Mnamo Desemba 10, 2024, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, alimtangaza Profesa Mohamed Janabi kuwania nafasi ya Mkurugenzi wa Kanda ya Afrika katika Shirika la Afya Duniani (WHO). Rais Samia alielezea imani yake katika uwezo wa Profesa Janabi katika masuala ya afya, akisema kwamba baada ya kupitia wasifu wa wagombea kadhaa, wasifu wa Profesa Janabi ulionekana kuwa wa kutosheleza zaidi kwa nafasi hiyo.
@moddyyakubu @ikulumawasliano #SamiaInAction
📍Ikulu, Chamwino.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC-Organ) Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akishiriki Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC kwa njia ya Mtandao pamoja na viongozi mbalimbali, kujadili hali ya ulinzi na usalama Mashariki mwa nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
@SuluhuSamia #SamiaInAction
Leo tarehe 11 Machi 2025, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa 39 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) uliofanyika jijini Dodoma, amewataka wakurugenzi wa halmashauri, wakuu wa wilaya, na viongozi wengine wa serikali za mitaa kutoa taarifa mapema iwapo wana nia ya kugombea ubunge katika uchaguzi ujao.
Rais Samia alisisitiza kuwa msingi wa ombi lake ni kuhakikisha nafasi zinazowachwa na viongozi hao zinaweza kujazwa kwa haraka na watu wenye sifa, ili kuepuka usumbufu katika utendaji wa serikali za mitaa kabla ya mchakato rasmi wa uchaguzi kuanza. Kauli hii inakuja katika muktadha wa maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania unaotarajiwa kufanyika mwaka huu wa 2025.
📍Dodoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akishiriki Katika Mkutano wa 39 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) Katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Centre jijini Dodoma , Tarehe 11 Machi 2025.
#SamiaInAction@SuluhuSamia@ikulumawasliano
Leo tarehe 10 Machi 2025, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameitisha na kuongoza kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kilichofanyika jijini Dodoma.
#SamiaInAction
MATUKIO KATIKA PICHA.
Taswira ya eneo la mtambo wa kutibu maji (Water treatment Plant ) katika mradi wa Maji wa Same-Mwanga-Korogwe uliopo wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro.
Leo, tarehe 9 Machi 2025, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kuzindua rasmi Mradi wa Maji wa Same-Mwanga-Korogwe. Mradi huu ni sehemu ya jitihada za serikali za awamu ya sita za kumudu changamoto ya upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi, hasa katika maeneo ya Same, Mwanga, na Korogwe.
Hii ni hatua nyingine inayoonyesha dhamira ya Rais Samia katika kutekeleza ahadi zake za maendeleo, hasa katika sekta ya maji, ambayo imekuwa kipaumbele cha serikali yake. Wananchi wameonyesha furaha yao kupitia mitandao ya kijamii, wakiushangilia uongozi huu wa vitendo unaoleta matokeo yanayoonekana.
Ikulu, Magogoni
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan afuturisha Watoto Yatima na Watoto wenye mahitaji Maalum, Ikulu Jijini Dar es Salaam, leo tarehe 3 Machi, 2025.
#SamiaInAction
Ofisi za Halmashauri za Mji Handeni, Mkoani Tanga zimezinduliwa rasmi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan. Ujenzi wa ofisi za Halmashauri unaenda Kuongeza kasi ya maendeleo wilayani hapo kwani wananchi watapata nafasi ya kusikilizwa na kuwasilisha maoni na malalamiko yao kwa viongozi katika ngazi ya Halmashauri.
Faida za Ofisi za Halmashauri ni kutatua na Kusaidia mambo yafuatayo;
• kuratibu huduma za umma
• Ukusanyaji wa Mapato
• Ushirikiano na wananchi
• Usimamizi wa Miradi
• Utatuzi wa Migogoro
• Kuhamasisha maendeleo ya Kiuchumi
• Ulinzi wa Mazingira
@wizara_ya_ardhi
#SamiaInAction
AHSANTENI SANA WANA KILINDI.
Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameendelea Kukusanya Kijiji katika Kila wilaya anayotia mguu Mkoani Tanga. Mhe. Rais kawashukuru wananchi kwa Kujaa kwa wingi kwenye kila kituo anachosimama na kutoa ahadi ya kuendelea Kutatua Changamoto zao na kuendeleza Miradi Mkoani hapo mpaka itakapokamilika.
#SamiaInAction
Sehemu ya Hotuba ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan baada ya kuzindua ofisi za Halmashauri ya Mji wa Handeni Mkoani Tanga. Mhe. Rais katika Hotuba yake amesisitiza na kuwaomba wafanyakazi wote wa Halmashauri hio kutokupandisha mabega yao na kutambua kuwa wao ni watumishi wa wananchi.
Aidha Mhe. Rais Dkt. Samia amesema lengo la Ujenzi wa ofisi hizi za Halmashauri ni kuweka ofisi zote Katika Jengo moja ili kumpunguzia mwananchi shida ya kuzunguka sehemu mbalimbali ili kupata haki yake.
🎥 @ikulumawasliano
#SamiaInAction
MHE. RAIS AZINDUA SHULE YA SEKONDARIA YA WASICHANA KILINDINI, TANGA.
Leo tarehe 25/02/2025 Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amefanya Uzinduzi wa Shule ya Sekondari ya wasichana ya “Tanga Girls’ Secondary School” yenye mchepuo wa Sayansi na Mafunzo ya Tehama iliyopo Wilaya ya Kilindini.
Katika hotuba yake Mhe. Rais ameomba jina la Shule hio kubadirishwa na Kuitwa Beatrice Shelukindo Secondary School, Jina la mbunge wa zamani wa Jimbo la Kilindini na Mpambanaji wa Masuala ya Jinsia ambaye sasa ni Marehemu.
@SuluhuSamia@ikulumawasliano
#SamiaInAction
Ziara ya Mhe. Rais leo Mkoani Tanga imeishia wilayani Handeni ambapo ameweka Jiwe la Msingi la Mradi wa Maji wa Miji 28 unaoenda kuimarisha upatikanaji wa maji katika Mkoa wa Tanga.
Mradi wa maji wa miji 28 mkoani Tanga ni moja wa miradi mikubwa ya kimkakati inayotekelezwa na Serikali ya Tanzania ili kuboresha upatikanaji wa maji safi na salama katika maeneo ya mijini. Mradi huu unahusisha wilaya nne za mkoa wa Tanga, ambazo ni Handeni, Korogwe, Muheza, na Pangani, na ni sehemu ya Mpango wa Kitaifa wa Maji unaolenga miji 28 nchini.
Lengo lake ni kuondoa changamoto ya uhaba wa maji kwa wananchi wa maeneo haya. Hadi sasa (Februari 25, 2025), utekelezaji wake umefikia asilimia 60, na unatarajiwa kukamilika katika muda uliopangwa ikiwa usimamizi utaendelea vyema.
@ikulumawasliano@maji_mowi
#SamiaInAction
Maelekezo ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa Waziri wa Utalii Juu ya fidia kwa wananchi wanaoingiliwa na wanyama kwenye mashamba yao.
Pia Mhe. Rais Dkt. Samia amesikia Kilio cha wananchi wa Bumbuli Juu ya Ujenzi wa barabara na kutoa ahadi ya Ujenzi wa barabara ya kilomita 22 panapo mwezi machi mwaka huu kuanzia Soni Kuelekea Bumbuli. Mhe. Rais amesema haya katika Muendelezo wa ziara yake ya siku 7 Mkoani Tanga ya Kukagua na Kuzindua Miradi ya Serikali ya Mkoani humo.
@SuluhuSamia@ikulumawasliano
#SamiaInAction
Ziara ya Siku 7 ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Mkoani Tanga imeanza na Uzinduzi wa Hospitali ya Halmashauri ya wilaya ya Handeni iliyopo Mkata leo tarehe 23/02/2025.
Ujenzi wa Hospitali na Vituo vya Afya imekuwa ni ajenda ya Muhimu sanaa kwenye Uongozi wa Mama Samia toka aingie Madarakani. Hii imesaidia Sanaa Kuboresha Afya ya mama, mtoto na kuzuia Vifo hasa wakati wa ujauzito na Kujifungua.
#SamiaInAction
Mhe. Rais akikata Utepe kuashiria uzinduzi wa Jengo la Halmashauri ya wilaya ya Bumbuli, Mkoani Tanga. Baada ya Uzinduzi wa Jengo hili Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amewashukuru sana wananchi wa Bumbuli kwa Mapokezi Mazuri na kuwasisitiza kutumia jengo hilo jipya la Halmashauri kutafuta huduma kwa Viongozi wao wa kila sekta.
Mhe. Rais kamalizia kwa kusema lengo la Ziara yake Mkoani Tanga ni kuangalia matumizi ya pesa za serikali katika kila Halmashauri na Miradi mbalimbali inayoendelea Mkoani humo na kwamba atatembelea wilaya zote kabla ya Kumaliza Ziara yake.