Nisaidie kuretweet
Mzazi ninazo rainboots na raincoats kwa ajili ya mtoto wako. Shule lazima aende na afike akiwa hajaloana wala kuwa na tope .
Tuna raincoats nyingi kwa sasa
0782388366
Rainboot ni 35,000
Raincoats frame 3 ni 10,000
Raincoats frame 4 ni 20,000
Hedhi haipaswi kuwa kikwazo cha elimu kwa mtoto wa kike.
Tuwekeze katika sera, bajeti na mazingira rafiki shuleni ili kila msichana apate nafasi sawa ya kujifunza.
#YouthLedSRHR@EngenderHealth@youngandalivetz
5/6
~Matumizi ya mashahidi wa kificho: Mashahidi wa upande wa mashtaka walitoa ushahidi wao wakiwa wamefichwa nyuma ya kizimba maalumu, hali iliyomzuia ndugu Lissu kuwatambua na kufahamu utambulisho wao. Hatua hii ilitokana na maombi ya upande wa mashtaka chini ya kifungu cha 194 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai. Katika shauri la kikatiba lililofunguliwa Mahakama Kuu, Kanda ya Mwanza, Mahakama ilitamka kuwa kifungu cha 194 kinakiuka Katiba. Kufichwa kwa utambulisho wa mashahidi kulimwekea mshtakiwa changamoto katika kuwatambua, kupima uaminifu wa ushahidi wao na kuwauliza maswali kwa ufanisi.
~Jaribio la upande wa mashtaka kuongeza ushahidi mpya: Upande wa mashtaka ulijaribu kuongeza ushahidi kuhusu matukio ya tarehe 29 Oktoba 2025, takribani miezi sita baada ya ndugu Lissu kukamatwa na kuwekwa mahabusu, licha ya kuwa tayari ulikuwa umewasilisha mashahidi 17. Mahakama Kuu ililikataa jaribio hilo, lakini upande wa mashtaka uliwasilisha maombi ya mapitio (Revision) katika Mahakama ya Rufani, jambo lililosababisha mwenendo wa kesi kusimama kwa takribani miezi sita. Jambo hili liliibua hoja kuhusu kanuni ya uhalali wa kosa (Principle of Legality) chini ya Ibara ya 13(6)(c) ya Katiba, na haki ya mshtakiwa kupata haki ndani ya muda unaofaa chini ya Ibara ya 13(6)(a).
~Ukiukwaji wa uhuru wa kuabudu: Uhuru wa kuabudu ni haki ya kikatiba inayolindwa na Ibara ya 19 ya Katiba, na haki hii inaendelea kulindwa hata mtu anapokuwa gerezani. Ndugu Lissu alilalamika mara kadhaa kuzuiliwa kwa viongozi wake wa kiroho kumtembelea gerezani, ikiwemo tukio la hivi karibuni la Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki la Singida kuzuiwa kuingia Gereza la Ukonga alipokwenda kumtembelea.
4/6
~Kuhamishwa kutoka Gereza la Keko kwenda Gereza la Ukonga bila taarifa kwa mawakili na ndugu zake: Ndugu Lissu alihamishiwa Gereza la Ukonga bila mawakili wake wala ndugu zake wa karibu kupewa taarifa kuhusu uhamisho huo. Kitendo hiki kilisababisha hofu na taharuki kwa familia na watu wake wa karibu kutokana na kutojua mahali alipo, na kuongeza wasiwasi kuhusu usalama na ustawi wake. Hali hii inaonesha umuhimu wa kuwepo kwa utaratibu wa wazi wa kutoa taarifa kwa ndugu na mawakili kuhusu uhamisho wa mahabusu na wafungwa.
~Kuingiliwa kwa mawasiliano ya faragha kati ya mawakili na mteja wao: Haki ya mshtakiwa kuwasiliana na mawakili wake kwa faragha ni sehemu muhimu ya haki ya kujitetea na kupata usikilizwaji wa haki. Mawasiliano hayo yaliingiliwa mara kadhaa na maafisa wa Gereza la Ukonga, huku baadhi ya mawakili wakizuiwa kabisa kuingia gerezani kumwona. Katika shauri la kikatiba Na. 7300 la mwaka 2026, Mahakama Kuu, Masjala Kuu ya Dodoma, iliamua kuwa hatua hizo zilikuwa kinyume cha Katiba.
~Kuwekwa pamoja na wafungwa waliohukumiwa adhabu ya kifo: Kwa mujibu wa kifungu cha 72 cha Sheria ya Magereza, Sura ya 58, Toleo la Marejeo la mwaka 2023, wafungwa hao wanapaswa kutengwa katika eneo maalumu (Death Row). Ndugu Lissu alilalamika hadharani kuwekwa pamoja nao, licha ya kuwa bado ni mshtakiwa ambaye hukumu dhidi yake ilikuwa haijatolewa. Kitendo hiki kiliibua maswali kuhusu dhana ya kutokuwa na hatia mpaka mtu athibitishwe kuwa na hatia, kama inavyoainishwa na Ibara ya 13(6)(b) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.
3/6
~Mahakama kukataa kurekodi baadhi ya mashahidi wa upande wa utetezi: Wakati wa mwenendo kabidhi, Hakimu alikataa kurekodi majina ya baadhi ya mashahidi waliotajwa na ndugu Lissu kwa maelezo kuwa angeweza kuwataja Mahakama Kuu. Alipowataja huko, upande wa mashtaka ulipinga kwa hoja kuwa hawakutajwa wakati wa mwenendo kabidhi, na Mahakama ikakubaliana na pingamizi hilo. Hali hii ilimnyima fursa ya kuwasilisha ushahidi wa baadhi ya mashahidi aliokuwa amewategemea katika utetezi wake, hivyo kuathiri haki yake ya kujitetea na kupata usikilizwaji wa haki.
~Jaribio la kuendesha shauri kwa njia ya mtandao: Katika shauri la uchochezi lililokuwa likimkabili ndugu Lissu, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ilijaribu kuanzisha usikilizwaji wa kesi kwa njia ya mtandao. Jaribio hilo liliibua maswali kuhusu uwazi wa mwenendo wa mashauri na haki ya wananchi kupata taarifa kuhusu shughuli za mahakama, kwa kuzingatia Ibara ya 18 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Baada ya kupingwa kupitia marejeo, usikilizwaji ulirejeshwa katika utaratibu wa kawaida.
~Kukamatwa, kuteswa na kurudishwa nchini kwao kwa waangalizi wa kimataifa: Baadhi ya waangalizi wa kimataifa, wakiwemo Martha Kalua, Jaji Mkuu wa zamani wa Kenya Willy Mutunga, mwanaharakati Boniface Mwangi na mwandishi wa habari Agatha Atuhaire kutoka Uganda, walikamatwa na kurudishwa nchini kwao. Hali iliyotia wasiwasi zaidi ni kutekwa kwa Boniface Mwangi na Agatha Atuhaire, ambao walipotea kwa siku kadhaa kabla ya kuonekana kwenye mpaka wa Tanzania na Uganda wakiwa wamejeruhiwa na kudaiwa kuteswa. Matukio haya yaliibua maswali kuhusu usalama wa waangalizi wa kimataifa na uhuru wa ufuatiliaji wa mashauri ya mahakama, na yalidhoofisha taswira ya Tanzania katika jumuiya ya kimataifa kuhusu heshima na ulinzi wa haki za binadamu.
2/6
Masuala muhimu tuliyobaini wakati wa ufuatiliaji wa mwenendo wa kesi.
~Ukamataji usiozingatia taratibu za kisheria: Maafisa wa Polisi waliomkamata ndugu Lissu hawakumweleza sababu za kukamatwa kwake, kinyume na kifungu cha 24(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai, Sura ya 20, Toleo la Marejeo la mwaka 2023, kikisomwa pamoja na Kanuni ya 1(31) ya Kanuni za Kudumu za Jeshi la Polisi (PGO), Toleo la mwaka 2021.
~Matumizi ya nguvu: Jeshi la Polisi Mkoa wa Ruvuma lilitumia mabomu ya machozi kuwatawanya mamia ya wananchi waliokuwa wakishiriki mkutano wa hadhara aliokuwa akihutubia ndugu Lissu. Baadhi ya wananchi walijeruhiwa na wengine kukamatwa, jambo lililoibua maswali kuhusu ulazima na uwiano wa nguvu iliyotumika.
~Muda wa kukamilisha upelelezi: Kwa mujibu wa Aya ya 7(iii) ya Mwongozo wa Mkurugenzi wa Mashtaka Na. 1 wa mwaka 2022, upelelezi wa kesi zinazoruhusiwa kufunguliwa kabla ya kukamilika kwa upelelezi unatakiwa kukamilishwa ndani ya siku zisizozidi 90. Hata hivyo, mwenendo kabidhi wa shauri hili ulichukua takribani miezi mitano bila upelelezi kukamilika, na upande wa mashtaka haukuwasilisha ombi la muda wa ziada. Ni msimamo wa Kituo kuwa upelelezi na mwenendo kabidhi wa mashauri ya jinai unapaswa kuendeshwa kwa kuzingatia muda unaofaa na miongozo iliyowekwa, ili kuepusha ucheleweshaji usio wa lazima unaoweza kuathiri haki ya mshtakiwa kupata haki kwa wakati.
1/6
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI, 12 Novemba 2026, Dar es Salaam.
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimetoa taarifa kuhusu mwenendo wa shauri la uhaini la ndugu Tundu Lissu. Moja ya majukumu yetu ni kufuatilia mwenendo wa mashauri yanayoendeshwa mahakamani yanayohusu haki za binadamu, Katiba na utawala bora. Katika kutekeleza jukumu hili, tumekuwa tukifuatilia mwenendo wa kesi ya ndugu Lissu tangu alipokamatwa tarehe 9 Aprili 2025, hadi tarehe 6 Novemba 2026, ambapo Mahakama ilitoa hukumu ya kumtia hatiani na kumhukumu kifungo cha miaka minne jela.
Ndugu Lissu alikamatwa na Jeshi la Polisi alipokuwa katika ziara ya kichama wilayani Mbinga, mkoani Ruvuma, na baadaye kusafirishwa kwenda Dar es Salaam, ambako tarehe 10 Aprili 2025 alifunguliwa mashtaka mawili, likiwemo la uhaini na jingine la kutoa taarifa za uongo. Hadi siku ya hukumu, alikuwa ametumia takribani siku 577 akiwa mahabusu. Hiki ni kipindi kirefu ambacho amekuwa akinyimwa uhuru wake na kutenganishwa na familia yake, wapendwa wake na maisha yake ya kawaida.
Moja ya majukumu ya Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) ni kufuatilia mwenendo wa mashauri yanayoendeshwa mahakamani yanayohusu haki za binadamu, Katiba na utawala bora. Katika kutekeleza jukumu hili, Kituo kimekuwa kikifuatilia mwenendo wa kesi ya ndugu Tundu Lissu tangu alipokamatwa tarehe 9 Aprili 2025, hadi tarehe 6 Novemba 2026, ambapo Mahakama ilitoa hukumu ya kumtia hatiani na kumhukumu kifungo cha miaka minne jela.
Tazama hapa live https://t.co/IolF6ijopq
Karibu utazame
Unahitaji huduma za TCAA? ✈️
Uliza Sky moja kwa moja kupitia tovuti ya https://t.co/ZNKQAeTSwI na upate majibu kuhusu huduma za usafiri wa anga kwa urahisi, saa 24 kwa siku, siku 7 kwa wiki.
#TCAATanzania#DondooZaSky#UsafiriWaAnga
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimekuwa kikifuatilia mwenendo wa kesi iliyokuwa ikimkabili Mhe. Tundu Lissu tangu alipokamatwa na kufunguliwa mashitaka ya uhaini hadi Mahakama Kuu, Masjala ya Dar es Salaam, ilipotoa uamuzi wake leo tarehe 6/11/2026.
Katika uamuzi huo, Mahakama imemwachia huru Mhe. Tundu Lissu dhidi ya shitaka la uhaini baada ya kubaini kuwa upande wa Jamhuri umeshindwa kuthibitisha shtaka hilo pasipo kuacha shaka yoyote. Hata hivyo, Mahakama imemkuta na hatia ya kosa la uchochezi na kumhukumu kifungo cha miaka minne jela.
LHRC itatoa uchambuzi wake wa kina baada ya kupata na kupitia nakala kamili ya uamuzi wa Mahakama, ili kutathmini hoja za kisheria na msingi wa uamuzi huo kwa kuzingatia sheria na viwango vya haki za binadamu.
#HumanRightsTz #HakiZaBinadamu #UtawalaBora
Mjadala umebainisha changamoto, pia katika kutafuta suluhisho. Wadau wa habari na mitandao ya kijamii wamechangia mawazo kuhusu usajili, kulinda utambulisho wa kidijitali & mfumo rafiki kwa wachapishaji wasio wa kibiashara, kwa lengo la kuandaa mapendekezo madhubuti ya kisera.
𝗞𝘂𝗺𝗯𝘂𝗸𝗶𝘇𝗶 𝘆𝗮 𝗠𝗮𝘁𝘂𝗸𝗶𝗼 𝘆𝗮 𝗧𝗮𝗿𝗲𝗵𝗲 𝟮𝟵 𝗢𝗸𝘁𝗼𝗯𝗮 𝟮𝟬𝟮𝟱
Mwaka mmoja tangu matukio ya tarehe 29 Oktoba 2025, TMC, kupitia Kikundi Kazi cha Utawala wa Mtandao Tanzania (IGTWG), inaungana na mashirika mengine ya kiraia kuwakumbuka waliopoteza maisha, kutoa pole na mshikamano kwa manusura na familia zilizoathirika, pamoja na wote ambao bado wanasubiri majibu.
Taarifa ya pamoja inaangazia umuhimu wa ukweli, uwajibikaji, msaada kwa familia zilizoathirika, heshima kwa haki za binadamu, na ulinzi wa haki za kiraia na haki za kidijitali.
Katika kuadhimisha siku hii, tunasisitiza umuhimu wa haki, uponyaji, maridhiano ya kitaifa na dhamira ya pamoja ya kulinda utu wa kila mtu.
📄 Soma taarifa kamili hapa: https://t.co/PINCeMfVax
#TMC #IGTWG #HakiZaBinadamu #HakiZaKidijitali #Tanzania
#Repost From Uhuru FM
Tech & Media Convergence (TMC) imeendesha mafunzo ya siku tatu kwa waandishi wa habari, wahariri na viongozi wa vyumba vya habari, kuanzia Oktoba 27 hadi 29, 2026, jijini Dar es Salaam, kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kutumia teknolojia ya Akili Unde kwa kuzingatia sheria, maadili na uwajibikaji katika uandishi na uhariri wa habari.
Katika siku ya kwanza, washiriki walijadili mifumo ya kisheria na kisera inayohusiana na matumizi ya Akili Unde nchini Tanzania na Kenya. Majadiliano hayo yaliongozwa na Wakili Robert Sylivester Majige, Kiongozi wa Sera na Teknolojia za Kiraia wa TMC.
Wakili Majige pia aliongoza mjadala kuhusu namna ya kubadilisha misingi ya usimamizi wa Akili Unde kuwa kanuni na sera zinazotekelezeka kulingana na mahitaji na majukumu ya vyumba vya habari.
Katika siku ya pili, Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania Media Foundation (TMF), Dastan Kamanzi, aliongoza majadiliano kuhusu hatua za kiufundi za kuhakikisha matumizi salama na yenye uwajibikaji wa Akili Unde. Washiriki pia walibadilishana uzoefu na kujadili maeneo muhimu ya kuzingatia wakati wa kuandaa sera za matumizi ya teknolojia hiyo.
Mafunzo hayo pia yalihusisha Anuar Said, mkufunzi na mshauri wa TMC, aliyesimamia majadiliano ya kubadilishana uzoefu, huku Janet John Kahindi, Mratibu wa Sera na Programu wa TMC, akiratibu maandalizi ya kazi za vikundi na uandishi wa rasimu za sera.
Katika siku ya mwisho ya mafunzo, leo Oktoba 29, waandishi wa habari wamepitia rasimu ya sera ya matumizi ya Akili Unde na kutoa mapendekezo ya kuiboresha ili iendane na mahitaji halisi ya vyumba vya habari. Mapendekezo hayo yamezingatia masuala ya usahihi wa taarifa, maadili ya uandishi wa habari, uhuru wa uhariri, ulinzi wa taarifa binafsi na uwajibikaji.
Mafunzo hayo yamehitimishwa kwa lengo la kusaidia taasisi za habari kuwa na miongozo iliyo wazi ya matumizi ya Akili Unde, huku TMC ikiendelea kuimarisha matumizi yenye uwajibikaji wa teknolojia hiyo, kulinda uadilifu wa uandishi wa habari na kuendeleza imani ya wananchi kwa vyombo vya habari katika mazingira ya kidijitali.
𝗥𝗲𝗴𝘂𝗹𝗮𝘁𝗶𝗻𝗴 𝘁𝗵𝗲 𝗦𝗺𝗮𝗹𝗹 𝗩𝗼𝗶𝗰𝗲: 𝗟𝗶𝗰𝗲𝗻𝘀𝗶𝗻𝗴, 𝗣𝗿𝗼𝗽𝗼𝗿𝘁𝗶𝗼𝗻𝗮𝗹𝗶𝘁𝘆 & 𝗣𝘂𝗯𝗹𝗶𝗰 𝗜𝗻𝘁𝗲𝗿𝗲𝘀𝘁
On 30th October 2026, TMC convened an FGD at its headquarters to examine Tanzania’s 2026 Online Content Amendments and their implications for small digital publishers.
The discussion explored the licensing requirements facing independent bloggers, community publishers, and citizen journalists, including concerns around the 12-month limit for Category C licences and the requirement to transition to commercial licensing. Participants also considered how registration requirements, including identity verification, may affect privacy and the ability of public-interest publishers to operate safely.
The conversation focused on proportionality, freedom of expression, and the potential impact of criminal penalties for licensing violations. Participants examined the need for safeguards that distinguish genuine public-interest concerns from lawful expression and help prevent arbitrary restrictions on digital content.
The dialogue brought stakeholders together to consider barriers facing small publishers and discuss policy options, including a fee-exempt notification approach for non-commercial publishers. The recommendations will inform TMC Policy Brief Issue 13 and a technical memorandum of proposed amendments for the Ministry of Information, Communication and Information Technology.
The FGD forms part of TMC’s work to promote a democratic digital framework that protects public-interest expression while addressing the regulation of online content in Tanzania.
#TMC #DigitalRights #FreedomOfExpression #OnlineContent #TDC2026
𝗔𝗗𝗩𝗢𝗖𝗔𝗖𝗬 𝗕𝗥𝗜𝗘𝗙 | 𝗕𝗲𝘆𝗼𝗻𝗱 𝗖𝗼𝗺𝗽𝗹𝗶𝗮𝗻𝗰𝗲: 𝗕𝘂𝗶𝗹𝗱𝗶𝗻𝗴 𝗗𝗮𝘁𝗮 𝗠𝗶𝗻𝗶𝗺𝗶𝘇𝗮𝘁𝗶𝗼𝗻 𝗮𝗻𝗱 𝗣𝗿𝗶𝘃𝗮𝗰𝘆 𝗶𝗻𝘁𝗼 𝗧𝗮𝗻𝘇𝗮𝗻𝗶𝗮’𝘀 𝗗𝗶𝗴𝗶𝘁𝗮𝗹 𝗦𝘆𝘀𝘁𝗲𝗺𝘀
TMC, in partnership with the Internet Governance Tanzania Working Group (IGTWG) and the Tanzania Technical Community, presents Issue 11 of the Tanzania State of Internet Governance Series. The brief examines excessive data collection and privacy risks arising from Tanzania’s expanding digital systems, highlighting the need to move beyond procedural compliance towards privacy-centred digital governance.
Key areas highlighted in the brief include:
✴️ Data minimization, necessity, and proportionality
✴️ Consent challenges and indefinite data retention
✴️ Personal and biometric data protection, including NIDA
✴️ Privacy risks associated with mandatory electronic payments under GN No. 158C of 2026
✴️ Stronger enforcement by the Personal Data Protection Commission (PDPC)
✴️ Data Protection Impact Assessments and accountability in ICT procurement
✴️ Privacy-preserving technologies, including Zero-Knowledge Proofs and Differential Privacy
✴️ Privacy by Design and strategic policy recommendations
The brief calls for stronger regulatory enforcement, responsible data collection, and privacy safeguards embedded into digital systems from the outset to ensure Tanzania’s digital transformation protects citizens’ fundamental rights.
📖 Read the full brief: https://t.co/3TwWXXSGWi
Produced with support from the U.S. Embassy in Tanzania, in collaboration with the Bureau of African Affairs at the U.S. Department of State.
#InternetGovernance #DataProtection #DigitalRights #TDC2026 #TMC #IGTWG
Zimebaki siku 8!
Huduma za matibabu zinakuja karibu nawe, bila gharama. Usikose fursa hii adhimu ya kuimarisha afya yako na ya familia yako.
📍 Kituo cha Afya Kinduni, Unguja
📅 3 – 7 Novemba 2026
#KambiYa6#ZMBF#AfyaBoraMaishaBora