaimba “Sikiliza” wa Unique Sistaz ft Hashim Dogo.
POOR PERFORMANCES
Watu walioenda kuimba ilipaswa wafanye mazoezi ya live. Yaani Unaandaa show unawaza kuwaweka Hotelini tu na sio kuwapa budget ya Rehearsal ya japo mwezi. Where are your priorities?
Audience ilikuwa ya watu wa Gen X na Millennials, na ni watu ambao wana-appreciate live music na quality performances. Wamefata Nostalgia, basi mngewapa zawadi ya quality show badala “Show Mazoea”!
KUTOKIDHI HADHI
Huwezi kuwa na Lineup ya “Kifiesta fiesta” alafu ukaipeleka Mlimani City; mngefanya Viwanja vya Posta au Leaders! Pia demographic inayovutiwa na Miaka 30 sio watoto wa miaka 25! So kuipeleka M-City na kujua kuwa audience ni majority of 35 - 55 yrs, basi ingekuwa a VIP and VVIP event. Kuna watu wana Gout mmewasimamisha masaa pale!
Tatizo Waandaaji ni wa Mchongo; Fid Q ambae show zake huwa zina mapungufu, na Madee ambae hajawahi hata andaa uzinduzi wa Video Launch. Na nyuma ya pazia yupo Mtoa Maboko namba moja, Paul Makonda na Babu Talent.
HITIMISHO
Watu wanataka burudani, mmewapa burudani mbaya, na kibaya zaidi mkataka kuchomeka siasa! Na Wasanii Njaa na Chawa nao wanaendelea kujiuza kirahisi tu kwa watu ambao hawawasaidii chochote!
Platform pekee inayoenzi Bongoflava ni BONGO FLAVA HONORS ya Deiwaka Ent (Sugu), huu upuuzi mwingine ulikuwa ni SAMIA KINGS & QUEENS 2.0 wakitaka kuturubuni ila TUMESHTUKA.
The Leader
Hii press ya GWAJI BOY ilifungua ndonga za watanzania wengi sana.
DIKTETA JIKE linaisoma namba huko.
Jitu linasema lilichaguliwa kwa asilimia 90 linaapishiwa MBUGANI.
Kila siku watu wanaongelea maandamano.
Miji mikubwa MAGARI YA MAASKARI, WANAJESHI na mabuduki wanazurura zaidi ya mwezi mzima.
Na huu sio mwanzo SAMIA huu ndio utakuwa UTARATIBU wetu kama taifa wewe si CHURA KIZIWI?
TUTAKUWEPO🫵🏾😎
Tarehe 7/7 SabaSaba
KITAWAKA SAAANAAA!!
Kwenye hii Round of 32
👇🏻
Argentina atamkanda Verde
Ataingia Round of 16.
Egypt atamshenyeta Australia
Ataingia Round of 16.
Tarehe 7/7 sabasaba
watakutana.
Utachezwa mchezo number 95
kati ya
Argentina vs Egypt.
Kitawaka sanaaa!!
🔥 🔥 🔥 🔥 🔥
Unajua kwanini kitawaka??
Kwasababu mmoja anasherekea Uhuru, mwingine anasherekea mapinduzi!!
Kumbuka mataifa yote haya mawili mwezi wa saba kwao ni mwezi mkubwa sana.
Argentina anasherekea uhuru July 9th
Egypt anasherekea mapinduzi July 23.
July 7/7 kwa moto sanaaaaa!!!
Zifungwe Big Screen Tu Mtaani.
Mechi kali hii.
Ukiachana na huo utani wa “Millennials” na “Gen Z”, kuna eneo moja nakubaliana na Gen Z 100%. Ni ukweli kwamba Millennials tumelifikisha Taifa letu matopeni. Hatuwezi kuiwajibisha Serikali hata inapokosea.
Millennials ndiyo uti wa mgongo wa utumishi wa umma kwa sasa; sisi ndiyo injini ya nchi. Lakini injini hii ikikubali kufanya kazi kwenye matope bila kuhoji kwanini barabara haitengenezwi, nchi inabaki palepale.
Kizazi chetu kwa sehemu kubwa ndiyo watumishi wa umma, hata tusipoongezwa mshahara na marupurupu kwa miaka 10, tunaona ni sawa tu. Tunaona ni kawaida na ndiyo kitu ambacho kama watumishi, tunastahili.
Kizazi cha wasomi wengi kimegeuka kuwa kizazi cha “ndiyo mzee.” Millennials wamekuwa watulizaji (stabilizers) wa mfumo hata kama ni mbovu. Gen Z ni wavurugaji (disruptors) wa mfumo ili ukae sawa.
Hofu ya kupoteza mshahara inayoweza kusababisha watoto wakose ada/familia ikose chakula imewafanya Millennials kuwa waoga (risk-averse). Hii imetengeneza kizazi kinachopendelea diplomasia ya unyenyekevu.
Kwa sababu ya familia, tumekuwa kizazi cha viumbe wabinafsi sana. Hatujui kudai haki zetu, na tumezalisha machawa na wapambe wengi. Kizazi chetu kimeasisi mfumo wa kusifu na kuabudu (sycophancy).
Tazama, hata machawa wakubwa na wazito (pro-max) wanaosifu na kuabudu Serikali hii ni kizazi cha Millennials. Wasanii wakubwa wa muziki wa kizazi kipya ambao ni wafuasi wa watawala ni Millennials.
Gen Z wengi bado hawajazama kwenye majukumu mazito ya kifamilia, hivyo wana ujasiri wa kupaza sauti bila kuwaza “kesho nitalishaje watoto.” Hawalazimiki kuwa machawa ili waweze kuendesha maisha yao.
Gen Z wanakuja na utamaduni tofauti: wako ‘connected’ na wanatumia teknolojia ipasavyo. Wanaona wenzao duniani wanavyowajibisha serikali zao, hawaamini katika uvumilivu wa miaka 10 bila ongezeko la maslahi.
Hawahitaji mikutano ya siri; wanatumia simu kuanzisha mijadala, kuumbua ubadhirifu, na kuungana kwa kasi ya ajabu. Hii imepunguza nguvu ya machawa ambao walizoea kutawala simulizi za mtandaoni. Safi sana.
Wakati Millennials walifundishwa kuwa na shukrani hata kwa kidogo (ile dhana ya bora mkono uende kinywani), Gen Z wanauliza: “Kwanini iwe kidogo wakati rasilimali zipo?” Hapa ndipo sasa nawakubali madogo hawa.
Hawa Gen Z wana uwezo wa kuungana kama kizazi bila kujali itikadi za vyama, kitu ambacho Millennials wengi wameshindwa kwa sababu ya kuweka mbele maslahi ya ajira zao. Wamekataa mambo ya “Status Quo.”
Gen Z wamevunja mwiko. Millennials wamefungwa na nidhamu ya uoga au hofu ya kupoteza walichonacho, sasa wanatazamana na kizazi kinachoongozwa na kanuni moja kuu: “Haki haiombwi, haki inadaiwa.”
Labda shinikizo hili la Gen Z litatumika kama kioo cha kuwafanya Millennials wajione walivyojipoteza. Binafsi, wananikosha sana. Gen Z wanaupiga mwingi. Mimi nawatia moyo, wasiogope. Kaka zao tupo pamoja nao.
Gen Z, take a bow, fellas.
Ukiona umekata tamaa, umechoka, hutaki hata tena kwenda ofisini, shambani, masomoni nk
Jitahidi hapohapo kabla ya kuacha uendelee tena mbele kidogo, ushindi umekaribia
Umechoka, hujisikii, unaumwa jitahidi ujisukume hivohivo