USHAURI: Nunua kibubu, tunza walau BUKUBUKU Kila siku.
KUNA SHEREHE HIVI KARIBUNI
Wakati wa nderemo na vifijo hatotoweza kukusikiliza unavyotuomba/gongea BIA.
TUNZA HELA YAKO UWE NA HATA BIA SITA ZA KUANZIA.
SHEREHE NI YA SIKU SABA MTAWALIA!!
Nawatakia utekelezaji mwema.
@ZPlanmaster Hao wengine walipaswa kuwa kwenye msafara wa presidential car, inakuaje wanataka kwenda njia tofauti?. Haya naamuru mara Moja ongozeni msafara! Alaa!.
Wanasiasa Tujifunze: Siasa za Upinzani Tanzania si Ushindani wa Vyama, ni Mapambano ya Maadili!
Katika anga ya kisiasa ya Tanzania, upinzani sio tu jukwaa mbadala la kusaka madaraka—ni mstari wa mbele unaotenganisha mifumo miwili inayokinzana kiitikadi na kiutu. Siasa zetu zimegawanyika kati ya:
• Utu uliotukuka dhidi ya Unyama wa mfumo.
• Uhuru wa kweli dhidi ya Ukandamizaji wa kikatili.
• Haki ya wanyonge dhidi ya Dhuluma.
• Ustaarabu dhidi ya Ukatili wa zama za giza.
• Ulinzi wa Rasilimali za Umma dhidi ya ufisadi
Unapoamua kuondoka upinzani na kuhamia Chama Cha Mapinduzi (CCM), hujabadili tu nembo ya chama au rangi ya sare; umeamua kusaliti mapambano ya kudai Utu, Uhuru, Haki, na Ustaarabu. Umesaliti.
Hapo ndipo usaliti wa mtu mmoja unapokuwa donda ndugu linalovuja damu nyingi sana; linakuwa tukio chungu, tukio la kikatili, na tukio lenye kukatisha tamaa kwa mamilioni ya Watanzania wengi.
Raia wanabaki nyuma wakisaga meno katika tanuru la mateso, umaskini, na hofu. Ni sawa na askari anayeasi mstari wa mbele wa vita na kukimbilia upande wa adui anayeshambulia kijiji chake.
Tukitaka kuelewa tulipo, tutazame jirani zetu, Kenya.
Kenya, wanasiasa wanaweza kutofautiana vikali, lakini wanatofautiana kuhusu ni kikundi gani kitakachoshika usukani wa nchi. Tofauti hizo za uhasama wa kutekana hadi kuua usiowapenda
Hata hivyo, wote—kuanzia rais hadi mwananchi wa kawaida—wanafurahia, wanalinda, na kuogelea katika anga pana ya kidemokrasia na ustaarabu wa kisiasa (Democratic space and civilization).
Rais wa Kenya anaweza kusimama jukwaani, akacheka akijibu mapigo ya wapinzani wake na kusema: “Hawa jamaa wa upinzani hawana ajenda, kazi yao kila siku ni kuniita ‘Kasongo’ tu!”
Pamoja na kejeli hizo za wazi kwa Rais, Hakuna anayetekwa na kupotezwa, hakuna anayemiminiwa risasi, na hakuna anayeuawa kwa kutoa maoni yake. Siasa zao zina ushindani, lakini zina UTU.
Kwetu Tanzania, hali ni tofauti kabisa.
Wakati jirani zetu wakipiga hatua mbele na kulinda hiyo democratic space, kwetu bado tunapambana na siasa za kishamba za kuona anayekukosoa anastahili kufutwa duniani au kuwekewa vizuizi kila kona.
Huwezi kujenga taifa imara kwa kutumia misingi ya uoga na ukatili; taifa bora linajengwa pale ambapo mawazo mbadala yanakaribishwa na kuheshimiwa.
Hapa kwetu, kumtania Rais ni ‘mwiko’ na kumkosoa tu ni kujikana nafsi na kuamua liwalo na liwe! Mazingira ya hofu yanadhihirisha kuwa hatushindani kwa hoja, tunashindana na nguvu ya dola.
Wito kwa Wanasiasa wa upinzani: Simamani Imara!
Ni wajibu wetu sasa kama wapigania haki kushiriki kikamilifu katika hatua zote za kutengeneza mazingira mazuri na sahihi yatakayomruhusu kila Mtanzania kufanya siasa za kistaarabu bila woga.
Na safari hii lazima ipiganwe tukiwa upande wa umma, tukiwa upinzani. mazingira yatakayomruhusu kila kijana, mwanamke, na mzee kufanya siasa za kistaarabu bila hofu ya kutoona jua la kesho.
Siyo lazima kuwa ‘chawa’ wa watawala hawa katili wanaonyanyasa ndugu zenu. Unapoamua kuhama upinzani kwa kufuata tonge la ugali au cheo cha muda mfupi, unapoteza vitu vitatu vikubwa:
(i) Unapoteza Utu wako: Unakuwa mtumwa wa fikra unazozichukia moyoni mwako, huwezi kuziishi.
(ii) Unajifuta kwenye Historia: Unakuwa takataka ya inayokumbukwa kwa usaliti badala ya ukombozi.
(iii) Unasaliti harakati: Unakuwa mshirika wa wale waliomwaga damu na kutesa wapigania haki.
Kama siasa kwako ni utumishi, utumishi wa kweli ni kusimama imara na wanyonge kwenye dhiki, hadi haki yao ipatikane. Tufanye siasa za dhamiri (politics of conscience) badala ya siasa za tumbo na fursa.
Ukikimbilia kwenye meza ya watesi wako ili ule makombo ya meza za ikulu, wewe si mwanasiasa tena; wewe ni mnada wa bei rahisi. Unanunulika. Thamani yako ina bei. Sokoni unanunulika.
Tujifunze, tusimame imara, Aluta Continua!
MMM, Martin Maranja Masese, Mtikila.
Zama za Ofisi ya Msajili wa Vyama kuwa mchezaji namba 12 wa CCM FC zimekwisha.
Dola isome alama za nyakati. The writing is on the walls!
Msajili STOP THIS NONSENSE ya kutaka kufuta CHADEMA. Utafutwa wewe, No doubt about this!
Tume ya Chande iliyoundwa na Rais imetoa Taarifa inayosema wananchi wanailalamikia Ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa kutokutenda haki kwenye kusimamia shughuli za vyama vya Siasa. Badala ya Msajili kuchutama, kuwajibika na kubadilika anarudia makosa yaleyale yaliyopelekea mauaji yaliyoanza Oktoba 29.
Msajili anajua, Watanzania wanajua na Dunia inajua kuwa Kuna ushahidi wa kutosha wa CCM kufanya makosa makubwa kuliko hata ambayo msajili ameituhumu Chadema, hatukuwahi kuona hatua zozote zimechukuliwa na Ofisi hii ya Msajili.
Ofisi ya Msajili ijue WATANZANIA SIO MABWEGE. Tunachukulia tishio lolote dhidi ya CHADEMA ni tishio dhidi ya Demokrasia. An attack to one, is an attack to all.
Iacheni CCM ifanye Siasa za Ushindani dhidi yetu. Nasi tufanye siasa za ushindani dhidi yao.
Acheni kuwa mbeleko ya CCM. Mtaanguka nayo. Ujumbe huu sio wa Msajili tu bali pia ni kwa VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA pia. Kaeni pembeni acheni vyama vya Siasa vifanye Siasa.
Mnataka watu wangapi wafe ili mpate somo?
🔴"Dear Michael Carrick,As a loyal United fan, I have to say it:
Bryan Mbeumo is a shadow of the player who lit up early under you. No goals in his last 5+ games, poor touches, missed chances: he's struggling badly up front.
He's a natural right winger, thrives running at defenders, not leading the line. Drop him for a bit or shift him wide to his best position before the form dip hurts the team more. We need the old Mbeumo back. Please reconsider.
Open letter from a concerned Red.