Today, @SenatorShaheen advanced multiple pieces of bipartisan legislation at the SFRC business meeting.
Read more about the bills here โก๏ธhttps://t.co/jbBhrG3PMi
HUU NDO UJUMBE WANGU AMBAO NIMEMTUMIA MKUU WA MAJESHI YA ULINZI TANZANIA, JENERALI JACOB MKUNDA.
๐๐๐๐
Kwako CDF Mkunda,
Ni matumaini yangu kwamba umzima wa afya.
Wewe unaitwa Mkuu wa Majeshi Tanzania kwasababu majeshi yote nchini yapo chini yako kwa mujibu wa Katiba yetu ya Tanzania.
Jeshi lenu linaitwa Jeshi la Wananchi sio Jeshi la Rais wala Serikali kwasababu moja kati ya majukumu yenu ni kulinda Uhuru wetu, kulinda Usalama, na mipaka ya nchi yetu.
Kabla ya Oktoba 29, kuna Wanajeshi kutoka nchi ya Uganda waliingia Tanzania, taarifa zilisambaa kila kona lakini wewe na vikosi vyako vyote mlikuwa kimya licha ya kwamba ulikuwa unajua kuwa kuna uwepo wa Jeshi kutoka Uganda na unajua Katiba ya Nchi hairuhusu jambo kama hilo.
Oktoba 29, tulipoteza Watanganyika wenzetu zaidi ya elfu kumi ambao waliuwawa kwa risasi na waliofanikisha mauaji hayo ni Jeshi la Polisi, TISS, KMKM na Wanajeshi mamluki kutoka Uganda.
JWTZ mmeshindwa kulinda mipaka ya nchi yetu ndo maana Wanajeshi kutoka nchini Uganda waliingia Tanzania kwa msaada wa Jeshi la Polisi Tanzania, na wakapewa majina feki na bunduki ili wauwe Watanganyika wenzetu, mamluki kutoka Uganda, TISS, KMKM, Polisi na baadhi ya Wanajeshi wako walishirikiana kikamilifu kuwamiminia risasi ndugu zetu bila hata chembe ya huruma.
JWTZ mmeshindwa kulinda usalama wetu na usalama wa nchi yetu ndo maana kabla ya Oktoba 29 ndugu zetu zaidi ya 600 walitekwa na kupotezwa na hata baada ya Oktoba 29 hali imezidi kuwa mbaya maana bado watu wanaendelea kutekwa na kupotezwa na wengine tunawindwa kila kona, tunaishi kama digidigi halafu bado nyie mnaguts za kujiita Jeshi la Wananchi, Jeshi gani la Wananchi ambalo haliwezi kulinda usalama wa hao Wananchi wake?
JWTZ mlishindwa kulinda uhuru na usalama wetu, maana kulinda Uhuru na usalama wetu ilikuwa ni pamoja na kuhakikisha Maandamano ya Wananchi ya Oktoba 29, yanafanyika kwa amani na yanaisha kwa amani, lakini nyie mlitulia tu mkaacha vikosi vya Samia vimwage damu za maelefu ya Watanganyika ambao waliuwawa kwa risasi.
Kibaya kuliko yote baadhi ya Wanajeshi wa JWTZ ambao walionekana wakilinda Maandamano ya Wananchi Oktoba 29 maeneo mbalimbali nchini.
Baada ya Oktoba 29, wewe CDF uliagiza wakamatwe na wafunguliwe kesi kwenye Mahakama ya Kijeshi (Court Martial) mkawabambika kesi kwamba walichochea Maandamano, yani kwa lugha nyepesi ni kwamba wewe CDF, ulichukizwa sana sana kwa kitendo cha baadhi ya Wanajeshi wako wa JWTZ kulinda Wananchi ili wasiuwawe kwenye maandamano ya Oktoba 29, means ulifurahishwa sana na mauaji ya Watanganyika wenzetu siku ya Oktoba 29.๐ญ
Mahakama ya kijeshi ( Court Martial) iliwatia hatiani Wanajeshi ambao walijitolea kulinda Wananchi siku ya Oktoba 29 ili wasiuwawe, Yani wanajeshi ambao walijitolea kutulinda Oktoba 29, Wamefungwa wapo magereza wanasota wakati huo Viongozi wa ulinzi na usalama walioshiriki kuuwa kwa risasi Watanganyika zaidi ya elfu kumi wapo mtaani wanatamba bila wasiwasi licha ya kwamba hata wewe mwenyewe unawajua kwa majina na sura zao.
Hii dhambi itakutafuna wewe na kizazi chako mpaka siku unaingia kaburini.
NB. Hii video ambayo nimekutumia hapa huyu ni Mwanajeshi wako wa JW, kamvua nguo raia na kumtesa hadharani, huu ndo ukatili ambao baadhi ya Wanajeshi wako walikuwa wakiwafanyia watu siku ya Oktoba 29, hili tukio lilitokea Tunduma siku ya Oktoba 29z
Ndimi Hilda Newton,
Mwanachama wa Chadema na Mwanaharakati wa Haki za Binadamu.