Mfumo Unaotumika Ni Mmoja Tu Na Huu Unafahamika Kama When The Mission Is Completed Then The Dog Must Die.
You Friend Shall Now Be My Enemy Osama Bin Laden Alitumika Na Marekani Miaka Ya 1980 Afghanistan Baade Wakamgeuka Kilichotokea Kimebakia Kua Historia
"Kwa wote wenye kadi za CCM bei hii mpya ya mafuta haiwahusu, hii ni kwa wapinzani tu hasa hasa CHADEMA, ukifika petrol station onyesha kadi yako ya CCM na utauziwa mafuta kwa bei ya zamani TZS 2800 na sio TZS 3800, nchi ni yenu bwana lazima mtambe!" @AdvMatata
KARAGWE
CHATO
GEITA
MWANZA
MUSOMA
SERENGETI
LAMADI
SIMIYU
BARIADI
MBEYA
LINDI
MTWARA
Yote imeenda hii, IMEENDA mapema kabisa
Hakuna namna hii imebaki
Kwa Kheri CCM kwa Kheri
Bado maeneo mengine yanayopitiwa yanapitiwa yatakwenda
"Leo CHADEMA imeamua kususia uchaguzi kwa maamuzi ya watu wachache, na jambo hili pasipo kujadilika na kupitishwa na kikao chochote cha ndani ya chama, na ikumbukwe na ninayeongea hapa mimi ni Mjumbe wa Kamati Kuu. Suasa la No Reform No Election lilizungumzwa, lakini kama Mjumbe wa Kamati Kuu hakuna popote tumewahi kusema tunakwenda kuzuia uchaguzi, hakuna popote ambapo tumewahi kusema tunasusia uchaguzi, lakini yanayoendelea sasa hivi ni maamuzi ya watu wachache ambao wameamua kuwahadaa Watanzania na kuwaambia kwamba CHADEMA itakuwa na uwezo wa kuzuia uchaguzi. Ukiangalia vizuri na ukisikiliza hotuba mbalimbali zinazoendeleaโฆMheshimiwa Mwenyekiti ambaye sasa hivi yupo gerezani, amekuwa akisema kwamba wananchi wataandamana kuzuia uchaguzi na kada wa CHADEMA Dkt. Slaa amekuwa akisema wananchi watalala yumbani siku ya uchaguzi, maamuzi hayo hayakuwahi kuamuliwa na kikao chochote cha Kamati Kuu, mimi nimekuwa mjumbe wa Kamati Kuu", - Devotha.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Kati, Devotha Minja akizungumza na wanahabari siku ya Alhamisi mkoani Morogoro.
Gazeti la @Nipashetz hongereni kwa kuipa uzito unaustahili habari ya kutekwa , kupigwa na kufichwa kwa @mdudenyagali.
Mungu awabariki sana. Mdude ni baba wa familia, kaka, uncle na ana ndugu zake. Mdude si ngโombe wa kupotezwa na kusiwe na kishindo. Muachilieni Mdude, akapate matibabu!
#FreeMdudeNyagali
Watu walitumia Ruzuku kama Agenda ya kuombea kura,
Sasa wanaoshauri kuhusu Uchaguzi wanaitwa wasaliti, walionufaika na Agenda ya Ruzuku Wamesahau bila uchaguzi hakuna Ruzuku.๐๐
Kaka, hujui hata 1% niliyofanya Shinyanga nikiwa Diwani 2015-2020!
Watu wa Shinyanga ndio wanafahamu na viongozi wako wa CDM. Kwa taarifa yako tu.
Shinyanga NASHINDA misa ya kwanz, hata bila reforms yoyote, tumejenga Chama na Chama kipo hai kuliko mahali popote pale.
โNimeshitushwa na uamuzi wa Mwenyekiti wa Chama Taifa (Tundu Lissu) ambaye pia ni Mwanasheria nguli kukiuka misingi ya Katiba ya Chama chetu na misingi ya haki za Binadamu hasa haki ya kusikilizwaโ Catherine Ruge
Nakiri kupokea ujumbe mfupi kwa njia ya sms kutoka kwa Katibu Mkuu wa Chama @jjmnyika kuhusu hatua iliyochukuliwa na Mwenyekiti wa Chama Taifa @TunduALissu kutengua nafasi yangu ya Mkuu wa Dawati la Jinsia la Chama.
Naomba kueleza kwa kifupi kama ifuatavyo;
Kanuni za Chama toleo la mwaka 2019, Kanuni ya 6.5 imeweka utaratibu wa kumchukulia hatua mwanachama na kiongozi yeyote ndani ya Chama .
Mathalani Kanuni ya 6.5.1 inaweka utaratibu wa kufuatwa namna ya kuchukua hatua za kinidhamu, mojawapo ni kuandikikiwa mashtaka yako na kupewa nafasi ya kusikilizwa.
Kwa tangazo la Mwenyekiti wa Chama lililotolewa leo na mimi kutumiwa ujumbe mfupi wa simu, ni wazi kwamba utaratibu huo umekiukwa.
Nimestushwa na uamuzi wa Mwenyekiti wa Chama Taifa ambaye pia ni Mwanasheria nguli kukiuka misingi Katiba ya Chama chetu na misingi ya haki za Binadamu hasa haki ya kusikilizwa.
Nimetenguliwa bila kupewa wala kuelezwa makosa yangu na sababu za kutenguliwa kwangu ambapo pia ni kinyume na Katiba ya nchi Ibara ya 13(6)(a) ambayo inaweka msingi wa haki ya kusikilizwa.
Hata hivyo mimi nilikuwa Kiongozi na nafasi yangu iliidhinishwa na Kamati Kuu ya Chama, kwa mujibu wa Katiba ya Chama ibara 6.2.3 (b) Mamlaka ya Utenguzi wa nafasi yangu ni Kamati Kuu na sio Mwenyekiti wa chama hivyo nilitegemea utaratibu wa Kikatiba na Kanuni ungefuatwa
Nitaeleza mengi huko baadaye.
CPA Catherine Ruge (Msubhati)
05.04.2025