Watu wameamua tuu kusambaza mahusiano yanayofeli kuliki yanayofanikiwa, ni jambo linafanyika kimkakati sana, lengo ni kuifanya Taasisi ya familia ionekane sio muhimu kama ilivyokua awali.
Nadhani madhara tumeanza kuyaona mdogo mdogo.
@VwalaViola@MarekaMalili Hahahahaa utapambana na Manka wenu hapa ndani kila siku ananiambia kwa kingereza chake broken “Mama Abi I want rain coat, me play in the mud with rain boots”
Karibuni kununua vitabu vyangu vioya kwa watoto wanaojifunza kiingereza. Ni vifupi naamini vimejaa ucheshi na mvuto wa kumshawishi mtoto kupendsa kusoma
@MarekaMalili Ukiwa na mtu wa ku-provide….sisi wanawake unaweza kabisa kupumzika 😄😄. Ila mwanaume unapumzikaje kama hujatengeneza channels za kipato zinazojiendesha. Ukipumzika tu familia inalala njaa 😄😄😄
Kangaroo Mother Care (#KMC) has been proven to make a positive impact on #Preterm babies. For #WorldPrematurityDay2023, explore how skin-to-skin contact is vital for premature babies and their development.
https://t.co/tQBUPzmLsY
"Mwenyezi Mungu amefinyanga watu tofauti kwa mahitaji na matumizi tofauti. Huwainua anaowahitaji kwa wakati unaofaa na kwa makusudi maalum." ~Togolani Mavura.
Kuna nguvu kubwa sana katika kusamehe, kukubali aibu, kukaa kimya pia kusimama na Mungu wakati wote, Kama tungelipiza visasi, tungewachafua waliotuchafua, tungewaharibia waliotuharibia leo tusingefika hapa tulipo.
Tumekuwa busy sana kutafuta pesa huku tukitunga misemo fake “Pesa ndio kila kitu “tukaachia malezi TV , Shule na wasidizi wa ndani.Tulisema nataka nihakikishe watoto wangu wanapofika chuo kikuu wawe tiyari na mashamba , nyumba na mali.
Tukifikiri hii ni highest achievement ktk maisha kuliko utu,tabia njema na heshima.Sasa tunaishangaa jamii imekuwaje huku wazazi tukisema watoto wa siku hizi hawana adabu na kumbe ni wazazi wa jana hatakujali vizuri.
Kaa chini siku moja tafakari wajibu wetu ktk familia zetu na utagundua kuwa tumenunua nyama nyingi na juice kuliko kujenga tabia za familia zetu. Ni kweli kwenye friji kuna kila kitu je watoto wetu wanajifunza attitude sahihi kutoka kwetu ?
Tuwe makini sana tusije kuwa na shimo la maji machafu lililojaa vinono mbali mbali kuliko maarifa kwa watoto wetu ktk fikra zao. Kuna tatizo kubwa ulimwenguni , kubwa kuliko mabadiliko ya Tabia Nchi na Dunia haioni wala haisemi.
Dunia inaangushwa na ukosefu maadili kuliko kitu chochote.Kizazi chetu tunaweza kupiga U turn kwani hatujachelewa sana.Kama tukitafakari kuamua kuwa walezi halisi na sahihi sasa.
Tuna confusion society sio kwa sababu hila za shetani zina nguvu ila ni kwa kuwa muda wetu hauko kwa Mungu na familia.
@SwahiliBible Na recently nimeskia wazazi kadhaa wakilalamika watoto kupewa homework ya vitu ambavyo bado hawajafundishwa……nikasema ikinipata mimi basi asubuhi itanikuta mlangoni ofisi ya Mwalimu Mkuu. Kwanza homework za nini hivi? 😄😄😄😄😄