Nawapongeza Madaktari na Wauguzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa kufanikisha upasuaji wa kuwatenganisha watoto mapacha walioungana. Hii ni hatua muhimu katika utekelezaji wa mpango wa serikali kuboresha matibabu ya kibingwa. Nawaombea watoto Rehema na Neema wapone haraka.