Dear Augustino Lissu, stay stronger and thank you for showing up to demand your father’s liberty. SC Tundu Lissu is extremely proud of you. Stay vigilant & unbowed, son. Wear that AURA and walk his talk, young🐐!
#BREAKING: JUKWAA LA MAJAJI AFRIKA LASISITIZA KESI YA LISSU KUAMULIWA KWA HARAKA
Jukwaa la Majaji na Wanasheria wa Afrika (AJJF) imeitaka Mahakama ya Tanzania kuharakisha mashauri ya jinai dhidi ya kiongozi wa upinzani Tundu Lissu, ikionya kuwa ucheleweshaji wa kesi unaweza kudhoofisha imani ya umma kwa taasisi za haki.
Katika taarifa yake, AJJF ilibainisha kuwa mashauri yanayomhusisha mwanasiasa maarufu huvutia uangalizi wa kitaifa na kimataifa, hivyo uwazi na kasi ya uendeshaji ni muhimu.
Jukwaa hilo lilionya kuwa “haki ikicheleweshwa inaweza kuathiri imani ya umma kwa mahakama na mfumo mpana wa utoaji haki.”
AJJF ilisisitiza kuwa uamuzi wa haraka na wa kuaminika unahudumia maslahi ya mtuhumiwa na ya Serikali, huku ukilinda uthabiti wa demokrasia.
Pia ilihimiza mahakama za Tanzania kutekeleza wajibu wao wa kikatiba kwa uhuru na weledi, kuhakikisha mashauri yanaheshimu viwango vya haki ya kusikilizwa na kuimarisha imani ya wananchi kwa utawala wa kikatiba.
MAHAKAMA KUU YA TANZANIA IMEMZUIA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA KUIFUTA CHADEMA AU KUITOZA FAINI.
Moja kati ya sababu zilizotolewa na Mawakili ni kwamba Msajili ameonyesha upande kwamba anaifuta CHADEMA au ataitoza faini wakati baruahiyo ilikuwa hata bado haijajibiwa na CHADEMA.
Kwamba kwenye barua hiyo Msajili yeye ndo mlalamika, yeye ndo shaidi na wakati huo huo yeye ndo Jaji kwa maana hii hawezi kutenda Haki.
Unaweza kusoma uamuzi wa Mahakama👇
Hii Video ni ya Oktoba 29,
Hapa ni Morocco hotel pale Magomeni kama mnavoona Watanganyika walikuwa wameandamana hawajashika silaha yoyote sio jiwe wala sindano lakini Polisi waliamua kuwatawanya kwa kutumia risasi za moto kuna wengi walipoteza maisha.
Lakin leo Waziri Kombo anasema kwamba siku ya Oktoba 29, Watanganyika walioandamana walikuwa wanawarushia mawe Polisi.
Nadhan sasa ni muda muafaka Nduli Idd Amin Mama na hao vilaza wenzake akina Kombo watuletee hiyo video ya Watanganyika wakiwarushua mawe Polisi.
Taarifa: Ili kumuunga mkono Mwenyekiti wetu Lissu na struggles zake gerezani, nimeamua kumuiga style yake mpya ya nywele…Sitachana wala kunyoa nywele zangu mpaka atoke jela akiwa HURU✌🏾✌🏾
#LiMwenyekiti#KatibaMpya#FREELISSU
Kenya itazidi kutuacha mbali mno kwa kila kitu… Chanzo cha ufisadi, wizi na ujambazi wa mali za umma ni usiri wa mikataba na makubaliano.
Kuna ujambazi mkubwa kwenye mikataba ya bandari zetu kupewa Waarabu, viwanja vya ndege, misitu kwa Oman, gesi yetu, dhahabu zetu ikiwemo mkataba mpya wa Sengerema Nyanzaga, huu mgodi utakua mkubwa kuliko yote Nchini..kuna mikataba ya mbuga za wanayama, mikataba ya nickel na cobalts kule Kabanga. Kuna mkataba wa uranium na Urusi kule Namtumbo..
Tunaweza kutaja maelfu ya mikataba ambayo inafanywa siri ya hawa mafisadi wasio na huruma na Watanzania.
Mkataba wa ujenzi wa SGR ya Tanzania ni uchafu mkubwa, kuna kipande kimejengwa kwa usd milioni 3.9 kwa kilometa na kingine kinajengwa kwa usd milioni 5.5 kwa kilometa bila ushindani. Mikataba ya manunuzi ya mabehewa ya hovyo.
Mikataba ya ujenzi wa barabara takataka ambazo zinabomoka siku ya pili baada ya kukabidhiwa, mikabata ya wizi ya BRT Dar, ununuzi na ujenzi wa Meli Mwanza.
Katiba ya Kenya inawapa Wakenya fursa ya kuona huo uchafu na kuchukua hatua.
Ndio maana Watanzania lazima tupiganie Katiba mpya ili tukomeshe huu ushenzi unaotutesa na kutuacha masikini kwa miaka mingi.
Tunataka katiba mpya sasa.