Mwenyekiti wa CHADEMA @TunduALissu akisalimiana na Jaji Mkuu Mstaafu wa Kenya @dkmaraga ambaye amefika Mahakamani kusikiliza kesi ya uhaini na uchochezi alizopewa Tundu Lissu. Wakati huo Jaji Mkuu Mstaafu wa Kenya @WMutunga amezuiwa kuingia Tanzania, anashikiliwa JNIA.
#TANZANIA:WALIODUKUA AKAUNTI YA POLISI TANZANIA KUSAKWA
Jeshi la Polisi nchini Tanzania limetoa taarifa rasmi likieleza kuwa linawasaka watu wote wanaodaiwa kuchapisha taarifa za uongo, za kupotosha, na zisizo na maadili kupitia akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa X (zamani Twitter), kwa lengo la kuupotosha umma kwa madai kwamba taarifa hizo zilitolewa na jeshi hilo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa mapema leo, Jeshi hilo limeeleza kuwa taarifa zilizoenea kwenye mitandao ya kijamii kupitia akaunti yake rasmi, pamoja na akaunti nyingine kadhaa, hazina uhalisia wowote na zimechapishwa na watu wasiojulikana.
Jeshi hilo limetoa onyo kwamba hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya mtu yeyote atakayebainika kueneza taarifa hizo kwa namna yoyote ile.
NINARUDIA kusema wanaoondoka CHADEMA ni wale walioingia kwenye siasa kwa ajili ya fedha na vyeo. Wanaobaki ni raia wema wenye uchungu na nchi na wanaumizwa na ufukara wa wananchi wengi na hivyo wako tayari kuunganisha nguvu kudai MABADILIKO, na Mungu yupo nao
Kisutu Resident Magistrate’s Court in Dar es Salaam.
Tukutane June 02, 2025. Upande wa Jamhuri wameagizwa kukamilisha upelelezi ili kesi ianze kuunguruma siku hiyo. Tutakuwepo kumsindikiza Mwenyekiti @TunduALissu. Twendeni, tujaze Kisutu kama tulivyofanya leo. #FreeTunduLissu
Jeshi la Polisi linapenda kuwajulish umma kuwa kuna taarifa za uongo, upotishaji, zisizo na maadili zilizokuwa zikisambazwa kwenye mtandao wa kijamii wa Jeshi la Polisi (tanpol) kwa lengo la kutaka kuuaminisha umma kiwa zimetolewa na jeshi la polisi kupitia mtandao wake wa X
Taarifa hizo sio za kweli na ifahamike kuwa Jeshi la Polisi haliwezi kuandaa na kusambaza taarifa kama hizo katika mitandao ya kijamii.
Aidha jeshi la Polisi limewaomba wananchi kuzipuuza taarifa hizo na kuepuka kuendelea kuzisambaza.
#CloudsDigitalUpdates
#TANZANIA:RAIS MSTAAFU WA AFRIKA YA KUSINI THABO MBEKI AWASILI TANZANIA KUSHIRIKI MAADHIMISHO YA SIKU YA AFRIKA
Rais Mstaafu wa Afrika ya Kusini Mhe. Thabo Mbeki amewasili nchini Tanzania Mei 20, 2025, kushiriki Mhadhara wa Siku ya Afrika (Africa Day Lecture) ulioandaliwa na Taasisi ya Thabo Mbeki kwa ushirikiano na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambao utafanyika jijini Dar es Salaam tarehe 24 Mei, 2025 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere.
Mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Mhe. Thabo Mbeki amepokelewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Cosato David Chumi (Mb.).
Mhadhara huo ambao ni wa 15 kuandaliwa na Taasisi ya Thabo Mbeki, unatarajiwa kujadili kuhusu mustakabali wa Bara la Afrika na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wakiwemo wanataaluma, wadau kutoka Serikalini, viongozi wastaafu, vijana, na wawakilishi wa sekta binafsi.
Sambamba na Mhadhara huo, Mhe. Rais Mstaafu Mbeki anatarajiwa kushiriki katika mijadala mbalimbali ikiwemo; mjadala kuhusu Uchumi wa Buluu na Utalii, mjadala wa Wanataaluma wa Vyuo Vikuu, halikadhalika majadiliano kuhusu Fursa ya Urais wa Afrika ya Kusini wa kundi la Nchi zenye Uchumi Mkubwa Duniani (G20) kwa ustawi na maendeleo ya Afrika.
Mhadhara wa Siku ya Afrika unafanyika nchini baada ya Taasisi ya Thabo Mbeki kuichagua Tanzania kuwa mwenyeji kwa ukanda wa Afrika Mashariki.
Hongera sana.
Tunawakaribisha katika Utumishi wa Umma, tunatarajia mtafanya kazi kwa weledi, huku mkitanguliza uzalendo. Watanzania wana matarajio makubwa katika utumishi wenu.
Nilikuwa Nairobi Wakati Mh Lissu Ni Mgonjwa Aliposhambuliwa Kwa Risasi , Kitu Kimoja Kikubwa Ktk Kinywa Chake Ni Nguvu Ya Ukiri Chanya.Katika Nguvu Ya Imani Kukiri Ni Zaidi Ya Maombi. Mkti Lissu Hajawahi Kukiri Hofu Hata Katikati Ya Matatizo Makubwa. Leo , Mahakamani Alikuwa Anawatia Moyo Watu Walioko Nje Ya Mahabusu. “ Msiogope , Msiogope , We are Fine , Itakuwa Sawa Tu , Msiogope “
Hakimu; suala la kumuacha mtuhumiwa akae Mahakamani wakati anasubiri kesi yake ni Jambo la Askari Magereza.
Hakimu Mkazi Mkuu; Nahairisha shauri kwa siku 14 angalieni ni lini.. Tarehe 02 June 2025
Utaratibu wa kawaida unatumika katika kesi zingine za mshtakiwa kukaa na mawakili wake utumike..
Natoa angalizo kwamba hapa ni Mahakamani, kushangilia na mayowe hayaruhusiwi
Nafikiri nimeeleweka..
Hakimu anasimama, anaondoka.. Mahakama imehairishwa.