“Mimi sishtakiwi kwa kuchana kura. They’re fishing expedition. Wamechukua mtumbwi wanazunguka nao pembeni kuokoteza vimaneno mtaani ili kutengeneza maana yao. Mimi nashtakiwa kwa kosa la uhaini siyo vinginevyo. Wanaleta mambo yasiyohusiana na kesi wanayonishtaki nayo. Kama wangetaka kunishtaki kwa kuchana karatasi za kura wangeleta mashtaka hayo hapa…,” - Tundu A.M Lissu, Mahakama Kuu, 10 August 2026.
Mzee Wa Miaka 90 , Mzee JOHN OUMA ODERO Akabidhi Kiwanja Bure Kwa Chadema Na Kuomba Kiwanja Hicho Kijengwe Kwa Kuipa Chama Hadhi Katika Kata Ya Nyathorogo Wilaya ya RORYA..
Kiwanja Hicho Kimepokelewa na Mwenyekiti Wa CHADEMA Mkoa Wa Mara Mwl Chacha Heche Akiwa Kwenye Ziara Yake ya Baraza la Uongozi Mkoa wa Mara, Mwenyekiti Amesisitiza Kiwanja Hicho Kitajengwa Kwa Haraka na Jina la Jengo Hilo Litapewa Jina La Mzee Huyo Mzee JOHN OUMA ODERO.
Huyu ni Simai Mohamed Said Mbuge wa Jimbo la Tunguun (Zanzibar)
Wasilisho la mbunge huyu leo hii akichangia bajeti ya wizara ya fedha, limebainisha dhahiri ndani ya serikali kuna msigano mkubwa.
Mbunge huyu alitoka kabisa nje ya mada kuchangia hoja iliyokuwepo mezani na kuanza kumshambulia mtu anayedai yupo ndani ya serikali kwa kumuita Yuda
Kwa mujibu wa video hii, Mbuge huyu anamtaja Yuda kwa sifa zifuatazo
1. Anatumia vibaya nafasi ya kuaminika na rais kumsaliti
2. Mtu huyo amefitini watu ambao walikuwa wanakaa siti za mbele bungeni (mawaziri) na sasa wako backbench. Amefitini sana wafanyabiashara na kupotezea wengi ndoto zao za kisiasa.
3. Mtu huyo amekuwa akilitumia kanisa kuifitini serikali
Hadi hapa nilikuwa nimetatizika sana kumjua mtu wenye wasifu hapo juu.
Lakini mbunge huyu akanirahisishia kazi alipoongeza kuwa
4. Yuda anajidai alikuwa anapendwa na hayati Magufuli wakati enzi za utawala wake alimtupa mbali huko nje ya nchi.
Hili halikuwa tena fumbo kwangu.
Ni hivi karibuni, katika msiba wa mama mzazi wa hayati rais Magufuli, John Nchimbi, Makamu wa rais, amenukuliwa akielezea jinsi alivyokuwa karibu na hayati Magufuli wakiitana watani.
Jinsi alivyokuwa akichukua pipi za Magufuli kwa kuwa hakuwa akila pipi, jinsi alivyotaka kumteua ubunge kupitia nafasi 10 anazopewa rais, na hadi jinsi alivyomteua balozi japo alishamwambia nia yake ya kutaka kupumzika.
Nchimbi katika kutaka kuthibitisha hili, akaomba wasaidizi wake wamletee simu yenye ujumbe aliotumiwa na Magufuli ambao ameutunza mpaka leo na aliuonyesha kwa familia yake yote.
Kwa hiyo, mbunge huyu Mzanzibari ameshaanza kutupa code kuwa kuna kutoaminiana ndani ya viongozi wa juu wa serikali.
Nachelea kusema mbunge huyu hakuingea haya kwa bahati mbaya bali imetokana na vikao vilivyofanyika sehemu na kuaminishana haya aliyoyaongea leo, na ametumwa kuyawasilisha.
Ujumbe mwingine unatumwa hapa ni vita dhidi ya kanisa ambalo halijatajwa.
Kama alimaanisha kanisa la Nchimbi, basi kuna vita visivyo vya wazi kati ya watu fulani ndani ya serikali na Kanisa Katoliki.
End of evening rant
Anaandika Dr. Chris Cyrilo
Wamakonde wanaamini; ukikuta katoto ka nyoka ndani ya nyumba, ujue wazazi wake wapo humo.
Kumbe katoto ka nyoka kamesafiri umbali gani hadi kafike ndani ya nyumba yako?
Wakati huyu ndugu akitoa hotuba yake, nataka kujua mwitikio ulikuwaje miongoni mwa kile kikundi kinachojiita bunge. Je! Anayejiita Spika alimkatisha au alimuhoji au alimuacha afunguke?
Tambua kwamba kitoto cha nyoka kinakuwa na wenzake. Ni nadra nyoka kutaga yai moja!
"Machache tunayoona na kusikia ni matokeo ya mambo mengi yanayoendelea sirini"
Kama nchimbi ni mtu wa haki na anafanya nini kwenye umakamo mpaka sasa hivi, kama anasimama na wananchi ajiuzulu ili harakati zake ziwe na nguvu.
Wananchi watamuamini Nchimbi kama atajiuluzu asijiingize kwenye sakata la Mauwaji ya okt 29 na utekaji wa wanamtandao unaoendelea
KWA WOTE WASIOFAHAMU:
YUDA ni mtu MUHIMU SANA katika historia ya UKRISTO DUNIANI. Alifanya kazi KUBWA na NZURI kuhakikisha YESU KRISTO ANATESWA, ANASULUBIWA, ANAKUFA, na hatimae ANAFUFUKA ili WAKRISTO WAKOMBOLEWE DHAMBINI. Tafadhali, YUDA ASITUMIKE KISIASA.🙏
Nilipoona huu ULINZI mkali nilijua tuu hakuna usalama hapa.
Leo tayari WABUNGE HARAMU wameanza kumuita NCHIMBI “YUDA”. Na inaonyesha tayari kuna makundi kati yao maana anaemuita NCHIMBI YUDA hapigiwi makofi kama ilivyokawaida yao (Wanamchora tuu).
Tupo mwishoni aisee—washaanza kugawana fito hawa, jambazi kuu limetoka kutafuta msaada kwa PUTIN, ndichi hakukaliki safi sana.
Tuendelee kupeleka moto hawa hawamalizi ROUND hawa.🔥🔥
Mchawi binadamu, paka anatumwa tu.
MPEMBA ametumwa kumshambulia NAMBA MBILI wao na amembatiza jina la YUDA. Kosa lake ni kusema alipendwa sana na JIWE. Wamekasirika sana. Jamaa anasema JIWE alimtupa Brazil. Wanasema ametengwa hadi na familia ya ‘WHITE HAIR’. Eti ni kweli, wazee wa ‘Safari ya Matumaini’ mmemtenga 'Mzee wa Mustachi'? Sisi wengine tunafurahi. Kazi yetu moja tu, kuchochea kunu. Ushirika wa 'wanyonya damu' hauwezi kudumu.
NB; kama wapo wengi, kwanini hakuna makofi? SIJAPENDA.
Mahita kaamua kumwaga ugali na mboga.
Tafsiri ya kauli yake inaweza kuwa watuhumiwa wanauwawa ktk vituo vya polisi.
Ukweli huu pia unatokana na wananchi wengi wanaowatafuta ndugu zao wanaodaiwa kushikiliwa vituoni bila kuwaona.
Hii ndio Tanzania; ni rahisi kuuwa mtu kuliko kuku.