Hebu tuwaze nje ya BOX!!🤔
What if, ni mchezo wanautengeneza ili kumfanya VICEnt apate sympathy kwa wapiga kura….kisha ndio iwe next kete yao 2030!!🤔
Yes, coz sio mara yao ya kwanza kuyafanya hayo!! Wameshaitumia sana hii strategy huko nyuma na wakafanikiwa!!
Nikurudishe 2017
TAL alipopigwa pyuu pyuu 🔫
wengi walimchukia Banza kwa lile
tukio!!
Hisia zangu zinanambia #MasterMind aliitumia hii opportunity akamtuma Kizim-Job akampe pole TAL!!
sidhani kama ile move ya kwenda kumuona na kumpa pole TAL ilikuwa bahati mbaya ile, huwa always nahisi it was strategically planned na pengine mtoa pole hakujua kama ni mchoro anachorewa, yeye aliamini anatenda utu….but kuna watu behind the scene walipush ile move!!
Ili kumjengea sympathy,imani na upendo kwa raia, kwamba kati ya wanachama waandamizi wooote, ni huyu pekee kajitoa kwenda kumuona mgonjwa.
Basi huyu ana upendo sana!
Basi huyu atatufaa kutuongoza!
Huyu sio katili kama Banza!!
Kumbe MasterMind anasema huyu
Ni next kete yetu tutamtumia siku za mbeleni, tayari anauzika kwa wapiga kura!!
Haya miaka imepita….
vipi leo bado sio katili!!?🤔
Sasa nashangaa sana kuwaona baadhi ya wanafamilia wakiingia kwenye huu mtego tena mapema sana, bila hata kuwaza nje ya box!!
Tena wengine ni watu senior na very influential kwenye siasa na harakati!!
Wanaanza kumpongeza VICEnt kuona huruma, kumfanyia PR na kumu-endorse kwa raia….Pasi kujua kufanya hivyo ni kurudia makosa yaleyale ya kujikuna Nyashi kisha unakata kucha kwa meno!!
Ni kweli VICEnt anaonekana kuwa mtu poa currently, lakini shida ni familia ileile!!
Iko hivii…..hawa jamaa ni very smart na calculated!
Wanajua fika now wako kwenye nyakati ngumu sana kujiuza kwa wananchi kutokana na waliyoyafanya….Nyama ngumu kwelikweli!!
Wana changamoto kubwa
ya who is next? ambaye wata msimamisha na raia wakampokea na kumkubali bila makwasukwasu yoyote!!
Hapo sasa kwenye Who is next, ndiyo nahisi #The_Master_Mind huwa anakujaga na mchoro wa kutafuta exit!!
Kwamba watengeneze beef/vita/misunderstandings wao kwa wao ndani kwa ndani, then habari zitoke nje kwa raia….kuwa kuna mpasuko ndani ya chama!!
Then ile kete wanayoitaka wao ndio ionekane kwa raia kama ndiyo inaonewa ndani ya chama au kama ndiyo shujaa inasimama na raia!!
Na raia tulivyo na mtindio wa ubongo tunajaa kwenye huo mfumo!
Tena wakati mwingine #MasterMind anaweza akachezesha huu mchoro bila hata kuwashirikisha wahusika wakuu, yaani main characters wakawa wanapasuana kiukweli, kumbe kuna mtu behind the scene anawachezesha filamu!!
Anagusanisha nyaya, anapigisha cheche bila wao kujua….
KUWENI NA MISIMAMO
KUWENI NA KUMBUKUMBU
WAZENI NJE YA BOX
MSIJAE KIZEMBE
Nways labda niko wrong na hisia zangu!!
Tatizo naangalia sana movies za watu waBad wanavyoRemote Gavoo na Viongozi!!
zinaniharibu sana!!
@Roma_Mkatoliki Kuna namna tokea itoke ripoti ya tume, kuna watu wamebadili gia angani
na kujifanya wako upande wa wananchi japo kiuhalisia sio kweli
Opportunistic wanaotafuta ulaji wasio na misimamo, bendera fwata upepo.
@mchina_jr94958 Huyo anatuzuga tu, kwanini chama chake kilishiriki uchaguzi huku wakijua kuna mapungufu, na hapo kati alipoa
Kunakitu kinapikwa hapo sio bure.
Ile interview ya Mzee Mahita, yule ka’mkubwa anayemuhoji namkubaligi sana✅
But amenishangaza kila mzee anapoongelea matukio yake aliyoyafanya yeye anacheka tu,
means anafurahia🤔
I was like, what's so funny here😳
Mzee anasema alivyokuwa katili, alivyomzingua Mrema na Cuf,
Ka’ mkubwa anafurahia kila punchline! Ni kama alikuwa ana mu-entertain.
Sout Out kwa SD, sista ako very calm!
Na ukisoma comments za ile interview kuna watu wamemsifia sana mstaafu yule kwa utendaji wake wa kazi!!
I can see miaka 10/20 ijayo wakina Mzee Murilo, Wambura watakuja simulia utendaji wao wa kazi walioufanya na watu watapiga makofi kuwapongeza!!
Watanzania tunawahi sana kusahau!!
Moja ya kitu kinaninyima usingizi recently ni hili swala la wanaharakati kuwa wanalipwa!! (Kama ni kweli)🤔
Hizo taasisi au watu binafsi wanaolipa wanaharakati, huwa wanatazama vigezo gani kukulipa?
Influence? au Numbers (Followers)
au uwezo wa kuongea na kuandika au engagement ya social media au nini?
Binafsi nimeanza hii course ya harakati tokea siku namaliza form six na kutoa wimbo wangu wa kwanza Tanzania (2007) nikiwa very young!
Hadi leo nina Teremsha bunduki 2026!
Miaka 19 kwenye hizi harakati
NA SIJAWAHI KUPEWA HATA SHING 10 TOKA KWENYE HIZO TAASISI!!
WALA KULIPWA NA MTU BINAFSI ILI NIFANYE HIKI NINACHOKIFANYA!!
Na kuna muda unakuwa na uhitaji haswa, tena sometimes ni uhitaji wa kufanya projects hizi hizi za kusaidia hizi harakati….. you just end up using your own pocket money!!
Kwenye hizi harakati nakutana na challenge nyingi, nakosa opportunities na michongo kwasababu naonekana niko against na gavoo na kuna muda napoteza hata kidogo nilichobakiza!!
Nabaki empty hadi familia inakwambia si utemane na hizo mbanga……nawajibu I WAS BORN TO DO THIS!!
Ni kama roho/nafsi inakataa ku-give up!!
Tunafanya haya kwa passion,
kuna a driving force tu inatusukuma kutetea, kukemea, kushauri na kupaza sauti tunapoona haki inakosekana, maendeleo hakuna, rushwa na ufisadi kwa viongozi vinakithiri, umasikini unazidi kwetu sisi raia, uongozi na utawala mbovu, shida za ajira na miundo mbinu, watu kutekwa, kufungwa na kuuliwa bila hatia na kucreate awareness kwa raia kuhusu issue za kisiasa na kijamii etc.
Nikisikia mtu anasema kuyafanya hayo ni unalipwa…..nawaza nakosa majibu!!
Wanatumia vigezo gani kukulipa?
Hebu mtu anieleweshe pengine napishanaga na gari la mshahara!!
Followers ninao (1.3M) influence pia si haba nikitoa miwa inapokelewa mtaani!! MBONA MIMI SILIPWI?
Nways tusiache hizi harakati hata kama hazitupi pesa kwa sasa, faida yake mbeleni ni kubwa zaidi kwa nchi nzima na vizazi vijavyo!!
Kama nimeandika kwa hisia sana ee?😁