Kama nilivyosema kwenye posti yangu iliyopita, I don’t care nani awe mwenyekiti wa Chadema, nachojali mimi ni process itakayotumika kumpata huyo mwenyekiti, nachojali ni demokrasia ya kweli itumike.
Ila kama mimi ningekuwa mpigaji kura huko kamati kuu ya Chadema basi ningempigia kura Tundu Lissu na sababu zangu ni hizi,
1. Chadema needs a new direction and new leadership. Chama kinaendelea kudondoka na kupoteza influence chini ya uongozi wa Mbowe. Unahitajika uongozi mpya.
2. Mbowe kwa namna moja au nyingine is directly responsible for the fall of Chadema, starting na grave mistake ya kumpokea Lowassa in 2015, huwezi kuwaaminisha Watanzania kwa zaidi ya miaka 10 kuwa Lowassa ni fisadi na ndo anaimaliza nchi alafu ghafla umkumbatie Lowassa na ujaribu kuwaambia Watanzania Lowassa anafaa kuwa Raisi wao, pale ndo Chadema ilipoteza trust ya Watanzania. He made many more mistakes after.
3. Inabidi tukubali kuwa pale ambapo wote tuliingia mkenge na uongozi wa Samia Suluhu, Lissu aliona mbali na alionya taifa, leo hii wote tumeona kuwa Lissu alikuwa sawa na Mbowe alikosea, which means Lissu ana vision kubwa zaidi na anaangalia bigger picture.
4. Huku nchi za wenzetu pale Chama kinapokosa muelekeo au kupoteza influence cha kwanza ni mwenyekiti wa Chama huwa anaondolewa ili kupisha uongozi mpya. Chadema haitoweza kurudi to its glory days chini ya uongozi wa Mbowe. His time has passed.
5. Mbowe ame slow down mno politically ila Lissu bado anayo drive and the fight in him. Mbowe doesn’t have this fight in him anymore. Ila kikubwa zaidi Mbowe hana influence tena, hata akiitisha maandamano hata wananchama wa Chadema hawatoki kuondamana, hilo ni tatizo kubwa sana, Mwenyekiti’s hawezi kuitisha maandamano then wanachama wa chama chake wanajificha ndani na wananchi wa kawaida.
Hao MaCCM mnaowaona kina Nape, Kingwangala mnaowaona wanamjaza Mbowe issue ni kwamba wanajua Lissu akitake over it will be a whole new ball game na wanajua akibaki Mbowe kama chairman it will be business as usual.
Baada ya kuongea hayo yoote naomba nirudi kusema kuwa yoyote atakaeshinda Mbowe au Lissu mi sina tatizo cha msingi ni demokrasia ila I wish sana sana Mbowe angestaafu, he has done big things for this country ila muda wake umepita, it’s time for new leadership and new direction. Hauwezi kuendelea kufanya kile kile kisha ukatarajia matokea tofauti, mabadiliko makubwa yanatakiwa ndani ya Chadema, na mabadiliko hayo yanaanza na uongozi.
Na huko mbeleni pia inabidi hata Lissu akae pembeni kupisha new generation of fighters, ambao wana nguvu mpya ya mapambano kama jinsi wao walivyokuwa 20 years ago.
La mwisho, mimi sio Chadema na wala sina chama. Haya ni maoni yangu tu ambayo naona yatasaidia kwenye siasa na demokrasia ya nchi.
@rfef#FutsalFemenino Amistosos Internacionales 🇦🇷-🇪🇸. Partido 1
Empezó el segundo tiempo, ya juegan, en el Pabellón de la Ciudad del Fútbol de Las Rozas,
🇦🇷 Argentina 0 - 2 España 🇪🇸
Mirá el partido, en vivo📺📲💻 https://t.co/0WjS8KJ1xM