Polisi wanasema 02/05/2026 saa tatu asubuhi eneo la Mburahati, Kinondoni alikamatwa Dammour Massoumbe Nyakairo, @Ninja_Damour na kupelekwa kituo cha Polisi Chang’ombe kwa tuhuma za kujihusisha na vitendo vya kihalifu (ambavyo hawajaeleza) na kwamba katika mahojiano ya awali ametoa ushirikiano kwa kueleza mambo mbalimbali (kwa mujibu wa taarifa yao). Hatua za kisheria zinakamillishwa ili afikishwe kwenye mamlaka zingine za kisheria.
Kimsingi, tutampa msaada wa kisheria. #FreeNinja #FreeDamour
TUMIA REMOTE CIU YA JIRANI YAKO KUWEKA UMEME.
kuna wakati unakuta kifaa chako cha kuingizia umeme yaani ile remote ya mkononi (CIU) imepasuka au imegoma kabisa kupokea token hata ukifanya troubleshooting kwa kuingiza code bado umeme hauwaki.
Leo ntakuonyesha namna...
HAPA SI KWAMBA BIBLIA ILIJICHANGANYA, HII INAITWA "ANOMALY TRANSCRIBING
Kosa hili si kosa la biblia, hili ni kosa la kunakili, na mtu hapaswi kusema BIBLIA ILIKOSEWA Bali huwa tunasema BIBLIA INAMAKOSA KATIKA KUNAKILI najua mna ugumu fulani katika kuelewa, Lakini ngoja nikueleweshe.
Katika kitabu cha ILLUSTRATIONS FROM BIBLICAL ARCHEOLOGY.
Uk 33. D. J. WISEMAN anatuambia,
"Waandishi wayahudi walikuwa wakifanya kazi yao kwa uangalifu Sana, wakajitahidi kwa bidii yote wasilikosee neno hata moja wala hata herufi moja katika biblia, na walipokuwa wakinakili neno baada ya neno walikuwa lazima walitamke kwa mdomo, ilimradi wasifanye kwa kumbukumbu tu, walipomaliza kunakili ukurasa mmoja walihesabu kila neno na kila herufi, na ilipobainika kuna hata kosa moja dogo, hawakusahihisha, Bali waliuchoma moto ukurasa huo mara moja, Kabla ya kuandika neno Mungu waliisafisha NIBU, na kabla ya kuandika neno Yehova walioga mwili mzima, halafu karatasi za zamani zilizokwisha kunakiliwa sawasawa na kuchakaa baada ya kutumika Sana, zikichomwa pia, kisha zikanakiliwa nyingine kwa bidii "
Lakini pamoja na yote wale wayahudi walikuwa ni binadamu ambao ni wanakili wa upili, sasa lazima waliweza kukosea Kama sisi, sasa hawa waliingiza baadhi ya Anomaly transcribing hata Kama walikuwa chini ya sheria kali za unakili.
Makosa ya unakili (Anomaly transcribing) huwa ni tofauti baina ya nakala moja na nyingine pengine huwa na tofauti ndogo.
Mfano wa makosa ya Kunakili ni hili ambalo jamaa hapa anaongelea bila kujua,
Ukisoma (2 wafalme 8:26) hapa tunaambiwa Ahazia alianza kutawala akiwa mwenye umri WA miaka 22.
Lakini ukisoma (2 Mambo ya Nyakati 22:2)
Hapa tena tunaambiwa Ahazia alianza kutawala akiwa na miaka 42.
Hili si kosa la biblia, hili ni kosa la kunakili, na mtu hapaswi kusema BIBLIA ILIKOSEWA Bali huwa tunasema BIBLIA INAMAKOSA KATIKA KUNAKILI
Makosa Yanayofanana na haya sio kwamba huwa Hayajulikani, Yanajulikana na yalishatolewa ufumbuzi.
Mfano kosa hili lilifumbuliwa na kusahihishwa na Biblia yenyewe, Kupitia kitabu cha (2 wafalme 8:17) utagundua kuwa (2 wafalme 8:26) ambayo inatuambia alikuwa na miaka 22 ndio inayosema kweli, maana Kama alianza kutawala akiwa na miaka 42 Kama tunavyosoma katika mambo ya Nyakati, basi Alizaliwa kabla ya baba yake Yoramu.
Vitabu Hunakiliwa na Binadamu na Binadamu hukosea hata awe katika Sheria Kali namna gani.
Ukizima internet, unathibitisha kuna kitu unaficha.
Ukizima internet, unasimamisha uchumi.
Ukizima internet, unafukuza watalii.
Ukizima internet, unafukuza wawekezaji sekta ya teknolojia (startups).
Ukizima internet, unachochea kusambaa kwa misinformation.
Ukizima internet, unavutia makini ya watu wa mataifa mengine wajiulize kuna nini kinaendelea Tanzania?
Ukizima internet, unajishusha hadhi ya mpatanishi wa amani kanda ya maziwa makuu.
Ukizima internet, unawapa maunjanja Watanzania kutumia mbinu mbadala.
UKIZIMA INTERNET, UMEAMUA KUJIZIMA AKILI.
May we also #PrayTogether for #Tanzania, where, following the recent elections, violent clashes have broken out, leaving many victims. I urge everyone to avoid all forms of violence and to follow the path of dialogue.
Pale TUMAINI la Mwanadamu linapoishia, ndipo UAMINIFU wa Mungu Unapoanzia!
UTUKUFU wa MUNGU ulionekana baada ya Lazaro kufa na kuanza KUNUKA, sio wakati anaumwa!
So Kuna wakati Mungu anasubiri ukate TAMAA ili yeye aingie kazini. Na mwishowe akuoneshe Ukuu wake.
MUNGU ANAJIBU!