I am who I am. A graduate of BA in Statistics (U DSM), PGD in M&E (TIPM) , Masters in Shipping Economics & Logistics (DMI) and Certified Lead Auditor (QMS)
You were duped. Again.
We all saw the “massive” walkout from the UN general assembly. It seemed like Bibi was talking to en empty room. Some journalists even reported that. Even some Israeli journalists made that claim.
Guess what. The media lied to you. Shocked?
Here are the facts.
The footage is real. As Netanyahu walked up to speak, dozens of diplomats got up and left. It looks like most of the world refused to listen to him. Some even called it proof that Israel is now a pariah state.
And now, reality.
More than 120 countries stayed. That's nearly two-thirds of the world.
All five veto powers stayed: the U.S., China, Britain and France.
So did most of Europe. Even Ireland, one of Israel's toughest critics remained.
So who walked out? And why does it look like so many?
Each country gets six seats in this hall, so when one delegation walks out, several people stand up and walk.
And the Palestinian mission had asked countries to bring as many staff as possible and walk out together.
That can make a walkout bigger than the number of countries behind it.
In Europe, Spain was the only major country to leave its seat empty.
In Latin America, Brazil walked out.
South Africa's seats were empty too.
The rest were mostly small Caribbean island nations, which skip most speeches anyway.
Even in the Muslim world, at least two countries, UAE and Bahrain, stayed.
The walkout was real, but most of the world stayed in the room.
Just thought you’d wanna know the truth.
Unataka kuwaambia umma wa Watanganyika na Watanzania kwa ujumla wao kwamba Jamhuri imepeleka kesi uchwara mahakamani? Kesi ya uchwara ya Lissu nani kafanya iwepo Mahakamani? Na aliyepeleka surmons kuwaita ni @TunduALissu au ni Mahakama za Jamhuri?
Kwamba mkuu wa majeshi aache kutulindia nchi na mipaka yetu aje asikilize kesi uchwara ya Lissu? Lissu apambane na mashahidi wake wa kimo chake asihahe kushirikisha viongozi wakuu kutafuta huruma wakati anajua kesi ameshindwa na atahukumiwa kifo kama ataacha ujeuri na kibri.
@Phbhimself kila nikisoma andiko zako sikosi kujiongeza ufahamu mwingine zaidi. Keep that gift brother . You know to how enlight people . You can be a good judge and hope you are good judge even now.
Nakuelewa sana unachosema, na kwenye hoja moja kubwa nakubaliana nawe asilimia mia..
Kwamba mwanaharakati hawezi kuwa shabiki wa chama kiasi cha kushindwa kukikosoa pale anapoona kinaenda kinyume na maslahi ya wananchi.
Kama mlisimama na Heche wakati alipokuwa anashambuliwa, ni haki kabisa kusema mlifanya hivyo na kudai chama kitambue mchango huo.
Lakini kuna kitu kimoja ningependa tukitenganishe vizuri. CHADEMA ni taasisi yenye Katiba, viongozi na vyombo vya maamuzi.
Maamuzi makubwa ya chama hayawezi kufanywa kwa pressure ya wanaharakati wala kwa pressure ya mitandao.
Wanaharakati wanaweza kuwa pressure group, watchdog na sauti ya wananchi, lakini hawawezi kuchukua nafasi ya organs za chama.
Na hapa ndipo nadhani nguvu yenu ipo, kwamba msijaribu kuwa CHADEMA, ila ibaneni CHADEMA iwe CHADEMA.
Yaani kama chama kinazungumza haki, demokrasia na uwajibikaji kwa Serikali, basi kanuni hizo hizo lazima zikubaliwe zinapokuja kwa chama chenyewe.
Mnaweza kuunga mkono msimamo wa chama leo na kukikosoa kesho bila kuwa wasaliti.
Na kuhusu Oktoba 29, naelewa kabisa kwa nini watu wana hasira na uchungu. Lakini hasira ya wananchi isiwe mbadala wa ushahidi.
Kama kuna waliouawa, waliotekwa au walioteswa, kinachotakiwa ni ukweli, accountability na justice na sio kumhukumu mtu kwa sababu tu ya hisia za umma.
Na wote tunatambua kwamba damu ya mtu haiwezi kutafutiwa haki kwa kuvunja due process.
Pia mara nyingi umekuwa ukisema kuhusu siasa za Mbowe au siasa za mshike mshike, hapa pia tuwe makini sana.
Kumbuka mwanasiasa anapaswa kuwajibika kwa wananchi, lakini mwanaharakati naye anapaswa kubaki huru kiasi kwamba hata chama anachokipenda kikikosea awe na ujasiri wa kusema, hapa mmechemsha.
Na hapo ndipo credibility ya mwanaharakati inakaa.
Pia kama mnawaambia CHADEMA, wasiwachukulie kama marafiki, mimi ningesema sawa, ila msiwe marafiki zao, kuweni watchdog wao.
Kwa maana rafiki anaweza kuficha kosa la rafiki yake, lakini watchdog hawezi. Kingine leo mtailinda dhidi ya Serikali inapobanwa, ila kesho mtailinda dhidi ya yenyewe inapopotoka.
Nafikiri hiyo ndio aina ya pressure ambayo chama cha upinzani kinapaswa kuiogopa kidogo, na sio kwa sababu ni uadui,
Bali kwa sababu inakikumbusha kwamba mamlaka ya kisiasa ni dhamana, na sio mali ya viongozi.
Wahenga waliwahi kusema aliyeng’atwa na nyoka akiguswa na jani lazima ashtuke.
Ipo hivi bwana @godbless_lema , watu wana haki ya msingi kabisa ya kutilia mashaka mienendo ya viongozi, haswa pale wanapoona anomalies.
Mbowe alikaa gerezani zaidi ya siku 200 kwa kesi ya ugaidi. Kesho yake Mbowe huyo huyo akaanza kupanda kwenye majukwaa mara kumpa mtukufu tuzo mara kusifu na kuabudu juhudi.
Wenje alikuwa persecuted na mtawala kwa miaka mingi tu kama wewe. Keshokutwa Wenje huyo huyo akaanza kutembeza mabegi ya pesa kuhonga watu.
Alikataa yote lakini mwishone akajieleza mwenyewe kandarasi zake na Abdul.
Nataka kusema ni kweli umejitoa katika haya mapambano kwa muda mrefu na umelipa gharama.
Hata hivyo hii haizuii kwenda rogue na umma una haki ya msingi kabisa ya kukutumbulia macho.
Je, hii inamaanisha watu wazushe tu mambo na kufanya character assassination?
Hapana, haipaswi kuwa hivyo.
Lakini pia haimaanishi kila kinachosemwa ni uzushi.
Tuliona kwa Mbowe tukaona kwa Wenje. Yale yale yaliyoitwa uzushi ndio hayo hayo waliyokuja kuyaweka wazi.
Nadhani somo kubwa hapa ni kwamba viongozi hampaswi kuwaweka wananchi katika mazingira ya kuzusha na hata kuamini uzushi.
Watu sio wapumbavu. Mkianza kuonesha tabia fulani fulani, lazima watu waanze kuunganisha nukta.
Tundu Lissu aliwahi kukiri kuwa kuna wakati matendo ya viongozi wa CHADEMA yaliwachanganya sana wananchi.
Ni wajibu wenu kama viongozi wa CHADEMA kuepuka kuwachanganya wananchi.
Wananchi wameshang’atwa na nyoka. Ni juzi tu Wananchi wametoka kuzika maelfu ya ndugu zao waliouawa kikatili na Samia. Wengine mpaka leo hawajapata hata nafasi ya kuzika ndugu zao.
Hauwezi kuwaambia hawa watu wasihoji inconsistencies zinazojitikeza kwa viongozi wanaojipambanua kuwapambania.
Hauwezi kuwaambia wasiunganishe dots pale wanapolazimishwa na maneno au matendo ya viongozi hao.
Act responsibly kama kiongozi, huu ndio ujumbe kutoka kwenye haya yote.
Iwe ni kwa bahati mbaya au makusudi, barua na tweet za juzi hazikuwa na uwajibikaji ndani yake.
Unaweza kuniuliza “kwa hiyo sipaswi kutoa maoni yangu?”
Nitakwambia “una haki ya msingi kabisa.” Lakini nitakukumbusha pia kuwa “umma nao una haki ya kuwa na maoni kuhusu maoni yako.”
Na mara nyingi, maoni ya umma ni mahakama.
Integrity integrity integrity!!!!!!!
I decide to believe you brother @godbless_lema kwa sababu najua yote yanataka uamuzi. Kutoendelea kukuamini au kukuamini vyote hujengwa katika kuamua. Mimi nimeamua kukuamini. God bless you man.
Mkutano wangu na waandishi wa habari niliokuwa nifanye katika Hotel ya Golden Tulip nimeuahirisha.
Nimesikiliza hotuba za Makamu Mwenyekiti na Katibu Mkuu. Wameeleza vizuri kuhusu uvumi na upotoshaji uliokuwa ukifanyika juu yangu na misimamo juu ya chama chetu.
Nimedumu katika mapambano haya kwa zaidi ya miaka 22. Nimeenda lock-up zaidi ya mara 50. Nimezunguka nchi hii usiku na zaidi ya mara tatu. Nimewahi kuwa magerezani mara kadhaa, nimekoswa kuuawa zaidi ya mara tatu, na nimewahi kukimbia nchi.
Katika yote haya, nimekuwa nikitoa sadaka kubwa kwa ajili ya mapambano haya, ikiwemo ku-sacrifice familia yangu mara zote.
Kazi hii kwangu si ajira, si cheo, wala si njia ya kujitafutia maslahi. Ni huduma. Ni wito. Ni kama injili ninayoamini na kuitumikia.
Kwa hiyo, siwezi kuruhusu uvumi, upotoshaji au tafsiri za watu kuniondoa kwenye misingi ambayo nimeisimamia kwa zaidi ya miongo miwili.
Nitakuwa kwenye mapambano haya kwa imani, ujasiri na dhamira njema siku zote.
Hongera sana kaka Lema
Umefanya jambo la maana sana. Kimsingi uamuzi wako huu umekiumiza sana @ccm_tanzania kwasababu walikuwa wanasubiria kwa hamu sana useme utakachokisema wakitumie kuweka mpasuko wa ndani ya Chama.
Umewaumiza sana hata washirika wa CCM kwa uamuzi huu in fact usiwe tu kwamba umeahirisha bali uwe umefuta habari ya ma-press.
Tulishakanyagana sana inatosha Mwenyekiti yupo ndani kwa makosa ya Uongo. Kazi yetu ni kumtia moyo na kumpigania kwa maneno na matendo yetu.
Big up sana kaka👊✊💪
Hongera sana @TunduALissu majitoleo yako kwa namna zote ndiyo yamekufukufikisha hapa. Hongera #Tanganyika kwa kuzaa na kulea mtoto huyu. Hongera @ChademaTZ2 kwa kuwa Kiongozi wa mfano wa @TunduALissu. Heri yetu #Tanzania kama tutaona mtu huyu wa thamani katikati yetu.
@Malyekete@davidmcallister@TunduALissu@EPPGroup What is happening now about the subject matter? Is LGBT not a reality in your street? Is it waiting for @TunduALissu to be honored because of his resolve to the fight of Democracy in his nation? You better learn to think indepently. Argument hiyo uliyoandika ni ya kukariri
If you are not sure imekuwaje unaambatisha kitu usichokijua na picha ya @HecheJohn ? Kwa kufanya hivi je umethibitisha kwamba ni yeye ? Wegesa Trading means @HecheJohn ? Is that what you mean kwa taarifa yako hapa?
Heche kwenye Bank nje ana zaidi ya USD 250K, hizi aliingiziwa kupitia Wegesa trading Limited, I am not sure yet kuwa hii kampuni yao au yake. Swali ni, Heche anafanya kazi gani ya kuingiziwa USD 250K, katika account ya nje ya nchi. Wanachadema, fedha zenu za Tonetone ziko huku.
Heche anakiri kuwepo kwa barua za Januari 2026 zilizomwalika yeye na CHADEMA kukutana na Tume.
Hapa prosecution inaweza kutaka kuonyesha kwamba kulikuwa na formal opportunity ya kutoa taarifa.
Lakini Heche pia anasema barua hizo hakutaka ziwe sehemu ya ushahidi wake, hilo ni muhimu.
Maana document kuwepo sio sawa na document kuthibitisha substantive truth ya allegations zinazohusiana na kesi ya Lissu.
Lazima mahakama ijue document hiyo inaletwa kwa purpose gani, na relevance yake kwa fact in issue ni ipi.
Jambo lenye uzito zaidi ni jibu la Heche kwamba, unampaje mtu ushirikiano bila kualikwa. Hapa prosecution inahitaji kuwa makini sana.
Kama ushahidi unaonyesha Tume ilimtumia Heche au CHADEMA mwaliko rasmi, swali la ushirikiano linaweza kuwa na weight.
Lakini kama prosecution inataka kuonyesha kwamba CHADEMA ilikataa kushirikiana bila msingi, lazima ionyeshe invitation, response, conduct ya chama na circumstances kwa ukamilifu.
Huwezi kubadilisha absence of appearance kuwa refusal to cooperate bila evidentiary bridge.
Pia kuna distinction muhimu kati ya kutoenda mbele ya Tume fulani na kuficha ushahidi wa tukio fulani, hayo ni mambo mawili tofauti.
Kwamba Heche anaweza kusema CHADEMA haikuitambua au haikuikubali Tume ya Chande, lakini hilo pekee halithibitishi kwamba CHADEMA ilificha taarifa, wala halithibitishi kwamba Lissu alihusika na matukio ya Oktoba 29.
Na hapa ndipo relevance inapoingia, kwamba Tume hiyo ilihusu matukio ya Oktoba 29, 2025, wakati speech inayomkabili Lissu ilitolewa Aprili 3, 2025.
Kwa hiyo prosecution ikitaka kutumia conduct ya CHADEMA mbele ya Tume hiyo kama circumstantial evidence dhidi ya Lissu,
Lazima ijenge causal and evidentiary nexus kati ya matukio hayo na alleged intention ya Lissu miezi kadhaa kabla.
Otherwise, tunakuwa na tukio moja likitumika kutafsiri tukio lingine bila bridge ya ushahidi.
Zaidi ya hapo, taarifa kwa umma inayowaalika wananchi kutuma SMS, WhatsApp au email kuhusu matukio ya Oktoba 29 inaonyesha kwamba Tume ilikuwa ikikusanya taarifa kutoka kwa umma.
Hiyo inaweza kuwa relevant katika kueleza mazingira ya uchunguzi, lakini sio proof kwamba kila taarifa iliyokusanywa ni true.
Kwamba, collection of evidence is not proof of the contents of that evidence. Hapo authenticity, source, corroboration na probative value bado vinabaki muhimu.
Na sehemu ambayo prosecution inaweza kuonekana imepata point, kwamba kulikuwa na watu waliowashawishi wengine kutokwenda kutoa taarifa bado inahitaji identification.
Kwamba, Who were those people? Walikuwa wakimshawishi nani? Walikuwa na authority gani? Lissu alihusikaje?
Bila majibu hayo, statement ya jumla haiwezi moja kwa moja kuwa attribution kwa accused.
Naweza kusema upande wa defence, hii ndio advantage inayojitokeza, kwamba prosecution inaendelea kuleta nyaraka na matukio ya baadaye,
Lakini lazima ionyeshe relevance yake kwenye ingredients za offence inayomkabili Lissu.
Tukumbuke mahakama sio mahali pa kukusanya political suspicion, ila ni mahali pa kuthibitisha facts in issue kwa kiwango kinachotakiwa na sheria.
Wewe ulivyotekwa na kutendwa je umechukua hatua gani? Kwa nini umekimbia nchi yako? Love thy enemies kwa nini hutaki kuwapenda ukiwa ndani ya nchi yako? Ulichofanya ni Action and reaction are equal but in opposite direction. Hi Sheria ya asili. Mtenda ukatili atatendewa ukatili.
Ni upofu unaotafuta wafuasi kwa njia nyingine mdogo wangu @Sativa255 . Nini kimemfanya akeshe kama hajishughulishi nayo? She hungry ndiyo maana anakesha kutafuta chakula kinachokidhi kusudi moyo wake. Anayoyasibilia ndiyo yanayo ujaza moyo na furaha yake ni kuyaona.
Sasa wewe huamini wanasiasa.
Sasa wewe Husikilizi wanaharakati.
Afu bado unafuatilia sakata la Mange na Lema mpaka usiku wa manane na unaweka comment yako.
Wabongo mnapenda kujofanya mko perfect, hapo unaona umeandika mwenyewe.🚮
Kama kweli No Reforms, No elections ya CHADEMA iliharibu Uchaguzi kwa hiyo kura milioni 30 na ushindi wa 98% mnataka kuthibitisha kwamba ni HEWA?(Maana wapo waliohoji kwa kina kura hizo na ushindi huo wenu) Au siku hizi Polisi na DPP wanashitaki watu kwa Ramli? BURE KABISA
Kama huyu ni deep state kama unavyotaka tuamini anafanya haya na hatujui mpaka tufikishane kwenye matukio kama haya ndipo tujue uovu kama uhuu kwatazamo wako basi TAIFA letu it is a failure state. Nani ataliokoa? It is you and me. Tuache ushabiki tufanye kazi. Saidia Taifa.
Tuliwaonya Mapema kuhusu huyu Deep State Boy (HECHE) na hamkutaka kuamini, sasa tutawaonyesha kuhusu Martini Maranja Masese (Zee la Pombe, Nyama na Pesa za Bure).
Ni suala la Muda tu
@Roma_Mkatoliki@ChademaTZ2 Uwajibikaji unaodaiwa na raia kutokana na yaliyojitokeza ni sehemu kuikamilisha Sheria asili ya Action and reaction are equal but in opposite direction @Roma_Mkatoliki. Na kama hali hiyo haijajitokeza basi hisia za wema kwa aliyekutendea ubaya zinapotea kiasili. @ChademaTZ2 knows
Sheria kuu ni hii "mtendee mwingine kama unavyotaka wewe utendewe" hivyo anayetenda ukatili @Roma_Mkatoliki maana yake anataka atendewe hivyo hivyo atendavyo Kwa wengine. Kwa mtazamo wako je waliotenda wema Kwa wengine hawastahili kurudishiwa wema wao?
Mwanamuziki wa HipHop, Roma Mkatoliki, amesema mjadala unaoendelea kati ya CHADEMA na baadhi ya wanaharakati ni jambo lenye ugumu na changamoto, akieleza kuwa chama hicho cha siasa kinapaswa kuonyesha tofauti ya tabia na mtazamo ili kujijenga kwa wapiga kura.
Kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii, Roma amesema, “Ukiniuliza mimi, nitakwambia game ya Chadema vs wanaharakati iko so tricky and kind’f complicated,” akidai kuwa baadhi ya watu wanaweza kuongozwa zaidi na hisia kuliko uhalisia wa siasa.
Roma amesema CHADEMA, kama chama cha siasa, kina lengo la kushika dola na moja ya majukumu yake makuu ni kuipinga, kuikosoa na kuishauri serikali. Kwa mantiki hiyo, amesema chama hicho kinapaswa kuonyesha kwa vitendo kwamba hakitafanya mambo kinayoyapinga kutoka kwa watawala.
“Hatutaua, kwaio inabidi wasiue hata sasa. Hatutaiba, inabidi wasiibe hata sasa. Hatutafurahia tukiona binadamu amekufa au ameuliwa hata akiwa ni adui,” ameandika Roma.
Ameongeza kuwa CHADEMA inapaswa kuonyesha utu hata pale inapokabiliana na wapinzani wake, akisema, “Adui akifa au akifiwa tutaenda kuzika na tutaenda kuhani msibani!!”
Kwa mujibu wa Roma, hatua hiyo ni muhimu ili mpiga kura asione kuwa chama kinachopinga utawala nacho kina tabia zinazofanana na zile kinazozikosoa.
“Otherwise mpiga kura ataona aaah mtawala wa sasa ni mkatili, lakini mbona hata huyu Chadema nayeye anaonekana ni mkatili kabla hata hajashika dola!!🤔 Huyu akishika dola si ndio atakuwa katili zaidi ya wa sasa!!”
Akizungumzia wanaharakati, Roma amesema hali inaweza kuwa tofauti kwa kuwa baadhi yao huongozwa zaidi na hisia za kulipiza kisasi.
“Kwa wanaharakati sasa ni tofauti…. hisia zinawapush wawe na mentality ya ngadu kwa ngadu, jino kwa jino, mwaga bapa namwaga kichanganyio!!”
Roma amesisitiza kuwa kwa mtu anayepinga mtawala, ni muhimu kutokuwa na tabia zinazofanana na mtawala anayempinga.
“Ni lazima anayempinga mtawala asiwe na characters za mtawala!!” ameandika, huku akihitimisha kwa kujiuliza kama mtazamo wake ni sahihi au ameamka akiwa na “wenge.”
@Roma_Mkatoliki@ChademaTZ2 Je umejaribu kuwatafuta waliokuteka wewe @Roma_Mkatoliki ? Na je Kwa nini umekimbia? That action but in the opposite direction, je kwa nini hukubaki kuonesha hisia za wema wako kana kwamba hakuna kilichotikea juu yako? Unajitaman kujaribu is theory katika hatua ya awali.
#Tanzania CHAMA gani kina wafuasi wengi mtandaoni kama sio wanaharakati? Naamini zaidi ya 80% ya walio mtandaoni hutegemea wanaharakati kama vyanzo vikuu vya taarifa au habari ambazo wanaziamini. Kama siasa ina mashiko kwa nini platform za vyama hazina wafuasi? Harakati ni UHAI
Wadau wa siasa nchini wamekitahadharisha Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) @ChademaTZ2 kujitenga na mienendo ya wanaharakati wanayoitaja kuwa inadhibitiwa na hisia za mtandaoni, ili kulinda uwezekano wake wa kuaminiwa na wapiga kura na kushika dola.
Akimulika tofauti kati ya uanaharakati na siasa za chama cha dola, msanii Ibrahim Musa maarufu kama Roma Mkatoliki ameeleza kuwa wanaharakati mara nyingi hufuata mtazamo wa "jino kwa jino" ambapo adui anapofikwa na maafa huchukulia hatua hiyo kwa hisia na hata kushangilia maafa hayo.
Kupitia andiko lake kupitia mitandao ya kijamii, Roma ameonya kuwa CHADEMA kama chama chenye ajenda ya kupinga, kukosoa, na hatimaye kushika dola hakiwezi kufuata mkondo huo wa hisia.
Roma ametahadharisha kuwa chama cha upinzani kinapaswa kujiepusha na viashiria vya ukatili kabla hata hakijashika dola, kwani mpiga kura anaweza kuingiwa na hofu na kuamua kubaki na mtawala aliyepo sasa.
“Kama unamkosoa kiongozi wa Chadema kwenye maoni kisha aka-kublock means huyo siku akiwa tu DC ukakosoa atakuweka ‘ndichi’ (ndani) masaa 72!! Ni lazima anayempinga mtawala asiwe na characters za mtawala!!”
Tahadhari hiyo inakuja katikati ya mjadala mzito ulioibuka nchini kufuatia kifo cha mume wa Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, Marehemu Hafidh Ameir Hassan, aliyefariki dunia Septemba 7, 2026, katika Hospitali ya Emilio Mzena na kuzikwa siku hiyo hiyo huko Kizimkazi, Zanzibar.
Wakati vyama vingine vya siasa vikienda msibani na kumfariji Rais Samia, viongozi wa CHADEMA hawakuonekana msibani wala chama kutoa taarifa rasmi ya rambirambi. Hata hivyo, Septemba 7, 2026, Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, anayekabiliwa na kesi ya uhaini na kukaa mahabusu kwa takribani mwaka mmoja na miezi sita, alisikika akiwaambia viongozi wake Mahakama Kuu Dar es Salaam: "Nasikia kuna msiba, wape pole... jamani pelekeni pole zangu kwa wafiwa".
Septemba 11, 2026, kabla ya kesi yake kuanza, Lissu alisikika akirejea salamu hizo na kuhoji kama zimefika alipomuuliza Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Zanzibar, Said Mzee: "Makamu umepeleka rambirambi zangu bwana?", na alipojibiwa kuwa zimefika, Lissu aliongeza: "Nimefurahi kama zimefika".
Septemba 13, 2026, Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Godbless Lema @godbless_lema , alichapisha ujumbe kwenye mitandao ya kijamii kuwasilisha salamu alizozitaja kuwa ni za Lissu na zake mwenyewe, jambo ambalo liliwawasha baadhi ya wanaharakati na wafuasi wa mtandaoni waliomshambulia Lema kwa matusi na kumwita msaliti. Wapo waliohoji ni kwanini ampe pole Rais wakati kuna watu walikufa au kuumizwa bila kupewa pole huku wengine wakidai kuwa hakuna mahali Lissu alipoashiria salamu na pole zake zilimlenga Dkt. Samia. Hata hivyo, baadhi ya wananchi walimuunga mkono Lema na Lissu kwa kile walichokiita kuonesha ukomavu wa hali ya juu.
Akijibu mashambulizi hayo Septemba 14, 2026, Lema amesisitiza kuwa hatua ya Lissu kutoa rambirambi si unyonge bali ni hekima na ukomavu akiandika, "Nimeona matusi na sintofahamu nyingi mtandaoni baada ya kuchapisha ujumbe wa kutoa pole kwa Mama Samia, hasa niliponukuu salamu za pole za Mwenyekiti Lissu kutoka gerezani. Kwa sisi jamii tunaodai kupigania uhuru wa maoni na demokrasia, hili linapaswa kutufikirisha. Kutofautiana kwa hoja hakuhitaji matusi, dhihaka wala chuki"
Naye mwanahabari Stanslaus Lambart ameeleza kuwa siasa lazima ziende na utu na kwamba Lissu na Lema walitumia nafasi hiyo kutuma ujumbe wa ubinadamu kwa washindani wao huku naye akitoa tahadhari kwa viongozi wa CHADEMA dhidi ya kutekwa na uanaharakati wa mtandaoni.
"Moja kitu kitakachoiumiza CHADEMA ni kuruhusu wanaharakati kuendesha siasa kwa shinikizo la mtandaoni (mob psychology) badala ya stadi za kisiasa zenye mikakati, diplomasia, na wakati mwingine lugha za staha hata kwa adui. Lakini mwanaharakati yeye anataka kila kitu kiwe cha ‘kupigana au kufa’ bila kuiachia akili nafasi”, ameandika Lambart na kuongeza,
"Ukiniambia niishauri CHADEMA, nitawaambia wajikite kwenye misingi ya siasa na wasikubali kuendeshwa kwa hofu ya nini kitasemwa X (Twitter) au Instagram na wanaharakati, otherwise itapoteza muelekeo".